15 Nov 2008

HILI JINAMIZI LA MIGOMO NA KUFUNGA VYUO VIKUU LINAONEKANA KAMA LINATAKA KUSAMBAA KILA MAHALI.ILIANZIA MLIMANI,IKAJA DUCE,IKAJA MKWAWA NA SASA SUA (as extracted from Mwananchi)

Mjini Morogoro, SUA ilitangaza kufunga chuo kwa wanafunzi wote wa shahada ya kwanza kutokana na mgomo uliodumu siku mbili wa kushinikiza serikali iwape mkono kwa asilimia 100.

Taarifa iliyotolewa na mshauri wa wanafunzi wa chuo hicho, Jonas Bisheko iliwataka wanafunzi wote kuondoka maeneo ya chuoni kabla ya saa 9:00 alasiri jana.

Mara baada ya tangazo hilo kutolewa, wanachuo wa chuo hicho walionekana kufungasha mizigo na kuondoka kwa amani kutoka katika mazingira ya chuo hicho.

Wanafunzi walio katika eneo la Solomon Mahlangu Mazimbu walionekana na mizigo yao wakiondoka kuelekea katika maeneo mbalimbali ya mji huku wengine wakielekea kituo cha mabasi.

Awali, kaimu makamu mkuu wa chuo hicho, Profesa Dominic Kambarage alisema kuwa chuo kilitoa muda wa siku tatu wanafunzi kurudi darasani lakini hawakukubali.

Makamu wa rais wa serikali ya wanafunzi wa chuo hicho, SUASA, Yulian Mizola aliwaambia wanafunzi wenzake kwenye mkutano kuwa uongozi wao ulikutana na kaimu makamu mkuu wa chuo, Profesa Kambarage ambaye aliagiza kuwa wanafunzi wote warejee madarasani mara moja kabla ya uamuzi mwingine kuchukuliwa.

Wakati huo huo, Bodi ya Mikopo imesema kuwa ili wanafunzi wote waliodahiliwa waweze kukopeshwa fedha kwa asilimia 100, serikali inatakiwa kutumia Sh160 bilioni kwa mwaka.

Kaimu mkurugenzi wa bodi hiyo, Lubambula Machunda, alisema kuwa idadi ya wanafunzi wanaotakiwa kukopeshwa ni 60,000 na kwamba wanafunzi hao walipatiwa jumla ya Sh140 bilioni, lakini akasema iwapo wanafunzi wote watatakiwa kupata mkopo kwa asilimia 100, basi Sh163 bilioni zitahitajika.0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.