23 Sept 2010Ukichanganya "nyomi" kama hilo la kampeni za Dokta Slaa mjini Moshi na matokeo "yaliyominywa" ya Synovate,ni dhahiri Kikwete na mafisadi wako tumbo joto na sasa wanahangaika namna ya kuchakachua matokeo ya Uchaguzi Mkuu ujao.Washindwe na walegee.HATUDANGANYIKI!

Slaa anasa waraka mzito
• NI ULE WA SERIKALI KUIMALIZA CHADEMA
na Janet Josiah na Charles Ndagula, Moshi
MGOMBEA urais wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, ametangaza kunasa waraka wa siri ulioandikwa siku nne zilizopita, ambao pamoja na mambo mengine unawaagiza watendaji wakuu wa serikali kufanya kila wawezalo kuhakikisha Chama Cha Mapinduzi (CCM) kinashinda uchaguzi.
Dk. Slaa mwanasiasa mwenye rekodi ya kunasa taarifa mbalimbali nyeti za serikali, alitangaza kuhusu kuuona waraka huo wakati akihutubia maelfu ya wananchi waliojitokeza kumsikiliza katika Manispaa ya Moshi.
Akizungumzia suala hilo, Dk. Slaa alimtahadharisha mgombea wa urais wa CCM, Rais Jakaya Kikwete kuhakikisha anachukua hatua ya kuvidhibiti vyombo vyake vya usalama ili visimwage damu isiyo na hatia kwa sababu tu ya kutaka kushinda urais kwa gharama zozote zile.
Dk. Slaa aliyekuwa akihutubia katika Uwanja wa Mashujaa mjini hapa, alisema dalili zimeanza kujitokeza katika mikoa mbalimbali aliyopita, ambako kumekuwapo na matukio ya watu kuonewa na viongozi wa serikali.
Akifafanua, alisema waraka huo unaokwenda kwa vyombo vya usalama, wakiwemo wakuu wa mikoa, wilaya na wakurugenzi wa halmashauri za wilaya, unawataka wafanye lolote ili kuhakikisha CCM inashinda.
“Ninao waraka ulioandikwa Septemba 19 (Jumapili iliyopita), mwaka huu na leo ni siku ya tatu, unakamilishwa na kusambazwa kwa viongozi hao kuwakumbusha kuwa lazima wahakikishe CCM inashinda, sikuupata hapa hapa, ila tayari umesambazwa nchi nzima,” alisema Dk. Slaa.
Dk. Slaa ambaye ni Katibu Mkuu wa chama hicho, kwa nafasi yake anatoa tamko hilo ili kumtahadharisha Rais Kikwete kuacha mara moja hujuma hiyo, na kuwa dalili zinaonyesha kwamba Watanzania wameamka na wanahitaji mabadiliko.
Alisema pamoja na kupata hujuma hizo, chama chake kimejipanga vyema kukabiliana na mashambulizi ya CCM na serikali yake, kwa kuweka mfumo imara wa ulinzi kwa viongozi wao na wapiga kura wao.
Alivitaka vyombo vya usalama kuacha kuhujumu msafara wake pamoja na watendaji wake, ambao wanatangulia katika vituo ambavyo anafanyia mikutano ya kampeni, kwa kuwa leo serikali ni ya CCM na kesho serikali itakuwa ya CHADEMA.
Dk. Slaa alitoa kauli hiyo baada ya kupata taarifa za polisi kutaka kuwakamata vijana wa chama hicho, ambao wanapima viwanja vya kufanyia mikutano yao, ambavyo helikopta itaweza kutua kwa urahisi (GPS).
Akizungumza na Tanzania Daima, mmoja wa vijana hao, Gwakisa Gwakisa, alikiri kutaka kukamatwa na polisi hao na kudai kuwa alipowaona alifungua mlango wa gari na kukimbia pamoja na wenzake wachache na kuacha gari la chama hicho, ambalo lilichukuliwa na polisi.
Hata hivyo, Tanzania Daima ilipomuuliza Kamanda wa Polisi Mkoa (RPC) wa Kilimanjaro, Lucas Ng’hoboko, alikiri kuwa wanalishikilia gari la CHADEMA na kwamba wanamsaka mpima ramani ili wamkamate.
“Bado tunamtafuta mpima ramani wa chama hicho ili baadaye tutoe taarifa kwenu nyinyi waandishi wa habari,” alisema RPC Ng’hoboko.
Akizungumzia tukio hilo, Dk. Slaa amewataka polisi kuwaacha Watanzania wanaotimiza mapenzi yao bila kuwabughudhi na kwamba kero hizo mwisho ni Oktoba 31.

Akiwahutubia wananchi hao mara baada ya kutoa tamko la chama chake, Dk. Slaa aliwaomba wawachague wagombea wa chama chao ili waweze kufufua viwanda ambavyo vimekufa kutokana na sera mbovu za CCM.
“Ndugu zangu wana Moshi, ichagueni CHADEMA kwa kuwa CCM imeshindwa kuwaletea maendeleo, kwa kushindwa kufufua viwanda vyenu kama vile kiwanda cha ngozi, magunia, vyuma na viwanda vingine,” alisema Dk. Slaa.
Mapema akimnadi mgombea huyo, Mwenyekiti wa CHADEMA, Freeman Mbowe, aliwataka Watanzania kuufanya mwaka huu kuwa wa maamuzi na si wa utani, kwa kuwachagua wagombea makini wa chama hicho.
“Mwaka 2010 hatudanganyiki ndugu zangu wa Moshi…kwa kuwa tutaingia Ikulu na watu makini kama Dk. Slaa, kwa kuwa na nyie ni makini, hivyo mtatuchagua.
“Kwa kuwa CCM ilitumia woga wenu Watanzania kuwatawala na kuwanyanyasa, lakini sasa Watanzania mmeondokana na woga…lakini imani kubwa ipo kwenu wana Moshi, kwa kuwa mmechangia mafanikio ya wana CHADEMA,” alisema Mbowe.
Mkutano huo ulitanguliwa na maandamano makubwa yaliyoanzia katika ofisi za wilaya za chama hicho zilizopo katika Kata ya Majengo na kupita katika barabara za Ghala na Mawenzi, maarufu kama Double Road, Florida hadi katika viwanja vya Mashujaa, huku waandamanaji wakisindikizwa na helikopta iliyokuwa ikiyahamasisha kwa saa nzima.
CHANZO: Tanzania Daima
PICHA KWA HISANI YA Jamii Forums


NAMNA MWAFAKA YA KUMWADHIBU KIKWETE NA MAFISADI NI KWA KUMPIGIA KURA DOKTA WILBROAD SLAA SIKU YA UCHAGUZI HAPO TAREHE 31 OKTOBA.KIKWETE NA CCM YAKE WATAJARIBU KUCHAKACHUA MATOKEO LAKINI HILO LITAWEZEKANA TU KAMA TOFAUTI YA KURA ZA DKT SLAA NA KIKWETE ITAKUWA NDOGO.LA MUHIMU NI KUMPATIA KURA NYINGI MKOMBOZI WETU DOKTA SLAA ILI KIKWETE NA MAFISADI WASHINDWE KUBADILI MATOKEO.KAMA KENYA WALIWEZA KUMG'OA MOI NA KANU BASI HATA SISI PIA TUNAWEZA KUING'OA CCM.


TIMIZA WAJIBU WAKO

5 comments:

 1. Tangulia Slaa tuko nyuma yako. Baada ya uchaguzi polisi ndio kati ya kundi lakuanza nao hao ndio mafisadi wakubwa. Mwaka huu mpaka kieleweke.

  ReplyDelete
 2. Chahali HATUDANGANYIKI.....Hilo nyomi la Moshi la Dk Slaa halina tofauti na la Mrema mwaka 1995...HAtuwezi kubadili bura yetu kwa rehani ya kiitwacho Dk Slaa...KURA ZA NDIYO Z KISHINDO KWA JK NA WABUNGE WAKE.....

  ReplyDelete
 3. Naona Bwana Laiza anasafari ndefu sana ya kujitambua na kuelewa umuhimu ya kuwa wanasiasa makini...Siasa na wanasiasa walopo madarakani ndiyo chanzo kikuu cha maendeleo...Wanasiasa wabovu waliopo madarakani kama hawa wa hivi sasa Wakiongozwa na JK...ndiyo matokeo yake wanategemea nguvu za giza(sheikh Yahya) kuongoza nchi na kuendesha mambo kiholela...Tunataka watu makini(Dr Slaa na pia tunahitaji mabadiliko ili tuondoe mafisadi ili sheria ichukue mkondo wake ili wapewe hukuma sawa na wale vibaka wanaiba kuku na bata. Ambao hivi sasa wapo Jela hivyo jela siyo tu kwa ajili ya Vibaka ni kwa wale wote wanaotenda uhalifu ukijumuisha lit of shame ambayo wewe Laiza unaifahamu fika kabisa...Hao watu wanafanya nini mtaani...Na JK anafanya nini madarakani...Mhalifu kwake ni jela ilo linafahamika kwa kila mtu mpenda haki.

  ReplyDelete
 4. Mtukuka meya, bado nasisitiza HATUDANGANYIKI....MASUALA YA SIASA MBOVU NA NGUVU ZA GIZA HIYO NI HOJA YAKO AMBAYO HAINA MASHIKO. HAKUNA MAHALI KATIKA GAZAETI LA SERIKALI KWENYE ANDIKO LINALOSEMA SHEIKH YAHAYA AMEIDHINISHWA KATIKA MIHIMILI YA DOLA. Tunaongozwa kwa kanuni na taratibu kwa mujibu wa sheria zilizotungwa na wabunge...akiwemo huyo SLAA wako.Bado tuna imani na JK na utawala wa sheria...Ukituhumiwa tu unataka uhukumiwe...mbona utakuwa wa kwanza kulalamika dunia nzima...wacha mahakama ziamue kama watuhumiwa wana mashtaka au wana hatia...tusije tukakumbushana ya Richmond ambayo ilikuwa ni hadithi za alfu lela u lela..na matokeo umeyaona kwa wale wapambanaji wakuu wengi wao wananchi wao wamewabwaga majimboni...NARUDIA TENA KURA ZA NDIYO KWA JK NA WABUNGE WA CCM

  ReplyDelete
 5. Laiza unafahamu issue ya ununuzi wa rada na matokeo yake? Je hao wanaotuhumiwa na hiyo kashfa wapo tuu mtaani...Sasa sifa ya JK ipo wapi hapo...Richmond tena ni wizi wa ma-misheni town kabisa uliyofanyika kwa baraka za watu wa juu kabisa seriklini na waziri mkuu kulazimika kujiuzulu badala kufukuzwa kazi. nani asiyejua kwa kujiuzulu kwake Lowasa anapata ruzuku za kustaafu...Ilani angefukuzwa angepoteza hiyo sifa kupata kupata hayo mafao...Kagoda na anamiliki!? Ndiyo sababu hiyo unayozungumza kwa sababu na wewe pia ni fisadi....Hapa mpaka kifahamike mali ya umma ilirudishwe kwa wezi(mafisadi) kufilisiwa na kufungwa jela....Tena kama wewe ni miongoni mwao tegemea tutabadilisha sheria kufanya vile nchini China hukumu ya anayepatikana hatia ya ufisadi ni kunyongwa mpaka afe na pia kuflisiwa mali zote. Big up Dr Slaa....

  Profesa Lipumba jitoe na muunge mkono Dr Slaa turudishe heshima na kujenga uchumi la Taifa letu.

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.