31 Mar 2010

Picha kwa Hisani ya Blogu ya Dina Marios
Mie kama Mkatoliki,siafikiani na ushoga au usagaji.Lakini kutoafikiana na kitu ni jambo moja na kukizuia ni jambo jingine.Ni ukweli usiofichika kuwa vitendo vya ushoga na usagaji vinaanza kuonekana kuwa vya kawaida katika jamii ya Kitanzania,hususan jijini Dar es Salaam.Je wakati umefika sasa kuhalalisha ushoga na usagaji?Na je kwa sheria za nchi ku-criminalise homosexuality inakiuka haki za binadamu?Na pengine swali la ziada,kuufanya ushoga na usagaji kuwa mithili ya laana kumesaidia chochote kuukomesha? Ni mjadala wa miaka nenda miaka rudi,karne baada ya karne.Je ushoga na usagaji ni tabia tu ya mwanadamu au ni asili?Ukitafuta jibu la mkato,unaweza kutotenda haki kwa upande mwingine wa mjadala.Kwa ufahamu wangu mdogo,kuna maelezo ya takriban aina mbili.Hoja ya kwanza,ushoga na usagaji ni suala la kimaumbile/kibaiolojia zaidi kuliko ridhaa ya mwanadamu.Maelezo haya yanazingatia wingi wa homini za jinsia tofauti kwatika mwili.Kwa maana kwamba mwanamke mwenye homoni nyingi za kiume ana uwezekano wa kuwa msagaji,na mwanaume mwenye homoni nyingi za kike anaweza kuwa shoga.Ni ishu complicated lakini nimejaribu kuieleza kwa kifupi.

Hoja ya Pili,ushoga na usagaji ni tabia tu ya mwanadamu kama zilivyo tabia nyingine.Yaani ni kama mtu anapoamua kuwa mvuta sigara au mtumia kilevi.Namna mhusika anavyoangukia kwenye tabia ya ushoga au usagaji nayo inaweza kuangalia kwa namna kadhaa.Kwa mfano,mwanadamu anaweza kuangukia kwenye ushoga au usagaji kwa tamaa.Au anaweza kuingia kwenye vitu hivyo kutokana na kuiga.Au pia anaweza kuwa 'majeruhi wa mchezo mchafu' i.e. alilawitiwa jela akaishia kupenda,alijaribu akanogewa,nk.La muhimu hapa ni kwamba uamuzi wa kuwa shoga au msagaji ni katika kile wanasosholojia wanakiita rational choice.Mtu anapima faida na hasara (cost and benefit analysis) kisha anachukua uamuzi anaoona unafaa.Pia hapa kuna suala la makuzi (socialisation) ambapo zawadi na adhabu (rewards and punishment),au tuseme sanctions,zinachangia kukua au kusinyaa kwa tabia husika.Kama familia,kwa mfano,haikemei tabia flani basi kuna uwezekano wa tabia hiyo kuonekana inakubalika.Lakini pia kuna vitu kama fedha ambapo mtoto analawitiwa kisha anapewa fedha inayoweza kumwaminisha kuwa alichofanya ni sahihi.Again,ni maelezo complicated sana na ni ya kitaaluma zaidi kuliko kimtaani.

Yote katika yote,ushoga na usagaji unazidi kushamiri katika jamii yetu licha ya 'jicho kali' la jamii.Je hiyo inamaanisha kuwa ukali huo dhidi ya tabia hiyo umeshindwa kuleta ufanisi?Tukiangalia suala hilo kwa mtazamo wa kisosholojia,inawezekana jibu lisiwe kuwa jamii imeshindwa bali ni ukweli kwamba katika jamii yoyote kuna uwezekano wa kuwepo tabia zisizokubalika.Hiyo ni katika kile wanasosholojia wanakiita deviance.Kila jamii ina walevi,wazinzi,vibaka,mafisadi,nk.Ni makundi yanayokwenda kinyume na kanuni na taratibu zinazoiongoza jamii husika.

Kwa huku nchi za Magharibi,ushoga na usagaji unazidi kuwa jambo la kawaida katika jamii.Lakini sio kirahisi hivyo kwani bado mashoga na wasagaji wanaangaliwa kwa 'jicho la shaka'.Na wao ni miongoni mwa makundi yanayolalamikia kubaguliwa.Hata hivyo,sheria zinawalinda na katika baadhi ya nchi hata ndoa zao zinatambulika kuwa ni ndoa halali.Lakini tena,kuwa na sheria ni kitu kimoja,na jamii kuiheshimu ni kitu kingine.Ni katika minajili hiyo,mashambulizi au uonevu dhidi ya mashoga na wasagaji si jambo geni katika nchi hizo.

Hawa wenzetu wanaamini kuwa mashoga na wasagaji hawastahili kubaguliwa,pasipo kujali kwanini mtu amekuwa shoga au msagaji.Na kinachoangaliwa hapo ni haki za binadamu.Wanasema ushoga au usagaji haumuondolei mtu haki zake kama mwanadamu.Je,kwa mtizamo huo wa Kimagharibi,ina maana jamii yetu huko nyumbani inawanyima haki wanajamii wenzao wanaojihusisha na ushoga na usagaji?Well,kuna wanaosema mila na desturi zetu zinapinga vitendo kama hivyo.Je mila hizo ziendelee kudumu hata kama zinawabagua baadhi ya wanajamii?Binafsi sina jibu sahihi bali nadhani swali hilo linabaki mikononi mwa jamii yetu.

Sijui wewe msomaji unaonaje lakini mie binafsi,nikiweka kando imani yangu ya Kikatoliki,sijali sana namna gani mtu anatumia uhuru wake wa kijinsia alimradi hanikwazi kwa namna yoyote.Naweza kutamka bayana kuwa namchukia zaidi fisadi anayekwaza maendeleo ya nchi yangu kuliko shoga au msagaji anayefanya anachoamini ni sahihi kwake.Lakini hiyo sio kusema naunga mkono vitendo hivyo hasa kwa vile imani yangu kiroho haiafiki.

1 comment:

  1. Hii ni mada nzuri na ngumu. Mada ya kuiangalia ki-undani kuliko wengi wafanyavyo. Ni suala ambalo linalelewa nasi kwa kuwa hatusaki chanzo cha tatizo.
    Mfano ni kule Uganda ambao wanaonekana kutaka kukurupuka na kuwaadhibu mashoga na wale wawajuao (ambao hawatawataja). Lakini ni vipi twawasaidia hawa watu kutokuwa jinsi walivyo? Ni vipi twakaa chini kuzungumza nao na kujua kwanini wanafanya vitendo ambavyo hata wao huwa vinawakwaza.
    Ninaloamini ni kuwa HATUWEZI KUWATEGEMEA WANASIASA kututatulia tatizo hili kwani hata wao hawajui lolote kuhusu mashoga hawa. Wamejitenga nasi.
    Ni sisi tunaostahili kuwapenda kisha kuwauliza na kuwaelewa kwanini wamekuwa walivyo na ni vipi tunaweza kuwashirikisha kuzuia suala hili (liwe ni la kibaiolojia ama maamuzi) lisiwatokee wengine ambao wanaweza kuja kuwa mashoga.
    Ni lazima mashoga wa sasa wawe sehemu ya mapambano . uelimishaji ili tuweze kusonga na kutatua.

    Niliandika kwa ufupi hapa http://changamotoyetu.blogspot.com/2010/02/wanasiasa-wetu-na-sakata-la-ushoga.html

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.