3 May 2010

Waziri Mkuu wa Australia,Kevin Rudd,amekuwa akifuatilia tovuti za ngono (porn sites),kwa mujibu wa kituo cha runinga cha Sky. 


Rudd,hata hivyo,amekuwa 'mfuatiliaji' wa tovuti hizo kutokana na mapungufu katika nyenzo za usalama/udhibiti (setting) katika akaunti yake ya Twitter.Kutokana na mapungufu hayo,kiongozi huyo amekuwa akifuatilia watu kama bloga wa mambo ya ngono,duka linalouza bidhaa za ngono,mwanamama aliye kifua wazi huku amjifunga pingu,na kadhalika.

Msemaji wa Waziri Mkuu ameeleza kuwa tatizo hilo lilitokana na akaunti ya Twitter ya Rudd kufuata wale wote wanaomfuata (auto-follow those who follow him)."Japo Waziri Mkuu anajitahidi kutoa majibu kwa wale wanaosema chochote kwake,kazi hiyo ni ngumu ukizingatia idadi ya watu ni 900,000", alieleza msemaji huyo.

Japo inamhitaji mtumiaji wa Twitter kuangalia kwanza wasifu wa mtu anayeomba kukufuata,kuna kipengele kinachoiwezesha akaunti imkubali moja kwa moja mtu anayeomba kumfuata pasipo haja ya mwenye akaunti kufanya hivyo.Uwezo huo unaonekana kuwa muhimu kwa watumiaji wa Twitter wenye wafuasi (followers) wengi.Katika akaunti yake KevinRuddPM,Waziri Mkuu huyo ni mfuasi wa wana-twitter wengine 200,000.

Wataalam wa teknolojia wanatahadharisha kuwa nyenzo za habari kwa jamii (social media)zinaweza kuhatarisha usalama wa mtuamiaji kama hataokuwa makini."Kuna imani kwamba kwenye vitu kama Twitter unaweza tu kufungua akaunti na mambo yakaenda mwanana",anasema Handsley,makamu mwenyekiti wa kampuni ya Young Media Australia."Tunapaswa kufahamu kwa undani kuhusu usalama wa chanzo husika cha habari kwa jamii kabla ya kuamua kukitumia",aliongeza alipoongea na gazeti la Herald Sun.

Kwa mujibu wa gazeti hilo,baadhi ya wengine 'waliofuatiliwa' na Waziri Mkuu Rudd ni pamoja na tovuti ya kamera-mtandao (webcams) za ngono na mmiliki wa kiota cha watenda ngono wa jinsia moja (gay resort) cha Phuket,Thailand.

Rudd amekuwa mtumiaji mzuri wa teknolojia ya habari huku nyakati nyingine akitumia nyenzo kama Twitter kubainisha sera zake.

Imetafsiriwa kutoka Sky News

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube