Showing posts with label ZIARA ZA JK. Show all posts
Showing posts with label ZIARA ZA JK. Show all posts

19 Jan 2013

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu kesho Rais Jakaya Kikwete atakutana na kufanya mazungumzo na MAMA FRANNIE LEAUTIERA,anayetajwa kuwa ni Mtendaji Mkuu wa MFUKO PRIVATE FUND.

Nimejaribu kufanya utafiti mtandaoni lakini jina la karibu linaloshabihiana na la mwanamama huyo ni FRANNIE LEAUTIER (pichani juu)

Lakini jitihada zangu za kutafuta MFUKO PRIVATE FUND (taasisi ambayo taarifa hiyo ya Ikulu inaeleza kuwa Mama Leautiera ni Mtendaji Mkuu) hazijazaa matunda.

Je Ikulu walimaanisha Frannie Leautier lakini wakaongeza herufi  'A' kimakosa, hivyo kusomeka LEAUTIERA badala ya LEAUTIER?

Tukiamini hilo ni kosa dogo tu la kiuandishi, je MFUKO PRIVATE FUND ni taasisi gani? Na kwanini Rais akutane na Mtendaji Mkuu wake?

Unaweza kudhani maswali haya hayana umuhimu lakini kwa vile taarifa zimeshasambaa duniani kuwa tuna utajiri 'mpya' wa gesi, basi ni vema kufahamu viongozi wetu wanakutana na watu wa aina gani wanapokuwa ziarani huko nje.

Kama mnavyojua, kabla na wakati wa ukoloni akina Karl Peters walipita huko na kule kusaini mikataba ya kilaghai ya kuchukua ardhi na raslimali zetu.Siku hizi, baadhi ya viongozi wa Afrika ndio wamegeuka akina Karl Peters kwa aidha kukaribisha 'wakoloni wapya' au kuwafuata huko makwao kusaini mikataba ya kuuza  nchi yetu.

Ni matarajio yangu kuwa Ikulu itajitahidi kutoa ufafanuzi kuhusu suala hili.



THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIADIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS
Telephone:


255-22-2114512,2116898

E-mail:
[email protected]

[email protected] Fax: 255-22-2113425
PRESIDENT’S OFFICE,THE STATE HOUSE,P.O. BOX 9120,DAR ES SALAAM
.
Tanzania
.
TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
RAIS wa Jamhuriya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa JakayaMrisho Kikwete anaanza ziara rasmi ya Kiserikali nchini Ufaransa leo, Jumamosi, Januari 19, 2013, kwa mwaliko wa Rais wa Ufaransa,Mheshimiwa Francois Hollande.Rais Kikwete na ujumbe wake aliondoka nchini usiku wa kuamkialeo, Jumamosi, kwa ndege ya Shirika la Ndege la Uswisi kuelekea Ulayakwa ajili ya ziara hiyo.Mara baada ya kuwasili kwenye Uwanja waNdege wa Charles DeGaul mjini Paris leo jioni, Rais Kikwete ambaye anafuatana na MamaSalma Kikwete atapokelewa rasmi katika Ufaransa kwa gwaride nakupokelewa na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ufaransa,Mheshimiwa Paschal Canfin.Kwa mujibu wa ratiba, kesho, Rais Kikwete atakutana na kufanyamazungumzo na Mama Frannie Leautiera mbaye ni Mtendaji Mkuu waMfuko Private Fund na baadaye atakutana na Mama Marie ChristineSaragosse, Mtendaji Mkuu wa
Redio France International (RFI).
Mkutano huo utafuatiwa na kikao kati ya Rais Kikwete na Jumuiya yaWatanzania wanaoishi nchini Ufaransa.Keshokutwa, Jumatatu, Rais Kikwete atakutana na kufanyamazungumzo na Mheshimiwa Francois Hollande, Rais wa Ufaransakwenye Kasri ya nchi hiyo ya Elysee Palace.Mazungumzo kati ya Rais Kikwete na Rais Hollande yatafuatiwana chakula cha mchana ambako Rais Kikwete atakaribishwa naWaziriwa Mambo ya Nje wa Ufaransa, Mheshimiwa Laurent Fabius. Baada yachakula hicho cha mchana, Rais Kikwete atakutana na kuzungumza na

Bwana Yves Louis Darricarere, Rais wa Kampuni ya Mafuta yaKimataifa ya Total.Mazungumzo hayo yatafuatiwa na mazungumzo mengine kati yaRais Kikwete na Kiongozi wa Madhehebu ya Ismailia Duniani H.H TheAga Khan na baada ya hapo, Rais Kikwete atakwenda Kasri laLuxemburg kukutana na kuzungumza na Rais wa Bunge la Seneti laUfaransa, Mheshimiwa Jean Pierre Bel.Usiku wa Jumatatu, RaisKikwete atakula chakula cha usiku naRais wa zamani wa Ufaransa, Mheshimiwa Valery Giscard d’Estaingambaye ni Mwenyekiti wa
Tanzania Wildlife Conservation Foundation
. Jumanne, Rais Kikwete atakuwa na siku nyingine yenye shughulinyingi ambako miongoni mwa mambo mengine atakutana na kufanyamazungumzo na mabalozi wa Afrika wanaowakilisha nchi zaokatikaUfaransa, na atakutana na Mheshimiwa Abdou Diouf, KatibuMkuu wa Umoja wa Kimataifa wa Nchi Zinazongumza Lugha yaKifaransa na Rais wa zamani wa Senegal.Rais Kikwete pia atashiriki majadiliano kuhusu masuala yakimataifa yaliyoandaliwa na Taasisi ya Mahusiano ya Kimataifa yaUfaransa – Institute Francais Des Relations International (IFRI) naatakutana na kuzungumza na Mkurugenzi Mkuu wa Shirika laMaendeleo ya Kimataifa la Ufaransa (AFD).Rais Kikwete ataondoka nchini Ufaransa Jumatano, Januari 23,2013, kwenda Uswisi ambako atatembelea Makao Makuu ya Shirikishola Soka Duniani (FIFA) mjini Zurich na baadaye kwenda Davoskuhudhuria mkutano wa mwaka huu wa Shirika la Uchumi Duniani –
World Economic Forum (WEF).
Imetolewa na
:Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu
.Dar es Salaam.19 Januari, 2013
Kuna mambo mawili  ya msingi yanayohusiana na taarifa hii:

 KWANZA, Ziara hii ya Rais Kikwete huko Ufaransa inazidi kuthibitisha kuwa Rais ameamua kuziba masikio kwa kelele kuwa ANASAFIRI MNO.Na kelele hizo si za chuki wala hazimaanishi 'Rais aote matende kwa kwa kutotoka nje ya Ikulu.' Ukweli ni kwamba safari hizi za mfululizoni mzigo mkubwa kwa nchi yetu ambayo inakabiliwa na jumla ya wastani ya deni la nje na ndani la takriban shilingi 40,000,000,000,000 (TRILIONI 40)! 

 PILI, ni fedheha kwa Rais Kikwete kupokelewa na Waziri wa Misaada ya Maendeleo wa Ufaransa.Hii inaonyesha kuwa ziara hiyo si muhimu kwa nchi hiyo,japo Rais Kikwete baadaye atakutana na Rais Hollande wa Ufaransa.Mkuu wa nchi anapozuru nchi nyingine shurti apokelewe na mwenyeji wake,yaani mkuu mwenzie wa nchi.

29 Oct 2008

Na Mwandishi Maalum, Tabora
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ametetea mila ya chagulaga kuwa haisababishi wasichana wengi kupata mimba kabla ya wakati, huku akionya dhidi ya vitendo vya viongozi kugeuza mila za watu kuwa adui, na kuziua kwa kisingizio cha kutatua matatizo.

Chagulaga ni kati ya mila za wenyeji wa mkoa wa Tabora ambayo huhusisha wasichana kujipanga ili kuwapa nafasi wavulana kuwaendea na kuchagua wachumba, lakini mamlaka za mjini hapa zimeichukulia kama moja ya njia zinazoongeza idadi ya wanafunzi wa kike kupata mimba wilayani Uyui.

“Haya ndiyo maisha ya watu hawa miaka yote" alisema Rais Kikwete wakati akipokea taarifa ya utendaji wa serikali wilayani Uyui iliyoonyesha kuwa wanafunzi wengi hupata mimba kabla ya wakati wao na hivyo kujikuta wakipoteza nafasi ya kuendelea mbele kimasomo.

"Tusije kugeuza mila za watu kuwa adui na tukaanza kuua mila hizo kwa kisingizio cha kujaribu kutafuta majawabu ya baadhi ya matatizo yanayotukabili,” Rais aliwaambia viongozi wa wilaya hiyo juzi asubuhi ikiwa ni siku ya tano ya ziara yake mkoani Tabora.

“Haya ndio maisha yao ya miaka yote? Hapa mjini watoto wa kike wa shule wanapata mimba na wala hakuna Chagulaga. Tusije tukageuza mila kuwa ndiyo adui. Inawezekana kuwa mila hiyo inawezesha tatizo hilo, lakini ngoma zimekuwepo miaka na miaka, na tatizo la mimba siyo la miaka mingi kiasi hicho.

“Sote hapa tumecheza ngoma, tena usiku. Ni ngoma tu za kawaida za makabila yetu. Na wale wanaowapa mimba watoto wa shule pengine hata kwenye ngoma hawaji. Inawezekana kabisa kuwa watu wanaowapa mimba watoto hawa ni mizee ambayo hata kwenye ngoma haendi. Na je si kweli kuwa sisi sote tumecheza dansi na disko, na si tulirudi nyumbani salama.”

Rais alisema kuwa ni kweli kwamba tatizo lipo laakini tulichambue zaidi ili kupata kiini chake cha msingi. Tusije tukaua mila za watu kwa visingizio tu. Hata kwetu kule tunayo mila ya kuchengula, na wala haina madhara ya kimaendeleo”.

Rais Kikwete, ambaye anatokea mkoa wa Pwani unaosifika kwa ngoma za sherehe, alisisitiza kuwa kwa jadi ya Waafrika kupata mimba nje ya ndoa ni aibu kubwa kwa familia yoyote na kwamba suala hilo halihusiani na mila yoyote.

"Na wala msije kukimbilia kupiga marufuku ngoma za watu, kwa sababu inawezekana kabisa ukasimamisha ngoma, lakini mimba zikaendelea. Kule Chunya (mkoa wa Mbeya) kuna mimba nyingi sana za watoto wa shule kuliko hata hapa, lakini hakuna Chagulaga,” alisema Rais Kikwete.

Awali, mkuu wa wilaya hiyo, Doreen Semali Kisamo alimwambia Rais Kikwete kuwa mila hiyo ya Chagulaga ni moja ya sababu ya mimba nyingi kwa watoto wa kike katika shule za sekondari wilayani humo.

Lakini alikuwa ameelezwa na viongozi wa wilaya hiyo awali kuwa moja ya sababu za kuwa na idadi kubwa ya wasichana wanaopata mimba ni mila za wakazi wa eneo hilo, hasa vijijini, ikiwamo ile ya Chagulaga.

Akiwa Tabora, Rais Kikwete alisimamisha kwa muda ziara yake Jumapili na kwenda Afrika Kusini kufungua kikao cha 10 cha Bunge la Afrika. Rais alirejea Dar es Salaam Jumatatu jioni na kurudi Tabora juzi asubuhi kuendelea na ziara yake.

Katika miaka miwili iliyopita, kiasi cha wanafunzi 44 wa kike wilayani humo walipata mimba.

Pia Rais Kikwete alishtushwa na ongezeko kubwa la watu wilayani humo na kutaka wahusika wa programu ya uzazi wa mpango, maarufu kama "Nyota ya Kijani" kuitupia macho wilaya hiyo.

Rais alielezwa kuwa ongezeko la watu katika wilaya hiyo kwa njia ya kuzaliana ni wastani wa asilimia 4.8 ikiwa ni kiwango cha juu sana ukilinganisha na cha taifa ambacho ni asilimia 2.8.

“Hizi ni takwimu si za kawaida. Ongezeko la asilimia 4.8 pengine ni kubwa kuliko katika eneo lolote nchini kwa sababu wastani wa taifa ni asilimia 2.8. Hii ni mara mbili ya wastani wa taifa,” alisema Kikwete.

Baada ya maelekezo hayo ya Rais, mzee mmoja kwenye mkutano huo alimweleza Rais Kikwete kuwa wakazi wa Uyui wanazaana sana kwa sababu “tunakula sana, na tunazaana sana, mkuu".

Lakini rais akasema: “Hili siyo jambo jema sana. It is striking (linastua). Wastani wa taifa ni asilimia 2.8. Nyota ya kijani lazima iangaze huku.”

Rais pia alionekana kushtushwa na idadi ya mauaji katika wilaya hiyo baada ya kutaarifiwa kuwa watu 34 wameauwa katika miezi sita iliyopita.

Kwa nini mauaji ni mengi mno kiasi hiki? Watu 34 katika miezi sita ni wengi sana katika wilaya moja. Wilaya nyingine zinakaa mwaka mzima bila hata kuuawa mtu yoyote.”

Jana asubuhi, Rais Kikwete alitembelea kijiji cha Kigwa ambako aliweka jiwe la msingi kwenye soko jipya la kijiji/mji hicho katika shughuli iliyohudhuriwa na mamia ya watu.

Akijibu maombi ya baadhi ya viongozi wa kijiji hicho kumtaka atoe maagizo ili kijiji hicho kiwe na hadhi ya kata, Rais Kikwete alisema:

“Kazi yangu si kugawa kata, na wala kata haigawanywi katikati ya kipindi cha uchaguzi. Kwa sababu tukigawa kata katikati ya kipindi cha uchaguzi ni lazima tufanye uchaguzi mpya wa madiwani. Hata hivyo, kugawa kata siyo tatizo, ili mradi tu mfuate taratibu za ugawaji kata.”

Katika kijiji cha mfano cha Milenia cha Mbola, tarafa ya Ilolangula, Rais alikagua miradi inayofanyika chini ya dhana hiyo mpya ya kuendeleza vijiji na kuzungumza na wananchi.

Rais aliwaambia mamia ya wananchi kwenye mkutano wa hadhara katika kijiji hicho kuwa wakazi wa kijiji Milenia wanaokataa kuchangia magunia mawili ya mahindi kwa ajili ya chakula cha watoto wa shule wa kijiji hicho, wasipewe mbolea ya bure mpaka wametimiza masharti hayo.

“Nasikia baadhi yetu hamjachangia magunia mawili ya mahindi kutokana na mazao yenu kama yanavyosema masharti ya uzalishaji katika kijiji hiki. Sasa wale wanaokataa kuchangia kama ilivyokubaliwa, wanyimwe mbolea ya bure kuanzia sasa,” alisema.

Moja ya masharti ya misaada ya Milenia kwa kijiji hicho ni wakulima kupewa mbolea ya bure. Mradi huo unafadhiliwa na wafadhili mbali mbali.

Rais pia aliwaambia wakazi wa kijiji hicho kuthamini elimu kwa watoto wao. “Halitakuwa jambo linalowezekana kuwarithisha watoto wenu fimbo za kuchungia ng’ombe. Bila elimu watoto wenu watapata taabu sana katika miaka ijayo,” alisema.

Kijiji cha Ilolangula ndiko alikozaliwa mwenyekiti wa Chama cha Wananchi (CUF), Profesa Ibrahim Lipumba.

CHANZO: Mwananchi

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.