2 Jun 2010

Kwa mujibu wa imani zetu za Kiswahili,aliyekuroga akifariki basi uwezekano wa kupona nao unakuwa kama umefariki.Na msemo huu unaonekana kurandana na hali halisi ya baadhi ya matendo yetu viumbe tunaojulikana kama Watanzania.Nafahamu kuwa si wote "tuliorogwa" lakini hiyo si sababu ya "kutowatolea macho" wenzetu "waliorogwa kisha aliyewaroga akafariki".

Mwishoni mwa wiki hii,timu yetu ya taifa inakabiliwa na mpambano muhimu dhidi ya timu ya taifa ya Rwanda katika kusaka nafasi ya kushiriki kwenye michuano ya CHAN.Taifa Stars inatarajiwa kucheza siku ya Jumapili kisha Jumatatu wanatarajiwa kuingia tena uwanjani kupambana na timu ya Taifa ya Brazil katika pambano lililonunuliwa kwa mamilioni ya dola na chama chetu cha soka.

Na kwa takriban wiki nzima sasa,uongozi wa FA umekuwa bize zaidi na maandalizi ya pambano hilo walilonunua kuliko kuelekeza akili zao kwa mpambano dhidi ya Rwanda.Japo natambua kuwa kila mpenzi wa soka duniani angependa kuiona Brazil ikicheza uwanjani lakini sio kwa kununua mechi ya mamilioni ya fedha ambazo hakuna uhakika kama zitarudi.FA hawajaweka bayana gharama za kununua mechi hiyo lakini taarifa zinasema wamelipa dola za kimarekani milioni mbili unusu  (zaidi ya shilingi bilioni 3 unusu).Na hiyo ni ada (fee) tu lakini kuna uwezekano wa kiwango hicho kuwa kikubwa zaidi tukichanganya na gharama za kumudu ziara hiyo.

Kuna hoja kuwa ziara hiyo itasaidia kutangaza utalii.Well,lakini tuwe wakweli,yaani kutangaza utalii kwa dakika tisini kwa gharama ya shilingi bilioni tatu!?Na kama tujuavyo tatizo sugu la wizi wa mapato kuanzia TRA hadi kwa watendaji ngazi ya kata,si ajabu muda huu mafisadi wameshapiga mahesabu ya pasenti ngapi watakwiba kwenye chochote kitakachpatikana kwenye mechi hiyo.

Na kuna hoja ya rankings za FIFA.Hivi mechi moja ya kununua kwa mabilioni itatupandisha kwa kiwango gani ukilinganisha na menchi dhidi ya Rwanda ambayo kama "tukikaza misuli" na kufanikiwa kucheza CHAN tutapata nafasi kubwa zaidi ya kupandisha ranking yetu huko FIFA?

Ukitaka kufahamu namna ubabaishaji na ufisadi unavyozidi kutafuna mfumo wa jamii yetu subiri mechi iishe kisha vianze visingizio vya namna FA walivyoshindwa kufikia lengo la mapato.Binafsi nisingekuwa na tatizo laiti FA wangeafikiana na wenzao wa Brazil kisha kuuza tiketi kabla ya mechi na hivyo kufahamu faida au hasara itakayopatikana.Lakini kwa hali yasasa ni sawa na kucheza bahati nasibu.Na si ajabu visingizio vimeshaandaliwa as to kwanini "mechi hiyo haikuweza kurejesha faida iliyotarajiwa".

Ndio maana nashawishika kusema kuwa inawezekana ALIYETUROGA KESHAFARIKI.

1 comment:

  1. Mzizi mkuu katika mti wa Mlimao ukioza matunda na majani yake yataonesha dalili za wazi hiyo ndiyo msingi wa uongozi na timu ya serikali hii ya sasa iliyojengwa kwa misingi ya ubabaishaji. Na ubabaishaji unaendela kwenye kila taasisi. Kimsingi soka ya tanzania haitaji kucheza na Brazili Kwa sababu hapo kitachotokea zaidi ni simanzi kuliko hamasa kwa wachezaji.

    Hiyo Bilioni tatu wangewekeza katika kupeleka wachezaji wastaafu wenye nia ya kusomea ukocha wa kisasa huko brazil ingeleta impact kubwa kuliko hiyo dk 90 for nothing

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube