SHAHIDI katika kesi ya kuomba na kupokea rushwa ya sh 600,000 inayomkabili Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbelekese, wilayani Iramba, Singida, Iddi Mughenyi, juzi alipata kipigo kutoka kwa mwanasheria wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU) kwenye viwanja vya Mahakama ya Wilaya ya Iramba, kwa madai kuwa alimgeuka katika ushahidi alioutoa mahakamani hapo.
Mtuhumiwa alipata kipigo kutoka kwa mwanasheria huyo aliyetambulika kwa jina moja la Mchumi, kwa madai kwamba alimgeuka katika ushahidi aliuotoa mahakamani hapo.
Tukio hilo la aina yake limedaiwa kutokea muda mfupi baada ya Mughenyi kutoa ushahidi katika kesi namba 14/2009 inayomkabili ofisa mtendaji huyo.
Akizungumza kwa njia za simu kutoka Iramba, mmoja wa watumishi wa mahakama hiyo ambaye hakutaka kutajwa jina, alisema kuwa kuna kila dalili kuwa ushahidi uliotolewa na shahidi huyo haukumridhisha mwanasheria Mchumi, kwa madai kwamba ulikuwa kinyume cha walivyokubaliana.
“Idd Mughenyi ni shahidi wa upande wa TAKUKURU kwenye kesi hiyo ambayo Ofisa Mtendaji wa Kijiji cha Mbelekese anatuhumiwa kuomba na kupokea rushwa, lakini juzi aliposimama kizimbani aliikana taasisi hiyo, kitendo ambacho kinawezekana kilimuudhi mwanasheria huyo ambaye ndiye alikuwa mwendesha mashtaka katika kesi hiyo,” alifafanua mtumishi huyo wa mahakama.
Aidha, mtumishi huyo alisema baada ya kesi hiyo kuahirishwa na kutoka nje ya mahakama, ndipo Mchumi alipomweka chini ya ulinzi shahidi huyo na kumtaka apande kwenye gari ili waende ofisi za TAKUKURU Wilaya ya Iramba.
Alisema kutokana na shahidi huyo kugoma kupanda gari kwa madai ya kutofahamu kosa, ndipo mwanasheria huyo alipoanza kumpiga makofi hadi kumuumiza kwenye jicho la upande wa kushoto na kumchania shati.
Alibainisha tukio hilo lilishuhudiwa na baadhi ya mahakimu, na kuongeza kuwa waliwaamru askari kwenda kuamua ugomvi huo, kisha kuwapeleka kituo cha polisi.

CHANZO: Tanzania Daima
RUSHWA NI RUSHWA,IWE NDOGO AU KUBWA.LAKINI INGEPENDEZA ZAIDI KUONA TAKUKURU IKITUMIA MISULI MINGI KWENYE RUSHWA KUBWA NA UFISADI SAMBAMBA NA HIZO RUSHWA NDOGO.MAPAPA WA KAGODA NA RICHMOND (achana na yule Mdosi aliyepandishwa kizimbani) BADO WANAPETA URAIANI SAMBAMBA NA MAFISADI WA RADA.
0 comments:
Post a Comment