Showing posts with label ROSTAM AZIZ. Show all posts
Showing posts with label ROSTAM AZIZ. Show all posts

17 Jan 2014

KATIKA hitimisho la makala yangu iliyochapishwa wiki mbili zilizopita, iliyobeba kichwa cha habari ‘Ni mwaka wa siasa za hovyo CCM, CHADEMA, niliahidi kuendeleza utabiri wa mwaka huu 2014, kwa kuangalia anga za kimataifa.
Kwa bahati nzuri, siku nne tu baada ya kuchapishwa makala hiyo, moja ya mambo niliyotabiri - kuendelea kwa mgogoro wa CHADEMA na uwezekano wa migogoro ndani ya vyama vya upinzani kuwa ya hadharani - limetokea.
Ninaomba niweke bayana kuwa masikitiko yangu kuhusu maendeleo mapya katika mgogoro wa CHADEMA ni makubwa zaidi ya furaha yangu kuona nilichotabiri wiki iliyopita kweli kimetokea. Nitakuwa mbinafsi na mnafiki ‘kusherehekea usahihi wa utabiri wangu’ katika jambo lisilopendeza. Laiti ingekuwa ni chaguo langu basi ningetamani mabaya yote niliyotabiri yasitokee, lakini kwa bahati mbaya hali halisi haikwepeki.
Takriban wiki mbili zilizopita, Mbunge wa Kigoma Kaskazini (CHADEMA) Zitto Kabwe alirusha ‘bomu zito’ ambapo alitoa tuhuma kubwa na hatari dhidi ya Mwenyekiti wake taifa wa chama hicho, Freeman Mbowe, na chama hicho kwa ujumla. Pengine ili kuleta ladha halisi ya alichosema Zitto ni vema nikanuu ‘waraka’ mzima kama ifuatavyo:
"Lissu anasema nimepewa magari 2 na Mzee Mkono. Anasema kaambiwa na Mkono. Naamini Mkono alimwambia pia mwaka 2005 alimpa Freeman Aikaeli Mbowe tshs 40m ili Mbowe asifanye kampeni Musoma Vijijini.
“Nadhani alimwambia pia mwaka 2008 (baada ya orodha ya mafisadi kutangazwa 2007) Mkono alimpa Freeman tshs 20m za uchaguzi wa Tarime na Freeman akasema kwenye chama ametoa mkopo na akalipwa. Nadhani alimwambia pia kuwa mwaka 2010 Mkono alimpa Mbowe tshs 200m za kampeni ya Slaa.
“Pia hakusahau kumwambia kuwa Rostam Aziz alimpa Mbowe tshs 100m za kampeni. Lissu anajua kuwa gazeti la Tanzania Daima limeanzishwa na fedha za chama kutoka Conservative Party?
“Nimefanya internship yangu kwa Mkono and Company Advocates kuhusu masuala ya mikataba. Mzee Mkono ni Mzee wangu na alisaini petition ya kumtoa Waziri Mkuu Pinda. Lissu awaambie waliyemtuma wamwambie ukweli wote. Lissu ajue yeye ni kifaranga tu, Mimi namtaka mama wa kifaranga ajitokeze. Aeleze aliingia deal gani na Kinana na Sumaye mwaka 2005 kufuatia deni lake NSSF. Aweke wazi mkataba kati yake na NHC kuhusu nyumba ya umma ilipo Club Bilicanas.
“They must know I am not a push over. Chacha died, I won't. Mtu ambaye hawezi kuheshimu mke wake aliyemzalia watoto hawezi kunyooshea mtu kidole kuhusu maadili."
Zitto alibandika waraka huo katika ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Facebook, lakini kwa sababu anazojua yeye pekee, baadaye aliuhariri na kutojumuisha tuhuma hizo. Aidha kwa kutofahamu au makusudi, uhariri uliofanywa na mwanasiasa huyo katika waraka huo haukuzuia kusambaa kwa kasi mtandaoni.
Niliposoma waraka huo nilipatwa na mshtuko mkubwa, nikabaki ninajiuliza iwapo Zitto alikuwa ‘mzima’ wakati anaandika alichoandika.  Japo inawezekana alifanya hivyo kwa kuzingatia kile kinachofahamika mtaani kama ‘umemwaga ugali na mie namwaga mboga...bora tukose wote,” ukweli ni kwamba bandiko hilo lina madhara makubwa, kwa Zitto binafsi na kwa pengine ustawi wa CHADEMA kwa ujumla.
Madhara kwa Zitto ni ya kisheria zaidi. Tayari Mbowe ameonyesha nia ya kumburuza Zitto mahakamani kuthibitisha tuhuma hizo nzito. Bila kujali kuwa tuhuma hizo zina ukweli au la, mtu yeyote mwenye uelewa wa ‘dili za siri’ atafahamu kuwa ni vigumu kuzithibitisha kisheria, yayumkinika kuhisi kuwa Zitto atakuwa na kazi ya ziada katika ‘kesi’ hiyo (iwapo itafunguliwa).
Iwe ni tuhuma za Nimrod Mkono kumpa Mbowe shilingi milioni 260 katika mazingira ambayo si tatanishi tu bali pia kwa namna fulani ni hujuma dhidi ya CHADEMA, au Rostam Aziz kumpatia Mbowe shilingi milioni 100, au ‘dili’ kati ya Mbowe na Waziri Mkuu wa zamani, Frederick Sumaye na Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana, sidhani kama Zitto anaweza kuthibitisha tuhuma hizo iwapo Mbowe atatimiza azma yake ya kufungua kesi. 
Je, inawezekana kuwa kwa kutambua ‘kosa hilo la kisheria’ ndio maana muda mfupi baadaye Zitto alihariri ‘post’ hiyo? Wakati jibu analo Zitto mwenyewe, ukweli unabaki kuwa tuhuma hizo ni nzito mno, na iwapo ni za kweli basi zinapoteza kabisa hadhi ya CHADEMA.
Ikumbukwe kuwa katika waraka uliopelekea Zitto kuvuliwa nyadhifa zake mbalimbali ndani ya CHADEMA, walioandika waraka huo waligusia walichokiita ‘udhaifu wa wanayemtaka’ (wakimaanisha Zitto), na kudai, “Maneno yake mara nyingine hayazingatii anayazungumza katika mazingira gani na hivyo kuwasha masikio ya wanataasisi jambo linalompunguzia kukubalika kwake taratibu.” 
Kadhalika, walieleza kuwa; “Kuna wakati tunayemtaka (Zitto) hujibu kwa taharuki kubwa dhidi ya mashambulizi yanayoelekezwa kwake jambo linalomfanya achukue maamuzi yasiyo sahihi kwa wakati huo. Kwa kifupi kuna wakati tunayemtaka (Zitto) huonekana kufanya maamuzi kwa hisia zaidi badala ya kutulia kwanza na kutafakari kwa kina ikiwa ni pamoja na kutafuta ushauri kwa wenzake kabla ya kujibu.”
Ndugu msomaji, huhitaji kuwa mwanasaikolojia kuhisi kuwa huenda kilichomsukuma Zitto kuandika ‘waraka’ huo kwenye ukurasa wake wa Facebook ni kile Waingereza wanakiita “putting emotions in front of common sense”, yaani kwa tafsiri isiyo rasmi, kuweka mbele jazba badala ya busara.
Kwa kujaribu kuonyesha kuwa Mbowe si mwadilifu (kwa maana ya kupokea misaada kutoka kwa ‘wanasiasa kama Mkono na Rostam waliowahi kutajwa na CHADEMA kuwa ni mafisadi’), linakuja swali la msingi, kwanini Zitto alikalia kimya tuhuma hizo nzito kwa takriban miaka minane hadi sasa baada ya kuvuliwa madaraka? Hivi kuna neno stahili kuelezea hali hiyo zaidi ya unafiki?
Tukiamini tuhuma hizo za Zitto, je naye si sehemu ya ‘uhuni wa CHADEMA’ wa kukemea mafisadi hadharani ilhali pembeni wanapokea misaada ya watu hao hao wanaowatuhumu? Ninasema hivyo kwa sababu Zitto hakuwa katibu wa shina bali Naibu Katibu Mkuu (taifa)  wa chama hicho, na mbunge, na kwa vyovyote vile naye ni mnufaika wa fedha hizo ‘za mafisadi.’
Laiti angekuwa haridhii vitendo hivyo basi aidha angejitoa mhanga na kuweka ukweli hadharani wakati huo (na hiyo ingeweza kuzuia kurejea kwa vitendo kama hivyo) au angeweza kujiuzulu kwa kuona ‘chama chake kinashirikiana na watuhumiwa wa ufisadi. Kwa nini hakufanya hivyo? Jibu jepesi ni hilo nililoandika hapo juu: alikuwa mnufaika wa vitendo hivyo (iwapo kweli vilitokea, maana tayari baadhi ya aliowataja wamekanusha ‘kumpa msaada’ Mbowe).
Binafsi, ninadhani moja ya matatizo yanayomkabili Zitto ni wanaojiita au kujitambulisha kama wafuasi wake. Wengi kati yao ni wenye mapenzi na CCM, na ushabiki wao kwa Zitto ni wa kirafiki (kimaslahi?) zaidi. Ndio, tofauti za kiitikadi hazimaanishi uadui, lakini wengi wetu tunaufahamu msemo ‘nionyeshe marafiki zako na nitakwambia wewe ni nani,’ yaani mara nyingi watu wanaotuzunguka hutoa picha fulani kuhusu sisi wenyewe.
Lakini tatizo jingine kuhusu ‘wafuasi na marafiki hao wa Zitto’ ni kutokuwa washauri wazuri kwake. Ukisoma mengi ya wanayoandika, hususan huko kwenye mitandao ya twitter, utabaini kuwa kimsingi wanachofanya ni ‘kumvimbisha kichwa Zitto’ bila kutoa ushauri unaoweza kusaidia ustawi wa kisiasa wa mwanasiasa huyo kijana.
Na mfano wa hivi karibuni ni baada ya Zitto kubandika waraka huo wenye tuhuma nzito huko Facebook. Wengi wa wafuasi wake walionekana kuchekelea ‘Mbowe alivyoumbuka’ bila kujali athari za kisheria kwa Zitto na ustawi wa CHADEMA kwa ujumla (kwanini wajali ilhali wengi wao ni wanaCCM)?
Kwa wafuasi wa Zitto, mwanasiasa huyo ni majeruhi wa siasa za chuki na mizengwe ndani ya CHADEMA. Lakini kwa wengine, Zitto anaonekana kama mtu anayeendeshwa na ‘ego’ kubwa inayomfanya kujiona yeye ndiye-au zaidi ya- CHADEMA.
Ni vigumu kubashiri hatma ya maisha ya kisiasa ya Zitto lakini kwa hali ilivyo ni vigumu mno kuona mustakabali wake ndani ya chama hicho. Ninakumbuka mwanasafu mmoja wa gazeti hili alimshauri mwanasiasa huyo hivi karibuni kuwa suluhisho la busara kwake kwa sasa ni kutosubiri kuvuliwa uanachama, ajiondoe mwenyewe huko CHADEMA, na kuitaka Mahakama isiingilie kazi ya chama.
Mwisho, bado ninaamini kuwa Zitto ni mwanasiasa mzuri lakini pengine kwa upungufu wa kibinadamu au makusudi, washauri wabovu au sababu nyinginezo, hazingatii umuhimu wa busara hizi tatu katika medani ya siasa: moja, waweke marafiki zako karibu lakini waweke maadui zako karibu zaidi, na pili, hakuna marafiki au maadui wa kudumu katika siasa, na tatu, hakuna mwanasiasa anayeweza kuwa mbadala wa chama (hasa katika mazingira ya siasa zetu ambapo kwa kiasi kikubwa chombo pekee cha uongozi wa kisiasa ni chama cha siasa. Bila chama, mwanasiasa hata awe maarufu kiasi gani anabaki kuwa raia wa kawaida tu).
Katika waraka wake, Zitto aliandika, “They must know I am not a push over. Chacha died, I won't” (lazima wafahamu mie sio mtu wa ‘kupelekeshwa.’ Chacha (Wangwe?) alikufa, mimi sitokufa). Hiki ni kiburi, utoto au? Ni mwanadamu mwenye uhakika wa kutokufa? Nihitimishe kwa kumshauri kwamba labda kweli ana uhakika wa kuishi milele lakini kwa kutanguliza hisia badala ya busara, yayumkinika kubashiri kuwa anaweza kuwa anajiua mwenyewe kisiasa (committing political suicide).



10 Apr 2011




Habari zilizopatikana kutoka Dodoma kwenye kikao cha CCM chini ya uenyekiti wa Rais Jakaya Kikwete zinaeleza kuwa baadhi ya viongozi waadamizi wa chama hicho wamevuliwa madaraka.Kwa mujibu wa vyanzo vya mtandaoni,waliokumbwa na panga la Kikwete ni pamoja na maswahiba wake wakuu kisiasa,Edward Lowassa na Rostam Aziz.Wengine wanaotajwa kwa mujibu wa habari hizo ni "Mzee wa Vijisenti" Andrew Chenge na "mgosi" Yusuph Makamba.

Ningependa kuichambua habari hii kwa kirefu lakini nasubiri kwanza tamko rasmi la CCM.Hata hivyo,tukiamini kuwa habari hizo ni sahihi,kuna uwezekano ya yafuatayo kutokea:

Kwanza,ni muhimu kufahamu watu kama Lowassa na Rostam wametoka wapi.Hawa walikuwa vioungo muhimu kwa ushindi wa Kikwete mwaka 2005.Wanaowajua vema wanawa-describe kwa mlolongo huu:Lowassa-mwanasiasa haswa (simaanishi kuwa ni mwanasiasa mwadilifu),Rostam-bwana fedha,na Kikwete-mtawala.Wajuzi wa siasa chafu wanaeleza kuwa ushirikiano huo wa watu hawa watatu ulitumia kila aina ya mbinu kuhakikisha Kikwete anaingia Ikulu hapo 2005.Na ikawa hivyo,baada ya viongozi hao wakuu wa "Mtandao" kufanikiwa kupenya takriban kila kundi la jamii;kutoka viongozi wa dini hadi wakuu wa taasisi za dola,kutoka wanahabari hadi wasanii.

Pasipo kuuma maneno,ushirika huu usio mtakatika wa Lowassa,Rostam na Kikwete ni mithili ya joka lenye vichwa vitatu.Sasa iwapo ni kweli kuwa Kikwete kaamua kubaki kichwa pekee kwenye joka hilo basi yayumkinika kubashiri kuwa uhai wa joka hilo nao uko matatani.

Pili,kwa kufuata mlolongo wa nilichoandika hapo juu,inaelezwa kuwa Lowassa ndiye aliyefanya kazi kubwa zaidi ya kutengeneza serikali ya Kikwete.Ikumbukwe kuwa japo wote wawili walishashika nyadhifa mbalimbali serikali kabla ya 2005,Lowassa alikuwa amejijenga zaidi kiuchumi na kisiasa ukilinganisha na Kikwete.Kadhalika-na hapa nafafanua kwanini niliandika hapo juu kuwa Lowassa ni mwanasiasa haswa(japo simaanishi ni mwanasiasa mwadilifu)-ni ukweli kuwa mwanasiasa huyo ana ushawishi wa kisiasa zaidi ya Kikwete.Japo wote wawili ni wapenda umaarufu (populists),wakati Kikwete amekuwa akitumia zaidi turufu ya "tabasamu la muda wote" na "kuwa karibu na watu",Lowassa amekwenda mbali zaidi na kujifanya anayafahamu matatizo ya wananchi na kuyatolea ufumbuzi mapema (ndio maana licha ya kulazimika kujiuzulu kutokana na ufisadi wa Richmond bado kuna wanaomwona kama mwajibikaji).Kwa kifupi,Lowassa ni mwepesi wa kuchukua maamuzi (hususan yale yatayopelekea yeye kuonekana kama "Sokoine flani hivi"),Kikwete ni mzito wa maamuzi (huku walio karibu naye wakidai tatizo sio uzito wa maamuzi bali hajui vipaumbele vyake).

Inaaminika kuwa Lowassa ana ufuasi mkubwa ndani ya CCM na serikalini kwa ujumla.Kwa mujibu wa wajuzi wa mambo,faida aliyonayo Lowassa ndani ya chama hicho ni uwezo wa kifedha,ambapo inaelezwa kwamba amewasaidia viongozi mbalimbali wa CCM kiuchumi na kuwawezesha kuwepo walipo leo.Kadhalika,akiutumia vema urafiki wake na Kikwete, na nafasi yake kama Waziri Mkuu kabla ya skandali ya Richmond,aliweza kutengeneza "mtandao ndani ya mtandao",kwa maana ya kuwaweka madarakani watu wenye utiifu kwake zaidi kuliko CCM au Kikwete.Inaelezwa wateuliwa wengi kwenye nafasi za kiserikali na kichama ngazi za mikoa na wilaya ni wafuasi wa Lowassa,kwa mfano ma-RC na ma-DC,na wenyeviti na makatibu wa CCM mikoani na wilayani.

Swali la muhimu ni je,kuondoka kwa Lowassa katika wadhifa mmoja kutazuwia nguvu na ushawishi wake kwa wafuasi wake,wengi wao wakiwa ni watu walio madarakani kutokana na fadhila za mwanasiasa huyo?

La tatu ni ukweli kuwa Lowassa anataka urais hapo 2015.Na hilo halikuanza jana au juzi bali wajuzi wa mambo wanaeleza kuwa kulikuwa na makubaliano rasmi kati ya Kikwete na Lowassa kuwa wangepokezana uongozi maara baada ya Kikwete kumaliza miaka yake 10.Japo suala la Richmond lilizua mfarakano wa aina flani kati ya wawili hao lakini ukweli unabaki kuwa "heshima" aliyotoa Kikwete kwa Lowassa kwa kutomtimua bali kusubiri ajiuzulu mwenyewe iliwaacha wawili hao wakiendelea na urafiki wao japo si kama ilivyokuwa mwanzoni.

Haifahamiki kama Kikwete bado anaheshimu "makubaliano" yake na Lowassa kuhusu "kupokezana kijiti cha urais hapo 2015" lakini hiyo haimzuwii Lowassa kuamini kuwa "piga au" lazima achukue nafasi hiyo.Of course,kuna majina kama Bernard Membe (mtu anayetajwa kuuweka uhusiano na Lowassa katika wakati mgumu kwa vile yeye na Lowassa "picha hazipandi" ilhali yeye na Kikwete ni "damu damu",na Kikwete na Lowassa ndio hivyo tena "hawakufahamiana mtaani" kama ilivyowahi kutamkwa hadharani ) lakini turufu ya Lowassa haitegemei sana baraka za Kikwete bali ushawishi na nguvu yake ndani ya CCM,sambamba na uwezo wake mkubwa wa kifedha (alizitoa wapi....waulize TAKUKURU).Na ana faida nyingine kubwa ambayo ni uswahiba wake na Rostam,mfanyabiashara mwenye asili ya kiasia anayetajwa kuwa na nguvu zaidi ya Kikwete-kutokana na utajiri wake unaoweza kumfanya kuwa mtu tajiri kuliko wote Tanzania.Kadhalika,inaelezwa kuwa Rostam ni mjuzi wa mbinu chafu hususan kwa kutumia fedha zake na "njaa" za wanaohitaji chochote kutoka kwake.

Jingine,ambalo linaweza kuwa si la msingi sana japo lina umuhimu wa aina flani ni ukweli kwamba Lowassa na Rostam wana siri muhimu kumhusu Kikwete na urais wake kwa ujumla.Njia pekee kuwadhibiti wawili hao kwa kutumia Idara ya Usalama wa Taifa.Katika siasa zetu za "ovyo ovyo" ni rahisi tu kwa rais kuiamuru taasisi hiyo imfanyie kazi zake binafsi badala ya zile za kikatiba.Hilo linawezekana zaidi kutokana na nafasi ya Rais kama consumer wa taarifa zote za kishushushu.

Nisingependa kutabiri matokeo kabla ya taarifa kamili ya CCM lakini tukiamini habari zilizopo na ikathibitika kuwa ni kweli basi nachobashiri ni mwanzo wa mwisho wa chama hicho tawala.Naomba unielewe vizuri: tatizo la msingi sio kutimuliwa kwa Lowassa na Rostam bali ukweli kuwa USHIRIKA WA WACHAWI HAUDUMU.Sambamba na hilo ni ukweli mwingine kuwa JOKA LENYE VICHWA VITATU HALIWEZI KUWA HAI MUDA MREFU PINDI VICHWA VIWILI VIKIKATWA.

Lakini la muhimu kuliko yote ni manufaa kwa Watanzania kutokana na mabadiliko hayo ndani ya CCM.Kwa kifupi,ukiacha vichwa vikubwa vya habari kwenye magazeti yetu,mabadiliko hayo hayana manufaa yoyote kwa masikini wasio na hakika ya mlo wao wa kesho,wanafunzi wanaokaa sakafuni kwa uhaba wa madawati,akina mama wanaoletewa bajaj za kuwawahisha hospitali wakiwa wajawazito japo wabunge wanapewa mashangingi ya uheshimiwa,nk nk nk.Wa kuondoka na CCM kama chama kilichopo madarakani.Wanapoondoana ndani kwa ndani haimsaidii Mtanzania wa kawaida.

17 Mar 2011


"Tiba ya Babu" imeibua kila aina ya vimbwanga.Nikianza kuviorodhesha vimbwanga hivyo basi tutakesha kwani kila kukicha kuna mapya.Mara tusikie wagonjwa waliotoroka mahospitalini "wamefumaniana" na madaktari waliotorokwa na wagonjwa hao,huku wote-wagonjwa na madaktari wakiwa kwenye foleni kusbiri "tiba ya Babu"

Lakini siui kama msomaji mpendwa umebaini "mpasuko wa kimtizamo" kati ya maswahiba wawili maarufu,Rostam Aziz na Edward Lowassa.Wakati Rostam alinukuliwa akiiponda "tiba" hiyo,swahiba wake-Lowassa-sio tu alitinga kwa "Babu kupata kikombe" bali pia inaelezwa amewalipia wapiga kura wake gharama za usafiri kwenda kupata "tiba" hiyo.

Je hii ni dalili ya mwanzo ya mpasuko kati ya wanasiasa hawa ambao majina yao ni kama synonymous na ufisadi?Au wanatuzuga tu mind games?You decide

Rostam aponda tiba ya Mchungaji Loliondo
Tuesday, 15 March 2011 21:22

Shija Felician, Igunga
WAKATI Watanzania wengi wakimiminika kwenda wilayani Loliondo, mkoani Arusha kupata dawa inayodaiwa kutibu magonjwa sugu, Mbunge wa Igunga (CCM), Rostam Aziz ameibuka na kusema tiba hiyo haina lolote akidai kwamba ndugu zake watano wameitumia lakini hawajapona.

Akihutubia wananchi katika mkutano wa hadhara wa kuwashukuru wapigakura uliofanyika kwenye Viwanja vya CCM wilayani Igunga, Tabora mbunge huyo alisema haiamini dawa hiyo kwa kuwa ana ushahidi kwa ndugu zake hao ambao anadai kwamba wanaendelea kuugua kisukari licha ya kutumia dawa hiyo siku saba zilizopita.

Aliwataka wale watakaokwenda Loliondo ambao wanatumia dawa za hospitalini kuendelea kuzitumia badala ya kuzipuuza na kuzitupa... “Ndugu zangu wananchi wa Igunga, mimi mjomba wangu Hassan mnamfahamu karibu wote hapa mjini ni mgonjwa wa siku nyingi wa kisukari. Ameshakunywa dawa hiyo lakini mpaka sasa ni mgonjwa kama mnavyomuona sasa hiyo dawa inaponyesha nani?”

Hata hivyo, aliwataka wananchi wote wenye imani juu ya dawa hiyo waende huku akiwasisitizia kutopuuza ushauri wa madaktari kwani.

Wakati Rostam akipinga dawa hiyo, wilayani Kahama, mamia ya wafanyabiashara wamefunga shughuli zao na kukimbilia Loliondo kwa Mchungaji Mwasapile kunywa dawa hiyo huku baadhi ya waliorejea baada ya kuinywa wakidai kuwa hali zao sasa ni nzuri.

Wafanyabiashara hao wengi wao wanaondoka kwa siri wakidai wanakwenda Dar es Salaam katika shughuli zao, lakini siri imefichuka baada ya baadhi yao kuoneka katika runinga wakiwa katika foleni wakisubiri kupatiwa huduma hiyo.

Mbali ya kuzungumzia suala hilo la tiba ambalo limegusa hisia za wananchi wengi wa Afrika Mashariki, mbunge huyo aliwapa pole wananchi wa Igunga ambao nyumba zao zimeezuliwa na upepo uliosababishwa na mvua kubwa zilizonyesha wiki iliyopita ambazo ziliathiri kaya 19. Aitoa msaada wa Sh500,000 kwa kila kaya iliyokumbwa na maafa hayo.
CHANZO: Mwananchi

Lowassa apata kikombe Loliondo
Tuesday, 15 March 2011 23:47

Waandishi Wetu

WAZIRI Mkuu wa zamani, Edward Lowassa juzi alipata tiba ya magonjwa sugu inayotolewa na Mchungaji Mstaafu wa Kanisa la Kiinjili la Kilutheri Tanzania (KKKT), Ambilikile Mwasapile katika Kijiji cha Samunge, Tarafa ya Sale, Loliondo, mkoani Arusha.Lowassa alifika katika eneo hilo mchana akiwa na viongozi kadhaa wa Halmashauri ya Wilaya ya Ngorongoro na Serikali kisha kupata kikombe kimoja chenye dawa kinachotolewa na mchungaji huyo kwa ajili ya tiba.

Tofauti na viongozi wengine, Lowassa ambaye ni Mbunge wa Monduli (CCM), Jimbo linalopakana na Kijiji cha Samunge, alikwenda huko akiwa na viongozi mbalimbali wakiwamo viongozi wa dini na baadhi ya wapigakura wake.

Akizungumza na gazeti hili kwa njia ya simu jana, Lowassa alithibitisha kwenda Loliondo na kuwataja viongozi wa dini alioambatana nao katika msafara wake kuwa ni Askofu Msaidizi wa KKKT, Dayosisi ya Kaskazini, Dk Frederick Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Dayosisi ya Kaskazini Kati (Arusha), Mchungaji John Nangole.

Katika ramani ya utendaji kazi ya KKKT, Jimbo la Masai Kaskazini ndipo kilipo Kijiji cha Samunge ambako ni makazi ya Mchungaji Mwasapile.“Ni kweli, nimekwenda pale na wapigakura wangu pamoja na viongozi wa dini, Msaidizi wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kaskazini, Dk Shoo na Mkuu wa Jimbo la Masai Kaskazini, Mchungaji Nangole,” alisema Lowassa na kuuliza: “Kwani hiyo nayo ni habari jamani?”

Baada ya Lowassa kufika katika kijiji hicho akiwa na ujumbe wake, aliongoza moja kwa moja hadi kwa Mchungaji Mwasapile na kuzungumza naye kisha akapata kikombe cha tiba na kuondoka.

Kabla ya Lowassa kwenda kupata tiba, amekuwa akitoa msaada wa nauli kwa wagonjwa mbalimbali wa jimbo lake kwenda kwa mchungaji huyo ambaye dawa yake inadaiwa kutibu magonjwa ya saratani, kisukari, pumu, shinikizo la damu na Ukimwi.Lowassa ni miongoni mwa wanasiasa maarufu nchini ambao wameshafika kwa mchungaji huyo kupata tiba hiyo wakiwamo mawaziri, naibu mawaziri, wabunge, wakuu wa mikoa na wilaya.
CHANZO: Mwananchi

5 Jan 2011

Picha Hii Inatoa Maelezo Alfu Kidogo.Ukiangalia kwa Makini Utamwona Rostam Kama Kalizimishwa Kuinua Mkono,huku Kikwete Akiwa as if Anampigia Debe Bosi Wake...na Tabasamu Juu!Lol,Ama Kweli Rais Tunaye,Si Mchezo

Dk. Slaa: Kikwete ajiuzulu
• Asisitiza anahusika na Dowans, aahidi kutoboa siri
na Janet Josiah

KATIBU Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Wilibrod Slaa, sasa amekuja na hoja mpya ya kumtaka Rais Jakaya Kikwete ajiuzulu kutokana na kuhusika moja kwa moja na sakata la Dowans iliyorithi mikoba ya Richmond.

Dk. Slaa ametoa kauli hiyo nzito jana katika mahojiano maalumu na Tanzania Daima Jumatano, ikiwa ni siku moja baada ya Ikulu kutoa taarifa ya kejeli na vijembe vya mitaani dhidi yake kuhusu sakata hilo.

Akizungumza kwa utulivu na umakini mkubwa, Dk. Slaa alisema Rais Kikwete alipaswa kujiuzulu kabla ya aliyekuwa Waziri Mkuu na swahiba wake mkubwa, Edward Lowasa, kuchukua hatua hiyo Februari 7, mwaka 2008, mjini Dodoma.

Yaani Kikwete Mpaka Kaikamata Mic Kuhakikisha Kuwa Debe Analompigia Swahiba Wake ni La Nguvu Kweli Kweli!Kama Alivyowahi Kusema Lowassa,Wawili Hawa Hawakufahamiana Mtaani.Wametoka Mbali.BIRDS OF A FEATHER..
Mawaziri wengine waliojiuzulu kutokana na sakata la Richmond lililozua mjadala mkali nchini ni pamoja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini wakati huo, Nazir Karamagi na Ibrahim Msabaha ambaye alikuwa waziri wa wizara hiyo kabla ya kuhamishiwa Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki (EAC).

Akitoa ufafanuzi wa taarifa ya Ikulu iliyotolewa juzi na Kurugenzi ya Mawasiliano, Dk. Slaa alisema mkuu huyo wa nchi hawezi kukwepa kuhusishwa na sakata la Dowans, kwani alilijua hata kabla mitambo yake haijaingizwa nchini.

"Nataka niwatoe Watanzania wasiwasi kwamba ingawa kurugenzi ya mawasiliano imetoa taarifa ya kumsafisha Rais Kikwete na kunikashifu mimi kwa lugha ya mtaani, nawaambia alipaswa kujiuzulu kabla na anatakiwa ajiuzulu sasa, kwani anahusika moja kwa moja na uingiaji wa mkataba wa Kampuni ya Richmond na baadaye na Dowans" alisema Dk. Slaa.

Alimtaka Rais Kikwete kutambua kuwa hawezi kukaa kimya kwa kisingizio cha kuhatarisha amani na utulivu wakati wananchi wanaibiwa mabilioni ya fedha na mafisadi wachache kupitia kampuni feki ya Dowans.

Akirejea historia ya vita dhidi ya ufisadi aliyoiasisi bungeni, Dk. Slaa aliwataka wananchi wakumbuke kuwa taifa lilipokumbwa na tatizo la umeme kabla ya mitambo ya Richmond kuingia nchini, Rais Kikwete alikwenda Marekani kwa ziara ya kikazi.

Alisema aliporejea nchini, alizungumza na waandishi wa habari kuhusu tatizo hilo na kuahidi kuwa serikali yake inalifanyia kazi na siku chache baadaye, rafiki yake wa karibu, Rostam Azizi, Mbunge wa Igunga (CCM), naye alikwenda Marekani.

"Rostam aliporejea kutoka Marekani baada ya siku chache tukaanza kusikia mitambo ya kuzalisha umeme wa dharura kutoka Kampuni ya Richmond inatarajiwa kuwasili. Kweli ilitua nchini katika Uwanja wa Mwalimu Nyerere na shughuli nyingine zilifungwa uwanjani hapo kupisha ushushaji wa mitambo ya Richmond" alisema Dk. Slaa.

Kwanini Rostam Asiwe na Furaha?Kuendesha Nchi ya Watu Takriban Milioni 50 kwa Kutumia Remote Control si Jambo Dogo Ati!

Huku akisisitiza kuwa ana ushahidi wa anachokisema, Dk. Slaa alisema hata baada ya Richmond kushindwa kuzalisha umeme na kusababisha mawaziri kujiuzulu, serikali ya Kikwete iliamua kuingia mkataba na Dowans iliyorithi shughuli za Richmond na hatua hiyo Rais Kikwete pia aliijua.

"Dowans nayo ikashindwa kuzalisha umeme, mwisho Bunge katika moja ya maazimio yake liliridhia uamuzi wa kuvunja mkataba huo, lakini leo Serikali inadaiwa fidia ya sh bilioni 185, je, Rais Kikwete anaweza kukwepa kwamba hana mkono wake hapo?" alihoji.

Kutokana na hayo, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete amtaje mmiliki halali wa Dowans ili kuwatoa kiu Watanzania wanaohitaji kumjua.

"Sitaacha kuzungumzia masuala yanayowagusa Watanzania na mali, hasa katika kipindi hiki ambacho Watanzania wanataka kuibiwa fedha zao, wakati wa kukaa kimya umekwisha" alisema Dk. Slaa.

Alisema hashangazwi na kejeli za Ikulu na kuwataka Watanzania kukumbuka alipoanza kuwalipua mafisadi, Rais Kikwete aliwahi kutamka kwamba kelele za mlango haziwezi kumnyima mwenye nyumba usingizi na kamwe kelele za chura hazimzuii ng ombe kunywa maji.

Kaaazi Kweli Kweli
"Lakini baada ya sisi kuamua kupambana na Richmond, Rais Kikwete alikiri linamnyima usingizi na hili la Dowans litamnyima usingizi zaidi katika kipindi hiki cha mwisho cha uongozi wake" alisema Dk. Slaa.

Ili kumaliza kelele za Dowans, Dk. Slaa alimtaka Rais Kikwete kumtaja mmiliki wake ambaye anataka kuwaibia Watanzania mabilioni ya fedha.


 
Wakati Dk. Slaa akimkaba koo Rais Kikwete, mjadala wa Dowans hivi sasa umewavuruga hata viongozi wa serikali tangu ilipoamriwa ilipwe sh bilioni 185.

Aliyekuwa Spika wa Bunge lililopita, Samuel Sitta, hivi karibuni alikaririwa akiitaka serikali iache kuilipa Dowans kwa madai kuwa ni mradi wa mafisadi watatu.

Kauli hiyo ilipingwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, ambaye alisema kuwa suala la malipo ya Dowans lipo kisheria na ikithibitika serikali haiwezi kukata rufaa, italazimika kulipa mabilioni hayo.

Juzi Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu imeelezea kukerwa kwake na hatua ya Dk. Slaa kumtaja Rais Kikwete kuwa alihusika katika uzembe uliosababisha taifa kutakiwa kuilipa Kampuni ya Dowans sh bilioni 185 kama fidia.

Taarifa hiyo kali ya Ikulu iliyobeba ujumbe wenye maneno ya kebehi na ya mitaani ya kumwita Dk. Slaa mtu aliyechanganyikiwa na mzabinazabina ilisainiwa na Salvatory Rweyemamu, ambaye kabla ya kwenda Ikulu alikuwa mmoja wa wahariri watendaji, aliyekuwa akiheshimika kwa kutumia lugha fasaha na ya staha.

Rweyemamu katika taarifa yake hiyo iliyoonyesha waziwazi kuandikwa na mtu mwenye hasira, chuki na dharau ama kwa Dk. Slaa, CHADEMA na Tanzania Daima, alikwenda mbali na kumwita kiongozi huyo wa kisiasa kuwa ni mtu hatari.

Katika mahojiano maalumu na gazeti la Tanzania Daima Jumapili, mwishoni mwa wiki, Dk. Slaa alikaririwa akisema chanzo cha suala la Dowans kutakiwa kulipwa fidia limetokana na uzembe wa serikali na Rais Kikwete mwenyewe anahusika kuileta Kampuni ya Richmond ambayo baada ya kuonekana ya kitapeli iliamua kurithisha kazi zake kwa Dowans.

VYANZO: Habari kwa Mujibu wa Tanzania Daima.Picha Kutoka Vyanzo Mbalimbali Mtandaoni.

1 Oct 2010

"Ufisadi Oyeee.Tupeni tena miaka mitano tuwakwangue kabisa".Of course ni unatarajia nini hapo?

Mgombea wa CCM,Jakaya Kikwete akiendelea na ngwe ya kuwatetea rafiki zake.Alianza na Lowassa,akaenda kwa Mramba,kisha kwa Mzee wa Vijisenti Chenge,na sasa kwa "baba lao" Rostam Aziz.Ama kweli Tanzania bila ufisadi inawezekana!

Wakati "ndege wenye manyoya yanayofanana wakiruka pamoja",Dokta Slaa anaendelea na darasa la kuwahamasisha wenye uchungu na nchi yao kufanya kila liwezekanalo kuwang'oa "ndege hao"


Wananchi mjini Songea wakimsikiliza Rais Mtarajiwa kwa makini
Picha zote kwa hisani ya Jamii Forums

26 Aug 2010

Rostam Aziz
Katika kuelekea uchaguzi mkuu wa mwaka 2005,mfanyabiashara controversial Rostam Aziz alitumia raslimali zake nyingi kuhakikisha mgombea wa nafasi ya urais kwa tiketi ya CCM,Jakaya Kikwete,anashinda kwa gharama yoyote ile.Na kutokana na utajiri mkubwa alionao pamoja na mbinu zake mbalimbali,mchango wake ulimsaidia sana Kikwete kuingia Ikulu,na sasa ni Rais wetu anayeomba tena ridhaa ya kutuongoza kwa miaka mitano ijayo.

Kati ya mwaka 2005 (baada ya Kikwete kuingia Ikulu) na sasa,Rostam ameibuka kuwa kiumbe mwenye nguvu za kutisha sio tu ndani ya CCM bali kwenye siasa za Tanzania kwa ujumla.Lakini kubwa zaidi katika kipindi hicho ni kwa mfanyabiashara huyo kuhusishwa na tuhuma mbalimbali za ufisadi na Kikwete na serikali yake kushindwa kuwaridhisha Watanzania kwamba "hamkumbatii swahiba wake huyo".Haihitaji kurejea namna Rostam alivyohusishwa na ufisadi wa EPA (Kagoda) na ujambazi wa Richmond.
Jakaya Kikwete

Mwaka 2010,yaani mwaka huu,Rostam anaelekea kurejea tena ulingoni japo si kwa wazi sana.Ushahidi wa kimazingira unaonyesha kuhusika kwa mfanyabiashara huyo katika kampeni za Kikwete.Vyombo vya habari vinavyomilikiwa na Rostam vimekuwa vikiendesha kampeni ya chuki dhidi ya mgombea urais kwa tiketi ya Chadema,Dokta Wilbroad Slaa,mwanasiasa anayeonekana kuwa  tishio kwa mfanyabiashara huyo na vitendo vyake dhidi ya maslahi ya taifa.
Magazeti yanayomilikiwa na Rostam

Na kama hilo la vyombo vya habari vya Rostam kumuandama Dkt Slaa halitoi mwangaza wa kutosha basi taarifa kwamba mwandishi mwandamizi wa kampuni ya Habari Corporation (inayomilikiwa na Rostam),Muhingo Rweyemamu,anatajwa kuwa mratibu wa kampeni za Kikwete.Itakumbukwa kuwa mwaka 2005,waliokuwa waandishi waandamizi wa Habari Corporation,Salva Rweyemamu na Dokta Gideon Shoo walitumika sana kwenye kampeni hizo.Baada ya kuingia Ikulu,Kikwete "alimzawadia" Salva ukurugenzi wa habari wa Ikulu,nafasi anayoshikilia hadi sasa.
Muhingo Rweyemamu

Kama alivyo Salva,Muhingo anasifika kwa uwezo wake wa hali ya juu wa kujenga hoja.Kwa bahati mbaya au makusudi,uwezo huo pia unatumika ipasavyo kutengeneza fitna.Wengi watakumbuka namna Dokta Salim Ahmed Salim,mmoja wa wana-CCM waliokuwa wanawania kuchuana na Kikwete,alivyoundiwa zengwe kubwa na kumhusisha na kundi la Hizbu la huko Zanzibar.Inaelekea kuwa mbinu hizohizo zimeanza kutumika dhidi ya Dokta Slaa,na kuna kila sababu ya kuamini kuwa kuna mengi yatakayoibuliwa dhidi yake.
Salva Rweyemamu  (kushoto) na Gideon Shoo

Yayumkinika kuamini kuwa waandishi wa habari wanaotumiwa kumchafua Dokta Slaa na Chadema kwa ujumla wanafanya hivyo kwa minajili ya "kupeleka mkono kinywani".Kubwa zaidi ni sapoti ya Rostam kwa Kikwete.Wakati mwaka 2005 alijibidiisha ili kufanikisha maslahi yake binafsi ya kibiashara (na amenufaika kweli-kwa kuangalia ishu za Kagoda na Richmond/Dowans) safari hii Rostam anahaha kumzuia Dokta Slaa kwa vile anafahamu fika kwamba laiti mwanasiasa huyo wa Chadema anayesifika kwa msimamo wake mkali dhidi ya ufisadi akiingia Ikulu,zama za mafisadi kutumia jeuri yao ya fedha "kuendesha serikali kwa remote control" itakuwa imefikia kikomo.

Kwahiyo,Dokta Slaa na Chadema kwa ujumla wanapaswa kuelewa kuwa safari hii Rostam ana "special mission" ya kuhakikisha "survival (kusalimika) yake.Atatumia kila raslimali aliyonayo kuhakikisha Dokta Slaa haingii Ikulu.Anafanya hivyo akifahamu wazi kuwa rais yeyote mwenye kujali maslahi ya nchi yake "atamkalia kooni" mfanyabisahara huyo na washirika wake.

Hata hivyo,kwa vile si fedha za Rostam au wanahabari wake zitakazopiga kura kwenye uchaguzi mkuu,bali mimi na wewe pamoja na kila Mtanzania aliyechoshwa kuona nchi yetu ikigeuzwa "shamba la bibi",ni muhimu kwa wapiga kura kusema HAPANA.Tusitoe fursa kwa watu wenye maslahi binafsi kuipeleka nchi yetu kwenye maangamizi.Na ni muhimu zaidi kutambua kuwa baadhi ya watu hao wana utata wa kutosha tu kuhusu asili ya mahali walipozaliwa.Hiyo inamaanisha kuwa "wakishaiingiza Tanzania kwenye mtaro",watakuwa na sehemu ya kukimbilia.

KILA MTANZANIA MWENYE KUITAKIA MEMA NCHI YETU ANAPASWA KUPAMBANA NA WAHUNI WA KISIASA WANAOTAKA KUTUWEKEA MADARAKANI VIONGOZI WANAOWAMUDU NA HIVYO KUENDELEA KUTUFISADI KAMA ILIVYOKUWA KATIKA KIPINDI CHA MIAKA MITANO ILIYOPITA.


INAWEZEKANA,TIMIZA WAJIBU WAKO

22 Feb 2010

WAZIRI Mkuu Mizengo Pinda amewashauri wananchi wa Jimbo la Igunga mkoani Tabora wasimkatae Mbunge wao Rostam Aziz wakati wa uchaguzi mkuu ujao kwa kusikia maneno yanayosemwa bungeni, badala yake wazingatie kile alichowafanyia.

Wakati Pinda anampigia debe Mbunge huyo jana kwenye mkutano wa hadhara katika uwanja wa Kumbukumbu ya Sokoine, baadhi ya wananchi wa jimbo hilo walimwomba Waziri Mkuu amshinikize Mbunge wao abaki jimboni humo, kwa madai kuwa haonekani.

Wananchi hao walitoa ombi hilo ili waweze kupata fursa ya kumweleza kero zao na awaeleze yanayosemwa bungeni kuhusu yeye (Rostam)...ENDELEA



5 Dec 2009


TOFAUTI na alivyojigamba kwamba ni mlipaji mzuri wa madeni anayodaiwa na serikali, Mbunge wa Igunga, Rostam Azizi anadaiwa Sh. 2,576,583,013 tokea mwaka 1993, MwanaHALISI limegundua.

Alikopeshwa Sh. 2 bilioni (2,025,739,660) mwaka 1993 na 1997 na Mfuko wa Kuwezesha Uagizaji Bidhaa (CIS) uliokuwa ukifadhiliwa na serikali ya Japan na kusimamiwa na Wizara ya Fedha na Uchumi.

Alitumia makampuni ya Africa Tanneries Ltd, Tanzania Leather Industries Ltd na Africa Trade Development.

Fedha nyingine alizokopeshwa ni Sh. 1,516,024,125. Hizi alikopeshwa na serikali ili kuagiza mchele kupitia mpango wa Counterpart Fund. Alitumia Kampuni ya African Trade Development.

Imethibitika kwamba Rostam ameshindwa au hataki kulipa deni hilo lililodumu kwa miaka 16 sasa.

Akizungumza na vyombo vya habari 3 Mei 2009, siku ya uhuru wa vyombo vya habari duniani, kwenye Hoteli ya Kilimanjaro Kempinski jijini Dar es Salaam, Rostam alitamba kuwa ni mlipaji mzuri wa madeni yake kwa serikali.

Alikuwa akijibu tuhuma mbalimbali za ufisadi anaodaiwa kufanya kwa kutumia makampuni yake mbalimbali. Gazeti hili lina kumbukumbu za jinsi alichukua fedha hizo, zilizokusudiwa kuboresha biashara nchini.

Uchunguzi umebaini kuwa mwaka 1993 alichukua Sh. 280 milioni kupitia Kampuni ya African Tanneries Limited. Mwaka 1997 alitumia Kampuni ya Tanzania Leather Industries Limited kuchukua Sh. 725,943,120.

Mwaka huohuo Rostam alitumia Kampuni yake nyingine ya African Trade Development kubeba Sh. 1,019,796,540 kutoka mfuko huo.

Mwishoni mwa mwaka jana, baada ya ‘mshike mshike nguo kuchanika,’ Rostam alilipa Sh. 500 milioni akikusudia kupunguza deni la “mchele.”

Lakini kutokana na kuwepo deni jingine la zaidi ya Sh. 1bilioni katika mfuko wa CIS, mamlaka husika zikaamua kutumia kiasi hicho kupunguza madeni hayo.

Kwa sasa anadaiwa na mfuko huo Sh. 1.060,558,888. Deni hilo likijumlishwa na deni alilokopa kuagiza mchele, Rostam anadaiwa jumla ya Sh. 2,576,583,013. Katika mazungumzo yake na serikali kwa nyakati tofauti, alikiri na kuahidi kulipa ingawa hadi sasa ameendelea kukaidi kulipa.

MwanaHALISI limebaini kuwa tayari mmoja wa wanasheria jijini Dar es Salaam, anayeshughulikia suala la kukusanya madeni hayo anaandaa taarifa ya kisheria itakayokabidhiwa kwa wadeni sugu wakati wowote kuanzia sasa.

Jukumu jingine analotekeleza mtaalamu huyo wa sheria ni kumshauri Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha na Uchumi, kufanya mpango wa kutumia mamlaka ya Kamishna Mkuu wa TRA ili kutekeleza azma ya kufilisi mali za Rostam na vigogo wenzake wanaodaiwa.

Pamoja na Rostam, wadeni sugu wengine ambao walizungumza na serikali, wakakiri kudaiwa na wakaahidi kulipa madeni kwa kadri walivyoomba lakini badala ya kulipa wakaingia ‘mitini’ ni pamoja na Mbunge wa Temeke, Abass Mtemvu (CCM).

Mbunge huyo mwaka 1998 alitumia Kampuni ya A.M. General Agency kukopa Yen 20,000,000 sawa na Sh. 280 milioni. Ingawa alikiri kudaiwa na kuahidi kulipa deni, hadi sasa hajalipa hata shilingi moja.

Aliyewahi kuwa Waziri wa Utumishi na Mbunge wa Mlangege, Zanzibar, Fatma Said Ali (CCM), mwaka 1998 alitumia Kampuni ya Tanzania Save Way Co. Ltd., kukopa Yen 20,000,000 lakini akakopeshwa Yen 10,000,000 sawa na Sh.140 milioni. Aliwahi kupunguza Sh. 23,400,000 tu.

Aliyewahi kuwa mkuu wa mkoa wakati wa serikali ya awamu ya pili na ya tatu, ambaye sasa ni Mkuu wa Mkoa wa Manyara, Henry Shekiffu, mwaka 2000.

Alitumia kampuni ya Shemshi & Sons Limited kukopa Sh. 399,560,000. Amewahi kupunguza Sh. 65,340,051. Hadi sasa anadaiwa Sh. 279,653,794.

Nicodemas Banduka, mwaka 2000 alitumia kampuni ya Kadolo Investment kukopa Yen 105,210045 sawa na Sh. 147,294,630. Aliwahi kulipa Sh. 22,500,000. Hadi sasa anadaiwa Sh.124,794,630.

Mwingine ambaye arobaini zake zimekaribia ni aliyekuwa Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL), David Mattaka, aliyetumia kampuni ya Petmon Investment, mwaka 2000. Alikopa Sh. 140 milioni, aliwahi kupunguza Sh. 24,712,200. Hadi sasa anadaiwa Sh. 115.287,800.

Ufuatiliaji unabainisha kuwa idadi kubwa ya makampuni yaliyotumiwa na vigogo hao yalianzishwa kwa lengo la kuchota fedha hizo. Mengi kati ya hayo hayapo tena.

Vigogo wengine waliobainika kukopeshwa na CIS lakini taarifa hazielezi kama mali wanazomiliki pia zitafilisiwa, ni aliyekuwa mbunge wa Sengerema, Dk. William Shija ambaye sasa ni Katibu wa Umoja wa Mabunge ya Jumuiya ya Madola.

Alikopa Sh. 140 milioni kwa kutumia kampuni ya Pyramid Investments Limited, mwaka 2000. Amewahi kupunguza Sh. 22,650,000.

Waziri wa Kilimo, Chakula na Ushirika, Steven Wassira, naye jina lake limo kwenye orodha ya wanaodaiwa ingawa taarifa muhimu, mathalani alikopa kiasi gani, lini na amelipa au bado hazionyeshwi katika kumbukumbu hizo.

Ingawa serikali inaelezwa kuwa kwenye hatua za kukamilisha mipango ya kufilisi mali za wadeni wake hao na wengine, bado inasuasua.

Mkataba wa kufanikisha mikopo hiyo unaruhusu serikali kupitia kwa Kamishna Mkuu wa TRA kufilisi mali za asiyetekeleza mkataba katika kipengele cha kulipa, tena bila kulazimika kwenda mahakamani. Haijafahamika kwa nini TRA haijachukua hatua hiyo.

Dhana inajengeka kwamba huenda “kigugumizi” hicho katika kukusanya madeni ya walipa kodi wa Tanzania, kinatokana na wadaiwa wengi kuwa vigogo ambao miongoni mwao bado wapo kwenye nyadhifa za juu serikalini.

CIS ilianzishwa kwa nia njema ya kukuza sekta ya biashara nchini, kwa kuwasaidia wafanyabiashara kufanya biashara za kimataifa. Kuagiza bidhaa mbalimbali kutoka nchi tofauti, zilizofadhili mpango huo.

Mpango huo ulikuwa ukitekelezwa chini ya usimamizi wa Wizara ya Fedha na Uchumi. Hata hivyo taarifa zinaonyesha kuwa jumla ya Sh. 44 bilioni zilichotwa na wizara nane katika mazingira ambayo hadi sasa serikali haijafafanua.

CHANZO: Mwanahalisi

INAUDHI,INAUMA NA KUSONONESHA LAKINI IT LOOKS AS IF NCHI HAINA WENYEWE KWANI WALIOIBIWA WAKO KIMYA KANA KWAMBA WAMERIDHIKA.JE TUMEKUBALI UFISADI KUWA SEHEMU YA MAISHA YETU YA KILA SIKU?

20 Jun 2009


Orodha ya wabunge bubu bungeni yawekwa hadharani

Na Leon Bahati

WAKATI tukielekea mwaka wa lala salama wa Bunge la mwaka 2005-2010, huku baadhi ya wabunge wakiibuka mashujaa kwa kutoa michango mizito inayoitingisha serikali, imebainika kuwa baadhi yao hadi sasa hawajawahi kuuliza hata swali moja wala kuchangia.

Uchunguzi huo umefanywa na Mwananchi Jumapili kwa msaada wa tovuti ya bunge ambako kila mchango wa mbunge hurekodiwa kwa kuonyesha swali la msingi au la nyongeza alilouliza, majibu yake na mchango aliotoa.

Kati ya wabunge 319 walioko katika Bunge la sasa ambao hawajawahi kuuliza maswali ya msingi wanakadiriwa kufikia 50 na wasiouliza maswali ya msingi wala nyongeza ni zaidi ya 30.

Mawaziri na wabunge ambao pia ni wakuu wa mikoa, hawajahusishwa kwenye hesabu hizo kwa sababu wapo upande wa serikali na wote wamekuwa hawaulizi maswali. Wengine ambao hawakuhusishwa kwenye vipengele hivyo ni Spika na Naibu Spika, lakini wote wameonyeshwa kuwahi kuchangia hoja mbalimbali.

Kwa mujibu wa mtandao huo, Mbunge wa Igunga, Rostam Aziz ndiye pekee ameonyeshwa kuwa hajawahi kuuliza swali lolote wala kuchangia jambo lolote tangu Bunge limeanza.

Wabunge wengine ambao wameonyeshwa hawajawahi kuuliza maswali, lakini wamekuwa wakichangia hoja mbalimbali nao ni Yusuf Makamba (Katibu Mkuu wa CCM); John Shibuda, Harith Mwapachu, Ali Haji Ali, Omar Sheha Musa, Abdallah Sumry, Gideon Cheyo, Juma N’hunga, Nazir Karamagi, Anna Abdalah, Ali Haji Ali, Thomas Mwang’onda, Salum Khamis Salum, Hassan Rajabu Khatibu na Felix Mrema.

Wengine ni Philemon Sarungi, Edward Lowassa, Andrew Chenge, Abdisaalam Issa Khatib, Dk Ibrahim Msabaha, Zakia Meghji, Kingunge Ngombale Mwiru, Salimu Yusufu Mohamed, Salum Ahamed Sadiq, Omar Sheha Mussa, Manju Msambya na Benedict Ole-Nangoro.

Wabunge ambao pia ni wakuu wa mikoa ufanisi wao wa kuchangia bungeni ni mdogo ni Abdul Aziz – Iringa (7); Dk James Msekela – Dodoma (6); Monica Mbega – Kilimanjaro (3); Dk Christine Ishengoma-Ruvuma (4) na William Lukuvi – Dar es Salaam (3). Katibu Mkuu wa CCM, Yusuf Makamba aliwahi kutoa michango bungeni mara mbili tu.

Katika Kundi la wabunge 13 wanaoongoza kwa kuuliza maswali ya msingi linaongozwa na Mgana Msindai (CCM) mwenye maswali 34 na kufuatiwa na William Shellukindo (29); Diana Chilolo (28), Paschal Degera (28), George Lubelege (25), Raphael Mwalyosi (24) na Mhoga Ruhwanya (23).

Wabunge wengine kwenye kundi hilo wana maswali 22 kila mmoja nao ni, James Msalika, Job Ndugai, Zitto Kabwe, Herbert Mtangi, Victor Mwambalaswa na Lucy Owenya.

Wabunge 11 vinara wa kuuliza maswali ya nyongeza ni Dk Wilbrod Slaa (71), Hamad Rashid Mohamed (71), Mgana Msindai (67), Esther Nyawazwa (58), George Lubelege (56), Diana Chilolo (54), Hafidh Ali Tahir (52), Geofrey Zambi (50) na wawili waliofungana kwa kuuliza 49, Jenista Mhagama na John Kilimba (49).

Katika kundi la kutoa michango mbalimbali kwenye vikao vya bunge linaongozwa na Naibu Spika Anne Makinda (495); akifuatiwa na Spika, Samweli Sita (494). Wengine ni Jenister Mhagama (193); Job Ndugai (147); Zitto Kabwe (125); Dk Slaa (106); Andrew Chenge (89); Suzan Lyimo (87); William Shelukindo (77); Geofrey Zambi (73); John Kilimba (69) na mawaziri wawili waliofungana kwa kufikisha michango 67 ambao ni Shamsa Mwangunga, Waziri wa Maliasili na Utalii na Waziri wa Miundombinu, Dk Shukuru Kawambwa.

Mawaziri wengine wanaofuatia ni Dk Mary Nagu (64); Profesa David Mwakyusa (59); William Ngeleja (50); Mwanasheria Mkuu wa Serikali; Johnson Mwanyika (47); Dk Makongoro Mahanga (45); Profesa Jumanne Maghembe (45); Stephen Wasira (41) na John Chiligati (40).

Akizungumzia kuhusu kumbukumbu hizo wiki iliyopita, Katibu wa Bunge, Dk Thomas Kashililah alisema kuwekwa kwa taarifa hizo hakuna maana zaidi ya kuweka kumbukumbu za michango ya wabunge, lakini akasema kulikuwa na marekebisho kwa wakati huo.

Alipotafutwa tena jana, alisema tovuti hiyo ya Bunge imefanyiwa marekebisho makubwa ili wananchi waweze kupata kwa undani kumbukumbu mbalimbali za vikao vya Bunge.

Pamoja na maboresho hayo, Dk Kashililah alisema: "Tuna mpango wa kuongeza maboresho zaidi yakiwepo ya kuwezesha watu kufuatilia vikao vya Bunge kupitia tovuti hiyo."

Licha ya baadhi ya wabunge kuwa na mchango hafifu, Bunge la sasa limeonekana kuwa mwiba mkali kwa viongozi serikalini hususan mawaziri, kutokana na baadhi ya wabunge kuwabana katika mambo mbalimbali ya utendaji mbovu na ufisadi, huku kufupishwa kwake kukipunguza nafasi ya kuuliza maswali na kuchangia kwa baadhi yao ambao walikuwa hawajafanya hivyo.

Katika kipindi hicho miongoni mwa hoja nyingine zilizosisimua ni mjadala wa Kamati Teule ya Bunge iliyoongozwa na Dk Harrison Mwakyembe kuhusu utoaji wa zabuni ya umeme wa dharura iliyotolewa kwa kampuni ya Richmond Development Limited (LLC); na kusababisha Rais Jakaya Kikwete kuvunja baraza la mawaziri baada ya aliyekuwa Waziri Mkuu, Edward Lowassa kujiuzulu pamoja na mawaziri wengine wawili.


CHANZO: Mwananchi

11 May 2009


HIVI KARIBUNI,WAZIRI WA NCHI OFISI YA RAIS (MENEJIMENTI NA UTUMISHI WA UMMA),USTAADHA HAWA GHASIA,ALITOA ONYO KALI DHIDI YA WATU WANAOJIHUSISHA NA KILE ALICHOKIITA "WIZI WA NYARAKA ZA SERIKALI".NISINGEPENDA KUREJEA REACTIONS MBALIMBALI ZILIZOTOKANA NA KAULI HIYO LAKINI MMOJA YA SAUTI ZILIZOPINGA VIKALI TAMK HILO LA GHASIA NI MBUNGE WA KARATU NA KATIBU MKUU WA CHADEMA,DR WILBROAD SLAA.MWANASIASA HUYO NGULI WA MAPAMBANO DHIDI YA UFISADI ALIELEZA WAZIWAZI KWAMBA NYARAKA ZINAZOFICHA UFISADI HAZIPASWI KUWEKWA KWENYE KUNDI LA NYARAKA ZA SIRI ZA SERIKALI.DR SLAA ALIELEZA BAYANA KWAMBA PINDI AKILETEWA NYARAKA ZA AINA HIYO ATAZIMIA PASI UOGA KWA VILE NI KWA NJIA HIYO NDIO TUMEFANIKIWA KUBAINI SKANDALI KAMA ZA EPA,RICHMOND NA NYINGINEZO.


NI DHAHIRI TAMKO LA WAZIRI GHASIA LILENGA KUWATISHA WATU KAMA DR SLAA.LAKINI PIA WAZIRI HUYO ALIFANYA HIVYO KWA VILE NI MIONGONI MWA VIONGOZI WA SERIKALI WENYE DHAMANA NA MASUALA YANAYOHUSU IDARA MBALIMBALI ZA SERIKALI.


BILA KUUMAUMA MANENO,HEBU TUJIULIZE: HIVI ROSTAM AZIZ ALIPOITISHA PRESS CONFERENCE YAKE NA KUTOA "USHAHIDI" MBALIMBALI KUPIGILIA MSUMARI HOJA YAKE KUWA REGINALD MENGI (MWENYEKITI MTENDAJI WA MAKAMPUNI YA IPP) NI FISADI NYANGUMI,ALIZIPATAJE NYARAKA MBALIMBALI ZINAZOPASWA KUWA KATIKA HIFADHI YA TAASISI HUSIKA ZA SERIKALI?

ROSTAM SI MTUMISHI WA MAMLAKA YA MAPATO AU MWAJIRIWA KATIKA WIZARA YA FEDHA KIASI CHA KUWA NA "DATA" ALIZOTOA KUHUSU MENGI.NA KWA VILE MAMLAKA HUSIKA ZIMEKUWA KIMYA KUHUSU WAPI MBUNGE HUYO WA IGUNGA ALIPATA NYARAKA HIZO NI WAZI KWAMBA ALIPATIWA KWA RIDHAA YA WAHUSIKA.

WATETEZI WA ROSTAM,KUANZIA WAZIRI SOPHIA SIMBA NA KAPTENI GEORGE MKUCHIKA WAMEKUWA KIMYA KABISA KUKEMEA "HUKUMU" ALIYOTOA ROSTAM DHIDI YA MENGI TOFAUTI NA WALIVYOKURUPUKA MARA BAADA YA KIPENZI CHAO KUTAJWA KUWA NA MENGI KUWA NI FISADI PAPA.BY THE WAY,MENGI SI MTU WA KWANZA KUMTUHUMU ROSTAM KUWA NI FISADI.HIYO NI OPEN SECRET,NA KINACHOKWAZA WATU HAWA KUCHUKULIWA HATUA NI NJAA TU ZA HAO WENYE WAJIBU WA KUFANYA HIVYO ZINAZOKIDHIWA NA JEURI YA FEDHA ZA MAFISADI HAO.

SASA,SIJUI WAZIRI GHASIA ANAWEZA KUTUELEZA NINI KUHUSU WIZI WA NYARAKA ZA SERIKALI ULIOFANYWA NA ROSTAM.NAUITA WIZI KWA VILE ROSTAM SIO TRA,DPP,MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI AU TAASISI YOYOTE YA SERIKALI YENYE DHAMANA YA KUWA NA NYARAKA ZILIZOTUMIWA NA MFANYABIASHARA HUYO KWENYE "KUJENGA KESI" YAKE DHIDI YA MENGI.

SASA NAELEWA KWANINI ROSTAM ANAWEZA KU-WISH ASINGEJIBU HOJA ZA MENGI KWANI WATAPOFIKA MAHAKAMANI ANAPASWA KUULIZWA YEYE ALIKUWA NA NYARAKA HIZO KAMA NANI?ALIZIPATAJE?NA JE KUWA NAZO SIO KOSA (KWA KUREJEA "MKWARA" WA WAZIRI GHASIA?

NA HIYO NI NJE YA TAARIFA ZA KUAMINIKA KUWA NYINGI YA DATA ALIZOTUMIA ROSTAM NI "MAKANJANJA" (FAKE DATA) AMBAPO WAJANJA WA MJINI WALIPOSIKIA KUNA TENDA YA FEDHA NYINGI YA KUWEZESHA KUPATIKANA KWA INCRIMINATING EVIDENCE DHIDI YA MENGI WAKACHANGAMKIA TENDA HIYO LAKINI KATIKA HALI YA UFISADI.WHY NOT,KUMFISADI FISADI NI SAWA KABISA NA KULIPA KWA NOTI BANDIA MANUNUZI YA CHENI ILIYOTENGENEZWA KWA DHAHABU FEKI.


MWISHO,NAPENDA KUSISITIZA KWAMBA SINA CHUKI NA ROSTAM AU MTANZANIA YEYOTE MWENYE ASILI YA NJE YA NCHI.ILA SIFICHI UKWELI KWAMBA NINA ZAIDI YA CHUKI,HASIRA,DUA BAYA (NA MENGINE NISIYOWEZA KUTAJA HAPA) DHIDI MAFISADI.UTETEZI WA KIPUUZI WA MAFISADI UMEKUWA KWENYE VITU KAMA RANGI,DINI,KABILA,NK.MTAKUMBUKA MKURUGENZI WA IPC,EMMANUEL OLE NAIKO ALIZONGWA KUHUSU KWANINI ALITOA KIBALI CHA UWEKEZAJI KWA KAMPUNI YA KITAPELI YA RCHMOND,KIMBILIO LAKE KUU LILIKUWA UKABILA.ETI "NAANDAMWA KWA VILE NATOKA ENEO MOJA NA LOWASSA"!

LEO HII AKINA ROSTAM,MANJI,SOMAIYA,JEETU NA SUBASH WANATAKA KUTUAMINISHA KUWA TUHUMA DHIDI YAO ZINACHANGIWA NA "UTANZANIA" WAO WENYE ASILI YA NJE YA NCHI.HUU NI UTETEZI MUFILIS NA NI WA KIFISADI KAMA WANAVYOTUHUMIWA.HIVI WANATAKA KUTUAMBIA KUWA TULIPOPAMBANA NA MKOLONI,MJERUMANI NA MWINGEREZA TULIKUWA WABAGUZI WA RANGI?

10 May 2009

PICHANI,NI MBUNGE WA IGUNGA,ROSTAM AZIZ,AKIKABIDHI KINACHODAIWA KUWA DOSSIER LENYE TUHUMA DHIDI YA MFANYABIASHARA RAGINALDMENGI.ANAYEKABIDHIWA NI AFISA UCHUNGUZI WA TAKUKURU GWAKISA.Picha hii ni kwa mujibu wa gazeti la The African.

HUU NI NI UPUUZI.YAANI HAINGII AKILINI HATA KIDOGO.JAMANI,HIVI LINI MMEWAHI KUONA TAKUKURU WAKIKABIDHIWA USHAHIDI/TUHUMA MBELE YA VYOMBO VYA HABARI AS SEEN IN THE PICTURE ABOVE?

HUYU ROSTAM AMEKUWA MITHILI YA MUNGU MTU: ALIPOTAJWA TU NA MENGI,MAWAZIRI WAZIMA NA BUSARA ZAO (SOPHIA SIMBA NA KAPTENI MKUCHIKA) WAKALIPUKA KUMTETEA (JAPO SASA WAMEKAA KIMYA ROSTAM ALIPORUDIA KILEKILE ALICHOFANYA MENGI).KISHA TAKUKURU NAO KATIKA HALI INAYOONYESHA NAMNA GANI TAASISI HIYO NI WABABAISHAJI WA DARAJA LA JUU WAKAANDAA MITHILI YA PRESS CONFERENCE YA KUMPOKEA ROSTAM NA KINACHODAIWA KUWA NI USHAHIDI WAKE DHIDI YA MENGI (JAPO KUNA MADAI KUWA WAJANJA WAMEMWINGIZA MJINI KWA KUMUUZIA "CHENI BANDIA"-ISOMEKE DATA FEKI).

HAWA TAKUKURU NI WAZEMBE ZAIDI YA WAZEMBE.HIVI UBABAIKAJI KAMA HUO WALIOFANYA KWA ROSTAM WANGEUELEKEZA KWA KAGODA SI TUNGEPIGA HATUA FLANI?AU WANGEKUWA "FASTA" NAMNA HIYO KATIKA,SIO KUITETEA BALI KUICHUNGUZA IPASAVYO KAMPUNI YA RICHMOND,KWA HAKIKA TUSINGEKUWA HAPA TULIPO SASA.

MBONA WENZETU MNAJIDHALILISHA KIASI HICHO?NI HIZO FEDHA ZA ROSTAM AU NJAA ZENU?THIS IS MORE THAN TOO MUCH.IT'S ABSURD,CRAZY AND UTTERLY NONSENSE.

8 May 2009


Dar es Salaam, Tanzania (PANA) 16/09/2005- Tanzania's controversial opposition leader, the Reverend Christopher Mtikila alleged Friday that ruling Chama cha Mapinduzi (CCM) presidential candidate Jakaya Kikwete had used funds from Iran to defeat his opponents at the party's recent convention.

The Chairman of the Democratic Party claimed at a press conference that the Iranian government through Tanzanian MP Rostam Aziz, had funded Kikwete's campaign for over 10 years.

The press conference was held ahead of a meeting by eight opposition parties to plan a common strategy against the CCM in Tanzania's October elections.

Mtikila alleged that the Iranian government had set aside a substantial amount to prop presidential candidates in countries where the Asian country has economic interests.

Aziz, a Tanzanian of Iranian extraction is representing Igunga constituency in Tanzania's Union Parliament on the platform of the CCM.

Mtikila did not say how much Aziz had allegedly received from the Iranian government for Kikwete's presidential campaign, but cited Tanzania's uranium deposit as possible motivation for the alleged assistance.

He said the Iranian government could not have given Aziz money for nothing: "they must be harbouring interests in Tanzania."

This is the second time that Aziz, Kikwete's campaign manager, would be accused of securing foreign funds for Kikwete's presidential campaign.

Last April, London-based journal, Africa Confidential claimed that he had been given two million US dollars by the Oman government as campaign funds for Kikwete.

Kikwete, Tanzania's Foreign Affairs and International Co-operation Minister had vowed to sue the journal over the report, but since his nomination as CCM presidential candidate in May, he has said nothing about the report.

The London journal has challenged him to go to court insisting it has overwhelming evidence to back its claims.

There was no immediate reaction to Mtikila's allegations from either Aziz or Kikwete.


SOURCE: PANAPRESS

NA KUNA MJADALA UNAENDELEA HUKO JAMII FORUMS KUHUSU URAIA WA BWANA ROSTAM AZIZ.


5 May 2009








CHANZO: Jamii Forums


4 May 2009


MWANASIASA MAKINI ANAPASWA KUCHUNGA ULIMI WAKE.ANAPASWA PIA KUELEWA KWAMBA LOLOTE LITOKALO MDOMONI MWAKE LAWEZA KUTAFSIRIWA KUWA NI KAULI YA SERIKALI.

KWA MAANA HIYO,KAULI ZA SOPHIA SIMBA NA GEORGE MKUCHIKA KUMTETEA ROSTAM AZIZ WAZIWAZI ZIMEWAFANYA WANANCHI WENGI KUWAONA MAWAZIRI HAO KAMA VIBARAKA WA ROSTAM,MFANYABIASHARA NA MWANASIASA ANAYEHUSISHWA NA TUHUMA LUKUKI ZA UFISADI.

SOPHIA SIMBA NA MWENZIE MKUCHIKA WALILIPUKA KUMTETEA ROSTAM PASIPO KUELEWA KWAMBA MHINDI HUYO NAE ALIKUWA ANA MPANGO WA KUJIBU SHUTUMA ZA MENGI.NA KATIKA KUJIBU SHUTUMA HIZO,ROSTAM AMEJIGAMBA KUWA MENGI AMEKEMEWA NA WAZIRI SIMBA NA MKUCHIKA.

HIVI WATU WAZIMA HAWA NA AKILI ZAO HAWAONI KUWA WAMEDHALILISHWA?YAANI INA-SOUND AS IF WALITUMWA NA ROSTAM IN THE FIRST PLACE KABLA YA MTUHUMIWA HUYO WA UFISADI KUITISHA PRESS CONFERENCE.MAWAZIRI WAZIMA WANA-ACT AS IF NI SPOKESPERSONS WA,SIO SERIKALI,BALI MHINDI FLANI MWENYE FEDHA?

BAADA YA PRESS CONFERENCE YA ROSTAM HAPO JANA,BAADHI YA WATU WANAULIZA "YUKO WAPI SOPHIA SIMBA?YUKO WAPI MKUCHIKA?" WAKITARAJIA MAWAZIRI HAO WATAMTENDEA HAKI MENGI KWA KUMKEMEA ROSTAM.HAWANA JEURI WALA UBAVU HUO.SIMPLY BECAUSE KAMA KUITWA FISADI PAPA KWA MHINDI HUYU KULIWAKURUPUA KUROPOKA WALIYOSEMA,NI DHAHIRI KUWA ROSTAM AKIKOHOA TU NA WAO WANALIPUKA.UJASIRI HUO WA KUMKEMEA WATOE WAPI.NA KATIKA SIASA HIZI ZA KIMAFIA ZILIZOLETWA NA WANAMTANDAO,MWANASIASA YEYOTE ATAKAYETHUBUTU KUMGUSA THE DON,MR UNTOUCHABLE,BASI NAYE ATACHAFULIWA.

YOTE HIYO NI TAMAA YA MADARAKA.WAKO RADHI KUUZA UTU WAO KWA AJILI YA KUMPIGIA MAGOTI FISADI FLANI AWASDAIDIE KUFIKIA MALENGO YAO.NA SI SOPHIA SIMBA NA MKUCHIKA PEKEE,KUNA WENGI TU WANAOWAOGOPA MAFISADI KWA VILE NDIO WALIOFADHILI HARAKATI ZAO ZA KISIASA.

HALAFU HAWA NDIO WA KUWATEGEMEA KUTULETEA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA?LABDA MAISHA BORA KWA MAFISADI NA VIBARAKA WAO!

SHAME ON THEM!


NA KUNA BOMU JINGINE LA ASKARI WASTAAFU.KILA NISOMAPO HABARI KUWA WASTAAFU WA JESHI WANAZUNGUSHWA KUHUSU MAFAO YAO,NAPATWA NA UOGA FLANI KWAMBA WASIJE KUAMUA KUTUMIA UJUZI WAO WA KIJESHI KUDAI HAKI ZAO.
NA NIPITAPO PALE MWENGE KWENYE FLATS ZA JESHI NA KUANA NAMNA "ZILIVYOCHOKA" NAPATWA NA HOFU NYINGINE SIKU WAUNGWANA HAWA WATAKAPOAMUA KUDAI KWA NGUVU MAISHA BORA KAMA YALE YA VIGOGO KULE MASAKI,MIKOCHENI,OYSTERBAY,NK.TALKING OF OYSTERBAY,NAPATA KUMBUKUMBU YA YALE MAHEMA WANAYOISHI ASKARI POLISI KATIKA "KAMBI" ILIYO JIRANI NA KITUO CHA POLISI OYSTERBAY.
BOMU JINGINE NI HAO MGAMBO AMBAO KULA NA ANASA ZAO ZINATEGEMEA KUVUNJA HAKI ZA BINADAMU ZA WAMACHINGA,WANAODIWA KODI ZA MANISPAA/HALMASHAURI NA WANYONGE WENGINE.MOST OF MGAMBO HAWA HAVE NO IDEA WHATSOEVER KUHUSU HUMAN RIGHTS.WANACHOJUA WAO NI PIGA,NYANG'ANYA,TAIFISHA!HAWA NI VIUMBE HATARI ZAIDI KWA VILE MAISHA YAO KWA KIASI KIKUBWA YANATEGEMEA UBABE WAO DHIDI YA WANYONGE WAO.KWA MFANO,MARA NYINGI LUNCH ZAO NI VYAKULA WANAVYOWAPORA MAMA NTILIE NA VITOWEO WANAVYORUDI NAVYO BAADA YA KUMALIZA KAZI NI VILEVILE WANAVYOWAPORA WANANCHI WANAOJITAFUTIA RIDHIKI ZAO HALALI.
KUNA MTU AMENINONG'ONEZA SOMETHING HE CALLED FACTS ETI HUO MLIPUKO WA MABOMU NI HUJUMA.I DIDNT TAKE HIM SERIOUS KWA VILE ALIKUWA AMEONJA KILEVI KIDOGO.HE WENT FURTHER TO ARGUE KWAMBA VIRUSI (VIRUS) WA HUJUMA WAMEANZA KUSAMBAA KUTOKA KWA MAFISADI KWENDA KWA PROFESSIONALS WALIOSAHAULIKA AU KUTELEKEZWA.REASONS HE CITED,KAMA MZEE WA VIJISENTI AMEJICHOTEA BILIONI ZAKE KADHAA NA BADO HAJAGUSWA,AU MAJAMBAZI WA RICHMOND BADO WANAPETA LICHA YA KUBAINISHWA NA KAMATI YA MWAKYEMBE,NA DOWANS NAO WANAENDELEA NA JEURI YA KUIPELEKA TANESCO MAHAKAMANI LICHA YA HIZO MILIONI MIA NA USHEE PER DAY WALIZOZAWADIWA,WAMILIKI WA KAGODA WAMEENDELEA KUWA GHOSTS WASIOTAJIKA,THEN MTU YEYOTE ANWEZA KUSHAWISHIKA KUWA FISADI,MHUJUMU WA UCHUMI AU USALAMA,AU MLIPUA MABOMU!DRUNK AS HE WAS BUT THIS KINDA MADE SENSE TO ME!
KUNA BOMU JINGINE KUBWA ZAIDI YA HAYO HAPO JUU,AU ZAIDI YA HAYO YALOKWISHALIPUKA.KWA UPANDE MMOJA NI RESERVE ARMY OF LABOUR,INAYOZALISHWA NA UBINAFSISHAJI,KUPUNGUZA MATUMIZI,"KEEP CITY/TOWN CLEAN OPERATIONS" (KAMA HIZO ZA MGAMBO ZINAZOISHIA KUWAFANYA WAMACHINGA WAJIULIZE "TUFANYE NINI ILI TUSIBUGHUDHIWE,AU TUWE WAPORAJI?"),WAKULIMA WALIOFIKIA HATUA YA KUTAFSIRI KUWA KILIMO NI SAWA NA KIFUNGO BCOZ CO-OPS HAZITAKI KULIPA MADENI HUKU WASSIRA NA WIZARA YAKE WAKIWA KWENYE SUINGIZI WA PONO KUHUSU KUTAFUTA MASOKO KWA WAKULIMA,NA MAKUNDI KAMA HAYO.KWA UPANDE MWINGINE NI WANANCHI WALALAHOI WANAOSIKIA NAMNA MAFISADI WANAVYOWADHIHAKI KWA PRESS CONFERENCES HUKU WAKITETEWA NA BAADHI YA VIONGOZI,WANANCHI WALIOCHOSHWA NA DANADANA ZA KUMWEKA WAZI MMILIKI WA KAGODA,WALIOKATISHWA TAMAA NA AHADI BAADA YA AHADI KUWA MAISHA BORA YAKO NJIANI (AS WE APPROACH THE GENERAL ELECTION,THEY WOULD KEEP ON REMINDING US THAT WE ARE NOW APPROACHING THE MAISHA BORA DESTINATION,EVERYBODY SHOULD REMAIN SEATED TILL WE ARRIVE i.e. BAADA YA GENERAL ELECTION,MEANING RETURNING THEM TO POWER AND GOING BACK TO SQUARE ONE.IF THEY BOTHER GIVING EXCUSES AS TO WHY IT'S FEBRUARY 2011 AND WE ARE YET TO ARRIVE AT MAISHA BORA,THEY WOULD PROBABLY SAY "OH,TUMEPOTEA NJIA.MSIHOFU TUTAFIKA MUDA SI MREFU...."
MABOMU HAYA NILIOBAINISHA KWENYE STORI HII NI HATARI ZAIDI KULIKO HAYO YANAYOLIPUKA HUKO MBAGALA.YATAKAPOLIPUKA,SI TUME YA MKUU WA MAJESHI WALA NGONJERA ZA "TUTALIPA FIDIA" ZITAKAZOWEZESHA KUREJESHA HALI KWENYE UTULIVU.THE TIME IN NOW.IT'S NOW OR NEVER!

ANYWAY,HEBU TUSIKIE HADITHI ZA ROSTAM KUHUSU TUHUMA ZILIZOTOLEWA (NA REGINALD MENGI) DHIDI YAKE NA WAHINDI WENZIE KWAMBA WAO NI MAFISADI PAPA.

Rostam amlipua Mengi, amwita nyangumi wa ufisadi


Ramadhan Semtawa na Salim Said


MFANYABIASHARA wa jijini Dar es salaam, Reginald Mengi aliwabatiza wafayabiashara wenzake watano jina la "mapapa wa ufisadi", na sasa mmoja wa waliotuhumiwa amejibu mapigo kwa kumbatiza jina la "nyangumi wa ufisadi".


Rostam Aziz, ambaye ni mmoja wa wafanyabiashara watano waliotuhumiwa na Mengi kuwa mapapa wa ufisadi, jana alitoa mlolongo wa tuhuma za ufisadi dhidi ya mwenyekiti huyo mtendaji wa makampuni ya IPP, na kueleza kuwa atawasilisha vielelezo kwa vyombo husika ndani ya saa 48 ili Mengi aanze kuchunguzwa.


Mapigo ya Rostam, ambayo yanazidi kupandisha joto la vita hiyo ya maneno, yametokana na tuhuma nzito ambazo Mengi alizitoa Aprili 23 wakati alipotaja wafanyabiashara watano akitaka wadhibitiwe mapema, akiwemo mbunge huyo wa
Igunga. Tofauti na Mengi ambaye hakutoa vielelezo na kusema yuko tayari kupandishwa kizimbani ili ukweli udhihirike, Rostam aliorodhesha tuhuma nyingi na kuahidi kuzikabidhi kwenye vyombo vya serikali ili hatua zichukuliwe. Huku akimtaja Mengi kwa majina yote matatu kila wakati, Rostam, aliwaambia waandishi jana akisema: "... nataka niweke wazi kwamba tuhuma zote zilizotolewa na Mengi dhidi yangu ni za uongo na ni upuuzi mtupu. Tuhuma hizo ni mwendelezo wa wimbo ule ule ambao amekuwa akiuimba kwa muda mrefu sasa na tayari nilikwishazitolea kauli huko nyuma.


"... nimeamua kuitisha mkutano huu ili kuwaeleza, na kupitia kwenu kuwaelimisha Watanzania, wamjue Reginald Abraham Mengi katika sura yake halisi na dhamira yake chafu na ovu, na kumtambua kwamba mtu huyu ni nyangumi wa ufisadi katika nchi hii," alisema Rostam katika moja ya aya zake za utangulizi. Nyangumi ni samaki wa baharini aliye mkubwa kuliko papa. Rostam alianza kwa kuorodhesha matukio 10 ya ugomvi ambayo anadai Mengi aliuanzisha dhidi ya watu mbalimbali, kuanzia maaskofu hadi kikundi cha uchekeshaji, wakati kwa mujibu wa Rostam maslahi ya Mengi ya kibiashara yalipoingiliwa na baadaye kuyageuza kuwa ni ugomvi wa nchi nzima.


"Sasa ameanzisha ugomvi na mimi baada ya kuona kwamba mimi nimekuwa mshindani wake mkubwa katika umiliki wa vyombo vya habari hapa nchini, anataka kuufanya ugomvi wa nchi nzima," anaeleza Rostam. Akiorodhesha tuhuma za ufisadi dhidi ya Mengi, Rostam alidai mwenyekiti huyo wa IPP alianza kuifilisi nchi kwa kushiriki kwenye vitendo vilivyochangia kuifilisi Benki ya Taifa ya Biashara (NBC) na kusababishwa iuzwe "kwa bei poa".


Alidai kuwa Mengi, akitumia kampuni yake ya Anche Mwedu Ltd katika miaka ya themanini, alichukua mkopo wa fedha NBC na amegoma kulipa hadi leo, huku akilazimisha suala hilo lifikishwe mahakamani. Rostam alidai kuwa mkopo wa kwanza uliotolewa kupitia hati ya maandishi ya makubaliano, ulifikia jumla ya Sh3.2 bilioni na kwamba hadi Januari mwaka 1996 ulifikia riba ya Sh 1.7 bilioni.


Alidai mkopo wa pili chini ya kampuni hiyo ulikuwa wa mpango wa Loan Agreements na ulihusu jumla ya Sh386,746,631.06 hadi kufikia Januari 1996. Akiongeza kudai kuwa mkopo wa tatu ulikuwa chini ya utaratibu wa udhamini wa serikali (government guarantee) ambao ulikuwa wa jumla ya Sh1,803,137,210 hadi kufikia Januari 1996. Rostam alidai kupitia utaratibu mwingine, Mengi alichukua mkopo mwingine ambao ulihusu jumla ya Sh417.6 milioni hadi kufikia Januari 1996.


"Jumla ya fedha zote za NBC ambazo amekuwa akidaiwa Mengi kupitia kampuni yake ya Anche Mwedu Limited (AML) hadi kufikia Januari 1996 zilikuwa ni Sh 5.8 bilioni, fedha hizi hadi kufikia sasa 2009 pamoja na riba zinafika takriban Sh28 bilioni," alidai Rostam huku akitaka akaunti za benki ambazo mikopo hiyo ilipitia. "Hivi ndivyo Mengi alivyochangia kuifilisi NBC, benki ya wananchi masikini wa Tanzania. Fedha hizi zilizochukuliwa na Mengi Sh28 bilioni zinaweza kujenga shule za sekondari 100 ambazo zingeweza kuwanufaisha watoto wa kimaskini wa Tanzania." Rostam pia alidai kuwa Mengi aliteketeza Sh2.5 bilioni kwa kutumia kampuni ya uwekezaji ya wazalendo ya NICO, kwa kununua hisa za kiwanda cha Interchem Pharma Ltd kinachomilikiwa na familia yake ambacho Rostam alidai kuwa Mengi alijua kuwa kingekufa.


"Huku akijua hali mbaya ya kiwanda hicho alitumia nafasi yake kuziteketeza Sh2.5 bilioni fedha za Watanzania masikini wasiopungua 22,000 wenye hisa NICO kwa kuifanya inunue asilimia 51 ya hisa. Kiwanda hicho sasa kimewekwa kwenye orodha ya kufilisiwa baada ya kushindwa kujiendesha chini ya mwaka mmoja tokea Mengi kuizamisha NICO," alisema. Rostam, ambaye pia ni mjumbe wa Halmashauri Kuu na Kamati Kuu ya CCM, pia alidai Mengi kwa kutumia mpango wa Mfuko wa Kuagiza Bidhaa kutoka Nje (Commodity Import Support-CIS), alichukua fedha nyingi kupitia msaada wa nchi wafadhili, lakini hadi jana alikuwa hajazilipa.


Rostam alikiri kwamba wafanyabiashara wengi akiwemo yeye walikopa, lakini wamelipa na wanaendelea kulipa hadi sasa na kuongeza kwamba Mengi "anayejidai ana uchungu na Watanzania amekuwa akiwaongezea umasikini kwa kuchota fedha hizo baadaye kuruka na kukataa kuzilipa". Rostam pia alitoa mchanganuo huo wa fedha za CIS ambazo alidai Mengi alizipata na kutaja nchi zilizotoa, akianza na Norway ambayo alidai mwaka 1988 hadi 1989 iliisaidia kampuni ya IPP kupitia kampuni ya Anche Mwedu kupata Krona 6milioni, na baadaye kupitia kampuni hiyo hiyo ilipata Krona 4 milioni.


Alidai mwaka 1991/92, Japan ilisaidia Bonite Bottlers kuchukua Yen 160 milioni na baadaye ikasaidia Medicare kupata Yen 115 milioni na Canada mwaka 1988/89 ikasaidia Anche Mwedu dola za nchi hiyo 0.5milioni. Pia alidai mwaka 1988/89 Italia ilisaidia Anche Mwedu kupata Lira 1.7milioni, Japan 1997 ilisaidia Anche Mwedu Yen 20milioni na Japan tena 1994 ilisaidia Bonite Bottlers kupata Yen nyingine 160 milioni.


Pia alidai Tume ya Uchumi ya Ulaya (European Economic Commission-EEC), katika kipindi cha mwaka 1988/89 ilisaidia Bonite Bottlers kupata EEU 0.5199. "Fedha hizi zilizo katika sarafu tofauti za kigeni zikibadilishwa kwa shilingi za Tanzania na riba kwa miaka yote tokea zilipochukuliwa zinafikia mabilioni ya shilingi," alisema Rostam. "... badala ya kurejesha fedha hizi... Mengi alizitumia kujitajirisha."


Pia alidai kuwa Mengi aliingia ubia na serikali katika umiliki wa kiwanda cha Tanpack Industries Ltd, lakini bila ya kumjulisha mbia wake (serikali) alitumia dhamana ya kiwanda kukopa Sh600 (sic) kutoka benki ya NBC na "kuzitumia kwa njia anazozijua yeye". "Benki hiyo ilipochachamaa kutaka ilipwe fedha zake, Mengi alitaka Tanpack ilipe lakini serikali ikakataa kulitambua deni hilo... Matokeo ya ufisadi huo wa Mengi, Tanpack ikafilisiwa na kufa," alidai Rostam. Miongoni mwa matukio ambayo Rostam alidai Mengi alikorofishana na watu mbalimbali ni pamoja na zabuni ya ubinafsishaji hoteli ya Kilimanjaro (sasa Kempiski).


"Alianzisha ugomvi na aliyekuwa Waziri wa Utawala Bora Mheshimiwa Wilson Masilingi baada ya kushindwa zabuni ya ubinafsishaji wa hoteli ya Kilimanjaro, akataka kuufanya kuwa ugomvi wa nchi nzima," alidai Rostam. "Katika kudhihirisha jinsi alivyo na chuki na visasi kutokana na kuikosa tu hoteli hiyo, amekuwa hakanyagi na hata kushiriki shughuli yoyote inayofanyika katika hoteli hiyo." Kuhusu kutajwa kwenye ufisadi katika Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA), Dowans na tuhuma nyingine, Rostam alisema "hizo zote nimekwishazitolea maelezo... ni porojo tu hakuna hata moja ninayohusika nayo".


Ni vema Watanzania wakafahamu kwamba kila anapokabiliwa na matatizo au anapotenda maovu, kimbilio lake la haraka la kujifichia limekuwa ni kusaka huruma kwa wananchi kwa kutaka aonekane ni sehemu yao na kwamba anaonewa kwa kuwatetea wao. Ukweli ni kwamba amekuwa akifanya hivyo ili kutafuta hifadhi na kinga akijua ana madhambi mengi."


Akijibu tuhuma chache kati ya hizo huku akikataa kuzungumza kwa kirefu, Mengi alisema "mafisadi papa wana uwezo mkubwa sana siyo tu kwa mali za umma bali hata kutunga uongo kama ilivyofanywa na Rostam Aziz leo (jana)".


"Naomba nimpe Rostam Aziz ushauri wa bure kama kweli anataka kujisafisha ama kuondokana na shutuma zinazomkabili za ufisadi aende mahakamani ikiwezekana kesho (leo) asubuhi," alisema Mengi.


"Hata baada ya kukutana na waandishi wa habari leo, hoja ya kushutumiwa kama fisadi papa inabakia pale pale. Watanzania wanasubiri kwa hamu kubwa kusikia kwamba Rostam Aziz ameenda mahakamani kwa sababu Watanzania wengi hasa wanyonge wana hasira nyingi dhidi ya ufisadi."

CHANZO: Mwananchi

LET'S HOPE SOPHIA SIMBA NA KAPTENI MKUCHIKA WATAMKOMALIA ROSTAM AS THEY DID TO MENGI ALIPOTOA TUHUMA DHIDI YA MAFISADI PAPA.I CANT SEE SOPHIA SIMBA SAYING "WATOTO WA MJINI WANASEMA ROSTAM AMECHEMKA" AS SHE DESCRIBED MENGI'S STATEMENT.

SOONER OR LATER HAWA MAFISADI WA KIASIA WATAINGIA IKULU KAMA RAIS KAMA WENYE UCHUNGU WA DHATI NA NCHI YETU HAWATAAMKA SASA.WAMESHAIFANYA NCHI HII KUWA IKO MIFUKONI MWAO,WANATUPUUZA NA KUONGEA CHOCHOTE WANACHOJISKIA KUSE,A,SIMPLY BECAUSE OF JEURI YA FEDHA ZAO ZA KIFISADI.COULD YOU EXPECT MHINDI MWENYE ASILI YA KITANZANIA KUFANYA HIVYO INDIA AU YEMEN,OR WHEREVER THESE FISADIs ORIGINATE FROM?


Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.