3 Sept 2010

Wenye busara zao wanatuusia kuwa pindi ukiwa unaishi kwenye nyumba ya vioo then sio wazo jema ku-entertain kurusha mawe.Mantiki ya msemo huo ni kwamba kama una ishu zenye utata katika maisha yako then sio wazo jema kuanza kushupalia ishu za watu wengi lest flani akakugeuzia kibao.

Lakini usemi huo umeonekana hauna maana kwa Katibu Mkuu wa CCM,Yusuph Makamba,ambaye kwa siku kadhaa sasa ameamua "kuvalia njuga maisha binafsi ya Dokta Wilbroad Slaa" na kuligeuza suala la ndoa ya mgombea huyo wa Chadema kuwa ajenda ya uchaguzi.

Pengine ni dharau au ujinga,Makamba alijisahau kuwa wakati anamnyooshea kidole Dkt Slaa,yeye mwenyewe (Makamba) alikuwa na doa linaloweza kabisa kumpeleka jela.Kwa mujibu wa taarifa zilizozagaa mtandaoni,Makamba anatuhumiwa kumbaka mwanafunzi wakati akiwa mwalimu mkuu wa shule moja na hatimaye kufukuzwa ualimu.

Hizi ni tuhuma nzito sana kwani licha ya kumtia doa Makamba kama mwanasiasa,ni suala linaloweza kumpeleka jela endapo victim wake atajitokeza hadharani,na kupatiwa msaada wa kisheria.Lakini tukiweka ishu za kisiasa kando,hapa kuna suala la binti asiye na hatia ambaye inadaiwa alibakwa na mtu aliyekabidhiwa dhamana ya kumpatia elimu na mwongozo katika maisha yake,mwalimu wake,lakini akaishi kubakwa.

Blogu hii inatoa ombi maalum kwa yeyote yule anayeweza kuipatia taarifa za uhakika kuhusu binti huyo anayedaiwa kubakwa na Makamba.Lengo si kumkomoa mtuhumiwa bali kuhakikisha sheria inachukua mkondo wake as well as kutoa reminder kwa watu wengine wanaotumia vibaya dhamana walizokabidhiwa,iwe mashuleni,makazini au hata katika ngazi ya familia.

Je unamfahamu binti anayedaiwa kubakwa na Makamba?Kama jibu ni ndiyo basi tafadhali sana tuwasiliane kwa barua pepe kwa anuani hii [email protected]

1 comment:

  1. Huyu mzee Makamba,sijui nimwite mchawi. Kwanza hana sera zaidi ya kupiga domo na majungu. Pili yeye na Chiligati Kikwete wote ni askari wastaafu, watu wa misuli.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube