6 Aug 2009


Na Awila Silla, Singida

RAIS Jakaya Kikwete ametangaza vita dhidi ya askari wa usalama barabarani ili waweze kufanya kazi kwa kufuata sheria na kanuni za nchi.

Kikwete alitoa kauli hiyo nzito mkoani Singida alipozungumzia kero kubwa ya ajali nchini ambayo alisema inakwamisha juhudi za serikali kuleta maendeleo kwa wananchi.

"Na nyie watu wa usalama barabani manaendekeza urafiki na madereva wa nini badala ya kukagua gari mnazunguka nyuma ya gari na makonda kufanya nini? huku umeona kabisa gari bovu na dereva hana leseni, nawambia, safari hii naanza na nyie," alisema Rais akionyesha ukali

"Msinilazimishe sana niendelee kufoka kila siku wimbo umekuwa huo huo nimechoka jamani , Wizara mnafanya nini fanyeni kazi yenu fukuzeni hawa watu kama hawataki kufuata sheria warudi nyumbani kufua au wakafanye kazi nyingine" alisisitiza .

Mbali ya kauli hiyo nzito pia alisema haoni sababu ya kuendelea kufoka kuhusu baadhi ya matatizo ya ajali na badala yake aliitaka pia Wizara ya Mambo ya Ndani kuchukua hatua mathubuti kutatua matatizo hayo.

Alisema jukumu la sasa kwa Wizara hiyo ni pamoja na kuweka mpango mkakati wa utaratibu mpya wa sheria ya usalama barabarani juu utoaji leseni kwa madereva na kufanya marekebisho ya adhabu ambazo alisema zimepitwa na wakati.

Rais alisema hatua ambazo zinaweza kuchukuliwa chini ya wizara hiyo ni unyang'anywaji wa leseni bandia kwa madereva wasio na taaluma au wanaokiuka sheria na masharti ya usalama barabarani.

Kutokana na hilo aliitaka Wizara hiyo kuongeza ukali na kuondoa urafiki na ulegevu kwenye mambo yanayozuika ili kuboresha usalama wa barabara na kulinda uhai wa watu.

Akifafanua juu ya hilo Kikwete alisema licha ya matatizo mengi yanayojitokeza kwenye miundombinu hiyo, lakini utafiti unaonyesha kuwa asilimia kubwa ya ajali nyingi inatokana na matatizo ya kibinadamu ikiwemo uzembe wa madereva hao.

Kwa mujibu wa utafiti huo takribani asilimia 88 ya vifo hivyo kwa mwaka vilisababishwa na uzembe wa madereva,ulevi wa kupindukia na mwendo kasi.

Katika hatua nyingine alitoa mfano wa kusikitishwa na ajali mbaya ya basi la Kampuni ya Mohamedi iliyotokea hivi karibuni Wilayani Korogwe mkoani Tanga na kusababisha vifo vya watu vya zaidi ya watu 28,jambo alilokemea kutohitaji lisikia tena.

Alisema badala ya serikali kufanya ubinadamu mwema kwa wananchi lakini imekuwa ikilazimika kutuma salamu za rambirambi kwa vifo vinavyotokana ama kusababishwa na uzembe wa wachache huku ikiwa na majukumu mengi hatua aliyosema kuwa imechangia kuzorotesha maendeleo.

Aidha ametaja sababu nyingine kuwa ni pamoja na mashindano ya uendeshaji baina ya magari unaotokana na matajiri wa magari hayo hususani wa mabasi kutaka madereva hao kufika mapema kwenye vituo lengwa kwa kile kinachodaiwa cha kuwapa takrima ama posho nzuri nje ya mshahara anaopata.

Rais Kikwete alisema hayo jana kwenye uzinduzi wa miradi mikuu 3 ya barabara iliyofanyi kwenye eneo la Kititimo yenye urefu wa km 224 ya mikoa ya Singida, Manyara na Arusha (Singida, Babati na Minjingu) iliyoko kwenye mchakato wa ujenzi kwa kiwango cha lami kwa miaka 3.

CHANZO: Mwananchi

KATIKA KUMSAIDIA MHESHIMIWA RAIS,AMBAYE PIA NI AMIRI JESHI MKUU WA MAJESHI YA ULINZI NA USALAMA,KIINI CHA TATIZO NI RUSHWA NA UFISADI.LAITI AHADI ZA 2005 ZA KUPAMBANA NA RUSHWA ZINGETIMIZWA NI DHAHIRI TATIZO LA AJALI ZINAZOSABABISHWA NA TRAFIKI KUTOTEKELEZA MAJUKUMU YAO IPASAVYO (BAADA YA KUSHIKISHWA KITU KIDOGO) LINGEPUNGUA KWA KIASI KIKUBWA.

RAIS ALIKASIRISHWA NA UFISADI KATIKA BANDARI YA DAR ES SALAAM NA KUELEZA KUWA ANAWAJUA WAHUSIKA NA ANGEWASILISHA MAJINA YAO KWA MAMLAKA HUSIKA ILI WACGHUKULIWE HATUA.YOU AND I KNOW WHAT TRANSPIRED....JUST LIKE ALIVYOSEMA 2006 ANAWAJUA WALA RUSHWA NA KUWAPA MUDA WA KUJIREKEBISHA...SOUNDS LIKE AN UNDEFINITE DEADLINE.

KUFOKA AU KUONGEZA UKALI HAKUWEZI KUWA UFUMBUZI WA AJALI ZA KILA KUKICHA,ESPECIALLY PALE UKALI WENYEWE UNAPOKUWA NI MITHILI YA KUTEKELEZA WAJIBU TU.YEAH,KWANI WANAOKARIPIWA HAWANA MASIKIO AU MACHO YA KUMAIZI KUWA KUFOKA NA UKALI KWA RAIS HUKO NYUMA HAKUJABADILI CHOCHOTE?

1 comment:

  1. unakuwa wataalamu wa "heri hii kuliko ile" hata kama ile na hii havina heri kwetua hauna ambacho kingeruhusiwa kusemwa.
    Rais anazunguka m'buyu na naona (kama alivyosema Kaka Ansbert Ngurumo) anasafishwa kwa majitaka.
    Kama serikali imeshindwa kutekeleza yaliyo mema kwa kuwa ameshindwa kusimamia basi ni nani wa kulaumiwa? Aaanza na nafsi yake kwa kuiwajibisha na kuachia ngazi. Kwani akulizwa ametekeleza asilimia ngapi ya ilani yake ya uchaguzi atasemaje? Na hiyo ambayo haijatekelezwa imekwamishwa na nani? Wasaidizi wake? Ni nani aliye na wajibu wa kuwachagua na kuwawajibisha? Si yeye?
    Come Onnnn Mr Prez.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.