Picha kwa Hisani ya Mjengwa |
22 Dec 2010
6 Oct 2010
BABA BABA BABA HUYO BABA BABA BABA BABA BABA HUYO...TUMBA TUMBA TUMBA TUMBA HILO TUMBA TUMBA HILO TUMBA TUMBA HILO...KIKWETE HOYEEEE...NILISEMA WALA RUSHWA NAWAJUA KAMA WAPIGA TUMBA ILA NAWAPA MUDA WA KUJIREKEBISHA...AKINA CHAHALI WANAOHOJI KUHUSU DEADLINE KWANINI HAWAHOJI PIA KUHUSU DEADLINE YA KUJIFUNZA KUPIGA TUMBA? (ACTUALLY,NIKIREJEA IKULU NTAMSHTAKI HUYU KIJANA HUKO KIBEREGE KWA MZEE MAGU%^&£$%^) |
NIMEISHIWA NA AHADI SASA.NGOJA NIJARIBU HII: NAWAAHIDI WATANZANIA KUWA MKINICHAGUA TENA NITAHAKIKISHA KILA MTANZANIA ATAKUWA NA TUMBA YAKE NYUMBANI AMBAYO UKIPIGA TU UNAPATA MAISHA BORA...SI NILIWAAMBIA KUWA MAISHA BORA KWA KILA MTANZANIA YANAWEZEKANA? |
UFISADI OYEEE,TUMBA OYEEEE |
MIE NI ZAIDI YA MORIS NYUNYUSA.ACTUALLY,ZILE NGOMA ZA ULE WIMBO WA TAARIFA YA HABARI YA RADIO TANZANIA NI KAZI YANGU.MCD (BADO YUPO TWANGA?) NA ALI JAMWAKA AJIRA YENU MASHAKANI. |
HUYU ZUMA ANATAKA KULETA HABARI ZA VUVUZELA,HAJUI KAMA MIE MTOTO WA MJINI.AI NEMA NEMA,AI NEMAA AAA,AI NEMA NEMA USIPONEMA LEO UTANEMA LINI |
NEMA MWANANGU NEMA |
SITAKI WATANZANIA WANIKUMBUKE KWA EPA,KAGODA NA RICHMOND PEKEE.NATAKA PIA WAELEWE KUWA MIE MIE KWA KUYARUDI NDIO MWENYE,IWE ENZI ZA NZAWISA,MAYENU AU HATA MSONDO....SHALO SHALO TINA TINA,YAANI SHAA MTU MZIMA (HEHEHEEE NGWEA NA JAY MO MPO?HATA MIE BONGOFLAVA NAZIJUA PIA.SI MNAWAONA WANABONGOFLEVA KWENYE KAMPENI ZANGU?) |
27 Sept 2010
Video zote kwa hisani ya Coby
25 Sept 2010
Si maneno yangu,bali nimenukuu kutoka gazeti la Mwananchi
...Kikwete aliyeonyesha uchovu katika mkutano huo alishuka ghafla jukwaani na kuondoka baada ya kuwatambulisha wagombea ubunge, akiwaacha wananchi wakimsubiri...Hata hivyo, kuteremka ghafla jukwaani kwa Kikwete kulimaliza mkutano huo bila kufungwa rasmi huku wananchi wakibaki na maswali juu ya mustakabali wa mkutano huo uliofunguliwa na mwenyekiti wa CCM wilaya.Marwa Mwita, mkazi wa Mugumu, alisema bado anajiuliza ilikuwaje mgombea huyo akaondoka bila ya kuaga.
"Hilo ni jambo la kujiuliza, lakini huenda amechoka na anasahau alitakiwa kufanya nini. Kwanza amechelewa kufika, hakuomba radhi, kahutubia mambo yale yale ya kila mwaka".
Jamani wapiga kura,huyu mtu kachoka na anastahili apumzishwe.Yawezekana kabisa kuwa udhaifu katika uongozi wake unachangiwa na uchovu huo ambao chanzo chake kimeendelea kuwa muujiza kama ulivyo muujiza wa nani anamiliki kampuni ya kifisadi ya Kagoda.
Na ukichanganya na utitiri huu wa ahadi za kuchakachua.....
(Katuni kwa hisani ya FEDE)
12 Sept 2010
Sijui ndio dalili kuwa mwenendo wa kampeni unakwenda ovyo au ni ubabaishaji tu,lakini "mkwara" uliochimbwa na mnajimu mahiri,Sheikh Yahya Hussein,kwamba anampatia Rais Jakaya Kikwete ulinzi wa majini ni suala linalopaswa kukemewa kwa nguvu zote.Na ukweli kwamba mtajwa-i.e. Kikwete- amekaa kimya ni ushahidi tosha kuwa ananufaishwa na majini hayo.
5 Sept 2010
4 Sept 2010
1 Sept 2010
30 Aug 2010
Stay tuned!
Kwa mujibu wa mwana-Jamii Forums
26 Aug 2010
Rostam Aziz |
Jakaya Kikwete |
Magazeti yanayomilikiwa na Rostam |
Muhingo Rweyemamu |
Salva Rweyemamu (kushoto) na Gideon Shoo |
6 Aug 2010
5 Aug 2010
28 Nov 2009
16 Nov 2009
NI KATIKA MINAJILI HIYO NAONA UMUHIMU WA KUHOJI BUSARA ZILIZOMO KATIKA HABARI IFUATAYO
Rais Kikwete Aota kujenga safu ya vijana katika uongozi wa kitaifa
Na Mwandishi Wetu
RAIS Jakaya Mrisho Kikwete ameahidi kuwa kama akijaliwa kupata kipindi cha pili cha kuliongoza taifa la Tanzania, atafanya jitihada kubwa kuubadilisha uongozi wa Tanzania kuwa uongozi wa vijana.Rais Kikwete akizungumza juzi, mjini Dar es Salaam na vijana kutoka nchi mbali mbali za Afrika wanaoshiriki katika Mpango wa Kulea Uongozi wa Afrika wa African Leadership Initiative, Rais Kikwete alisema kuwa anauthamini Mpango huo.Alisema kuwa vijana ndiyo Tanzania ya kesho, na kama Tanzania haikuwekeza vya kutosha katika vijana na maendeleo yao, basi itakuwa haiwekezi katika hali yake ya baadaye.Aliwaambia vijana hao ambao wanashiriki katika Mpango huo unaodhaminiwa na Askofu Mkuu (mstaafu) wa Kanisa la Anglikan Desmond Tutu wa Afrika Kusini kuwa kwa kadri miaka inavyokwenda ni lazima rika la wazee lipishe lile la vijana....INAENDELEACHANZO: Mwananchi
9 Oct 2009
RAIS Jakaya Kikwete aliweka hadharani matokeo ya uchunguzi wa vipimo vya afya yake, yanayoonyesha kuwa kiongozi huyo wa nchi ana afya njema baada ya tatizo la kuishiwa nguvu akiwa jukwaani mjini Mwanza Oktoba 4, kuibua mjadala.
Lakini vipimo hivyo vinaonyesha kuwa tatizo pekee linalomsumbua Rais Kikwete ni maumivu ya shingo ambayo yanatokana na kuumia nyakati za ujana au utoto.
Afya ya Rais Kikwete ilizuia mjadala baada ya kuishiwa nguvu akihutubia kwenye Uwanja wa Kirumba mjini Mwanza na kulazimika kubebwa na wasaidizi wake hadi chumba kidogo cha uwanjani hapo na ilielezwa baada ya rais kuzinduka kuwa tatizo hilo lilitokana na uchovu baada ya safari ndefu kati ya New York, Marekani na Dar es salaam na baadaye Arusha na Mwanza.
Pamoja na uchovu huo kuhusishwa na safari ndefu ya Rais Kikwete taarifa iliyopokelewa kutoka Radio Jamaica jana jioni zinasema kuwa rais atakwenda nchini Jamaica kwa ziara ya kikazi itakayoanza Novemba 24 na kumalizika Novemba 26.
Na jana daktari wa rais, Peter Mfisi alirejea tena kauli hiyo akisema uchovu, hasa wa safari, ndio uliosababisha kiongozi huyo wa nchi kuishiwa nguvu jukwaani, huku kukiwa na habari kuwa ataenda Jamaica mwezi ujao kwa safari ya kikazi.
Hii ni mara ya kwanza kwa Ikulu kuweka hadharani vipimo vya uchunguzi wa afya ya Rais Kikwete, ambaye pia aliwahi kuishiwa nguvu siku ya mwisho ya kampeni zilizomuingiza Ikulu, na kuanguka akiwa jukwaani.
Daktari wa rais, Peter Mfisi aliwaambia waandishi wa habari jana kuwa vipimo hivyo ni pamoja na cha damu kwa ajili ya kuangalia virusi vya Ukimwi ambacho huchukuliwa kila baada ya miezi sita.
"Nimekuja kufafanua afya ya mheshimiwa rais kutokana na tukio la Oktoba 4, 2009 (la kuishiwa nguvu jukwaani) pale Mwanza. Tukio hilo limesababisha mshtuko kwa watu wengi na kuendelea kuwa jambo linalozua mjadala kuhusu hali ya afya ya mheshimiwa," alisema daktari huyo.
"Naelewa sababu ya wananchi kuwa na hofu na kuwepo kwa mjadala miongoni mwao. Tatizo pekee ambalo limekuwa likimsumbua rais mara kwa mara ni maumivu ya shingo yanayotokana na kuumia utotoni na wakati wa ujana.
"Baadhi ya pingili za uti wa mgongo sehemu ya shingoni ziliathirika kutokana na kuumia huko na humsababishia maumivu. Mara nyingi matatizo hayo huwapata wanamichezo na wanajeshi."
Dk Mfisi aliongeza kusema: "Tumekuwa tunamfanyia mheshimiwa rais uchunguzi wa damu yake kwa vipimo mbalimbali vinavyotumika kutambua maradhi mbalimbali yanayohusu damu yenyewe na mwili mzima wa mwanadamu. Tumekuwa tunafanya hivyo hapa nchini na hata nje kwa nia ya kulinganisha matokeo yetu na kwa vipimo ambavyo sisi tunavyo.
"Matokeo ya uchunguzi wetu yameonyesha mheshimiwa rais yuko salama, hana maradhi ya damu au kisukari, wala Ukimwi au wingi wa mafuta (Cholestrol), kiwango cha madini, tezi la kibofu wala shingo, au ya ini, au ya homoni mbalimbali zilizoko mwilini na mengine."
Dk Mfisi alifafanua kwamba, uamuzi huo wa kutoa vipimo hivyo umetokana na ridhaa ya rais mwenyewe.
"Ni ridhaa ya mheshimiwa rais mwenyewe... kutokana na kiapo changu cha udaktari na maadili yangu ya kazi, siruhusiwi kutoa hadharani undani wa habari yoyote inayohusu mgonjwa ninayemtibu bila ridhaa yake," alisema Dk Mfisi.
Kwa mujibu wa daktari huyo, baada ya Rais Kikwete kuishiwa nguvu jukwaani, alichukua vipimo muhimu wakati akiwa kwenye chumba maalumu uwanjani hapo kama ilivyo kawaida na kwamba vipimo hivyo vimeshafanyiwa uchunguzi.
Alifafanua kwamba matokeo ya vipimo vilivyochukuliwa siku ya tukio la Mwanza yalionyesha shinikizo la damu (BP) lilikuwa kati ya 130 kwa 85 (vipimo vya kitaalamu), kitu ambacho ni cha kawaida kwa mtu mwenye umri kama wa Rais Kikwete.
"Mapigo ya moyo wake yalikuwa ni 76 kwa dakika ambayo pia ni ya kawaida; sukari kwenye damu ilikuwa 5.5 ambayo nayo ilikuwa ya kiwango cha kawaida; joto la mwili lilikuwa nyuzi 37.5 ambalo ni la kawaida," alifafanua Dk Mfisi.
"Mheshimiwa Rais pia hakuwa na kiungo chochote kilichoonekana kutetereka, jambo ambalo lilithibitisha kuwa hakupata kiharusi. Mheshimiwa Rais hakuwa na matatizo yoyote ya kiafya ambayo yangeweza kuhusishwa kuwa chanzo cha tukio lile (la Mwanza)."
Hata hivyo, Dk Mfisi alisema baada ya kurejea Dar es Salaam alijaribu kuwasiliana na madaktari wenzake wa ndani na nje ya nchi ambao wamekuwa wakishirikiana nao katika kuchunguza na kufuatilia afya ya Rais Kikwete.
"Wote hao baada ya kuwasimulia kilichotokea na matokeo ya vipimo nilivyomfanyia mheshimiwa rais, kwa tafakuri zao hawakuwa na wasiwasi wowote kuwa tukio hilo lilisababishwa na jambo jingine lolote isipokuwa uchovu," alisisitiza daktari huyo wa rais.
Aliongeza kwamba mmoja wao alimuona rais siku moja kabla ya kuondoka New York ambako alipata nafasi ya kumchunguza afya ya mkuu huyo wa nchi.
Dk Mfisi, akitoa mtiririko huo wa vipimo mbalimbali na matokeo alisema: " Blood Pressure (shinikizo la damu), tunafuatilia kwa karibu sana msukumo wa damu, mwenyewe tunampa mashine ya kujipima kila siku na anafanya hivyo, kwa jumla presha yake iko kwenye viwango vya kawaida.
"Aidha, uzito wake wa mwili unaendana ipasavyo na urefu wake, mheshimiwa Rais ni mtu mwenye mazoea ya kufanya mazoezi na yuko makini katika chakula anachokula."
Daktari huyo wa rais aliweka bayana kwamba, wanahusika kwa ukamilifu na kuelekeza kuhusu chakula anachokula na kuongeza kwamba "ana nidhamu ya kujipima pamoja na mazoezi na chakula."
Kuhusu moyo, Dk Mfisi alisema tayari walishamfanyia rais vipimo vya kitaalamu vinavyofahamika kama ECHO na ECG na vingine, na kwamba matokeo yameonyesha hakuna tatizo lolote.
Akizungumzia ubongo, alisema mwaka jana Rais Kikwete alifanyiwa uchunguzi wa afya ya ubongo wake katika Hospitali ya Taifa Muhimbili kwa kutumia kipimo cha CT-Scan na matokeo yake yalionyesha kwamba, hakuwa na tatizo pia.
Dk Mfisi alisema Rais Kikwete aliwahi kufanyiwa uchunguzi wa ini, figo, bandama na kongosho kwa kutumia kipimo cha mionzi (ultra sound), uchunguzi ambao ulibaini viungo vyote hivyo viko salama.
"Kila mwaka tunapomfanyia uchunguzi wa afya ya mheshimiwa rais, tumekuwa tunafanyia uchunguzi wa viungo vyake muhimu vya tumboni kama vile ini, figo, bandama na kongosho na kwa kupima damu yake kwa vipimo vyote muhimu," aliongeza Dk Mfisi.
Kuhusu mfumo wa njia ya chakula, ambayo huhusisha koromeo la chakula, tumbo, utumbo mdogo, Dk Mfisi aliweka bayana kwamba matokeo ya uchunguzi yameonyesha hakuna tatizo lolote.
Alisema mwaka 2007 walimfanyia kipimo cha kitaalamu cha colonoscopy mjini Paris, Ufaransa, kuchunguza hali ya afya ya utumbo mkubwa na kwamba matokeo ya uchunguzi yalionyesha kuwa hana matatizo yoyote.
Alisema daktari aliyemfanyia rais kipimo hicho aliwaambia kuwa mkuu huyo wa nchi hahitaji kufanyiwa kipimo kama hicho tena mpaka baada ya miaka saba na kwamba daktari huyo alimtania rais kwa kusema kuwa "angefurahi kuazima utumbo" wake.
Kuhusu tezi la shingo, Dk Mfisi alisema kuwa akiwa mjini New York katika safari yake ya juzi, Rais Kikwete alifanyiwa uchunguzi wa afya ya tezi la shingo pamoja na kiwango chake cha utoaji wa homoni, matokeo yaliyoonyesha hakuna tatizo, hali kadhalika uchunguzi wa tezi la kibofu ulionyesha hana tatizo.
Dk Mfisi alisema rais hana tatizo la macho, masikio na pua na kwamba uvaaji miwani wa Kikwete haumaanishi kuwa ni maradhi.
"Tunapofanya uchunguzi wa macho ukiacha ile ya kuchunguza uwezo wa kuona, tunaangalia presha ya macho na hali ya viungo vya nje na ndani, mheshimiwa Rais hana matatizo yoyote," alisema.
Urais si Kikwete binafsi, ni mfumo wa kitaasisi. Ni wazi kuwa Rais amesema yeye ndiye hakuzingatia ushauri wa wataalamu wake kutokana na kuwaondolea lawama. Ameamua kuwalinda kwa kubeba lawama, lakini ukitazama jambo hili kwa upana wake wasaidizi wake walipaswa kutambua tangu awali kuwa urais ni system nzima Ikulu hata mlinzi wa getini. Kwa hiyo, wasaidizi ndiyo wenye kuamua na si kila kitu kifanywe na Rais kama ambavyo wanasema sasa watajaribu kumpunguzia ratiba,” ALISEMA DR SEMBOJA NA KUSISITIZA KWAMBA“Sidhani kama ni sahihi kukubali kuwa Rais ndiye alikataa ushauri, kwa taratibu za kimfumo Rais anapangiwa kila kitu ni kama anaamriwa hivi. Kwa tukio hili ameamua tu kuwa na nidhamu ya kuwalinda wasaidizi wake, namwombea afya njema lakini ni muhimu tuzingatie kuwa wengi walioamua kufanya kila kitu wenyewe walipata matatizo, Ikulu sasa ifanye kazi kama Ikulu.”
BINAFSI NAAMINI TATIZO NI LA KIMFUMO ZAIDI.KUNA TAASISI ZENYE MAMLAKA NA WAJIBU WA KUPANGA RATIBA ZA RAIS SAMBAMBA KWA KUZINGATIA UHALISIA,USALAMA NA MAMBO MENGINE KAMA HAYO.KWA WENZETU WANAOZINGATIA KANUNI NA TARATIBU ZA KITAASISI,SI RAHISI KWA RAIS KUJIAMULIA MAMBO YAKE MWENYEWE PASIPO KUZINGATIA USHAURI WA KITAALAM.SI RAHISI,KWA MFANO,BARACK OBAMA KUJIAMULIA KWENDA MAHALA FLANI KINYUME NA USHAURI WA U.S. SECRET SERVICE.UBISHI WA RAIS KAMA BINADAMU HAUNA NAFASI KATIKA UFANISI WA TAASISI INAYOZINGATIA TAALUMA NA MAADILI.IKUMBUKWE KWAMBA LAITI RAIS AKING'ANG'ANIA KUFANYA ZIARA MAHALA FLANI KINYUME NA USHAURI WA WASAIDIZI WAKE KISHA AKAPATWA NA JANGA,WATAKAOBEBA LAWAMA NI WASAIDIZI HAO NA SI RAIS.LAKINI PIA KUNA SUALA LA FEDHA ZA WALIPA KODI ZINAZOTUMIWA NA TAASISI HUSIKA KUILINDA ASASI YA URAIS NA BINADAMU ALIYEKABIDHIWA DHAMANA YA URAIS.NI DHAHIRI KWAMBA RAIS AKIPUUZA USHAURI WA WA TAASISI HUSIKA INAMAANISHA PIA UPOTEVU WA FEDHA ZA WALIPA KODI.
UTENDAJI WA AINA YA ZIMAMOTO,AU VIBAYA ZAIDI,KULENGA SHABAHA BAADA YA RISASI KUFYATUKA,UTATUGHARIMU HUKO MBELENI.LEO HII TUSINGEHITAJI DAKTARI WA RAIA KUWEKA HADHARANI TAARIFA NYETI ZA AFYA YA JK LAITI TAASISI HUSIKA ZINGEMLAZIMISHA JK KUFUATA USHAURI WA KITAALAMU KUHUSIANA NA RATIBA AU ZIARA ZAKE.TUSISUBIRI JAMBO LITOKEE NDIPO TUANZE KUTOA MAELEZO YA KITAALAMU. BY THE WAY,TAARIFA HIYO YA DAKTARI WA RAIS INAWEZA KUZUA MJADALA USIO NA TIJA KUHUSU MANTIKI YAKE.JAPO NI VEMA KUTOA UFAFANUZI KATIKA MASUALA YANAYOZUA UTATA (I WISH NA KWELI ISHU YA KAGODA INGEKUWA HIVYO) LAKINI KUNA UWEZEKANO WA "WABISHI" KUHOJI KAMA DAKTARI WA RAIS WA AFRIKA ANAWEZA KUTOA TAARIFA "MBAYA" DHIDI YA BOSI WAKE!
KWA SASA,MAMLAKA HUSIKA ZINAWEZA KUFARIJIKA BAADA YA KUPATA UTETEZI KUTOKA KWA JK.LAKINI NI VEMA ZIKATAMBUA KUWA JUKUMU LAO SI KUMWOGOPA MHESHIMIWA BALI KUFANYA KAZI ZAO KWA KUZINGATIA MAADILI NA TAALUMA.JK KAMA MTU ANAWEZA KUTOZINGATIA USHAURI WA MAMLAKA HIZO,LAKINI JK KAMA RAIS HARUHUSIWI KUJIAMULIA MAMBO YANAYOWEZA KUATHIRI ASASI YA URAIS.UOGA NA KUJIKOMBA NI MAMBO YASIYO NA NAFASI KATIKA PROFESSIONALISM.
5 Oct 2009
CHANZO: Mwananchi
28 Apr 2009
UMAARUFU wa Rais Jakaya Kikwete unaonyesha kuendelea kuporomoka, kwa mujibu wa ripoti ya matokeo ya utafiti uliofanywa na taasisi ya Mpango wa Utafiti wa Elimu ya Demokrasia nchini (Redet).
Ripoti hiyo pia inaonyesha kuwa utendaji kazi wa Rais Kikwete, ambaye aliingia madarakani mwaka 2005 kuongoza serikali ya awamu ya nne, umeshuka kwa asilimia 28 mwaka jana ukilinganisha na matokeo ya utafiti ya mwaka 2006.
Pamoja na kushuka kwa asilimia hiyo, utafiti huo umeonyesha kuwa wananchi waliohojiwa wanaridhika zaidi na utendaji wa Rais Kikwete, kuliko wanavyoridhishwa na utendaji kazi wa baraza lake la mawaziri ambalo utendaji wake umekubaliwa na asilimia 18 tu.
Kwa mujibu wa utafiti huo, watu wanaoridhika sana na utendaji kazi wa Kikwete ni asilimia 39.5 tu kulinganisha na asilimia 69 iliyoonyesha kuridhika naye sana mwaka 2006.
Akitoa taarifa ya utafiti huo jana kwa waandishi wa habari, mtafiti mkuu wa Redet, Dk Benadetha Killian alisema kuwa ukilinganisha takwimu za Oktoba 2006 na Oktoba 2007, asilimia ya wale wahojiwa ambao wanasema wanaridhika sana na utendaji kazi wa Rais Kikwete imepungua kutoka asilimia 69 Oktoba 2006 hadi asilimia 44 mwezi Oktoba 2007 na sasa imefikia asilimia 39.5 hadi Novemba mwaka jana.
Dk. Killian alisema kuwa ukichambua undani wa mwenendo huo utaona kwamba wakati idadi ya wanaosema wanaridhika sana iliteremka kwa tofauti ya asilimia 23, kati ya mwaka 2006 na 2007, kasi ya kutoridhika sana imepungua ukilinganisha na matokeo ya mwaka 2007/08 wakati idadi ya wahojiwa ambao walisema wanaridhika sana ilipungua kwa tofauti ya asilimia 4.5 tu.
Kwa mujibu wa Dk. Killian, ukusanyaji wa maoni kwa ajili ya utafiti huo ulifanyika katika mikoa yote ya Tanzania Bara na Visiwani na sampuli ilichaguliwa katika ngazi tatu ambazo ni wilaya na vijiji/mitaa na katika kila ngazi sampuli ilipatikana kwa kutumia mtindo wa sampuli nasibu.
"Katika kila wilaya, watafiti walitakiwa kuchagua vijiji viwili (kwa maeneo ya shamba) au mitaa miwili (kwa maeneo ya mjini) kwa kutumia njia ya sampuli nasibu. Katika kila wilaya, jumla ya watu 50 walichaguliwa kwa ajili ya kuhojiwa, 25 kutoka kila kijiji/mtaa," alisema.
"Na kati ya watu 50 waliohojiwa katika kila wilaya, 25 walitakiwa wawe wanawake na wengine 25 wawe wanaume na uchaguzi wote wa wahojiwa ulifanyika kwa kutumia njia ya sampuli nasibu."
Alisema ukiacha masuala mengine ya utendaji wa mawaziri, waliohojiwa walitakiwa kutoa tathimini yao kuhusu utendaji kazi wa Rais Kikwete katika kipindi cha takriban miaka mitatu ya utawala wake kwa kutoa maoni yao kama wanaridhika sana, wanaridhika kiasi au hawaridhiki.
Dk. Killian alisema kati ya wote waliohojiwa, asilimia 39.5 walisema wanaridhishwa sana na utendaji wa Rais Kikwete, asilimia 39.0 walisema wanaridhika kiasi na asilimia 19.3 walisema hawaridhiki na utendaji kazi wa mkuu huyo wa nchi.
Alisema hata hivyo kwa ujumla, matokeo ya utafiti wa Novemba mwaka jana yanaashiria kwamba, utendaji kazi wa Rais Kikwete bado unaonekana kuridhisha idadi kubwa ya watu pale ambapo makundi mawili ya wahojiwa yanapojumlishwa pamoja yaani wale wanaosema wanaridhika sana asilimia 39.5 na wale wanaosema wanaridhika kiasi asilimia 39 ikiwa inafanya idadi hiyo ya wahojiwa wote kufikia asilimia 78.5.
Dk Killian alisema sababu za kuridhika au kutoridhika na utendaji kazi wa serikali ya Rais Kikwete ni kutoridhishwa na ahadi yake ya kuboresha hali ya maisha. Asilimia 31.0 ya waliohojiwa walisema ameshindwa kuboresha hali ya maisha, wakati asilimia 24 walisema hajatimiza ahadi na asilimia 12.2 walisema hafuatilii utekelezaji wa ahadi zake.
"Sababu nyingine zilizotolewa na wahojiwa ni kuchagua viongozi wasiofaa asilimia 10.8, ameshindwa kupambana na rushwa asilimia 8.0, lakini pamoja na kwamba utafiti huu ulifanywa kipindi ambacho "vigogo" walikuwa wanapelekwa mahakamani kuhusiana na tuhuma za matumizi mabaya ya ofisi na wengine kutuhumiwa na wizi wa fedha za akaunti ya madeni ya nje (EPA), ni asilimia 6 tu ndiyo waliotaja moja kwa moja suala hili kama sababu ya kutoridhishwa au kuridhishwa kiasi na utendaji kazi wa rais," alisema.
Alisema sababu za wananchi kutoridhika na utendaji wa serikali iliyo madarakani ni kutofuatilia utekelezaji asilimia 30.7, serikali kujihusisha na rushwa asilimia 29 na inapitisha mikataba mibovu asilimia 10.0.
Utafiti huo pia unaonyesha kuwa bunge ndio linaongoza kwa kutoridhisha wananchi baada ya asilimia kubwa ya waliohojiwa kueleza kuwa hawaridhishwi na taasisi hiyo ya kutunga sheria.
Bunge limeonekana kutoridhisha wengi tofauti na taasisi za serikali kama polisi, taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa nchini, serikali za mitaa na kadhalika.
Dk. Killian alisema bunge linaongoza kwa kuwa na asilimia kubwa ya kiwango cha kutoridhika ambacho ni asilimia 77.4, ikifuatiwa na serikali za mitaa asilimia 75.6 wakati baraza la mawaziri linashika nafasi ya tatu kwa asilimia 63.
Kwa upande wa utendaji kazi wa Rais Amani Abeid Karume wa Zanzibar, utafiti unaonyesha kuwa asilimia 44 tu ya wote waliohojiwa wanaridhika sana, wakati asilimia 24 wanaridhika kiasi na asilimia 26 walisema hawaridhiki.
Alisema kiwango cha utendaji wa Rais Karume kimeonekana kupanda kwa asilimia 9 ukilinganisha na utafiti wa Oktoba 2007 wakati asilimia 35.5 tu ilimkubali baada ya kuporomoka kutoka asilimia 47.8 aliyopata kipindi cha hadi Oktoba 2006 na baadaye kupanda kutoka asilimia 35.5 Oktoba 2007.
CHANZO: Mwananchi
Watanzania walio wengi, zaidi ya asilimia 80, bado wana imani na Rais Jakaya Kikwete, kuliko miaka minne iliyopita alipochaguliwa kuwa Rais. Pia asilimia kubwa ya Watanzania inaridhishwa na utendaji kazi wa Rais na Serikali yake.
Kura ya maoni iliyoendeshwa na taasisi ya uchunguzi inayojitegemea ya REDET kuhusu utendaji wa Serikali ya Kikwete katika miaka mitatu iliyopita ya uongozi wake, inaonyesha kuwa asilimia 83.7 ya Watanzania wana imani naye.
Kundi hilo la Watanzania wanaothibitisha kuwa na imani na Rais Kikwete likigawanywa katika makundi ya ulinganisho wa imani, asilimia 50 inasema ina imani sana kwa kiongozi huyo, asilimia 33.7 inasema ina imani kiasi cha kutosha kwake.
Asilimia hiyo ni kubwa kuliko ile ya ushindi wa urais mwaka 2005, alipochaguliwa kwa kishindo ambapo alichaguliwa kwa asilimia 82. Hakuna mwanataaluma yeyote wa REDET ambaye alikubali kuzungumza na gazeti hili kuhusu kura hiyo ya maoni licha ya kupatikana kwa nakala ya matokeo ya utafiti huo.
Lakini habari zinasema matokeo kamili ya kura hiyo yanatarajiwa kutangazwa rasmi wiki ijayo na uongozi wa REDET. Kubwa zaidi katika ripoti hiyo, ni ukweli kuwa asilimia ya Watanzania wenye kuridhishwa na utendaji kazi wa Rais Kikwete bado iko juu.
Utafiti huo wa kisayansi na wa kina uliofanyika katika sehemu mbalimbali za nchi mijini na vijijini unaonyesha kuwa asilimia 78 ya Watanzania wanaridhishwa na utendaji kazi wake. Matokeo ya kura hizo yamethibisha kwa mara nyingine, ukweli ambao umebakia bila kubadilika kuhusu imani ya wananchi kwa Rais Kikwete na utendaji wake tangu alipoingia madarakani.
Kura zote za maoni ambazo zimefanyika tangu wakati huo, zimekuwa zikionyesha kuwa kiwango cha imani ya wananchi wake na kwa utendaji kazi wake kimebakia kwenye eneo la asilimia 80. Kura hizo pia zinaonyesha kuwa imani ya wananchi kwa wasaidizi wake wakuu ni ya juu.
Zinaonyesha pia kuwa asilimia 82.7 wana imani na Makamu wa Rais, Dk. Ali Mohammed Shein akiwa nyuma ya Rais kwa asilimia moja, wakati Waziri Mkuu Mizengo Pinda anavutia asilimia 84. Utafiti huo pia unathibitisha kuwa wananchi kiasi cha asilimia 70 wana imani na Baraza la Mawaziri, wakati asilimia 66 wana imani na wakuu wa mikoa. Imani ya wananchi inashuka kidogo kwa Bunge ambalo lina asilimia 65.
Katika namna ambayo pia itakipa nguvu na kuifurahisha CCM, asilimia ya Watanzania ambao wanasema wanaridhishwa na utendaji kazi wa chama hicho ni 72.8 wakati asilimia 75.6 wanasema wana imani na chama hicho. Matokeo hayo yatakifurahisha chama hicho kwa sababu asilimia hiyo kubwa ya kukubaliwa na Watanzania imebakia ya kiwango hicho hicho kwa karibu miaka 17 tangu kuanzishwa kwa vyama vya upinzani nchini.
Mwaka 1992 wakati CCM na serikali zilipoongoza mageuzi ya kuingia katika mfumo wa vyama vingi, ilikuwa baada ya uchunguzi uliothibitisha kuwa ni asilimia 20 tu ya Watanzania waliokuwa wanataka mfumo wa vyama vingi. Kwa namna moja au nyingine, asilimia hiyo imebakia na kujithibitisha mara nyingi kupitia njia mbalimbali ikiwa ni pamoja na kupitia uchaguzi mkuu ambao umefanyika tangu wakati huo na hasa uliopita uliomwingiza Rais Kikwete madarakani mwaka 2005. Kwa upande wa vyama vya upinzani, asilimia ya Watanzania ambayo inasema haina imani na vyama hivyo inabakia juu kwa asilimia zaidi ya 31.
CHANZO: HabariLeo