4 Aug 2009


Mkutano mwingine wa Bunge umamilizika huko Dodoma huku danadana ziliendelea kuhusu ufisadi wa Richmond.Wakati Watanzania wakiendelea kumwagiwa "changa la macho",gazeti la Mwananchi linaripoti kuwa Mwanasheria Mkuu,Johnston Mwanyika,ambaye anahusishwa kwa karibu na ufisadi huo,anatarajiwa kustaafu kabla ya kuanza kwa kikao kijacho cha Bunge.Na akistaafu ndio habari imekwisha!Kama unabisha,jiulize kwanini uamuzi wa Lowassa,Msabaha,Karamagi na Chenge ndio ulikuwa mwisho wa kuhusishwa kwao na tuhuma zote zinazowakabili.Yaani mtu anaiba,au anawezesha wizi,au kwa lugha mwafaka ANAFISADI kisha anajiuzulu!Kwa lugha nyingine,anahitimisha utumishi wake uliotukuka kwa heshima zote.


Kwa wale wanaotarajia jipya kwenye kikao kijacho cha Bunge hapo Novemba wanapoteza muda wao.Ngonjera zitakuwa zilezile za "Bunge kuwaka moto kuhusu Richmond","Wabunge wampania Masha","Ngeleja kuwekwa kitimoto",na uzushi mwingine.Kikao kitaanza,wahehimiwa watalambishwa mamilioni yao ya mishahara (huku Watanzania wenzao waliokodoshwa kwa wahindi wa TRL wakizungungushwa kila kukicha na wawekezaji hao feki),na hatimaye kikao kitafikia ukingoni kwa ahadi kuwa "ishu x,y na z zitajadiliwa katika kikao kijacho"


Na bado itapojiri 2010 utaskia watu wazima na akili zao wamefungiwa baa au shuleni (na mgombea mmoja) ili wasinunuliwe na mgombea mwingine!Wawakilishi wetu wanafahamu kuwa hata wakizembea namna gani bado siasa itaendelea kuwa shughuli yenye mvuto mkubwa miongoni mwa wananchi kuliko jambo lolote lile.


Halafu tunaambiwa eti tuna BUNGE LENYE MENO!Labda ya plastiki!

2 comments:

  1. Meno ya plastiki mbona ni nafuu. meno yake ni kama papai. Hawajaribu hata kuyatumia, maana ni yataharibika badala ya kuharibu

    ReplyDelete
  2. Dah!! Mie jamani nachoka kusema kuhusu UPUUZI tunaofanyiwa na serikali. Halafu RAIS anasema kachoka kufoka na ataanza ku-deal na madereva. Ameshindwa kuwashughulikia waliokuwa chini yake na wasaidizi wake ataweza walio TRubafu huko Kagera ama Nanjilinji na Namatula?
    Politricks na si vema kuwaamini hawa POLICHEATEANS

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.