10 Aug 2007


Further Updates: "Majibu" ya Mrisho na Tulizo Kilaga.USIKOSE KUSOMA COMMENTS MBALIMBALI MWISHO WA MAKALA HII NA KWENYE BLOGU YA MRISHO

Latest Updates: Baada ya "washtaki" kuwa judge,jury and prosecutor,hatimaye mtuhumiwa apewa nafasi ya kujieleza

Updates: Mashambulizi yaendelea

Updates: Kaazi kweli kweli

Mtanzania huyu kumponza Mengi

Ni mropokaji, anayeandika bila kufanya utafiti
Na Mwandishi Wetu
Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Aberdeen, Scotland, Evarist Chahali huenda akamponza Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, ambaye pia ni mmiliki wa gazeti la Kulikoni, kufuatia habari potofu aliyoiandika kwenye gazeti hilo dhidi ya gazeti la Risasi.

Kwa mujibu wa habari hiyo, mwandishi huyo ambaye ni Mtanzania anayedai kuchukua kozi ya Udaktari wa Falsafa (PhD) katika chuo hicho, aliandika makala ya kuyashutumu magazeti ya Udaku kuwa yanaandika habari feki na kutolea mfano gazeti la Risasi.

Katika makala yake ya Jumatano Agosti 8, mwaka huu, Chahali alidai kuwa habari zilizoandikwa kwenye gazeti la Risasi ambalo ni dada la hili, zilizoambatana na picha hazikuwa na ukweli wowote.

Chahali alitolea mfano wa habari iliyochapwa kwenye gazeti hilo la Julai 18-20 iliyokuwa na kichwa cha habari 'Warembo wa TZ wapiga picha za X tupu'.

Habari hizo ambazo chanzo chake ni mtandao, zilieleza kuwa wasichana hao ni Watanzania waliopiga picha wakiwa watupu kwa nia ya kutangaza biashara ya kuuza miili ambapo waliweka bayana mawasiliano yao.

Hata hivyo, Chahali alidai kuwa habari hiyo ni ya uongo (feki), kwani picha zilizotumika ni za nyota wa sinema za ngono (porn star) wa Marekani na si Watanzania.

Mwandishi huyo alieleza katika makala yake hiyo kuwa, aliamua kuandika hivyo baada ya kuambiwa na rafiki yake anayeishi Marekani.

Akiongea na gazeti hili, Meneja Mkuu wa Kampuni inayochapa gazeti hilo, Abdallah Mrisho, alisema kuwa amesikitishwa na makala ya gazeti la Kulikoni ambayo haikufanyiwa utafiti wa kutosha.

"Habari iliyoandikwa na gazeti la Risasi ni ya kweli, hatujawahi kuandika wala haturuhusu wahariri wetu kuandika habari za uongo ndani ya magazeti yetu, ila Chahali ameropoka.

"Kimsingi mwandishi wa makala hayo, (Chahali) ameonyesha udhaifu mkubwa kwa kuandika habari bila kufanya utafiti na kufikia uamuzi wa kushambulia gazeti letu bila kuwa na uhakika na alichokiandika", alisema Mrisho.

Mrisho aliendelea kusema ana wasiwasi hata na shahada alizonazo Chahali, kwani mtu mwenye elimu kama yake hawezi kuandika habari za kuambiwa bila kufanyia utafiti, hivyo kuupotosha umma na anaweza kumponza mmiliki wa kampuni inayochapisha gazeti hilo, ambaye anaheshimika sana.

"Chahali hakupaswa kutoa shutuma nzito kama zile kwa maneno ambayo hakuyafanyia uchunguzi na kuchapa kwenye gazeti, kwani anaweza kumponza mmiliki wa kampuni hiyo tunayemuheshimu, anapaswa kuona aibu (shame on him)," alisema Mrisho.

Kuthibitisha kuwa habari iliyoandikwa ni ya kweli, wahariri wa gazeti la Risasi wamelazimika kutaja anuani ya tovuti ambako wasichana hao wanapatikana, ili umma kwa ujumla uelewe nani mkweli kati ya Chahali na gazeti la Risasi, ingawa haikuwa kusudio lao kufanya hivyo.

Anuani hiyo ni http://swallowmyjuice.hi5.com ambako picha zilizotumika, mahali wanakoishi na utambulisho wa wasichana hao vinapatikana.

Aidha, kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari cha kuaminika kilichoko ndani ya chuo cha Aberdeen, Chahali ni miongoni mwa wanafunzi wasiofanya vizuri sana katika masomo yao.

"Chahali sio miongoni mwa wanafunzi wanaofanya vizuri sana chuoni," kilisema chanzo hicho.

Baadhi ya wanafunzi wanaosoma kozi moja na Chahali katika chuo hicho ni pamoja na Timofei Agarin, Gordon G. Davidson, Joyleve Elliat, Anna Gustavon, Jeremy Lamoreaux, Giseong lee, Yang Lia, Khristus Vassis, Lortraine Whitty na Anna Zawak.

Mrisho alimtahadharisha mhariri wa gazeti hilo kuwa asipokuwa makini na waandishi wanaoandika makala zao kwa chuki binafsi kama Chahali, wanaweza kujikuta kwenye matatizo makubwa.

Akiongea na mwandishi wetu kwa simu juzi, Mhariri Mtendaji wa magazeti ya This Day na Kulikoni, Evarist Mwitumba alisema kuwa hana habari kuhusu makala hayo.

"Nipigieni kesho asubuhi, kwa sasa niko barabarani naendesha gari na sijasoma gazeti lililoandika habari hiyo," alisema Mwitumba.


HAYA NI MAONI YA WATU MBALIMBALI KATIKA BLOGU YA IJUMAA/RISASI http://abdallahmrisho.blogspot.com KUHUSU MASHAMBULIZI DHIDI YANGU


mkandamizaji said...
Mrisho

Mimi sio mtaalam wa masuala ya mtandao, lakini hakuna mtandao ambao unavurugwa sana na watumiaji kama hi5.com. Kama hichi ndo chanzo chako pekee cha hiyo habari, nasikitika kuwa nitakuwa upande wa chahali kukusuta kuwa picha zile ni za Wamarekani na kuwa nyie mmedanganya watanzania.

Tupe mitandao yenye URL zinazoeleweka sio hi5.com. Mtu anaweza kuweka picha ya mtu yeyote kwenye hi5.com. Na kama nakumbuka kuhusu maelezo ya ile habari, ulisema kuwa kuna namba za simu, eno wanakopatikana hao wadada na mambo kama hayo. Lakini kwa hi5.com ambayo ni mtandao wa marafiki tu, bado hajani conivnce kuwa ulikuwa na source nzuri ya habari.

Najua unaweza kuamua kutotundika hii comment, lakini ujumbe utakuwa umeupata.

Asante

August 9,:53 PM
================================================================
Anonymous said...
Nyote mnahitaji kuwa makini.Mbona hakuna cha ajabu katika hizo picha mnazozizungumzia?Bikini ni nguo za kawaida tu jamani..tuache ushamba na ushambenga watanzania.

August 10, 2007 1:02 AM
===================================================================
kichuguu said...
Nimeangalia picha zile pale Hi5, nina wasiwasi kuwa naweza kukubaliana na chahali kuwa wale ni pornstar wa kimarekani. mambo matatu yanawezekana:

(a)wasichana wa kitanzania wametumia picha za mastar hao.

(b) mastar wameamua kudanganya kuwa wako Tanzania.

(c) mastar hao ni watanzania.

Picha hizo hazikupigwa katika mazingira ya Tanzania. Baadaye nitakutafutia picha nyingine za yule anayejiita Melanie ndipo utakapogundua kuwa siyo za kutoka mazingira ya Tanzania.

August 10, 2007 6:40 AM
===================================================================
mzalendo said...
tumesikitishwa sana kuona vyanzo vyetu vya habari havina uhakika na habari zao. hiyo website iliyotolewa na gazeti la ijumaa inaonyesha moja kwa moja kuwa hao watu mmoja ni MGANDA na wote ni GAYS/ LESBIANS!
mbili ni kuwa hamkuhakikisha kama hizo picha ni za hao MNAOWAITA WAREMBO wa KIBONGO na MMEWASILIANA NAO. Mnauhakika gani kama ni picha za wabongo???? mpaka mkaamua kuandika gazetini?? ....au ndo mnafanya chochote kuuuza magazeti yenu?

August 10, 2007 7:59 AM
===================================================================
Anonymous said...
website mliyotupatia inahakikisha kuwa muandishi wa RISASI hana uhakika na alichokisema, kwa vile website hiyo inaonyesha kuwa wale ni GAYS/LESBIANS na pia HAILAZIMISHI kuwa zile picha ni za hao walioziweka na wala hamkutupa ushahidi kuwa mlihakikisha hao mlowapigia simu ndio wenye picha zile.

August 10, 2007 8:02 AM
====================================================================
Anonymous said...
na kwa vile hakuna uhuru wa kujielezea , na jua nilichokiandika hutokipublish

August 10, 2007 8:04 AM
===================================================================
Anonymous said...
nyote hapo juu nahisi mnamiss point, chahali aliamua kuwakandia wenzake bila kujua kama zile picha kweli zipo na wahusika wamejitambulisha kama wabongo, hivyo ishu sio kama ni wabongo au sio wabongo, ila ishu iliyopo hapa ni kwamba kwa nini Chahali amewakandia jamaa wa risasi na kudai wanaandika habari feki? kwa nini, wakati vitiu hivyo vipo? kama jamaa angefanya utafiti kidogo, angekuwa na ishu tofauti ya kuwabana.. hapa nawaunga mkono jamaa wa risasi..

August 10,:27 AM
===================================================================
Anonymous said...
Mimi naungana na Chalali kuwa magazeti hayo mara nyingi wanaandika habari za uongo ili watu wanunu e magazeti, utakuta mtu anaandika eti kapigiwa simu na mtu wanaandika habari kwenye gazeti je hii ni sawa??? unatunia uongo kupata pesa za watu???? I think tuungane watanzania tuanzishe kampeni za kutonunu magazeti ya udaku!!! Hongera chalali, najua unaweza usitoe hii lakini msg will be sent

August 10, 2007 1:10 PM
===================================================================
Anonymous said...
kwanza hii habari mbona imepindishwapindishwa jamani, kichwa cha habari cha muhusu Mengi, Ndani ya habari main content gazeti la Risasi.Mambo tofauti tofauti.

Simtetei Chalali...ila swala la kutofanya vizuri darasani linawahusu nini hasa, au linahusika vipi na habari yenyewe?...Huo ni mpindisho tosha na ni kupakana matope. Hatuelewi huyu jamaa anasoma katika mazingira gani, isitoshe level anayosoma Phd. haijadiliwi tena kama anafanya vizuri au vibaya darasani. Watanzania tuangalie cha kuandika.
Last point, magazeti ya udaku yapo hata Ulaya, ila cha muhimu ni kuandika mambo ambayo kweli yapo, au yametokea, si kubahatisha ili kuuzisha gazeti.

August 10, 2007 1:19 PM
===================================================================
mkereketwa said...
kama hiyo website ya porn iliyowekwa , chahali alikuwa na haki ya kupinga maelezo ya RISASI kwa vile hao watu hawapo TZ bali wanafanya kazi ya porn Marekani.
tusingefurahi kudanganywa na magazeti kwa kutofuatilia vyanzo vyao vya habari kikamilifu.
kosa la RISASI ni kutokufuatilia kikamilifu hao waliotowa namba zao na wapi wanapatikana kama ni sawa na hao walioweka picha za uchi kwenye Hi5. ushahidi mkubwa unaonyesha kuwa walitumia picha za hao watu tu kujipa umaarufu na kinachoshangaza ni kuona RISASI haikusema kuwa haikutuambia kuwa kuna uwezekano kuwa zile picha si zao.

August 10, 2007 2:45 PM


PIA NIMEONA MAONI HAYA HUKO JAMBO FORUMS

Vyanzo vya Habari vya Magezeti Mengine
Mimi ni msomaji sana wa blogu ya Abdallah Mirosho ya http://www.abdallahmrisho.blogspot.com. Blogu hii hunipatia udaku safi sana kutoka mitaa mbali mbali ya Dar es Salaam. Habari niliyonukuu hapa ilinishtua sana kwamba badala ya wao kukubali kuwa magaxeti yao ni ya udaku, wakaamua kumtukna mwandishi aliyewasema kuwa habari waluyokuwa wameandika haikuwa sahihi.

Quote:

Mtanzania huyu kumponza Mengi

Ni mropokaji, anayeandika bila kufanya utafiti

Na Mwandishi Wetu

Mwanafunzi wa Chuo Kikuu cha Aberdeen, Scotland, Evarist Chahali huenda akamponza Mwenyekiti wa Makampuni ya IPP, Reginald Mengi, ambaye pia ni mmiliki wa gazeti la Kulikoni, kufuatia habari potofu aliyoiandika kwenye gazeti hilo dhidi ya gazeti la Risasi......Kwa mujibu wa habari hiyo, mwandishi huyo ambaye ni Mtanzania anayedai kuchukua kozi ya Udaktari wa Falsafa (PhD) katika chuo hicho, aliandika makala ya kuyashutumu magazeti ya Udaku kuwa yanaandika habari feki na kutolea mfano gazeti la Risasi.Katika makala yake ya Jumatano Agosti 8, mwaka huu, Chahali alidai kuwa habari zilizoandikwa kwenye gazeti la Risasi ambalo ni dada la hili, zilizoambatana na picha hazikuwa na ukweli wowote......Chahali alitolea mfano wa habari iliyochapwa kwenye gazeti hilo la Julai 18-20 iliyokuwa na kichwa cha habari 'Warembo wa TZ wapiga picha za X tupu'.....Hata hivyo, Chahali alidai kuwa habari hiyo ni ya uongo (feki), kwani picha zilizotumika ni za nyota wa sinema za ngono (porn star) wa Marekani na si Watanzania................Kuthibitisha kuwa habari iliyoandikwa ni ya kweli, wahariri wa gazeti la Risasi wamelazimika kutaja anuani ya tovuti ambako wasichana hao wanapatikana, ili umma kwa ujumla uelewe nani mkweli kati ya Chahali na gazeti la Risasi, ingawa haikuwa kusudio lao kufanya hivyo.Anuani hiyo ni http://swallowmyjuice.hi5.com ambako picha zilizotumika, mahali wanakoishi na utambulisho wa wasichana hao vinapatikana....Aidha, kwa mujibu wa chanzo chetu cha habari cha kuaminika kilichoko ndani ya chuo cha Aberdeen, Chahali ni miongoni mwa wanafunzi wasiofanya vizuri sana katika masomo yao...."

Nilipoangalia picha zilizosemekana za watanzania pale http://swallowmyjuice.hi5.com, nilikuta mwanadada mmja anayejiita Melanie ambaye kwa bahati mbaya ninadhani namfahamau vizuri na picha hiyo imepigwa zaidi ya miaka saba iliyopita. Mwanadada yule alikuwa mmoja wa ma-hooker wazuri sana pale South Beach Miami na nadhani kuwa alikuwa damu mchanganyiko mwasia na mwafrika. Nimeweza kupata baadhi ya picha zake nyingine kwenye websites chafu kama hii hapa. (ONYO: PICHA HIZO NI CHAFU SANA USIZIFUNGUE MBELE YA WATOTO NA WATU WA HESHIMA.)


Swali, je mwandishi wa Risasi kweli alifanya haki kumtolea matusi ya kashfa mwandishi wa Kulikoni kuhusu uhalali wa picha zile kama kweli zilikuwa za akina dada wa kitanzania?
__________________
Kichuguuu: Nyumba inayohifadhi mchwa na nguchiro kwa pamoja bila mkwaruzo

6 comments:

 1. ukweli bado ni kitendawili!mi naona bora chahali awasiliane na huyo mtu aliyempa hizp habari kwamba ni wacheza porn wa marekani,ili yeye(chahali)aweke hadharani hiyo website huenda ukweli ukaeleweka..e

  ReplyDelete
 2. Kwa vile naamini kuwa blog hii inatembelewa na watu wa rika tofauti wenye heshima zao,nachelea kwa kiasi flani kuweka picha hizo hapa.nachoweza kufanya ni kutoa links zitakazomwezesha mwenye kiu ya kulinganisha picha zilizo kwenye habari ya RISASI na hizo za mtandaoni

  http://www.doctorassmaster.com/rb/66/?id=keezah1
  http://www.doctorassmaster.com/rb/69/?id=keezah1

  http://www.doctorassmaster.com/rb/153/?id=keezah1

  Hizo links mbili za mwanzo ni mbili kati ya picha tatu zilizodaiwa kuwa ni za Watanzania.Picha ya tatu iko Hi5 katika page inayodaiwa kuwa ni ya Mtanzania (katika "ushahidi" uliotolewa kwenye gazeti la Ijumaa).

  Hivi vitu vinakera machoni mwa wengi na nalazimika kuweka links hizi kwa vile tu nataka kuthibitisha kuwa picha zilizotumiwa kwenye stori ya gazeti la RISASI zilikuwa si za Watanzania bali porn stars walio Marekani.Kama kuna mtu ana kiu zaidi ya kuni-prove right or wrong,nashauri kufanya search hiyo kwenye mtandao na nina hakika ya asilimia 101 atakubaliana nami.

  ReplyDelete
 3. safi sana bwana chahali bg up sana tu..nilikuwa nafuatilia kwa kina habari za bro mrisho,naona bado anatapatapa,eti anadai kwamba kama wewe(chahali) una source kuhusu hiyo web kwanini hujaiweka hadharani..sasa mi nishamwambia kwamba kwenye blog yake kwamba source tayari chahali kaiweka,kazi kwake bro mrisho..(nyingine ni hii. www.wannawatch.com) naona kichuguu kaiweka pia,kazi kwake mrisho,chahali unaweza usihitaji sana ila nimemuomba bro mrisho aombe radhi kwako na kwa umma kwa ujumla kwa kitendo chake cha kulisha watanzania 'matango pori';na ajue wazi kwa kufanya hivyo 'moto utawaka' siku hiyo...e

  ReplyDelete
 4. mi nasubiri mwisho wake tu utakuwaje,manake naona bro mrisho kawa mpole kwa kudai kuwa kuna sehemu flani tu ndio iliyowakera wakati alikutupia matusi lukuki kuhus habari yako nzima ya "feki ya risasi' sasa nawasubiri watajitetea vp hao wakina mrisho..

  ReplyDelete
 5. Hivi hauna wanasheria mkuu, naona jamaa wanataka Law suit ndo wakubali. Wameshindwa kutuletea URL ya picha hizo. Mana kwenye URL ile tutaweza kujua kweli kuna Amina, Janie na Candy na namba zao za simu kama walivyoandika kwenye habari yao ya kwanza. Anachoendeleza Mrisho ni ubishi wa kitoto na kijinga sana. Kwanza kuanza kusema kuwa kwa mujibu wa habari zao, wewe unafanya vibaya sana kwenye masomo, ni dharau ya ajabu kwa mtu anaowakosoa wao.

  Mimi nimeudhika sana hasa baada ya kutoa URL ya hi5 eti ndo chanzo chao cha habari, what a shame. Shame on Mrisho, shame on Global Publishers and shame to everyone working with him. Ndo maana mie sikutilia maanani habari ile, ila alipokuja na URL ya hi5, ndo akili yangu ikaklick. Shame to them, shame shame shame to journalist, shame to Tanzania.

  ReplyDelete
 6. Mzee Abdallah Mrisho na Mhariri wa Risasi, heshima zenu kwa mpigo!

  Jamani, hoja hujibiwa kwa hoja. Hakuna mahala popote katika maelezo yako na maelezo ya uongozi wa gazeti la Risasi ambapo kumejengwa hoja inayo dhoofisha hoja kuu ya Chahali ya kuwa habari mliyoitoa kwenye gazeti lenu haikuwa saihi. Badala yake mmeanza kujenga hoja uchwara zisizo na mantiki za kumshambulia mjenga hoja badala ya kushambulia hoja yenyewe. Eti “makala hiyo, kama uongozi, tuliiona ilikuwa na nia ya kulichafua jina la kampuni”. Kampuni haichafuliwi jina bali hujichafulia yenyewe.

  Kilichoonekana kuchafua jina la kampuni yenu sio mwandishi wa makala bali ni ukweli ndani ya ile makala. Alafu Mhariri anatuhubiria mambo ya “Elimu humsaidia mwanadamu kupanua uwezo wa kufanya maamuzi sahihi”. Sasa hiyo elimu mbona haikuusaidia uongozi wa gazeti la Risasi wakati wa kumjibu Chahali? Au Mhariri sio sehemu ya Uongozi? Si wanasema kuwa usibishane na mpumbafu kwani watu wanaweza wasione tofauti? Mbona mmetumia njia ile ile ya kebehi na dharau kumshushua Chahali? What kind of “elimu” do you ascribe to? Au ni yale ya kuazima busara za Kasisi za kututaka tuzingatie mahubiri yake lakini tusiangalie matendo yake? (Yeah right!)

  Mhariri wa Risasi anamtuhumu Chahali kwa “kujenga hoja kwa misingi ya dharau na kebehi huku ukionesha kutokuwa tayari kufungua milango ya taarifa kuingia kwenye ubongo wake”. Hakuna dharau na kebehi kubwa kama kuwalisha wasomaji habari za uongo au za kutunga. Hii inaweza kufanyika kwa makusudi au kwa bahati mbaya. Lakini ikigundulika kwa njia zozote zile kuwa habari iliyochapishwa haikuwa ya ukweli, basi kosa inabidi lisaihishwe haraka sana na wasomaji waombwe radhi bila kujali njia gani ilitumika kugundua huo ukweli. Je mhariri amefungua milango ya taarifa kuingia kwenye ubongo wake? Au bado hajagundua kuwa habari iliyochapishwa ilikuwa ni ya uongo?

  Umeandika kwamba “tunaheshimika vya kutosha na wanaotuchukia ni wale wasiopenda mabaya na uovu wao kuwekwa hadharani.” Hii ni dhana ya Mkuki kwa Nguruwe lakini kwa binadamu ni mchungu. Kwa maneno yako, uongozi wa Gazeti la Risasi unaona ni jambo la heshima kuanika maovu ya wengine hadharani, lakini Chahali alipoanika nguo zenu chafu juani ili mzifue, badala yake mnamshambulia. Yaani ninyi mnaona raha kukodolea macho vikalio vya wengine lakini mnavionea nongwa vikalio vya kila mmoja wenu ndani ya uongozi wa gazeti la Risasi. Ama kweli Nyani haoni kundule. Heshima gani unayoiongelea inayopatikana kwa kuondoa boriti ndani ya macho ya wengine wakati mnaleta hoja zisizo na vichwa wala miguu zenye tafsiri ya kuficha vibanzi ndani ya macho ya uongozi wa gazeti la Risasi?

  Umeandika kwamba ulilazimika kuwa “delete” wachangiaji wengine kwa kuandika matusi badala ya hoja. Pamoja na maendeleo ya sayansi na teknolojia, sioni haja ya kupiga teke mila na desturi zetu. Wanasema ukienda Roma fanya kama waroma wafanyavyo, lakini tusisahau ukweli kuwa Waroma wakija kwetu wanatakiwa kufanya kama sisi tufanyavyo. Kama tumeamua kuuzika utamadunu wetu na kuanza kutukuza ule wa Roma, sijuhi tunaiandaa jamii ya aina gani? Kumbuka hatuwezi kuwa Waroma hata siku moja. Mtanzania atakuwa Mtanzania tu.

  Matusi yamekuwepo toka enzi za kale, lakini tulijitahidi kujenga jamii iliyostaharabika isiyo na matusi. Mfano Marekani Baba anamwambia mtoto wake “bring your ass here”, lakini Tanzania tuliyoridhi kutoka kwa wazazi wetu husingesikia maneno kama hayo kutoka kwa mzazi wako. Malezi bora yalianzia kwenye familia mpaka ngazi ya taifa. Watu waliadhibiwa kwa kuwatukana wenzao. Mantiki hii ilieleweka kwenye vyombo vya habari vyote. Tulikuwa na magazeti ya burudani kama Sani, lakini matusi na uchafuzi wa lugha havikuvumiliwa. Wahariri walikuwa wabunifu, hivyo magazeti yao yalinunuliwa kwa wingi bila wao kushiriki katika matendo ya kubomoa malezi mema tuliyojijengea.

  Siku hizi mambo yote ambayo yalikuwa yanafanyika jando, yamewekwa hadharani. Mzazi hawezi kukaa sebureni na watoto wake wakiangalia miziki wa kizazi kipya kwenye TV au kusikia maneno redioni. Picha zinazowekwa kwenye baadhi ya magazeti ya kisasa huwezi kuziangalia mbele ya mzazi wako. Zamani hata kutamka neno “matiti” mbele ya kadamnasi ilikuwa haikubaliki. Siku hizi picha zinatolewa kwenye magazeti matiti yakiwa nje nje. Zamani ilikuwa ni matusi kutamka neno lolote la sehemu za siri za mwili wa binadamu. Siku hizi picha za watu wakiwa uchi wa mnyama zinatolewa kwenye magazeti huku sehemu za siri zimewekewa vizibio, lakini ujumbe ni ule ule kwamba huyu mtu yuko uchi.

  Frankly speaking, we are promoting and cerebrating ignorance. Huu sio utamaduni wetu bali ni mambo ya kuiga kutoka nje. Nimewahi kuwandika mahala kuwa nachukia unafiki wa kumpinga shetani kwa kutumia mkono wa kushoto na kumhalalisha kutumia mkono wa kulia. Hivi kuna matusi yanayozidi baadhi ya picha zinazochapishwa na gazeti la Risasi? Ni bora kukubali matokeo ya matendo yetu. Kuna mantiki gani ya kuchapisha picha za matusi wakati huo huo tuna “delete” maandishi ya matusi. We are trying to groom hiki “kizazi kipya” kinachofanana na magazeti yetu, na kinaongea lugha inayofanana na picha tunazo ziweka magazetini. Maandiko yao hayawezi kuwa matusi kwetu kwasababu ndio kioo cha matendo yetu kwao. We have to swallow these pills as bitter as they are.

  Unasema kwamba magazeti ya namna hii yanapendwa na watu. Lakini hii sio hoja ya maana ya kumjibu Chahali. Tafsiri ya hoja ya Chahali iko kwenye ubora wa haya magazeti na sio kama yanapendwa na watu au hapana. Kama suala la kupendwa ni hoja, mbona pamoja na sheria kali zilizopo kote duniani, lakini bado Bangi inapendwa na watu wengi. Kuna tofauti kati ya kupendwa na ubora wa kitu. Hata Madawa ya kulevya yana wateja wengi tu. Nani kasema Bangi au Madawa ya kulevya ni bora?

  Kibaya zaidi, faida ipatikanayo kutoka katika biashara ya Bangi na Madawa ya kulevya inapeleka watu shule, inasaidia vituo vya watoto yatima, inasaidia matibabu ya wagonjwa, inachangia hata pato la taifa-GDP, n.k. Hata wafanya biashara wa haya majinamizi makubwa, wakishapata faida, wanaanzisha biashara mpya na kuajiri vijana wengi tu. Matendo yote yote haya yanafanyika nyuma ya pazia la usamalia wema na kujali utu wa watu katika jamii zetu. Lakini matendo haya yote hayafuti maana nzima ya unyama utokanao na madhara ya Bangi na Madawa ya kulevya kwa binadamu.

  To you Chahali, Heshima yako!

  Kumbuka, not all that glitters is true Gold. A clarion call inherent of close-mindedness is a monster you have encountered in decent search for truth. For sure that is not the way you should have gone, but who knows, truth seekers have cursed tyrants.

  Thanks
  Kyoma
  e-mail: [email protected]

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.