23 Sept 2010


Nimetundika tangazo la taasisi ya Policy Forum ambalo kimsingi ni kwa maslahi ya kila Mtanzania mzalendo.Sababu zilizopelekea Shirika la Utangazaji la Tanzania kuzuwia kurushwa kwa tangazo hilo ni bayana; hawataki Watanzania wafumbuke macho na kuondoa kikwazo kikuu cha maendeleo ya nchi yetu,yaani Chama Cha Mafisadi (CCM).

Video ya tangazo hilo ipo hapo juu ya picha ya Rais Mtarajiwa Dokta Wilbroad Slaa.Hiyo haimaanishi kuihusisha Policy Forum na Dkt Slaa au Chadema bali nimeonelea ni vema kuitundika mahala itakapoonekana kirahisi.

Wito wangu na blogu hii kwako Mtanzania mzalendo ni kuibonyeza video hiyo kisha pale chini ya maneno "YouTube" utaona kitufe kinachokuwezesha kuisambaza kwa mwenzio.Tafadhali sana,kwa maslahi na ustawi wa taifa letu,jitahidi kuisambaza kwa watu wengi kadri inavyowezekana.

Njia nyingine nyepesi ya kuisambaza video ya tangazo hilo ni kwa kukopi kiungo (link) kifuatacho kisha mtumie mwezio kwa barua pepe,SMS au hata katika maongezi ya simu.Kiungo chenyewe ni hiki

http://www.youtube.com/watch?v=A3fJTCd9PWY


Tafadhali tuwasiliane kama una tatizo la namna ya kukopi.

ASANTE.KWA PAMOJA TUNAWEZA

1 comment:

  1. Kuhusu hili suala la madini, ni bora wa-Tanzania watafakari pia taarifa zingine zilizopo, sio kusikiliza upande moja tu, yaani ule wa CCM na serikali yake. Wa-Tanzania wana wajibu wa kujipanua ufahamu, na kwa msingi huo napenda kuwahimiza kuwa wawe wanazifuatilia taarifa kama hizi hapa: http://protestbarrick.net/

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube