22 Jan 2011


Imagine wale vibaka wanaowanyima raha pale mtaani wasingekuwepo!

Imagine baba au mama mwenye nyumba angeheshimu mkataba mlowekeana kuhusu jengo unalopanga kwake,na kutambua kuwa kodi unayolipa ina-cover uhuru na haki zako kama mpangaji!

Imagine waandaaji wa filamu za kibongo wangezingatia zaidi uwezo na vipaji vya waigizaji badala ya maumbile au "jina kubwa" (kama sio rushwa za ngono)!

Imagine vituo vya redio vinavyojigamba kuwa vinawalenga vijana vingeachana na watangazaji vilaza wanaojifanya kuifahamu siasa (na hivyo kujipachika wadhifa wa political analysts/commentators) japo wanatambua uwezo wao ni zero,zilch,nada,sifuri,kaput!

Imagine ajira na promosheni makazini vingezingatia ujuzi na uwezo badala ya kujuana plus undugunazesheni (not forgetting rushwa za ngono)!

Imagine baadhi ya wachunga kondoo wa Bwana wangetambua kuwa wanamkasirisha Muumba kwa "kugeuza kondoo wake kuwa vitoweo vya bure" japo wakiwa madhabahuni wanakemea kwa nguvu zote ubanjuaji wa Amri ya Sita!

Imagine na sie mabloga tungejifunza kutoka kwa kampeni ya Rais Obama na,kwa hivi karibuni kabisa,Tunisia,na kuwekeza nguvu zetu katika matumizi ya social media ku-address matatizo yanayoikabili nchi badala ya hali ilivyo sasa ambapo baadhi yetu wako bize zaidi kujikomba kama sio kuripoti tu matukio (na hapa tunaweka kando wenzetu ambao wako bize zaidi na "flani kafanya hili au lile" badala ya nini kifanyike kuikomboa jamii yetu)!

Imagine vyombo vya habari vinavyoendeshwa kwa fedha za walipa kodi vingetambua kuwa kazi ya kupigia debe CCM inapaswa kuachwa kwa Uhuru,Mzalendo na Redio Uhuru pekee!

Imagine Kamati Kuu ya CCM ingekuwa na wazalendo wa kutambua kuwa hata kichaa akiporwa hawezi kumlipa aliyempora,sembuse wao watu wenye akili timamu na wenye dhamana ya kutuongoza lakini wanaendekeza ufisadi na kuhalalisha malipo kwa majambazi wa Dowans!

Imagine....Imagine...Imagine...Too much imagination

And imagine,fani ya siasa Tanzania ingeachwa kwa wenye wito,uwezo na uzalendo badala ya hali ilivyo sasa ambapo kila Tom,Dick and Harry anayeweza kununua wapiga kura anaweza kulala jambazi akaamka mbunge,kama sio waziri au mkurugenzi wa hovyo hovyo!

Na imagine ulimwengu wa siasa za Tanzania ungekuwaje laiti baadhi ya viumbe wangetambua umuhimu wa co-ordinationa kati ya ubongo na mdomo kabla ya kuropoka lolote hadharani.Kwa hakika dunia ingekuwa mahala bora sana pa kuishi laiti baadhi ya wanasiasa wasemaovyo,vichwa maji,vichwa makabati matupu,nk wasingepewa fursa ya kuongoza hata kundi la mifugo,let alone kuongoza wananchi.

Yes,dunia ingekuwa mahala bora kabisa laiti watu kama Yusuph Makamba na Tambwe Hiza wasingeruhusiwa kutamka lolote hadharani hadi itakapothibitika kuwa watakachoongea hakitazidi kuisogeza Tanzania yetu kuelekea kwenye mshikemshike kama wa huko Ivory Coast, au mahala kwingine kwenye mapigano ya wenyewe kwa wenyewe.

Talking of Tambwe Hiza,nimeshindwa kujizuwia kupaliwa na kicheko baada ya kukutana na habari ifuatayo:

Tambwe Hiza alazwa

na Betty Kangonga

SIKU moja baada ya kumshambulia Katibu Mkuu wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Dk. Willibrod Slaa, kaimu katibu mkuu wa kitengo cha propaganda wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Richard Hiza, amelazwa katika Hospitali ya Regency akisumbuliwa na maradhi ya pumu.

Akizungumza na Tanzania Daima jana kwa njia ya simu mmoja wa ndugu wa karibu ambaye hakupenda jina lake litajwe kwa kuwa si msemaji wa familia, alisema Hiza alilazwa kwa mara ya kwanza katika Hospitali ya Mbagala Kizuiani akisumbuliwa na maradhi hayo.

Alisema Hiza alizidiwa usiku wa juzi muda mfupi baada ya kurejea kutoka kazini na kukimbizwa katika hospitali hiyo kwa ajili ya kupatiwa matibabu.

Alisema baada ya vipimo vya kiuchunguzi Hiza alibainika kusumbuliwa pia na shinikizo la damu hivyo kulazimu kumhamishia Hospitali ya Regency kwa matibabu zaidi.

“Kwa kweli hali yake haikuwa nzuri na alikuwa hawezi kuzungumza; maana tatizo lake limemuanza ghafla sana ingawa ana tatizo la pumu kwa muda mrefu lakini tumeshangaa hali yake kuwa hivi,” alisema.

Hiza ameugua ikiwa ni siku moja tu baada ya kukaririwa na gazeti moja la kila siku siyo Tanzania Daima akidai Dk. Slaa ana wazimu, amebakiza kuvua nguo na kwamba ni mfa maji anayetapatapa.

Hiza alitoa kauli hiyo akidai kwamba Dk. Slaa ana hofu ya kufungwa kwani serikali ya CCM imepania kufanya hivyo ili kumnyamazisha.

Akitumia lugha ya matusi, Hiza alinukuliwa akisema, “Ninachoweza kusema kwa sasa ni kwamba kiongozi huyo amepandwa na wazimu, alichobakiza ni kuvua nguo tu…amechanganyikiwa na ndiyo maana anatapatapa kutafuta lolote la kusema.

CHANZO: Tanzania Daima
Lol!Mchimba kisima katumbukia mwenyewe kisimani.Jitu zima ovyooo!Linaropoka tu,na kujipachika udaktari wa magonjwa akili to an extent of kum-diagnose Dkt Slaa na maradhi ya akili,kumbe lenyewe lina matatizo makubwa ya afya.Msomaji mpendwa,huhitaji hata dakika moja ya kozi ya utabibu kumaizi kuwa kichaa cha kuzuzshiwa hakifui dafu kwa gonjwa la hatari kama PUMU na SHINIKIZO LA DAMU.

Naomba nisiwe mnafiki kumwombea Tambwe apate nafuu.Ndio,Biblia inatuasa kuwapenda maadui zetu lakini busara katika jamii zinatuasa pia kuwa ADUI YAKO MWOMBEE NJAA (njaa hapo symbolises mambo mabaya kama hayo yalomkuta Msema Ovyo Tambwe Hiza).

Kufungika kwa mdomo mmoja mchafu kunaifanya dunia kuwa mahala bora kabisa kuishi.Sio siri kwamba laiti maradhi yanayomkabili Tambwe yakipelekea kupunguza,kama sio kumaliza,tatizo lake la kuutumia ubongo wake kama matope,kisha kuunyima ubongo huo ushirikiano na mdomo wake,and therefore kupelekea uropokaji usiosahili hata kwenye vilabu vya gongo,siasa za Tanzania zinaweza kuchukua sura mpya.Yaani,siasa minus mbwatukaji mmoja ambaye kauli zake za ovyo ovyo ni maarufu zaidi kuliko madaraka yake.

Ndio maana nimeandika hapo juu kuwa MUNGU SI TAMBWE HIZA.Yeye anajifanya kumsemea ovyo Dokta Slaa,na kumhukumu kuwa ana kichaa,ilhali yeye Tambwe ndiye mwenye matatizo makubwa ya kiafya yanayoweza kabisa kuwa na uhusiano na tabia yake ya kuropokaropoka.

IMAGINE SIASA ZA TANZANIA MINUS UROPOKAJI WA TAMBWE HIZZA!SURELY,THAT WOULD MAKE THE WORLD SUCH A WONDERFUL PLACE TO LIVE...Lol!

2 comments:

  1. Evaist kweli umetoa. Imagine tungekuwa na watanzania 10% wenye uwezo wa kudigest mambo kabla ya kuyatoa mdomoni au kabla ya kuyaweka kwenye vitendo tusingefika hapa tulipo. Hivi unafikiri Dr. anaweza kupata wanasheria wa kumsaidia kumfikisha Tambwe hiza na CCm vijana mahakamani kwa kosa la kumdhalilisha kumwita kichaa?

    Je, hawezi kwenda kupata vyeti vya madaktari kuhusu hali yake ya ubongo halafu aitumia kwenda kuwashitaki Chukua Chako Mapema?

    Imagine nchi yetu ingekuwa na watu wanaotoa hukumu kufuatana na haki, Zombe angekuwa huru au mzee wa vijisenti angekuwa huru wakati yule kijana aliyemsababishia kifo Wangwe yupo jela? Aloua awatatu na mwingine wawili wapo huru wanapeta pamoja na kwamba kama umeshitakiwa na kuhukumiwa huna sifa ya kuwa kiongozi wa serili au chama chochote kikatiba.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube