14 Jun 2009







Yote ni katika kuendeleza mila.Ni katika kabila la wahamaji (nomads) la Vadi katika jimbo la Gujarat nchini India.Kabila hilo lenye takriban watu 600 hivi,lina mila ya kuwapatia watoto mafunzo ya sanaa ya kucheza na nyoka (snake charming).Lakini,hilo sio suala la siku moja,wiki,mwezi au mwaka bali ni muongo mzima (mika 10)!
Watoto huingizwa kwenye mafunzo hayo wanapotimiza miaka miwili tangu wazaliwe.Inatarajiwa kuwa watapofikisha umri wa miaka 12,watoto hao watakuwa wakielewa kila kitu kinachohusiana na nyoka.

13 Jun 2009


AHMADINEJAD AMEKUWA AKISHUTUMIWA KWAMBA AMESHINDWA KUBORESHA UCHUMI WA IRAN

Kwa mujibu wa televisheni ya taifa ya Iran,Rais Mahmoud Ahmadinejad amefanikiwa kutetea nafasi yake kwenye uchaguzi mkuu uliofanyika nchini humo wiki hii.Kwa mujibu wa taarifa hizo,Ahmadinejad amepata asilimia 67 ya kura huku mgombea wa mwenye mrengo wa mageuzi,Waziri Mkuu wa zamani Mir Hossein Mousavi,akiambulia asilimia 30. SURA YA MAGEUZI.UKURASA WA MOUSSAVI KWENYE FACEBOOK.

Hata hivyo,kuna taarifa kwamba Mousavi nae anadai ameshinda uchaguzi huo.Wagombea wengine ni pamoja na mwanazuoni mwanamageuzi Mehdi Karroubi (picha inayofuata chini) na kamanda mhafidhina wa Revolutionary Guard Mohsein Rezaei (picha ya mwisho chini).

VYANZO: Kurasa mbalimbali mtandaoni

12 Jun 2009


Bajeti ndio hiyo ishasomwa.Ila nimeonelea nami niiweke hapa.Isome hapo chini baada ja mjadala huu kiduchuTunaambiwa kuna maeneo takriban sita yaliyopewa kipaumbele katika bajeti hiyo.Naamini hata bajeti ya mwaka jana ilikuwa na vipaumbele vilevile lakini sote tunajua hali ikoje muda huu.Tatizo letu kubwa halipo katika kuainisha vipaumbele.Wala hatuna tatizo kuja na grand schemes zinazoweza kabisa kukuaminisha kuwa huenda sooner or later "maisha bora kwa kila Mtanzania yatakuwa sio tena slogan bali ukweli halisi".Tatizo la msingi ni kuvifanya vipaumbele hivyo viwe na maana,in the sense of kuvitafsiri kwa vitendo na si porojo.Sambamba na hilo ni namna vipaumbele hivyo vitakavyoweza kuruka vihunzi vya mafisadi.

Anyway,hilo sio la muhimu sana kwa sasa kulinganisha na uwezekano wa kufanikiwa kwa hizo tahadhari tunazoelezwa.Kwanza,yote yaliyoelezwa yanawezekana kwa sababu nia ipo,sababu zipo na njia zipo pia.Kinachoweza kukwamisha utekelezaji wa mpango mzima wa kunusuru uchumi ni ufisadi.

Nilitarajia bashasha zilizoambatana na bajeti hii zingegusia ishu ya ufisadi lakini wapi!Tuwe wakweli,hivi kuna uhakika gani kuwa hizo fedha zinazotengwa kwa ajili ya kufidiwa sijui watu gani hazitaishia kwa mafisadi?Ni muhimu kuuliza hilo kwa vile akina Kagoda bado wako huru uraiani na yayumkinika kuamini kuwa watashawishika kuchangamkia tenda hii ya "kunusuriwa na mtikisiko wa uchumi wa dunia."Simple logic ni kwamba kama waliweza kuiba bilioni 40 za EPA na taasisi husika zinaogopa hata kuwataja hadharani,kwanini safari hii wasikwapue tena fedha za umma kwa "njia halali"?

Naomba nitoe mfano hao katika kupigia mstari wasiwasi wangu kuhusu hatma ya hizo tahadhari tulizopewa kuhusu mtikisiko wa uchumi duniani.Hivi karibuni ulifanyika mheshimiwa mmoja aitwaye Peter Noni aliteuliwa kuwa Mkurugenzi wa Benki wa Raslimali Tanzania (TIB).Uteuzi huu unaweza kuashiria ni kwa namna gani kelele dhidi ya watu wanaohusishwa kwa namna moja au nyingine na ishu za ufisadi zinavyopuuzwa.Jina la Noni limekuwa likitajwa sana kwa wanaojua undani wa ishu nzima ya EPA.Sasa sijui inamaanisha nini kumpeleka sehemu kama TIB,ambayo kwa hakika itapaswa kuwajibika ipasavyo kama tunataka tahadhari ya bajeti iwe na maana.Hii si ni mithili ya kumpa "teja" usimamizi ya stoo ya madawa?

Pasipo kudhibiti ufisadi na mafisadi,yayumkinika kuamini kuwa jitihada zote hizi zitaishia kunufaisha mafisadi na nyumba ndogo zao.Ni kweli kwamba Watanzania wengi wameonyesha umahiri mkubwa wa kukabiliana na hali ngumu ya uchumi na wameshazowea "kukaza mikanda kila wanapotakiwa kufanya hivyo" lakini hii inapswa iwe kwa Watanzania wote na si walalahoi pekee.Ikumbukwe kuwa mikanda hiyo imekuwa ikikazwa tangu wakati na baada ya Vita vya Kagera,na hatujawahi kusikia tamko kwamba WAKATI UMEFIKA KULEGEZA MIKANDA HIYO.Inwezekana kuwa tamko kama hilo halijatolewa kwa vile wakati huo (wa kulegeza mikanda) bado haujafika lakini inauma kuona kufunga mikanda kwa wengi kunatoa fursa kwa walafi wachache kufumuka vitambi (kiasi cha kushindwa hata kuvaa hiyo mikanda,let alone kuikaza) kwa matendo yao ya ufisadi.

Tuweke ushkaji pembeni,tuweke siasa za 2010 pembeni,tutambue kuwa mtikisiko wa uchumi ulimwengini ni kitu halisi na hata wafadhili wetu wanasumbuliwa nao.Tukiendeleza hadithi nzuri pasipo utekelezaji mzuri,tutajikuta pabaya.Tukumbuke kwamba tulikuwa masikini kabla hata ya huu mtikisiko wa sasa.Kinachotuweka pabaya kwa muda huu ni ukweli kwamba tofauti na huko nyuma,sasa hivi wafadhili wetu nao wana matatizo pia.Na kwa vile hakuna uhakika as to lini mtikisiko huu utapungua makali,ni vema pia tukatambua kuwa wafadhili hao wanaweza kutusahau kabisa ili waweze kumudu matatizo yao binafsi.

Inawezekana,only if kukiwa na dhamira thabiti pamoja na kuweka mbele maslahi ya nchi badala vikundi vya watu wachache.Na katika hilo,tayari kuna ishara isiyopendeza kwani waliofikiriwa katika stimulus plan ni wafanyabiashara (kwa maana ya taasisi na watu binafsi) pekee huku wakulima wakipuuzwa.Yet,tunaambiwa KILIMO KWANZA!I hope sio kilimo cha fedha za walipakodi kitachopelekea mavuno mwanana kwa mafisadi na kampeni zao za 2010!

Mungu ibariki Tanzania,na waadhibu pasipo huruma mafisadi wote.


BAJETI YA SERIKALI KWA MWAKA WA FEDHA 2009/2010











Kwa hisani ya The Daily Mail.

10 Jun 2009












"I am proud of being the smallest girl. I love all the attention I get. I'm not scared of being small, and I don't regret being small",says Jyoti Amge,a 1ft 11 tall Indian girl.For more about this smallest girl in the world CLICK HERE.


















Pics from The Daily Mail

9 Jun 2009


Kukua kwa teknolojia kuna faida na hasara zake.Kuna nyakati faida huwa kubwa kuliko hasara,na kinyume chake.Kuna nyakati faida huwa kubwa zaidi kwa eneo au sekta flani na hasara kuwa kubwa zaidi kwenye eneo/sekta nyingine.Na ndivyo ilivyo kwa athari za teknolojia ya intaneti kwa "boksi la uzembe" (runinga au televisheni).

Ni dhahiri kwamba kinachoifanya intaneti "iipige bao" runinga ni nafasi ya mtumiaji katika kutumia chombo husika.Chukua mfano huu: unataka kutafuta nafasi za masomo na/au ufadhili sehemu mbalimbali.Unajua mahala mwafaka pa kwenda ni kwa Da Subi.Unafika hapo,unaambiwa "scholarships zitaletwa kwenu saa 2 kamili usiku"!Mfano huo wa kufikirika unasaidia kuonyesha ni kwa namna gani runinga imeendelea kuhodhi uhuru na wepesi wa kupata na kutafuta habari.Kwa upande mwingine,kwa kutumia mfano huohuo,mtumiaji ana uhuru wa kwenda moja kwa moja kwenye tovuti ya Da Subi,au ku-google maneno kama "nukta 77","Subi","Scholarships",nk.


Kingine kinachoikwaza runinga ni namna watumiaji wanavyoweza "kujichanganya" (sio kuwa confused bali namaanisha interactivity).Japo teknolojia ya runinga inajitahidi kwenda na kasi hiyo ya "kujichanganya",kwa mfano kwa kukaribisha maoni yanayoweza kusomwa "laivu",kupiga kura kwenye vipindi kama Big Borther,American Idol,nk,au kutuma video na picha kama ilivyo kwa i-Report ya CNN,ukweli unabaki kuwa maendeleo hayo ni "cha mtoto" ukilinganisha na internet inavyowezesha mambo kwenye social networks kama facebook,myspace,nk.




Kama hiyo haitoshi,mtumiaji wa intaneti anaweza kuangalia runinga pasipo na matatizo (ali mradi kompyuta yake iwe na vifaa stahili na spidi mwafaka) ilhali ku-access intaneti kwenye televisheni bado ni tatizo japo baadhi ya vinajitahidi kumwezesha msomaji kutembelea kurasa flani flani.Tatizo bado linabaki kuwa kurasa hizo ni chache na zinaamuliwa na kituo husika


Wanaopenda uhuru wa kufanya mambo wanavyo taka wao wanaiona teknolojia ya runinga kama ya "kidikteta" ambapo ushiriki wa mtumiaji ni mdogo zaidi kulinganisha na ule wa kwenye intaneti.Unapoingia mtandaoni,huhitaji kuangalia "ratiba ya vipindi" (kama ilivyo kwenye tv) bali una uhuru wa kuzurura upendavyo.


Kwa mujibu wa kituo cha runinga cha Channel 4 cha hapa Uingereza,idadi ya vijana wanaoangalia televisheni imekuwa ikishuka kwa kasi kubwa kulinganisha na matumizi yao ya intaneti.Na pengine katika kutambua hilo ndio maana hata gwiji la umiliki wa vyombo vya habari,Rupert Murdoch,aliamua kununua tovuti ya "kujichanganya" ya Myspace.Tajiri huyo ni mmiliki wa Fox News,Wall Street Journal,New York Times,Sky na mlolongo wa vyombo vya habari duniani anaamini kuwa future ya sekta ya habari iko kwenye intaneti.

Unaonaje?

8 Jun 2009


WHY SHOULD WE ALWAYS LESS,IF NOT NOTHING AT ALL?HIVI TUNGEKUWA NA WAWEKEZAJI NCHINI INDIA (WANAKOTOKA WABABAISHAJI WA TRL) HALAFU WASHINDWE KUKIDHI MATARAJIO YA WAHINDI,UNADHANI WASINGETIMULIWA?POROJO KWAMBA PASIPO TRL HUDUMA ZA RELI YA KATI NDIO KWISHNE HAZIINGII AKILINI HATA KIDOGO.KAMA TUNAWEZA KUWALIPA WABUNGE WETU MAMILIONI YA SHILINGI KILA MWEZI PASIPO KUHITAJI MSAADA WA WAWEKEZAJI,SIONI KWANINI TUSHINDWE KUMUDU UENDESHAJI WA HUDUMA YA TRENI RELI YA KATI.




Abiria 552 waliotakiwa kusafiri na treni ya kati juzi, wamekwama jijini Dar es Salaam baada ya wafanyakazi wa Kampuni ya ReliTanzania (TRL), kugoma kwa lengo la kushinikiza uongozi wa shirika hilo, kusaini mkataba wa Maisha Bora unaojulikana kwa jina la Mkataba wa Hiyari.

Wakizungumza na 'HabariLeo Jumapili' katika nyakati tofauti, baadhi ya abiria waliokuwa wakitarajia kwenda Tabora, Mwanza na Kigoma, walisema walipaswa kusafiri juzi lakini ilipofika saa mbili usiku, walitangaziwa kuwa safari hiyo haipo na kutakiwa kusubiri hadi kesho yake (jana) kujua hatma ya safari hiyo.

“Kweli tulisubiri na ilipofika leo (jana) saa tano, tulitangaziwa kuwa safari haitakuwapo hivyo tujipange kwenye mstari ili turudishiwe nauli zetu. “Sisi tumefedheheshwa sana na kitendo hiki hivyo tunaiomba serikali ichukue hatua madhubuti ili abiria wanaotegemea usafiri wa treni wasiendelee kuumia,” alisema abiria aliyejitambulisha kwa jina la Masanja Said.

HabariLeo Jumapili imeshuhudia abiria wakiwa katika mistari mirefu wakisubiri kurejeshewa fedha za nauli wakati watoto na wazee walikuwa wamelala sakafuni kwenye jengo la kampuni hiyo. Meneja Uhusiano wa TRL, Midladjy Maez, alisema mgomo huo hautambuliki kisheria kwa kuwa viongozi wa Chama cha Wafanyakazi wa Reli (Trawu) wanasema hawajatangaza mgomo.

“Baada ya wafanyakazi kugoma, uongozi uliwasiliana na viongozi wa Trawu lakini viongozi hao walisema hawajatangaza mgomo kwani kisheria tangazo la mgomo linatolewa saa 48 kabla ya kuanzamgomo. Hata hivyo hakuna tangazo lolote wala kiongozi wa mgomo hajulikani,” alisema Meaz.

Inadaiwa kuwa wafanyakazi hao waligoma baada ya viongozi wa Trawu kuwapatia ripoti kwamba uongozi wa kampuni umegoma kusaini mkataba wahiyari na kwamba uongozi umeondoa kipengele kinachomtaka mwajiri kuwalipa wafanyakazi wanaopunguzwa kazi mishahara ya miezi 20 hadi 40 kama mkono wa heri.

Meaz alisema, uongozi wa TRL uliamua kurejeshea abiria fedha zao baada ya juhudi za kuwataka wafanyakazi hao kusitisha mgomo kutozaa matunda. Alisema uongozi umejaribu kuwasiliana na TRAWU Taifa na kujibiwa kuwa hakuna mgomo ila ni shinikizo.

“Tatizo haijulikani nani kiongozi wa mgomo, kila anayeulizwa anasema hajui lolote. Kisheria hakuna mgomo lakini katika hali halisi wafanyakazi wamegoma na ndio maana abiria wamerudishiwa fedha zao za nauli,” alisema Meaz. Juhudi za kuwapata viongozi wa Trawu haikuzaa matundakwa kuwa ofisi zao zilikuwa zimefungwa pia simu za mkononi zilikuwa zimefungwa.

CHANZO: Habari Leo


Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.