27 Nov 2009


Uwajibikaji uliotukuka au kupitiliza majukumu?Who cares as long as we are kept safe.Katika magazeti mbalimbali ya hapa Uingereza kuna habari kwamba Waziri wa Usalama,Lord West,amehenyeshwa na askari baada ya kusimamishwa na kusachiwa (stop and search) kwa mujibu wa sheria za kuzuia ugaidi.Uzuri wa hawa wenzetu ni ile tabia ya "hapendwi mtu",yaani kutekeleza majukumu kwa maadili badala ya kuangalia urembo au haiba.

Sidhani kama kuna haja ya kuwakumbusha madudu ya Waziri wetu mwenye jukumu la utawala bora (which includes mapambano dhidi ya ufisadi) alivyojitokeza kuwa mama mlezi wa mafisadi.Ni katika tawala ambazo mtu anaweza kuropoka chochote na akaendelea kuitwa mheshimiwa ndipo hadi muda huu Sophia Simba anaendelea na wadhifa unaohitaji uadilifu wa hali ya juu,including umakini katika kauli.

Sasa kama askari wanaweza kudili na bosi wao kama raia mwingine iweje basi waziri wetu mwenye dhamana ya kuhakikisha mafisadi "wananyea ndoo" gerezani awe mtetezi wao mkubwa?Jibu jepesi ni kwamba Waziri Simba anapata jeuri hiyo kutoka mahala flani.Na si yeye tu bali viongozi wetu wengi wametokea kuwa na jeuri ya ajabu kwa vile wanafahamu fika hakuna wa kuwaadhibu.Kama aliyekuteua haonekani kuerwa na madudu yako why would you care kurekebisha madudu hayo?

Unfortunately,lawama nyingi zimekuwa zikielekezwa kwa watendaji wabovu badala ya kumkalia kooni aliyewapa fursa ya kuweka hadharani udhaifu wao.Ni kama katika futiboli;kocha akipanga kikosi kibovu basi lawama zaidi zitaelekezwa kwake kwa vile kikosi alichopanga hakijichagua chenyewe.Na ndio maana hivi majuzi kocha wa timu ya taifa ya Scotland alijikuta akifungashiwa virago vyake baada ya timu hiyo kufanya vibaya kwenye kampeni yake ya kushiriki Kombe la Dunia hapo mwakani.

Na ukidhani mie ni malalamishi nisiye na hoja basi SOMA HAPA uelewe chanzo cha tatizo kiko wapi.

2 comments:

  1. kuna haja ya kuanzisha shule ya kusomea uwaziri!

    ReplyDelete
  2. Kiburi inatoka wapi! Anayemwezesha huyu waziri kuwajibika kinyume na kanuni na taratibu zilizopo basi wote wawajibika, na iwapo kama hakuna wa kufanya hivyo watanzania wapiga kura waonyeshe hasira zao kupitia chaguzi za kisiasa kwa kuacha kupigia kura wavunja sheria na watenda uahalifu

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.