1 Oct 2010

"Ufisadi Oyeee.Tupeni tena miaka mitano tuwakwangue kabisa".Of course ni unatarajia nini hapo?

Mgombea wa CCM,Jakaya Kikwete akiendelea na ngwe ya kuwatetea rafiki zake.Alianza na Lowassa,akaenda kwa Mramba,kisha kwa Mzee wa Vijisenti Chenge,na sasa kwa "baba lao" Rostam Aziz.Ama kweli Tanzania bila ufisadi inawezekana!

Wakati "ndege wenye manyoya yanayofanana wakiruka pamoja",Dokta Slaa anaendelea na darasa la kuwahamasisha wenye uchungu na nchi yao kufanya kila liwezekanalo kuwang'oa "ndege hao"


Wananchi mjini Songea wakimsikiliza Rais Mtarajiwa kwa makini
Picha zote kwa hisani ya Jamii Forums

5 comments:

 1. Hapa unaweza kuona wazi mantiki ya CCM kuwa chama cha mafisadi tena kwa sana. Hawa lao ni moja na adhabu yao inapaswa kuwa moja hasa wakati huu. Huyu hakika hawezi kuondosha ufisadi. Atajifanya anapambana nao wakati anaupamba.

  ReplyDelete
 2. Pole sana Chahali....hayo ya ndege wenye mbawa zinazofanana ni yako wewe na akina Dk. Slaa...wazushi... Ati kwa kuwa tu Dk Slaa amemtaja Chahali kazini na mke wake basi chahali ni mzinzi na apigwe mawe mpaka kufa...bila idhibati thabiti...wapi utawala wa sheria hapo?
  Ni kweli kuwa unaichukia CCM na ni kweli kuwa ninaipenda CCM..basi tutatofautiana sana.. HUWEZI KUTUDANGANYA...Kama mafisadi basi ni ninyi maana ingekuwa wananchi wamewaelewa ninyi basi wangewanyima kura katika kura za maoni, lakini utashangaa wameshinda kwa kishindo na watachukua ubunge ninyi mkibaki mna bwata tu..mafisadi...msema kweli sanduku la kura na uamuzi wa wananchi

  ReplyDelete
 3. Laiza inaonekana kuna mambo mawili yanakukabili katika maisha yako moja unawezakuwa na ugonjwa wa akili ama uelewako unafanana JK ambaye aliulizwa na Rais wa marekani kwa nini Tanzania maskini akasema hafahamu kwa nini...Unatakiwa kutambua siasa mbovu zinazaa viongozi wabovu na kutengeneza wapiga kura mbumbumbu. Nchi iliyowana siasa bora na pia inakuwa na maisha bora yenye uwiano sawa na wapiga kura makini. kama wewe Laiza unatoa maoni kwa sababu ya kuleta mzaha basi hakuna sababu kukujibu hoja zako. Na iwapo unaamini unachokitetea ni sahihi basi angalia kutoka hapo juu kwa unaangukia kundi gani.

  ReplyDelete
 4. Chahali unachekesha..wewe unataka wale wanaokuunga mkono na upuuzi wako tu wala huwataki wanaokupinga. wewe umezaliwa kwenye siasa mbovu na wapiga kura mbumbumbu, umezinduka umekimbilia ughaibuni unakaanga mbuyu unatuachia wenye meno tutafune..HATUDANGANYIKI...MIMI SIO ANONYMOUS KWA SABABU NINASIMAMIA NINACHOELEZA.SILETI MZAHA NINATOA MAONI kama hunifahamu muulize mmiliki wa gazeti la mwananchi mtukuka Saeed kubenea, ananijua ninavyochallenge

  ReplyDelete
 5. Pole sana kwa chanjo uliyopatiwa naq CCM nadhani itatoka kwa kwenda jela ama kufa kwa kutokana matokea ya rushwa...Rushwa ina madhara mengi sana na kuanzia blog ya chakarika itakuletea hiyo elimu bure wewe Laiza na wengine kama wewe iwapo tuu kama utakuwa na akili timamu kuelewa kitachoandikwa ili kuweza kuelewa watu kama Huyu Bwana chahali wanamaanisha nini kwa wanachoeleza

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.