3 Oct 2010
Blogu hii inapenda kutoa salamu za pongezi kwa mpambanaji na mwanaharakati mahiri,Mwalimu Nkwazi Mhango (a.k.a Mpayukaji Msemaovyo) mwenye makazi yake nchini Kanada kwa kutuletea mpambanaji mwingine wa kiume.Ujio wa mwanaharakati huyu mchanga unaweza kuwa dalili njema hasa kwa vile tupo kwenye mchakato wa kuwatimua mafisadi wanaofakamia keki ya taifa letu kama hawana akili nzuri.

Naungana na Mwalimu Nkwazi na familia yake kumtakia kijana wetu afya njema na kila mafanikio ili pindi muda utapowadia ajumuike nasi katika harakati zetu za kupigania usawa katika jamii.

3 comments:

 1. HONGERA SANA KAKA, HAWA NDIO CHACHU YA SERIKALI YETU BONGO, TUWALEE KATIKA UKWELI WAKIJUA WAZI LIFE NI KUPAMBANA ILI UPATE HAKI YAKO, WATAKAPO PIKIKA NA KUIVA TUNAWASHUSHA TARATIBU BONGO. BLESSED

  ReplyDelete
 2. sasa mmegeuza globu zinazosomwa na dunia nzima mahali pa kutuonyesha uzao wenu...angalieni tutawapiga zongo..ohooo
  tupeni habari za kuchallenge msituletee malaika asiyejua alif wala bee

  ReplyDelete
 3. Laiza we mwanga nini ua senge? Kila mara ukiandika unaandika upuuzi kuonyesha usivyo na maana.
  Kosa si kuzaa wala kutangaza uzao bali kuwa na uzao wa laana kama wenu na CCM.

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.