16 Aug 2013
15 Aug 2013
15.8.13
Evarist Chahali
RAIA MWEMA
No comments

Ni maswali ya ‘kipuuzi’ lakini yanaweza kuamsha hisia za msingi tukiangalia mwenendo wa taifa letu hivi sasa.
Sijui Mungu atupe nini. Ametubariki na nchi iliyoishi kwa amani na upendo kwa miaka kadhaa. Akatupatia Baba wa Taifa, Mwalimu Nyerere ambaye licha ya kuhimiza umoja miongoni mwetu kama Watanzania, lakini pia alipigania umoja wa Bara la Afrika.
Nyerere alitambua mapema kuwa ni rahisi kwa nchi yenye makabila zaidi ya 120 kuwa vipande vipande kama isipounganishwa na itikadi ya kutufanya tuwe na umoja. Akahimiza siasa ya Ujamaa ambayo kimsingi ililenga kuondoa matabaka na tofauti za kinadharia na kihalisia, kutuacha sote tukiwa Watanzania.
Mungu pia ametujalia nchi yenye raslimali nyingi, utajiri ambao hata mataifa tajiri kabisa duniani yanatamani ungekuwa katika nchi zao.
Katika mazingira ya kuchafua kabisa, jitihada alizofanya Nyerere kutuunganisha zikaanza kuhujumiwa mara tu baada ya kung’atuka kwake. Chama alichokiasisi, CCM, kikamgeuka kupitia Azimio la Zanzibar, ‘uhuni’ uliotangaza kifo cha itikadi ya Ujamaa.
Tangu wakati huo, nchi imekuwa kama ‘imerogwa’ vile. Kwenye ubepari hatupo (maana kila Ilani ya Uchaguzi ya CCM inasema Tanzania ni nchi inayofuata misingi ya Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea) na Katiba yetu inabainisha hivyo pia. Kwenye Ujamaa nako hatupo, kwa sababu kila msingi uliobeba itikadi hiyo umetupwa.
Pamoja na rasilimali zetu lukuki tumeendelea kuwa nchi masikini kabisa duniani. Badala ya kuwa soko la bidhaa zinazotokana na utajiri wetu, tumekuwa ombaomba wakubwa huku viongozi wetu, bila haya, wanadiriki kutamka bayana eti tusipofanya ziara huko nje hatutopata maendeleo.
Sawa, safari za mfululizo huko nje zimefanikiwa kuleta viongozi wa mataifa makubwa zaidi duniani, Rais Xi Jinping wa China na baadaye ‘rais wa dunia’ Barack Obama wa Marekani. Kama kawaida, viongozi wetu wakatembea vifua mbele na kujigamba nchi sasa imepiga hatua ndio maana viongozi muhimu wa dunia wanatutembelea.
Ni kweli, ziara za marais Jinping na Obama zilifanikiwa kuiweka Tanzania kwenye ramani ya dunia (kututangaza vizuri duniani).
Nakumbuka wakati wa ziara ya Rais Obama, taarifa moja ya Shirika la Utangazaji la Uingereza (BBC) ilibainisha kuwa Tanzania ni moja ya nchi zenye uchumi unaokua kwa kasi duniani. Nani angebisha ilhali Wachina na Wamarekani wanapigana vikumbo kuitembelea nchi yetu?
Lakini kama vile tumerogwa, siku chache tu baada ya ziara ya Obama zikapatikana taarifa kuwa kulikuwa na ufisadi wa mabilioni ya shilingi katika maandalizi ya mkutano wa Smart Partnership, uliowakutanisha marais kadhaa wa Afrika.
Je, inaingia akilini maandalizi tu ya mkutano huo wa Smart Partnership yazue ufisadi wa mabilioni ya shilingi, kabla mpango husika haujaanza kutekelezwa? Niliwahi kuandika huko nyuma kuwa wakati Obama anahangaika na mawazo yake mazuri ya kutumwagia dola za Marekani, mafisadi nao wanahaha kuandaa mabakuli ya kudaka fedha hizo. Huo ufisadi wa fedha za maandalizi ya mkutano huo ni kama ‘utangulizi’ tu, filamu yenyewe inasubiri fedha zianze kumiminika.
Kama hiyo haitoshi, siku chache baada ya ziara ya Obama, jina la nchi yetu likianza kuvuma tena kwenye anga za kimataifa, safari hii tatizo likiwa ni kwenye biashara ya dawa za kulevya. Kwa hakika huwezi kumshangaa mtu anayedhani huenda tumerogwa, kwa sababu licha ya kupata bahati ya mtende ya jina letu kusikika kwa uzuri katika takriban kila kona ya dunia kutokana na ziara ya Obama, kwa makusudi tumechafua sifa hiyo.
Ni kama vile uamuzi fyongo wa Obama kufumbia macho ukiukwaji mkubwa wa haki za binadamu Tanzania ulikuwa ni ruhusa kwa vyombo vya dola na wahalifu (wakati mwingine ni vigumu kutofautisha kati ya chombo cha dola na wahalifu) kuendelea kuhatarisha usalama wa Watanzania. Tumeendelea kushuhudia matukio mbalimbali yanayozidi kuchafua taifa, ndani na nje.
Kutoka mahala kusikoeleweka, Jeshi la Polisi ambalo halioni aibu kuonekana linakitumikia chama tawala CCM kuwakandamiza wapinzani, likakurupuka na mkakati hatari wa ‘kuzusha’ kesi za ugaidi dhidi ya wanasiasa wa upinzani. Ni nchi iliyorogwa pekee inayoweza kufanya mzaha katika ugaidi. Ndio maana, majuzi tu, Jaji Simon Lukelelwa alitoa onyo kali kuhusu ‘kuchezea ugaidi’ wakati akitoa hukumu katika kesi iliyokuwa ikiwakabili viongozi kadhaa wa CHADEMA huko Tabora.
Wakati polisi na CCM wanacheza ‘mchezo mbaya’ wa tuhuma za ugaidi bila kujali madhara yake kwa hadhi ya nchi yetu, bado tumeendelea kuwa gizani kuhusu hatima ya mauaji ya Padre Evarist Mushi aliyeuawa kikatili huko Zanzibar, shambulio la bomu kanisani Arusha, na shambulio la bomu katika mkutano wa CHADEMA huko huko Arusha.
Na ghafla Jiji la Arusha limegeuka ‘uwanja wa vifo vya matajiri’, tukio la hivi karibuni ni la mauaji ya kinyama dhidi ya mfanyabiashara tajiri jijini humo, Erasto Msuya. Mauaji ya mfanyabiashara huyo yameibua hisia kuwa hata vifo vya hivi karibuni vya matajiri wengine wa maeneo hayo si vifo vya asili bali mauaji.
Lakini kama kuna tukio baya kabisa ni hili la majuzi la mabinti wawili kutoka Uingereza kumwagiwa tindikali Visiwani Zanzibar. Tangu nifike hapa Uingereza, zaidi ya miaka 10 iliyopita, sijawahi kusikia au kuona Tanzania ikitawala katika vyombo vya habari vya hapa kama ilivyo sasa kuhusiana na tukio hilo la tindikali.
Tukio hilo la tindikali limetuathiri hata akina sie, kwani majuzi tu kuna jamaa aliniuliza asili yangu ni wapi, na nilipomjibu "Tanzania" akakunja sura na kuniuliza “kule mlikowamwagia tindikali mabinti wetu waliokuja kujitolea kuwasaidia (volunteer)?” Aibu niliyopata inabaki nafsini mwangu.
Na sijui ni katika kutapatapa au kutaka kuwahadaa Waingereza, sakata la Sheikh Ponda Issa Ponda, ambaye inadaiwa amepigwa risasi na polisi, linafanya kile wanachoita Waingereza a bad case gets even worse (jambo baya linakuwa baya zaidi). Nisingependa kujadili kwa undani suala la Ponda, ambaye kwa hapa Uingereza anatajwa (kimakosa, kwa mtizamo wangu) kuwa ndiye mtuhumiwa wa uchochezi uliosababisha shambulio la tindikali kwa mabinti hao wa Kiingereza.
Ninaweza kuandika makala mfululizo zisizo na kikomo kuorodhesha masuala mbalimbali yanayoweza kumfanya mtu adhani tumerogwa (au tumejiroga) lakini cha muhimu sio lawama pasi kukaa chini na kujiuliza kulikoni?
Kuna udhaifu mahala fulani unaomwathiri kila Mtanzania. Tunaweza kumlaumu Rais Paul Kagame wa Rwanda kuwa ndiye tishio kubwa kwa Tanzania kwa sasa, lakini ukweli mchungu ni kwamba chanzo cha matatizo yetu ni ombwe la uongozi. Nchi imegeuka lawless (isiyo na sheria, ila sheria zipo tu linapokuja suala la kesi ‘feki’ za ugaidi wa CHADEMA).
Uhuni wa kuua siasa ya ujamaa umezaa ombwe la itikadi unganishi (integrative ideology) sambamba na kundi la maharamia ambao wapo tayari kwa lolote kwa ajili ya maslahi yao binafsi.
Nimalizie kwa kuhadharisha tena kuwa nchi yetu sio tu inaelekea kubaya bali imeshafika mahala pabaya. Ni matumaini yangu Rais Jakaya Kikwete na wasaidizi wake wanasikia kelele zetu. Anaweza kuamua kupuuza kelele hizi na kuiacha nchi itumbukie katika korongo la kina kirefu, au achukue hatua za haraka kuinusuru nchi yetu.
- See more at: http://raiamwema.co.tz/viongozi-nadhifu-kwa-suti-wahuni-kifikra#sthash.T1aviKJ2.dpuf14 Aug 2013
14.8.13
Evarist Chahali
DRC, PAUL KAGAME, Rwanda, TANZANIA, Uganda, Yoweri Museveni
No comments
Ijue Rwanda, Kagame, Mseveni na Uvamizi wao katika Ardhi ya Kongo
Rwanda ilikuwa eneo penye utawala wa kifalme tangu karne ya 16 BK kabla ya kufika kwa ukoloni. Mwanzo wake ni katika eneo la Ziwa la Muhazi. Watawala wenye cheo cha "mwami" kutoka kikundi cha wafugaji (Watutsi) walitanua himaya zao tangu miaka ya karne ya 16 BK hadi kufika eneo la leo hii. Wafugaji wa ng'ombe Watutsi walikalia nchi pamoja na wakulima wa Kihutu na wawindaji Watwaa.
UKOLONI WA KIJERUMANI
Ukoloni ulichelewa kufika Rwanda, mwaka 1890 Ujerumani na Uingereza walipatana ya kuwa Rwanda na Burundi ziwe ni sehemu ya Afrika ya Mashariki ya Kijerumani. Lakini ilikuwa mwaka 1908 tu ya kwamba Wajerumani walimtuma afisa wa kudumu aliyekaa Rwanda kama mwakilishi wa serikali ya Ujerumani. Mwaka 1916 Ubelgiji na Uingereza walivamia Rwanda katika Vita Kuu ya Kwanza ya Dunia. Baadae ikawa chini ya Ubelgiji pamoja na Burundi kama "Rwanda-Urundi" katika hali ya eneo la kudhaminiwa kutokana na azimio la Shirikisho la Mataifa (UNO).
Utawala wa Wabelgiji ulikuwa wa moja kwa moja na mkali zaidi kuliko wa Wajerumani. Wabelgiji walijaribu kutoa faida ya kiuchumi wakilazimisha wenyeji kupanda mikahawa na kutekeleza kazi za serikali ya kikoloni. Katika utawala wao Wabelgiji walitumia zaidi Watutsi wakiwapa nafasi za elimu na kuwatumia katika shughuli za serikali. Wataalamu wengine huamini ya kwamba siasa hii ilisababisha kukua kwa chuki dhidi ya Watutsi kwa upande wa wakulima Wahutu iliyoleta kumwaga kwa damu baadaye.
Katika miaka ya 1950 ilionekana na kudhihirika ya kwamba ukoloni unaelekea mwisho wake. Uhusiano kati ya Wahutu na Watutsi ukawa vigumu kwa sababu Wabelgiji walibadilisha siasa yao yakupendelea Watutsi wakidai haki zaidi kwa ajili ya Wahutu waliokuwa wengi. Ni hasa wamisionari wa katoliki Mapadre Weupe waliosimama upande wa Wahutu wakiona ndio wagandamizwa.
Mwami Mutara Rudahigwa aliyejiita pia Charles alijaribu kuleta upatanishi kati ya vikundi katika nchi. 1954 aligawa nchi ya kifalme kati ya Wahutu na Watutsi. Lakini alikuwa na wapinzani Watutsi waliomua mwaka 1959. Mtoto wake Mwami Kigeri V. alisimikwa kwenye kiti hicho. Hatua hii ilisababisha ghasia na vurugu nchini kwa sababu Wahutu walidai kuwa na neno katika mabadiliko ya serikali. Mwezi wa Novemba 1959 Mwami Kigeri V. alilazimishwa kuondoka nchini akikimbilia Uganda. Watutsi wenye siasa kali walijaribu kumwua kiongozi wa Mouvement Democratique Republicain (MDR) chama kikubwa cha Wahutu. Wahutu walijibu kwa kuwashambulia na kuua Watutsi. Wabelgiji walitumia wanajeshi wao kupoza hali hiyo nchini Rwanda. Katika uchaguzi wa kwanza wa halmashauri ya tarafa na miji kabla ya uhuru chama cha Parmehutu ndicho kilichopata kura nyingi. Viongozi wa Parmehutu walitangaza serikali mpya mwaka 1961. Uchaguzi wa Bunge ulileta kura ya 77% kwa ajili ya chama cha Parmehutu kilichomchagua kiongozi wake Grégoire Kayibanda kuwa Rais.
Tarehe 01.07.1962 Rwanda ilipata uhuru wake kamili. Wakati huo zaidi ya Watutsi 350,000 tayari walishakuwa wamekimbilia nchi za jirani. Mwaka uliofuata vikundi vya Watutsi kutoka nchi hizo za jirani walijaribu kufanya mapinduzi kwa kushambulia serikali mpya wakitokea uhamishoni. Kitendo hicho kilifuatiwa na uangamizaji wa kwanza wa Watutsi zaidi ya 100,000 waliouawa na Wahutu.
Hata katika miaka iliyofuata mauaji dhidi ya Watutsi iliendelea. Wanasiasa Wahutu walizoea kuita Watusi ndio "Wadudu". Kila kitu kilichokuwa si sawa kilielezwa ni kosa la Watutsi waliokuwa raia bila haki. Idadi kubwa ya Watutsi walikimbia Burundi, Uganda na Tanzania.
Mwaka 1973 Generali Habariyama alimpindua rais Kayibanda na kuanzisha serikali ya kijeshi akijaribu kupatanisha vikundi ndani ya taifa. Lakini hata mwaka uliofuata 1974 mauaji ya Watutsi yalitokea tena.
Mnamo 1990 ilikuwa wazi ya kwamba Rwanda ilikuwa na hali ngumu. Kwa upande moja nchi za mataifa zilisukuma serikali za Afrika kuruhusu kura huru za kisiasa.
Katika Rwanda ongezeko la wakazi lilileta msongamano mkubwa na uhaba wa ardhi ya kilimo na Ufugaji. Uchumi ulikuwa duni, Wakati huohuo wapinzani Wahutu walikusanyika nje ya nchi hiyo kudai demokrasia. Na katika makumi elfu ya watoto wa Watutsi waliokuwa nje ya nchi hiyo, sauti zikasikika zilizodai warudi tena kuijenga Rwanda.
Habyarimana alijaribu kutafuta suluhisho na ungamano wa kitaifa, akaanza kujadiliana na Watutsi wa nje lakini alikutana na upinzani kwa upande wa Wahutu wakali waliochukia uelewano na Watutsi.
Safari ya Kagame na RPF kurudu Rwanda kutoka Uganda.
Oktoba 1990 Watutsi waliokaa Uganda walianzisha chama cha RPF (Rwanda Patriotic Front) wakiwa na wafuasi wahutu wachache wakavamia Rwanda kwa silaha. Kiongozi wao alikuwa Paul Kagame aliyeondoka Rwanda akiwa mtoto wa miaka minne. Alikuwa amejiunga na jeshi la Yoweri Museveni na kupanda ngazi katika jeshi la Uganda hadi kuwa mkuu wa huduma ya usalama ya kijeshi ya Uganda. Walitaka kulazimisha serikali ibadilishe hali ya Watutsi kuwa raia bila haki. Lakini uvamizi huu ulisababisha kuongezeka kwa ukali wa Wahutu dhidi ya Watutsi ndani ya Rwanda na siasa kali kwa upande wa viongozi Wahutu. Kikundi cha kihutu cha Interahamwe kilipewa silaha kujibu mapigo dhidi ya uvamizi wa Kagame, Maelfu ya Watutsi Warwanda waliuawa. Vita kati ya wapinzani kutoka Uganda na jeshi la serikali iliendelea mpakani hadi pande zote mbili zilikutana hapa Arusha Tanzania na kupatana kukoma kwa vita 1992 chini ya uangalizi wa Umoja wa Mataifa na Umoja wa Afrika.
Sehemu ya viongozi Warwanda walijiandaa kutafuta utaratibu mpya lakini wengine walifanya mipango ya kumaliza swali la Watutsi kabisa wakipanga kuua Watutsi wote nchini.
Tarehe. 06.04.1994 rais Habariyama akirudi nchini kutoka safari ya Tanzania, Ndege yake ilipigwa kombora kabla ya kutua ikaanguka chini akafariki. Uwezekano ni mkubwa ya kwamba ni Wahutu wenye msimamo mkali ndio waliomua, lakini wengine walisema ni Jenerali Paul Kagame na RPF yake.
Tendo hili ilikuwa mwanzo wa mauaji ambayo hayakuwahi kutokea Afrika. Viongozi wa Interahamwe, wa jeshi la kitaifa na vikundi vikali vya Kihutu walitekeleza mipango ya kukusanya Watutsi kila mahali na kuwaua. Haiwezekani kuwa na idadi kamili lakini makadirio ya chini yanataja Watutsi 750.000 na Wahutu wasio wakali zaidi ya 100.000 waliuawa na Interahamwe na wanajeshi wa serikali ya Kihutu. Watu walikimbilia na kutafuta hifadhi makanisani lakini hata huko walichinjwa bila neema. Wahutu waliokataa kushiriki katika mauaji waliuawa pia.
RPF chini ya uongozi wa Paul Kagame iliamua kutumia nguvu zote kusimamisha machinjo haya. Kwa miezi miwili mauaji na vita yalienda sambamba hadi RPF iliposhinda Julai 1994 na kuchukua madaraka ya serikali.
Jeshi, Waparmehutu na serikali ya Kihutu walikimbilia Kongo wakiwalazimisha wakazi wengi kuongozana nao hali iliyosababisha kutokea kwa makambi ya wakimbizi makubwa sana katika Kongo ya mashariki yaliyokuwa na idadi ya Wahutu milioni mbili. Walio wengi wamerudi baada ya kuimarika kwa serikali mpya.
Tangu ushindi wa kijeshi mwaka 1994, RPF walianzisha serikali ya umoja wa kitaifa. Rais alikuwa Pasteur Bizimungu mwanasiasa Mhutu aliyeshikamana na RPF Kagame akiwa makamu wake. Baada ya kupinduliwa kwa Bizimungu mwaka 2000 Kagame akawa Rais. 2003 palitokea uchaguzi wa kwanza wa kirai ambapo chama cha RPF chimi ya Jenerali Paul Kagame kilishinda.
Jeshi la Rwanda limeendelea kuwa na vita ndani ya Kongo likipigana na mabaki ya Interahamwe waliokuwa wanashambulia Rwanda mara kwa mara kutoka Kongo.
Kutokana na mauaji hayo ya 1994, mahakama ya kimataifa iliyopo nchini Uholanzi imeendesha hukumu nyingi kwa wahusika wake, vilevile mahaka ya kimataifa ya Arusha nchini Tanzania nayo imeendesha huku stahiki kwa wahusika,
Ndani ya Rwanda mahakama za vijijini zinazoitwa "gachacha" vilevile zimejaribu kutoa hukuma juu ya waliohusija na mauaji ya mwaka 1994.
Mapatano ndani ya Rwanda yamezidi kushamiri, huku Paul Kagame akionsha kuijenga vema Rwanda kwa mkono wa chuma, Mathalani: D.Gasangwa wa EACU arisisitiza kwamba "Sometime in April(2004)" movie, ilikuwa "ETHNIC CLEASING", si HOLOCOSTI!, kama ilivyoandikwa na Wazungu wa Magazeti ya Ulaya. Watu karibu 600,000 waliuawa Rwanda, na hapo Mkoa wa Kivu, Congo.
Afrika ina ujuzi sasa; kama ujuzi wa Kiarabu, Kiswahili, Kilingala, Kiwolof, Kiamharic. Utengamano wa siasa mpya rasima utatupa na fasi ya kujenga inchi mpya kama EACU na Rwanda Kazembe.
Lakini huku mapambazuko mema yakitamalaki Rwanda, Kiongozi wa utawala wa nchi hiyo ndogo, anatajwa kuwa ni miongozi mwa viongozi makupe barani Afrika, ukupe wake sio waufisadi bali ukwasi wenye chembe za kiyunani
Lakini leo yale mabaki ya vikundi vile vya Interahamwe vilivyokimbilia uhamishoni kaskazini mwa Kongo mji wa Goma na Kivu si vikundi vya uasi dhidi ya Rwanda tena bali ni vitendea kazi muhimu dhidi ya upanuzi wa miliki mpya ya Watusi,
Wale watusi waliokimbilia Uganda enzi za Mwami Kigeri V, Inatajwa na kuaminika kuwa Jenerali Paul Kagame, Yoweri Mseveni na Watutsi waliokimbilia Goma baada ya kushika dola zao, walikuja na malengo mujarabu yanayotekelezwa kwa hatua na kwa vipindi virefu sana,
Mpango huo ulikuwa ni kusimika dola imara la Watutsi barani Afrika hasa nchini Kongo katika Goma-Kivu ya Kasiskani mpango siri walioupa jina la "Nchi mpya ya ahadi ya Watutsi". Ni mpango endelevu ulio na lengo la kuwakusanya Watutsi duniani kote na kuwaweka pamoja wakimiliki ardhi na rasilimali zake!
Hili linathibitika katika kile walicho "Mkataba wa kuigawa Kongo" ulisainiwa na Yoweri Mseveni, Paul Kagame na Laurent Kabila akiomba msaada wa kuingia madarakani kwa mtutu wa bunduki,
Naam baada ya Laurent Kabila kuingia madarakani kwamsaada wa Kagame na Mseveni kupitia ule mkataba, Kabila alikataa kuheshimu mkataba ule nakusema yale yalikuwa ni maneno ya porini tu hivyo hawezi kuiuza nchi kwa karatasi za mstuni!
Hapo sasa ndipo tunapoingia kwenye madhila ya Kongo tuliyoyaona tangu mauaji ya L. Kabila na tunayoyashuhudia hii leo chini ya J. Kabila, M23, Kagame na Mseveni
.............................. ...........
MKATABA WA KUIGAWA na KUIUZA KONGO
Kinachoitwa vita vya sasa nchini Kongo ni utekelezaji wa “Makubaliano ya Lemera” ya mwaka 1996 yenye shabaha ya kuigawa nchi hiyo kubwa kuliko yoyote ile Afrika Mashariki na Kati.
Makubaliano yalifanywa kati ya Laurent Desire Kabila, akiwa kiongozi wa chama cha “kuikomboa Kongo” kutoka utawala wa dikteta Mobutu Sese Seko, kwa upande mmoja; na wapiganaji wa Kinyarwanda kutoka Rwanda na Mashariki mwa Kongo.
Makubaliano ambayo yalifanyika kwenye vilima vya Lemera vilivyoko Kivu ya Kusini na kujulikana kwa jina hilo, yalitaka Kabila, baada ya kuwa rais wa Kongo, aruhusu mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kuwa makazi ya Wanyarwanda wa kabila la Kitutsi.
Taarifa zilizopo zinaonyesha makubaliano yaliandaliwa mapema mjini Kigali na pale Lemera yalikuwa yanazinduliwa tu. Ilikubaliwa wakati huo kwamba hiyo ndiyo ingekuwa “asante” kwa Rwanda “kwa ukombozi wa Kongo.”
Desire Kabila alikuwa tayari amechoka. Kwa takriban miaka 20 alikuwa akipambana na utawala wa Mobutu Sese Seko. Alikuwa amefikia hatua ya kukata tamaa na kutulia jijini Dar es Salaam.
Mwaka 1996, mjini Kigali, Rwanda kilikuwa kimeundwa kikundi cha wapiganaji waliojiita “wapinzani wa dikiteta Mobutu.” Hawa walikuwa Wakongomani na Wanyarwanda kutoka Rwanda na wengine waliokuwa wakiishi mkoa wa Kivu Kusini, Mashariki mwa Kongo.
Katika kundi hilo alikuwemo Mkongomani, Jenerali Andre Kisasi Ngando; askari mtaalam wa kusomea. Anadaiwa kupata mafunzo nchini Cuba, Ujerumani na Bulgaria. Alikuwa akiongoza Wakongomani wapatao 600 katika kikundi hicho.
Wakati kikundi hicho kinataka kuanza vita, kilitaka kuwa na msemaji. Mungu akupe nini! Hakuna uthibitisho wowote, lakini taarifa zinaeleza kiliomba ushauri wa Mwalimu Julius Nyerere “ambaye aliwapa Laurent Desire Kabila kuwa msemaji wa wapiganaji.”
Mwanzoni mwa vita ya kumg’oa Mobutu kikundi hiki kilijulikana kama cha Wanyamulenge. Dunia nzima ikaambiwa na kuaminishwa kuwa hayo yalikuwa “maasi ya Wanyamulenge.”
Wanyamulenge ni watu wanaodaiwa kutoka kwenye vilima vya Mulenge vilivyoko wilaya ya Uvira katika mkoa wa Kivu Kusini. Makabila ya asili ya hapa ni Wavira na Wafuliro. Wanaojiita Wanyamulenge ni Wanyarwanda wakuja.
Vita vilianza kwa propaganda kuu kwamba serikali ya Mobutu haitambui Wanyamulenge ambao walidai ni raia wa Kongo; inawanyanyasa na inawanyima uraia. Haya yalikuwa madai makubwa sana yaliyovuta hisia kali na huruma kwa wapiganaji.
Wapinzani, chini ya Jenerali Andre Kisasi Ngando, na msemaji mkuu wao Laurent Kabila waliteka, kama mchezo, mji mkuu wa Kivu Kaskazini, Goma. Wakavuka Ziwa Kivu na kuingia Kivu Kusini.
Ilikuwa baada ya kukamata mji wa Bukavu, makao makuu ya Kivu Kusini na sehemu nyingi za mkoa huo, wapiganaji wa Kinyarwanda waliingiza pendekezo la rais ajaye wa Kongo, kutoa Kivu Kaskazini na Kusini kwa Rwanda.
Lakini kabla suala hilo nyeti kupewa uzito unaostahili, wapiganaji wa Kinyarwanda, baada ya kuteka Bukavu, wanadaiwa kuanza kupora mali – magari, vifaa vya nyumbani, dawa katika maduka – hatua ambayo ilielezwa kuwa uhamishaji wa mali za wakazi wa Bukavu na maeneo mengine.
Alikuwa Jenerali Ngando anayeripotiwa kupinga uporaji usiomithilika, jambo ambalo lilimletea uhasama kwa baadhi ya wapiganaji. Kuona hivyo, Laurent Kabila akamwasi Ngando.
Ngando anasemekana kuuawa siku chache baada ya kutofautiana na wapiganaji juu ya uporaji. Inaelezwa kuwa alimiminiwa risasi na kuuawa na mwili wake kuchomwa moto katika mbuga ya wanyama ya Virunga.
Kabila aliulizwa mara nyingi juu ya Ngando. Alikuwa na majibu tofauti. Akiwa bado msituni alisema Jenerali Ngando amekamatwa na majeshi ya serikali na mara ametekwa na wanamgambo wa Mai Mai.
Baadaye Kabila alisema Ngando alijeruhiwa na kupelekwa Ujerumani kwa matibabu. Na wakati akiwa rais, aliwaambia waandishi wa habari mjini Kinshasa kuwa Ngando alikuwa askari kama askari wengine na kwamba alikufa kwenye mapambano.
Ilikuwa baada ya kifo cha Jenerali Ngando ndipo Kabila aliingizwa kwenye makubaliano ya kumega Kongo. Kwanza, kikundi cha wapiganaji kiligeuzwa kuwa chama – AFDL – Alliance de front Democratique pour la Liberation du Congo.
Kabila akapanda cheo na kuwa kiongozi wa chama cha ukombozi wa Kongo kutoka kuwa msemaji tu wa wapiganaji.
Baada ya kuundwa kwa AFDL, jina la Wanyamulenge likatoweka kabisa. Wapiganaji wakaitwa waasi wa Kongo. Taarifa zinasema kabla wapiganaji kutoka Bukavu na kuanza safari iliyomfikisha Kabila madarakani, waliingia katika mkataba ambao ndio umekuja kuitwa “Makubaliano ya Lemera.”
Kuna madai kwamba viongozi wakuu wa wakati huo wa baadhi ya nchi walipata nakala ya makubaliano hayo ya kumega Kongo. Miongoni mwa nchi hizo ni Namibia, Uganda, Burundi, Zambia, Ethiopia, Eritrea, Zimbabwe, Angola, Namibia, Sudan na baadhi ya nchi za Ulaya na Marekani.
Imeelezwa kuwa makubaliano ni pamoja na kufanya mikoa ya Kivu Kaskazini na Kusini kutawaliwa na Wanyarwanda wa Kitutsi kutoka mataifa ya Rwanda, Burundi na Uganda; na kwamba utawala huo ambao ungefanya kazi kwa ushirikiano na serikali ya Kabila, ungetekelezwa kwa awamu tatu katika kipindi cha miaka 10 kuanzia 1998.
Chini ya mpango huo, raia wa Kongo, wakazi wa Kivu Kaskazini wangehamishiwa Kivu Kusini, “taratibu na kwa utulivu huku makazi yao yakichukuliwa” na wavamizi.
Imeelezwa kuwa hatua ya kwanza isingekuwa ngumu kwani Rwanda ingedai kuwa inapambana na wanamgambo wa Kihutu walioitwa Interhamwe ambao itaelezwa kuwa wanatishia amani nchini Rwanda. Hivyo ndivyo imekuwa ikifanya hadi sasa.
Makubaliano yanadaiwa kueleza kuwa kuchukuliwa kwa miji ya Goma na Butembo mkoani Kivu Kaskazini, sharti iwe hatua ya kwanza kwa kuwa hayo ndiyo maeneo yenye upinzani mkubwa. Kufanikiwa kwa awamu ya pili, kungetegemea mafanikio ya awamu ya kwanza, makubaliano yanadaiwa kueleza.
Wafuatiliaji wa mahusiano ya Rwanda na Kongo wanasema ingawa mpango huo ulishindikana kutekelezwa kuanzia mwaka 1998, kuingia kwa majeshi ya Rwanda nchini humo hivi sasa, ni utekelezaji wa hatua ya kwanza ya Makubaliano ya Lemera; na tayari miji ya Goma na Butembo iko chini ya kile kinachoitwa “majeshi ya ushirikiano” ya Rwanda na Kongo.
Kwa mujibu wa masimulizi juu ya makubaliano hayo, awamu ya pili ingekuwa kujaza wakazi wa Kaskazini katika Kivu Kusini na kufanya uchaguzi wa serikali za mitaa ambapo wazawa wangeenguliwa, kukosa uongozi na hivyo kunyimwa sauti.
Hatua nyingine ilikuwa kuanzisha benki ya kusaidia wavamizi katika Kivu mbili, kujenga nyumba zipatazo 600,000 na kujiimarisha katika nchi ya kigeni – Kongo.
Imeelezwa kuwa Kabila alikubaliana na masharti ya makubaliano kwa kuwa lengo lake lilikuwa moja tu: Kuingia ikulu ya Kinshasa kwa msaada wowote kutoka kwa yeyote; Mungu au shetani.
Ilikuwa baada ya makubaliano hayo, Kabila alisonga mbele na hatimaye kushinda na kuingia ikulu ya Kinshasa akiwa na wapiganaji wa Rwanda, akiwemo mkuu wa sasa wa majeshi wa Rwanda, James Kabarebe.
Baada ya kuingia ikulu, Kabila anadaiwa kuwageuka wenzake. Ilikuwa baada ya miaka miwili ya urais, alitangaza, tena kwa jeuri, kuwa wageni wote waondoke nchini. Aliongeza kwa kufafanua, kwamba Wanyarwanda warudi kwao na kusema anawashukuru kwa kazi waliyofanya.
Kabila alikuwa tayari amesoma mwelekeo wa makubaliano yake na kuona kuwa yanatoa mwanya kwa kile kilichoitwa “Nchi ya Ahadi” ya Watutsi kutoka Rwanda, Burundi, Uganda, Somalia, Ethiopia, Eritrea na Tanzania.
Alitakiwa atangaze, akiwa rais, kuwa Kivu mbili zote ni makazi ya Watutsi; ili hata wananchi wa Kongo watakaobaki humo, wawe wanafahamu kwamba siyo kwao.
Kabila alinukuliwa akisema kuwa hayo (Makubaliano ya Lemera) ni “makubaliano ya porini” na kwamba yeye hakuwa na madaraka ya kuuza nchi. Alisema hakatai kuwepo mkataba, lakini akataka hilo “lipelekwe kwa wananchi – kupitia bungeni – ili wananchi wenyewe waamue.”
Kilichomshangaza zaidi Kabila, baada ya kutangaza kuwa Wanyarwanda warudi kwao, ni kwamba aliyekuwa wa kwanza kuondoka na kukimbilia Afrika Kusini, alikuwa waziri wake wa mambo ya nje aliyeitwa Bizima Karaha (Bizimana Karahamuheto).
Katika mshangao na labda kejeli, Kabila alisema, “Kumbe nchi ilikuwa imevamiwa! Hata waziri wangu wa mambo ya nje alikuwa Mnyarwanda?”
Hiyo ilifuatiwa na kufukuzwa kwa James Kabarebe aliyekuwa mkuu wa majeshi ya Kongo na sasa mkuu wa majeshi ya Rwanda. Hatua hizi na nyingine, ndizo zilisababisha kutotekelezwa kwa Makubaliano ya Lemera.
Lakini wachunguzi na wafuatiliaji wa mahusiano ya nchi hizi mbili wanasema, makubaliano yameandikwa na yapo; hayajafutika. Kilichofanyika ni “ukaidi wa Kabila” wa kutotaka kutimiza ahadi yake baada ya kuingia ikulu.
Kabila anasemekana alikuwa amesoma kitabu cha Raphael Ntibazokiza kikieleza mahusiano ya Watutsi na wabantu, kiitwacho Plan de la colonisation tutsi au Kivu et region centrale de l’Afrique – Mpango wa ukoloni wa Kitusi katika Kivu na eneo la Afrika ya Kati.
Raphael anaandika, “Mhutu ameumbwa kufanyia kazi watu wengine; hawezi hata kujaribu kupata uongozi. Chukua nafasi zote za mikoa na wilaya na atakayekuwa mtawala ahakikishe kuwa analinda maslahi yetu... Baadaye watakapokuja kustuka, watakuwa wamechelewa…”
Mmoja wa waliokuwa karibu na Laurent Kabila amenukuliwa akisema hakuna kitu kilichomsononesha Kabila kama kauli ifuatayo ndani ya kitabu cha Raphael:
“Tutumie ukarimu wao. Tujinyenyekeze kwao kama sisi ni watumishi wao.
Tukiishachukua nafasi zao tuwatelekeze na ‘kuwalipa ujira wa nyani’- payez-les en monnaie de singe pour montrer leur incapacite – ili kudhihirisha kuwa hawana uwezo.”
Kabila aliuawa kabla hajamaliza kunyukana na Rwanda. Aliuawa na mmoja wa “watoto” wake – vijana wadogo waliokuwa watu wa karibu sana na waliomlinda tangu akiwa msituni.
Kuna maelezo tatanishi juu ya kifo chake. Kuna wanaodai aliyemuua alitumwa na waliokuwa wakitaka atekeleze makubaliano ya Lemera; lakini wengine wanadai ni karata za nchi za Magharibi.
Kwa kuwa Jonas Savimbi aliuawa katika wiki moja tu baada ya kifo cha Kabila, inadaiwa kulikuwa na mkono wa mataifa makubwa; hili likitaka kuingia Kongo na hivyo kuomba msaada wa kuondoshwa kwa Kabila huku likiwezesha kukamatwa na kuuawa kwa Savimbi. Siasa hizi hazijafafanuliwa.
Kuingia kwa Joseph Kabila, anayedaiwa kuwa mtoto wa kufikia wa Laurent Kabila, kunaonekana kuleta mgeuko mwingine kuelekea kule ambako “baba” yake alikataa.
Kinachoitwa makubaliano kati ya serikali ya Rwanda na ile ya Kongo kinaonekana wazi kuwa utekelezaji wa mpango wa awali ambao Laurent Kabila alikataa.
Aidha, kukamatwa kwa Jenerali Laurent Nkundabatware na kuhifadhiwa nchini Rwanda kunaelezwa kuwa sura kamili ya “kuheshimu kazi ya maandalizi aliyokuwa akifanya nchini Kongo.”
Kuna madai kuwa Nkundabatware, Mnyarwanda kutoka Rwanda, lakini Rwanda inasema ni Mkongomani, hakuwa na jeshi lolote nchini Kongo. Aliongoza majeshi ya Rwanda hadi hapo ilipoonekana kuwa mazingira yamekuwa mazuri kwa Rwanda kuingilia kwa kisingizio cha “kufukuza Interhamwe na kuweka usalama mpakani.”
“Hata akipelekwa Kongo leo hii, Kabila atamlinda Jenerali Nkundabatware, labda kama wakuu wa Kongo na Rwanda watakuwa wamegundua kuwa amewasaliti,” kimeeleza chanzo cha habari hizi mjini Goma.
Rwanda imeingia Kongo. Nani ataiondoa? Baadhi ya nchi jirani zimekuwa watazamaji tu wakati nyingine zikiwa katika maandalizi ya kunufaika kutokana na mgogoro wa nchi hii.
Moses Byaruhanga, waziri katika ofisi ya rais (Siasa) nchini Uganda, amesema nchi yake inaunga mkono “shirikisho la Kivu na Kisangani” na kwamba wanasubiri kuona serikali ya Kinshasa inalionaje suala hilo.
Katika siku za karibuni kumekuwa na taarifa za kukamilisha kumegwa kwa mikoa miwili ya Kivu Kaskazini na Kusini kutoka Jamhuri ya Kongo na kuzifanya muungano wa Jamhuri ya Kivu.
Kauli ya msemaji wa ikulu Uganda inaongeza uwezekano wa kuimega Kongo pale inapohusisha jimbo jingine la Kisangani ambako majeshi ya Uganda yanadai kuwinda waasi wa Lord’s Resistance Army (LRA).
Kiongozi wa LRA, Joseph Kony amekuwa akipambana na majeshi ya serikali ya Yoweri Museveni kwa zaidi ya miaka 15. Uganda sasa inadai kuwa Kongo inatumika kama kichaka cha waasi hao.
Kauli ya Uganda haipishani na mipango inayodaiwa kufanywa na Rwanda ingawa Rwanda, kupitia balozi wake mjini Dar es Salaam ilikaririwa ikisema haina mpango wowote wa kuigawa Kongo.
Jumuiya ya kimataifa imetekwa kwa propaganda za Interhamwe, Wanyamulenge, waasi wa LRA na kumbukumbu za mauaji ya kimbari.
Isipokuwa Barrack Obama ambaye angalau amesema anataka Kongo tulivu na kwamba atasaidia kuleta hilo, mataifa mengine, pamoja na Ufaransa, yanataka kuimega Kongo.
Vielelezo:
Moabi KKK/BKK
Yunani
Wikipedia
Tutsi
Hutu
Twa
Paul Kagame
Laurant Kabila
Yoweri Mseveni
MwanaHalisi
Mimi Mwenyewe

Leo ni kama vita hapa Uingereza, lakini sio vita inayohusisha majeshi bali timu za taifa za England dhidi ya Scotland, na Wales dhidi ya Jamhuri ya Ireland
Vita kubwa zaidi leo ni mpambano 'wa kisasi' kati ya England na Scotland katika Uwanja wa Wimbley. Kwa hakika nchi hizi zina uhasama mkubwa kisoka japo kama tunavyofahamu wengi, England ipo katika sayari nyingine katika anga za soka la kimataifa. Pengine tatizo kubwa la soka la Scotland ni ukweli kwamba kwa miaka mingi ligi kuu ya hapa imekuwa kati ya timu pinzani kupindukia, Celtic na Rangers zote za hapa Glasgow.
Jana kulikuwa na pambano la utangulizi kati ya Timu za Taifa za England na Scotland kwa wachezaji wenye umri wa chini ya miaka 21, na kama matokeo ya mechi hiyo yanatabiri chochote, basi Scotland leo ina kazi kubwa.Hadi mechi inamalizika, matokeo yalikuwa England 6 Scotland 0

13 Aug 2013
13.8.13
Evarist Chahali
SPORAH NJAU
No comments
HAPPY NEWS...!
NOW YOU CAN WATCH THE SPORAH SHOW TWO DAYS
A WEEK IN UK ON SKY 232..!
TUESDAYS 3:00PM ON Klear TV SKY 232 &
THURSDAYS 10:30PM ON Klear TV SKY 232
.
Very Exciting SHOWS, GUESTS and of course the HOT
CORNER. Stay Tuned Tomorrow TUESDAY 3:00pm ON
SKY 232 and THURSDAY 10:30pm on SKY 232.
DON'T MISS OUT
More On www.sporah.com
Subscribe to:
Comments (Atom)






























































