Awali nilitundika taarifa ifuatayo baada ya kuiona huko Jamii Forums kabla ya post husika kufutwa.Mzembe mmoja akanitumia email akidai mie ndio mtunzi wa taarifa hiyo.Mchumia tumbo huyo alikuwa na kila sababu ya kukasirika just like mafisadi wanavyokasirika kusikia uwezekano wa Dokta Slaa kuingia Ikulu baada ya Uchaguzi hapo Oktoba 31.Anyway,naiwasilisha tena kama ilivyo (lengo sio kumridhisha huyo mzushi aliyenituhumu bali kusambaza ujumbe husika)
Taarifa ya Siri-Mikakati ya Kuiba Kura Inavyoendelea
From:
Kama nilivyoipokea nami nawatumia. Napenda kuwajulisha mikakati michafu ya kupora na kuzuia maamuzi ya umma yanayofanywa na ccm kwa uratibu wa usalama wa taifa. Baada ya kubaini dalili za kuanguka vibaya katika uchaguzi wa mwaka huu idara ya usalama wa taifa imeandaa mikakati ya kuiba kura ili kuzuia CHADEMA msiingie ikulu. Mikakati hii inaeleweka vizuri kwa tume ya taifa ya uchaguzi ambayo inashirikiana bega kwa bega na idara ya usalama wa taifa kumtengenezea jk ushindi bandia wa 80%.
Wana hakika watanzania watagundua wizi huo na watakataa matokeo ndiyo maana kwanza waliwatumia viongozi wa dini waliotembelea makao makuu ya CHADEMA wawasihi CHADEMA wakubali matokeo yatakapotangazwa na juzi wamelitumia jeshi kutisha wananchi watakaoamua kupinga matokeo ya kupikwa yanayoandaliwa na NEC/Usalama wa taifa. MAJID KIKULA ambaye ni Government Security Officer ndiye mratibu wa zoezi la kuiba kura, ni mtaalamu aliyebobea katika kazi za aina hii aliratibu vizuri zoezi kama hilo mwaka 2005.
Pia mwaka 2007 alitumwa kenya kwenda kumsaidia Kibaki kupora ushindi wa Odinga. Kikula ww.yahooanatumia muda wake mwingi hivi sasa ofisi za tume ya uchaguzi kwa ajili ya uratibu wa uvurugaji daftari la kudumu la wapiga kura akiifanya kazi hiyo kwa karibu na baadhi ya watendaji wa NEC na maafisa kadhaa wa usalama wa taifa kutoka Kurugenzi ya IT ya idara ya Usalama (DITA) ambao wako ndani ya NEC kwa zaidi ya miezi sita sasa, nitawapatia majina yao.
Pia kuna vijana wataalamu wa IT waliochukuliwa kutoka maeneo mbalimbali wamepewa nyumba upanga mtaa wa Undali. Shughuli kubwa wanayofanya ni kuandaa utaratibu wa ku-access remotely daftari la kudumu la wapiga kura. Hawa wanafanya kazi chini ya SALVA RWEYEMAMU na MINDI KASIGA kutoka Kurugenzi Ya Mawasiliano Ikulu. Wapo vijana kadhaa leo nawapa majina ya wawili; MAHARAGE CHANDE ambaye ni mfanyakazi wa VODACOM na EDGAR MASATU wanafanya kazi kwa karibu na NZOWA wa Idara Ya Usalama ambaye ndiye aliyeratibu shambulio la kumwagiwa tindikali KUBENEA. Pia kuna kundi linalojumuisha wataalamu wa printing wa kiwanda cha uchapaji cha usalama wa taifa kilichopo MALINDI ambao hivi karibuni walikuwa mjini TANGA kwa semina fupi ya jinsi ya kughushi kura kupitia fake ballot paper, timu hii inaongozwa na Ndg. SINYAU.
Kwa hiyo utaona kwamba imeandaliwa mikakati mingi kuufanikisha uovu huo ili mmoja ukikwama basi mwingine utatumika ila wameamua ni lazima JK ashinde kwa 80%.
Ndani ya Idara Ya Usalama Wa Taifa maafisa wengi wamechoshwa na uongozi mbovu wa CCM hivyo wanataka mabadiliko ya uongozi idara imechukua hatua kadhaa kuhakikisha maafisa wote wa idara wanampigia kura JK, wote wameagizwa kuwasilisha vitambulisho vyao vya kupigia kura ili vinakiliwe namba ili atakayepigia upinzani afukuzwe kazi baada ya uchaguzi.
Fuatilieni kwa karibu haya niliyowaeleza nimeyapata kwa nafasi yangu ndani ya TISS. Huyu KIKULA mfuatilieni kwa karibu ni hatari. HAKIKISHENI DUNIA NA WATANZANIA WOTE WANAJUA MAPEMA HILA HIZI. Jambo la kujiuliza maafisa Usalama Wa Taifa wanafanya nini ndani ya Tume Ya Uchaguzi wakati huu
.
Kaka Chahali, Kuna habari imekosekanasana hapo kkwenye display yako kama inavyonesha baada ya maneno haya,,,,
ReplyDeleteTaarifa ya Siri-Mikakati ya Kuiba Kura Inavyoendelea
From: