4 Sept 2010

Tunafahamu kuwa mgombea wa CCM,Jakaya Kikwete,ni mahiri sana katika kutoa ahadi.Wakati wa kampeni zake za kuwania urais kwa mara ya kwanza mwaka 2005 alitoa rundo la ahadi ambazo hata angekuwa na uwezo wa kutekeleza basi ingebidi awe rais wa milele.Kwa makusudi,badala ya kufanya marejeo ya ahadi zake lukuki za 2005,Kikwete ameendelea kutoa ahadi zaidi akijaribu kuwaghilibu Watanzania kuwa safari hii akipewa madaraka atazitekeleza.Swali la msingi ni kipi kilichomzuia kuzitekeleza katika kipindi hiki (2005-2010) na kipi kitamwezesha kutekeleza ahadi hizo katika awamu ijayo (2010-2015).

Alipokuwa kwenye kampeni zake huko mikoani aliahidi (bila aibu) kuwa tatizo la umeme sasa litakuwa historia.Last time aliposema hayo,walikuja matapeli wa Richmond.Sijui safari hii watakuja wasanii gani "kuvuna wasichopanda".Angekuwa na busara,angewaeleza Watanzania kwanini umeme umeendelea kuwa tatizo sugu nchini.Ufumbuzi wa tatizo hilo hauwezi kupatikana kwa ahadi zaidi ya zilizokwishatolewa.Kikwazo kikubwa katika upatikanaji wa ufumbuzi wa tatizo la umeme ni maslahi binafsi na ufisadi.Kuna watu wanaoombea Tanzania iwe kizani kila siku ili wauze jenereta zao.Kuna wengine wanaotaka umeme uendelee kuwa tatizo ili wapate fursa ya kutengeneza dili za kifisadi kama za IPTL,Richmond na Dowans.Na Kikwete anawajua sana watu hao lakini hana nia wa kuwachukulia hatua.Ikumbukwe kabla ya kuukwaa urais,Kikwete alishawahi kuwa Waziri wa Nishati!!!

Kadhalika,katika mwendelezo wa ahadi,Kikwete ameahidi kuleta ufumbuzi wa kudumu wa tatizo la maji jijini Dar es Salaam.Utadhani kwamba tatizo hilo halikuwepo wakati wa utawala wake,au limeanza majuzi.Na kama hiyo haijatosha,akaahidi tena kuwa daraja la Kigamboni litajengwa kwa vile zabuni ya kumpata mkandarasi imeshakamilika.Kwanini iwe baada ya kumchangua tena na sio alipochaguliwa 2005?Haihitaji hata elimu ya chekechea kutambua kuwa ahadi hizi ni hewa.ZITAENDELEA KUWA AHADI TU.

Ukimsikiliza kwa makini utagundua kuwa Kikwete hayuko serious na anachoongea.Pengine ni kwa vile anafahamu kuwa hahitaji kuwa serious kupata tena nafasi ya urais.Pengine ni tatixo la upeo tu.Hata hivyo,kumlaumu JK ni kumwonea kwa vile kama ilivyokuwa Desemba 2005,come Oktoba this year HATAJICHAGUA MWENYEWE KUWA RAIS BALI ATATEGEMEA KURA ZA WATANZANIA.Mwaka 2005 waliompigia kura na kumpa ushindi wa kishindo wanaweza kuwa na excuse kwa kudai walikuwa HAWAMJUI VEMA.Five years later,naamini kila Mtanzania anafahamu udhaifu wa kiongozi huyu.Kumrejesha tena Ikulu kwa miaka mingine mitano ni kosa ambalo litawagharimu sana Watanzania.

Ikumbukwe kuwa kama atarejea tena madarakani,kuna uwezekano mkubwa wa kuendesha nchi kwa mtindo wa BORA LIENDE kwa vile hiyo itakuwa awamu yake ya mwisho kwa mujibu wa Katiba.Kama ameweza kuwapuuza Watanzania katika kipindi hiki cha miaka mitano inayoisha huku akielewa fika kuwa itambidi awabembeleze tena wampigie kura mwaka huu,kwanini basi asiwapuuze zaidi kwa vile hatagombea tena urais hapo 2015?

Ni muhimu kwa Watanzania kutambua kuwa tusipoziba ufa tutajenga ukuta.Ufa wetu kwa sasa ni Kikwete na CCM yake.Tukiwarejesha tena madarakani hapo Oktoba tutakuwa tumejichimbia kaburi refu.Tuweke kando ushabiki wa vyama vya siasa na tuangalie maisha yetu na hatma ya taifa letu.Tusifanye mzaha kwa kuendekeza kauli "JINI LIKUJUALO HALIKULI LIKAKWISHA" (i.e. Bora Kikwete na CCM kwa vile tunawajua kuliko hao akina Dkt Slaa na Chadema tusiowajua).Problem is,jini hili safari hii litatumaliza na kutukomba kila kitu.Wameiba mabilioni ya EPA,wametutapeli na Richmond,Dowans,IPTL,Kiwira,Meremeta,Tangold,nk na hawajatosheka.Tukiwarejesha tena madarakani watatukomba kila kitu.

Bahati nzuri Mungu si Athumani.Ametuonea huruma na kumwibua mkombozi Dokta Wilbroad Slaa.Hii ni nafasi adimu,na ndio maana nguvu za giza zimekuwa zikimwandama.CCM wanajua bayana kuwa Dkt Slaa ana dhamira ya dhati kuwatumikia Watanzania.Hawampingi kwa vile ni mwanasiasa wa upinzani bali wanahofia atawafungua macho waliolala,na pia atawapora mtaji wao- yaani masikini wanaonunuliwa kwa pishi za mchele na sukari huku wakiahidi maisha bora "hewa".

Kama wewe si fisadi basi unapaswa kuwa na NIA,SABABU na UWEZO wa kumtosa JK na CCM yake hapo Oktoba.Maisha Bora ya Kweli (na sio ya kuzugana) Yanawezeka,Ila tu sio kwa wazushi hawa waliopo madarakani bali kupitia kwa Dokta Slaa na CHADEMA.

1 comment:

  1. KAZ ANAYOWEZA NI KUWA MWALIMU CHUO CHA USANII

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.