9 Oct 2010


Majuzi tumemsikia Mwenyekiti Mwenza wa REDET,Dokta Benson Bana akilipuka tena na utafiti wao wa kuchakachua kuhusu mwenendo wa uchaguzi,ambapo kwa mujibu wao wanadai mgombea wa CCM,Jakaya Kikwete anaongoza kwenye kura za maoni.

Huko nyuma nilishawahi kuandika post moja kuhusu Dokta Bana,na tabia yake ya ulipukaji.Katika post hiyo nilikuwa nazungumzia kauli ya Mhadhiri huyo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam kwamba tuhuma zilizokithiri dhidi ya ufisadi zinaweza kusababisha taifa kukosa viongozi wazuri.Yani mhadhiri mzima alikosa busara ya kufahamu kuwa kukalia kimya ufisadi hakuwezi kusababisha taifa kupata viongozi wazuri.

Bana na Redet yake wanadhani Watanzania ni wajinga ndio maana wakakurupuka na uchakachuaji huo wakiamini wanaisaidia CCM na Kikwete.Sio ubishi wala kulazimisha matokeo tunayotaka sie bali hali halisi ya mwenendo wa kampeni inaonyesha dhahiri kuwa CCM na Kikwete wamekaliwa kooni na Dokta Wilbroad Slaa na Chadema,huku uthibitisho mkubwa ukiwa kwenye vioja kama kauli ya vitisho ya Mnadhamu Mkuu wa JWTZ Brigedia Jenerali Shimbo.

Hivi huyo Kikwete angekuwa 'anapendwa' na zaidi ya asilimia 70 ya wapiga kura watarajiwa (potential voters) angekuwa anahangaika huku na kule ku-recycle lundo la ahadi zake za mwaka 2005?

Lakini tungetarajia nini kutoka kwa Dokta Bana na REDET yake?Waseme umaarufu wa Kikwete umeshuka?Waseme Dokta Slaa anaongoza kura za maoni?Hayo hayawezekani katika utawala huu wa kifisadi unaotaka kusikia habari njema tu hata kama hazina ukweli.Tunafahamu kuwa Synovate walishindwa kutueleza nani anaongoza kura za maoni kwa vile CCM ilihofia matokeo ya ripoti hiyo yangewaadhiri.Sasa kwa vile REDET 'wameshafungulia mbwa' sintoshangaa Synovate nao wakikurupuka na ripoti yao iliyochakachuliwa itakayoonyesha Kikwete na CCM wanaongoza.

Haina haja ya kuwashutumu wachakachuaji hawa.Dawa yao iko kwa wapiga kura waliochoshwa kuona nchi yao ikigeuzwa maabara ya uchakachuaji kwenye kila eneo.Hebu pata picha iwapo kila Mtanzania aliyechoshwa na ufisadi akipiga kura ya kuwaadhibu mafisadi na hatimaye Kikwete akan'goka madarakani,Dkt Bana na REDET yake watakuwa katika hali gani!

Hilo linawezekana.Wapiga kura wasianze kukata tamaa kuwa CCM wataiba kura.Of course wataiba lakini ili 'kura zitoshe' watalazimika kufanya wizi wa 'mchana mweupe' (day light robbery) jambo ambalo sio rahisi sana,japo linawezekana.Wanaweza tu kuchakachua matokeo kama,kwa mfano Dokta Slaa akipata asilimia 51 na Kikwete asilimia 49.Hapo watarejea uchakachuaji kama ule wa Zanzibar.Lakini kama ni tofauti ya double digits,wanaweza kupatwa na kigugumizi katika kufanikisha ujambazi huo.

Ni muhimu kutovunjwa moyo na hujuma hizi.Yatupasa kufahamu kuwa Kikwete na CCM yake ni kama mgonjwa mahututi ambaye yuko tayari hata kuning'inia kwenye uzi ili asalimike.Tutashuhudia vituko zaidi ya huo uchakachuaji wa REDET au vitisho vya akina Brigedia Shimbo.Cha muhimu ni kusimamia dhamira yetu.

Inawezekana.Timiza wajibu wako

2 comments:

  1. Pengine hiyo PHD nayo ilipatikana kifisadi na yupo pale kwa ajili kuendeleza ufisadi, na kuwashabikia huyu adui yetu ufisadi

    ReplyDelete
  2. Mie huwa nawaita 'wasomi' kama hawa wa REDET wasomi nepi ambao, kwa njaa zao na ujuha na ufisi, wanaweza kutumiwa na kila kibaka kuzoa mavi yake ashakum si matusi.

    Tunao wengi waliopo walipo kutokana na fadhila na si usomi wao. Hata huyo mkuu wa UDSM ni aina hii ya vyangudoa wa kitaaluma. Wapo wengi sana hata kwenye media. Mnamkumbuka Gideon Shoo wa Habari Corp na Salva Rweyemamu walivyotumiwa na Richmond kuitakasa? Hawa si wasomi bali waliopoteza muda wao darasani wakitafuta namna ya kujaza matumbo yao. Wamesheheni ujinga vichwani na si elimu. Vinginevyo elimu na macho yao vingewawezesha kuona huu uoza wanaotetea hata kama ni kwa kuhongwa makombo ya ufisadi.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.