3 Apr 2009


Na Alfred Lucas


MFANYABIASHARA na mbunge wa Igunga, Rostam Aziz amesitisha uchapishaji magazetini wa taarifa yake ya kukana tuhuma za ufisadi.

Taarifa iliyokuwa inakwenda kwa njia ya tangazo, ilikuwa inakana kuhusika kwake na kampuni ya kufua umeme kwa njia ya upepo ya Wind East Africa Limited.

Kampuni hii inatuhumiwa kupora ardhi ya wananchi katika kijiji cha Kisasida, mkoani Singida na taarifa zinasema tayari watu wameanza kuhamishwa kwa nguvu kama inavyofanywa kwenye maeneo yenye migodi ya madini mbalimbali.

Taarifa zinasema uhamishaji watu kwa nguvu unafanywa kwa msaada wa Mkuu wa Mkoa wa Singida, Parseko Kone.

Hata hivyo, madai hayo yamekanushwa vikali na Kone akisema, “Mimi sijaenda huko na wala si kazi yangu kuhamisha watu. Kuna watu hapa wanafanya siasa na wanadhani kwamba mimi ni kikwazo katika kufanikisha malengo yao.”

Alisema, kampuni zinazodaiwa kugombea eneo awali zilikuwa kampuni moja. “Hizi kampuni awali zilikuwa moja. Zimegawanyika kutokan na sababu zao binfasi,” alisema Kone katika mahojiano na gazeti hili kwa njia ya simu.

Wananchi waliohojiwa katika eneo anapotaka kujenga mradi, wamesema kampuni ya Wind East Africa Limited haijawahi kuwalipa hata senti tano kama fidia.

Tayari kampuni ya Rostam imepewa mkataba na Shirika la Umeme nchini (Tanesco) kwa njia ya upendeleo. Wameingia mkataba bila kuwa na miliki ya ardhi.

Hata hivyo, katika taarifa yake aliyositisha uchapishaji wake, Rostam anamtuhumu mbunge wa Karatu, Dk. Willibrod Slaa kuwa anampakazia kwa kudai kuwa anamiliki kampuni ya Wind East Africa Limited.

Taarifa hiyo (MwanaHALISI inayo nakala), inasema anazushiwa na kwamba hahusiki na kampuni hiyo, bali imekuwa kawaida ya Dk. Slaa na washirika wake kumchafua yeye kwa kumpachika tuhuma zinazomhusisha na kampuni zilizokumbwa na kashfa za ufisadi.

Dk. Slaa anamtuhumu Rostam kuwa ni fisadi mkubwa, na kwamba ni mmiliki wa kampuni ya Kagoda Agriculture Limited iliyochota zaidi ya Sh. 40 bilioni kutoka Benki Kuu ya Tanzania (BoT). Hata hivyo, Rostam hajakana kumiliki Kagoda.

Rostam pia hajakana taarifa zilizohusu andishi la wakili wa Mahakama Kuu, Bhydinka Michael Sanze kuwa aliitwa na Rostam ofisini kwake 50 Mirambo, jijini Dar es Salaam , kusaini nyaraka zilizowezesha Kagoda mabilioni kutoka BoT.

Katika andishi hilo la wakili Sanze, Rostam anatajwa kuwa ndiye kinara wa mpango wa kuchota mabilioni ya shilingi kutoka Akaunti ya Madeni ya Nje (EPA) ndani ya BoT akitumia Kagoda.

Ni katika andishi hilo ambamo Rostam anadaiwa kuwahusisha rais mstaafu Benjamin Mkapa, katibu mkuu wa zamani wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Philip Mangula na aliyekuwa Gavana wa BoT, Dk. Daud Ballali.

Wakili Sanze anaeleza kuwa Rostam, Peter Noni na Bered Malegesi walimthibitishia (yeye Sanze) kuwa Rostam alikuwa kwenye kikao ambapo Mkapa alitoa maelekezo kwa gavana Ballali kutoa fedha hizo kwa Rostam, kupitia Kagoda, kwa ajili ya shughuli za uchaguzi ndani ya CCM.

“Rostam mwenyewe alisema, ‘system yote inajua,’” anaeleza Sanze. Hata katika taarifa aliyotaka ichapishwe katika vyombo vya habari, Rostam hakukana Kagoda.

Akizungumza kwa njia ya simu kutoka Karatu juzi, Dk. Slaa alisema ana uhakika kampuni ya Wind East Africa Limited ni mali ya Rostam akishirikiana na aliyekuwa waziri mkuu, Edward Lowassa.

“Sikiliza bwana. Hii ni kama Kagoda. Kwenye nyaraka za usajili hakuna wanapoonekana. Lakini katika baadhi ya nyaraka nilizonazo, wanaonekana wamesaini vitu mbalimbali na kutumia anuani ya kampuni ya Rostam wakati wa kusajili.

“Nawasubiri wakane. Nitawaumbua maana nimejiandaa kikamilifu. Mimi si mtu wa kukurupuka na Rostam anajua hivyo,” anasema Dk. Slaa.

Anasema bado anaamini kuwa hakuna mgongano wa maslahi, isipokuwa ufisadi unaofanywa na Rostam Aziz na rafiki zake, wakisaidiwa na mkuu wa mkoa wa Singida.

Dk. Slaa anasema akina Rostam wanataka kuzalisha umeme wakati hawana eneo. “Hicho ndicho chanzo cha ugomvi wao na Dk. Mwakyembe (Harrison Mwakyembe, Mbunge wa Kyela).”

Alisema, “Nimekwenda Singida. Naufahamu vema mradi unaodaiwa. Nimeongea na wanakijiji Singida na viongozi wao. Kina Mwakyembe wanataka kuwakomboa wananchi, lakini kina Rostam wanataka kuwakandamiza.
I CAN'T AVOID THIS QUESTION WHICH KEEPS ON LINGERING IN MY MIND;WHO IS THIS INVINCIBLE ROSTAM AZIZ!!!!?

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.