22 Feb 2011


Kuna taarifa kwamba mtu aliyetambulishwa kama mmiliki wa kampuni ya Dowans, Brigedia Jenerali (Mstaafu) Sulaiman Mohammed Yahya Al Adawi ni kiini macho.

Chanzo cha kuaminika kinaeleza kuwa tukio zima la "mmiliki wa Dowans kuzungumza na baadhi ya wahariri wa vyombo vya habari" ni sehemu tu ya mkakati mahsusi na endelevu kuughilibu umma wa Watanzania katika sakata la malipo ya fidia kwa kampuni hiyo.

Kwa mujibu wa vyanzo hivyo,sababu iliyopelekea "Bilionea huyo wa Dowans" kukataa kupigwa picha mgando wala kurekodiwa na kamera za televisheni ni hofu kuwa "danganya toto" hiyo ingebainika kirahisi pindi Watanzania wangekwenda mbali zaidi kuchimba undani na ukweli.

Lakini hata katika mazingira ya kawaida tu,haiyumkiniki mfanyabiashara anayejitambulisha kuwa amewekeza zaidi ya dola bilioni moja (USD 1,000,000,000,000) nchini India akwepe kupigwa picha kwa madai dhaifu kuwa anaendesha biashara zake kwa "low profile".

Na kama hiyo haitoshi,itakumbukwa kuwa Waziri wa Nishati William Ngeleja aliwahi kutangaza wamiliki wa kampuni ya Dowans (ambao bosi wa Ngeleja,Rasi Jakaya Kikwete,alidai hawajui) ni Brigedia Jenerali Sulaiman Mohamed Yahya Al Adawi ambaye ni raia wa Oman, Guy Arthur Picard raia wa Canada, Stanley Munai raia wa Kenya. Wengine ni Andrew James Tice raia wa Canada, Gopala Krishnan Balachandran kutoka India na Hon Sun Woo kutoka Singapore.Lakini katika mkutano wake na wahariri hao,'Bilionea huyo wa Dowans' alidai kuwa yeye pekee ndio mmiliki wa kampuni hiyo.


Na kama hiyo haitoshi, 'Bilionea huyo wa Dowans' alishawahi "kuruka kimanga" huko nyuma akidai yeye si mmiliki wa kampuni hiyo LAKINI SASA ANADAI SI TU MMILIKI BALI MMILIKI PEKEE.Hizi ni dalili za wazi za ubabaishaji wa "Bilionea" huyu! (And shame on you gazeti la Tanzania Daima kwa habari iliyoonyesha bayana mnalamba miguu ya mtu huyu ambaye laiti ikibainika ni yeye basi mahala panapomfaa ni Segerea kama sio Keko au Ukonga).

Tovuti hii inaendelea na uchunguzi wa kina kuhusu suala hilo na inaahidi kuwafahamisha maendeleo (ya uchunguzi huo).Kwa wakati huu,tunatoa wito kwa waandishi wetu wa habari kuacha uzembe wa kuripoti kinachotamkwa tu badala ya kwenda mbali zaidi na kufukua data mbalimbali.Kadhalika,wahariri walioalikwa na Brigedia huyo walipaswa kuwa na msimamo wa kuhoji kwanini hataki picha zake zionekane kwenye vyombo vya habari.

2 comments:

  1. Hivi swala hili linachukuliwa siriasi kweli na viongozi wetu?:-(

    ReplyDelete
  2. Mtu huyu amekuta angalao na waziri wa nishati kweli? Maana habari zilizopo ni hizi za kuongea na waandishi wa habari na kutembelea mitambo ya dowans tu! Kama hili nalo halijafanyika, basi "ukiini macho" unazidi kujidhihirisha

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.