26 Dec 2010





Kwa mara ya kwanza kabisa,nalazimika kumpongeza Mbunge wa Monduli kwa tiketi ya CCM,Edward Lowassa.Tuweke kando ishu nyingine ambazo blogu hii zimepelekea kumshutumu kiongozi huyo mara kwa mara,hadi kufikia hatua ya aliyekuwa Mwandishi wake wa habari (Press Secretary),Bwana Said Nguba,kutoa comments bloguni hapa kumtetea bosi wake wa wakati huo (Lowassa).

Majuzi,Lowassa alitoa wito kwa chama chake cha CCM na Chadema wakae pamoja kutafuta mwafaka kuhusu sakata la umeya wa Arusha.Waziri Mkuu huyo wa zamani alifanya kile kiongozi yoyote anayejali maslahi ya umma anachopaswa kufanywa kwa kuweka kando itikadi za kisiasa na badala yake kutilia mkazo umuhimu wa kupata mwafaka katika sakata hilo la umeya wa Arusha.Lowassa alionya kwamba kama hatua za haraka na za makusudi hazitachukuliwa basi kuna hatari ya kuzalisha 'Ivory Coast nyingine ndani ya Tanzania yetu' akirejea hali tete inayozidi kusumbua katika taifa hilo la Afrika Magharibi baada ya Rais aliyemaliza muda wake na kushindwa uchaguzi mkuu kugoma ''kuachia ngazi".

Lakini wakati baadhi yetu tukivutiwa na uzalendo wa Lowassa,akaibuka mmoja wa wanasiasa wenye rekodi nzuri ya kubwatuka na "kusema ovyo",Katibu Mkuu wa CCM,Yusuph Makamba.Kiongozi huyo mwenye rekodi ya uropokaji alimvaa Lowassa akidai amekosea kusema aliyosema kwani hayo yalipaswa kujadiliwa kwenye vikao vya chama hicho tawala.Sina hakika kama Makambaanatumia kilevi cha aina yoyote lakini mchemsho huu wa safari hii unapaswa kuwa "wake up call" kwa (Mwenyekiti wa Taifa wa CCM),Rais Jakaya Kikwete,kwamba Makamba anastahili kupatiwa msaada wa kuchunguzwa akili yake.Ni mpuuzi asiye na mfano ambaye kwake usalama wa wakazi wa Arusha una umuhimu mdogo kulinganisha na taratibu za chama hicho tawala.Angalizo aloloyoa Lowassa kuwa Arusha inaweza kugeuka Ivory Coast halikuweza kuingia kwenye ubongo wa Makamba,sio kwa vile haelewi umuhimu wa political consensus bali kwa vile kwa akili yake nayohisi ina mapungufu kitendo cha CCM kukaa kitako na Chadema ni sawa na kuvunja Amri ya Mungu.

Mpuuzi huyu amesahau kuwa mgogoro mkubwa wa kisiasa visiwani Zanzibar ulimalizwa baada ya CCM na CUF kuweka mbele maslahi ya taifa na kukaa pamoja kutafuta mwafaka wa kudumu.Na kwa tunaokumbuka kauli za kitoto za Makamba katika nyakati tofauti za jitihada za CCM na CUF kutafuta mwafaka huko Zanzibar,yayumkinika kuamini kuwa suluhu hiyo isingepatikana laiti mwanasiasa huyo "angepewa rungu" la kupitisha maamuzi ya mwisho.

Kwa akili yenye mapungufu ya Makamba,vyama vya upinzani ni mithili ya wanyama wasiopaswa kuwepo nchini.Ni sahihi kusema kuwa laiti CCM ingekuwa ile ya Baba wa Taifa,basi Makamba asingepewa hata fursa ya kuwa Mjumbe wa Nyumba Kumi.Inakuwaje kiongozi wa kitaifa wa chama tawala haoni umuhimu wa kutafuta ufumbuzi wa haraka wa matatizo yanayoendelea huko Arusha?Haihitaji PhD ya Siasa kutambua kuwa anayemlea Makamba ni Kikwete ambaye anakiendesha chama hicho kwa mtindo wa "bora liende".Na Kikwete asipoamka kutambua kuwa CCM inazidi kujiweka mbali na wananchi,si ajabu chama hicho kichovu kikamvunjikia kabla hajamaliza muda wake hapo 2015.Mwenyekiti gani asiye na ujasiri wa kumwambia Katibu wake kuwa achunge mdomo wake?

Enewei,tuweke kando tofauti zetu na tusapoti mawazo ya busara ya Lowassa kuhusu umuhimu wa kutafuta suluhu huko Arusha.Sambamba na hilo,tumpuuze Makamba na pengine tumshauri aruhusu ubongo wake uwe na mawasiliano na mdomo wake kabla hajaropoka jambo lolote lile.

6 comments:

  1. Umekwishalipwa pesa ngapi na huyu fisadi Lowassa? Acha sheria ichukue mkondo wake, watu hawawezi kufanya fujo halafu jawabu liwe ni kikao. Idadi ya madiwani inajulikana, Chama kilichoongoza kwa idadi ya madiwani kinajulikana, utaratibu wa kuchagua Meya unajulikana. Kikao nje ya utaratibu kinatoka wapi? Lowassa anataka kujipendekeza tu apate umaarufu kwa uchaguzi wa 2015. Kakosa ujasiri wa kusimamia ukweli kwasababu wakati huu ni fasheni kuisema CCM na kutaka mazungumzo. Mjumbe wa NEC kama yeye hawezi kukemea Chama chake bila kusema kimefanya kosa gani kwenye mchakato wa uchaguzi wa Meya. Vilevile, mchakato wa uchaguzi wa Meya hausimamiwi na CCM wala Chadema bali na Serikali. Vyama vikikaa hakuna cha kujadili. Serikali ndio inapaswa kusimamia uchaguzi huu kwa mujibu wa Kanuni na Sheria.

    ReplyDelete
  2. MTU ALISHABAKA MTOTO WA SHULE MPAKA AKAFUKUZWA UALIMU!! UNATEGEMEA ANAAKILI HUYO? AKILI YAKE YA KUBAKABAKA TU, COMON PEOPLE, NI WAKATI WA KUPANGUA SASA. TUYAWEKE HADHARANI JAMA

    ReplyDelete
  3. Wakati wote suluhisho la kweli linakuja mkikaa pamoja nakutafuta ufumbuzi sheria is not always a solution inaweza kuacha makovu yasiyotibika kamwe na visasi visivyokwisha. Huo ni mtizamo wangu.

    ReplyDelete
  4. Yap anon 12:26 naona mzee Makamba anabaka mpaka demokrasia kazi kweli kweli.

    ReplyDelete
  5. Lowasa hana chembe ya upendo kwa watanzania na taifa kwa jumla....alichokifanya hapa kutumia fursa hii kuwadanganya watanzania kwa sababu anafahamu fika kuwa uwezo wetu wa kukumbuka na kufafananisha mambo ni mmdogo miongoni mwetu sisi watanzania tuliyowengi.

    Huyu LOWASA ni mshiriki ktk mkataba misheni town wa RICHMOND, na kupewa jina lingine la DOWANS angalia yalitokea hapo...walalahoi ndiyo watakahumia kulipa uhuni uliofanywa na mafisadi.

    Hivyo Bwana Chahali hakuna mtu yeyote mzuri kwa watanzania na Taifa hili miongoni wa hawa wote wababaishaji Lowasa na Makamba.

    Leo hii CHADEMA ndiyo chama pekee kilichoonesha na kuutangazia umma wa watanzania wazi kwa vitendo ni kikwazo chetu cha maendeleo, uhuru na vita vya kupinga ufisadi ni katiba iliyopo. Hivi wanachama viongozi wa mafisadi wote wanaleta unafiki wa kuunga mkono juhudi za chadema kwa lengo la kwanza kupata anttetion from press halafu wa wateuliwe ktk kushughulikia kuunda katika mpya ili waje waichachue tena kama walivyofanya kwenye sheria fedha za uchaguzi.

    Watanzania tuamke kuwa makini matapeli,wezi,majangili ya haya ya ufisadi

    ReplyDelete
  6. JAMAN WANANCHI TUSIDANGANYIKE NA HUYU LOWASA ETI LEO HII ANAJIDAI KUINGILIA KAMA VILE MWEMA JAMAN TUFUNGUKE MACHO RICHMOND ILITUTOSHA, AKAE PEMBENI AMETUMALIZAAAAAAAAAA

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.