25 Sept 2010

(Katuni kwa hisani ya FEDE)
Si maneno yangu,bali nimenukuu kutoka gazeti la Mwananchi


...Kikwete aliyeonyesha uchovu katika mkutano huo alishuka ghafla jukwaani na kuondoka baada ya kuwatambulisha wagombea ubunge, akiwaacha wananchi wakimsubiri...Hata hivyo, kuteremka ghafla jukwaani kwa Kikwete kulimaliza mkutano huo bila kufungwa rasmi huku wananchi wakibaki na maswali juu ya mustakabali wa mkutano huo uliofunguliwa na mwenyekiti wa CCM wilaya.Marwa Mwita, mkazi wa Mugumu, alisema bado anajiuliza ilikuwaje mgombea huyo akaondoka bila ya kuaga.

"Hilo ni jambo la kujiuliza, lakini huenda amechoka na anasahau alitakiwa kufanya nini. Kwanza amechelewa kufika, hakuomba radhi, kahutubia mambo yale yale ya kila mwaka".

Jamani wapiga kura,huyu mtu kachoka na anastahili apumzishwe.Yawezekana kabisa kuwa udhaifu katika uongozi wake unachangiwa na uchovu huo ambao chanzo chake kimeendelea kuwa muujiza kama ulivyo muujiza wa nani anamiliki kampuni ya kifisadi ya Kagoda.

Na ukichanganya na utitiri huu wa ahadi za kuchakachua.....

(Katuni kwa hisani ya FEDE)

5 comments:

  1. Kikwete na Chama Chake cha Mafisadi wanajidanganya. Laiti wangejifunza toka kwa Yar'Adua hata Yassir Arafat ukiachia mbali Hosni Mubarak wasingekumbwa na aibu inayowakumba. Kama watanzania watamrejesha mchovu huyu au kuridhia wizi wake wa kura basi sitaacha kusema watanzania ni mabwege hakuna mfano duniani. By the way, umemuona rais mwana Ridhiwani anavyokaribishwa kama baba yake? Huu nao ni ufalme wa nyuma ya pazia!

    ReplyDelete
  2. Siasa si lelemama,rais anatakakiwa kuwa mwenye afya imara. Lakini kwa viongozi wetu wa kiafrika mambo ni kinyume kabisa kwa kutawaliwa kwao na tamaa ya madaraka hadi umauti! Nigeria ni mfano katika hili.

    ReplyDelete
  3. WATANZANIA CHAGUE VIONGOZI WENYE AFYA BORA TUTALIINGIZA TAIFA HASARA UCHAGUZI MWINGINE MSIDANGANYIKE TUNAWAOMBA CCM WAJE KWENYE MDAHALO HAPO TUTAONA SERA ZAO WANKAZANA NA ELIMU TUUU WAKATI HAKUNA KITU

    ReplyDelete
  4. http://samsonmalisa.blogspot.com/

    ReplyDelete
  5. Chahali mdogo wangu...pole kwa kuwa hujui kanuni za kampeni na muda wa kampeni. JK Hakuchoka bali alichelewa kutokana na ratiba kuwa inambana mno. mkutano wa mwisho wa kampeni kabla ya kufika hapo ulipodai kachoka ulichelewa kumalizika hivyo akachelewa kufika, na kwa bahati kwetu mbaya au nzuri kwako muda wa kampeni ukawa umebaki dakika kumi na tano. kilichofanyika ni kuwatambulisha wagombea na kuwaombea kura na kuondoka kabla ya saa kumi na mbili. Je unataka tupigwe bao la kisigino? kwa kupitiliza muda uliowekwa na tume ya uchaguzi? Pole mdogo wangu...CCM tunaenda mbele...kura yako moja na "wafanyakazi" wako unaowashawishi hazitunyimi usingizi. Tunao mtaji wa kura lukuki...na utashuhudia kwenye ballot boxes...ILA TU NAKUPA ANGALIZO...UISWE WA KWANZA KULALAMIKA ATI UMEIBIWA KURA

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.