4 Sept 2010

Kwa mujibu wa blogu ya Utakapojua Hujui Ndipo Utakapojua (mwanahabari mahiri Ansbert Ngurumo),Msajili wa Vyama vya Siasa John Tendwa alionekana Ikulu siku ya Alhamisi majira ya saa 9 alasiri ambapo inaelezwa alikutana na Rais Jakaya Kikwete,mgombea wa CCM ambaye amelalamikiwa na Chadema kwa kukiuka Sheria y Gharama za Uchaguzi.Awali,Tendwa alisema kuwa angetoa "hukumu" keshokutwa (Jumatatu).

Kwa hakika,haihitaji utaalam wowote kuhusisha tukio hilo (la Tendwa kukutana na Kikwete) na pingamiz la Chadema.Na haihitaji ujuzi wa sheria kubashiri matokeo ya "hakimu kukutana faragha na mshtakiwa" siku chache kabla ya hukumu.

Wengi wetu tunafahamu Tendwa atasema nini hiyo Jumatatu.Most likely,ameshafanya maamuzi ila kinachoshughulikiwa sasa ni usanii wa lugha ya utoaji wa maamuzi hayo.Na ni katika hilo ndio maana inamlazimu awasiliane na JK ili "ajenge mazingira ya hukumu ya haki".Katika mazingira tuliyonayo ambapo Msajili wa vyama vya siasa ni kama kibaraka wa CCM,haiwezekani kabisa kiongozi huyo kutoa maamuzi ya haki yatakayokiathiri chama hicho.

Na dalili za "usanii" zimeonekana tangu Chadema wawasilishe malalamiko yao.Hivi Tendwa anaweza kuwaambia Watanzania kwanini imchukue takriban wiki nzima kutoa maamuzi kuhusu malalamiko ya Chadema?Je hiyo pekee sio dalili ya uzembe na kutowajibika ipasavyo?Awali aliwaeleza waandishi wa habari kuwa angetoa maamuzi Jumatatu lakini hakueleza kwanini itachukua muda wote huo kutoa maamuzi hayo muhimu kwa mustakabali wa demokrasia nchini mwetu.Jibu jepesi ni kwamba hana ubavu wa kutoa maamuzi kabla ya kupata ridhaa ya CCM.Na kwa vile CCM ndio watuhumiwa,ni dhahiri maamuzi ya Tendwa yataelemea kuipendelea CCM.

Nafahamu kuna wataosema "aah,sasa kelele za nini wakati maamuzi hayajatolewa?" Wana haki ya kusema hivyo lakini wanapaswa pia kutambua vema mapungufu ya Katiba yetu yanayomfanya mgombea wa chama tawala kuwa na advantage kubwa dhidi ya wagombea wengine kutokana na ukweli kwamba Katiba inampa rais nguvu kubwa mno.

Kikwete ameendelea kupuuza malalamiko ya Chadema kwa kuzidi kutoa rushwa ya ahadi katika mikutano yake ya kampeni.Sote tumemsikia akiwazuga wapigakura huko Mbagala kuhusu daraja la Kigamboni na ahadi nyingine hewa ya huduma ya uhakika kwa maji jijini Dar es Salaam.Huyu mtu hana aibu kwa sababu ahadi anazotoa sasa zinatoa picha ya mgombea anayeomba idhini ya kuingia madarakani kwa mara ya kwanza na sio aliyekuwa rais wetu kwa miaka mitano iliyopita.Kama tangu 2005 hadi leo ameshindwa kuwezesha ujenzi wa daraja hilo la Kigamboni,kwanini tumwamini kuwa ataweza katika mhula wake wa mwisho (2010-2015) hasa ikizingatiwa kuwa kipindi hicho cha pili kitatumika zaidi kwa yeye kujitengenezea mazingira ya "kustaafu kwa amani"?

Jeuri ya Kikwete inasababishwa na ufahamu kuwa Chadema,na vyama vingine vya upinzani,havina mahala pa kukimbilia pindi wasiporidhishwa na mwenendo wa kampeni za Kikwete na CCM kwa ujumla.Anafahamu kuwa Tume ya Taifa ya Uchaguzi,Ofisi ya Msajili wa Vyama vya Siasa,Mahakama na taasisi nyingine za kusimamia uchaguzi na sheria nza nchi kwa ujumla,ziko mikononi mwa CCM.Hata hivyo,wapinzani hawapaswi kukata tamaa kwa vile nchi yetu kama masikini wa kutupwa inategemea sana misaada ya wafadhili.Japo kuwapigia magoti wafadhili kunaweza kutafsiriwa kama "kuegemea kwenye ukoloni" lakini tufanyeje kama nchi yetu inaendeshwa kiholela.Binafsi,nina matumaini makubwa kuwa nchi wafadhili zinafuatilia kwa karibu mwenendo wa kampeni za vyama vya siasa nchini na hazitasita kuchukua hatua mwafaka pale CCM itakapotumia ubabe wake kulazimisha ushindi.

Hata hivyo,wakati we keep on hoping for the best and expecting the worst,Tendwa afahamu kuwa he wont get away with this issue as easily as he might think.Blogu hii inaamini kuwa Chadema ni chama makini na chenye rekodi nzuri ya ufuatiliaji mambo.Ni katika mantiki hiyo basi blogu hii inatarajia kuwa Chadema hawatamruhusu Tendwa kufanya uhuni wa aina yoyote ile katika maamuzi yake.Ni heri uchaguzi uvurugike lakini haki ipatikane.Kutoa fursa ya sheria za nchi kupindishwa kwa namna watawala wanavyotaka ni hatari sana hasa tukizingatia ulevi wa madaraka unaowakabili viongozi wengi wa "dunia ya tatu".

Kama alivyoandika Ngurumo katika blogu yake,nami narejea kumkumbusha Tendwa kuwa HATUDANGANYIKI!

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.