11 Nov 2008


Msanii wa muziki wa kizazi kipya, Khalid Mohamed maarufu kama TID, amekata rufaa katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam kupinga adhabu ya kifungo cha mwaka mmoja jela alichohukumiwa mwaka huu. 

Rufani hiyo ya msanii huyo ambaye tangu ahukumiwe kifungo hicho amekwishatumikia adhabu hiyo kwa miezi minne, itaanza kusikilizwa leo na Jaji Robert Makaramba; kwa mujibu wa habari zilizotolewa na ofisa mmoja wa mahakama hiyo. 

TID alihukumiwa kwenda jela mwaka mmoja kutokana na kutiwa hatiani kwa kosa la kushambulia na kumjeruhi kichwani na mkononi kijana aliyefahamika kwa jina la Ben Mashibe. Msanii huyo alimjeruhi Mashibe kichwani na mkononi kwa kutumia chombo cha kuwekea majivu ya sigara ‘ash tray’ na alisomewa mashtaka hayo mara ya kwanza Julai 10, mwaka huu mbele ya Hakimu Hamisa Kalombola wa Mahakama ya Wilaya ya Kinondoni. 

Mwendesha Mashtaka wa kesi hiyo, Inspekta Nyagabona alidai TID alitenda kosa hilo Julai 2, mwaka jana saa sita na nusu usiku katika Hoteli ya Slipway iliyopo Msasani Dar es Salaam. TID mwenye umri wa miaka 26, alitiwa hatiani na Hakimu Kalombola baada ya hakimu huyo kuridhika na ushahidi uliotolewa na mashahidi wanne walioletwa mahakamani na upande wa mashitaka

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.