29 Apr 2011Baada ya miezi,wiki na masaa,hatimaye ile siku ya kihistoria imewadia.Leo,Ijumaa ya tarehe 29 April 2011,mjukuu wa Malkia Elizabeth wa Pili,Prince William,anafunga ndoa na mchumba wake Kate Middleton,jijini London.Inatarajiwa zaidi ya watu bilioni mbili duniani kote watakuwa wakifuatilia harusi hiyo kwenye runinga zao.

Kwa bahati nzuri,dada yetu Miss Jestina,anatarajia kufuatilia tukio hilo la kihistoria kwa karibu zaidi,na kila kitu kikienda kama kilivyopangwa basi atatuletea up-to-the-minute updates kuhusu tukio hilo la aina yake.Pamoja na mengineyo,anatarajiwa kufanya mahojiano na watu mbalimbali watakaohudhuria shughuli hiyo.

Wakati tunawatakia Prince William na mkewe mtarajiwa Kate ndoa njema na ya amani basi usikose kufuatilia shughuli hiyo ya kihistoria katika blogu ya dada yetu Miss Jestina,live and direct from London hapa Uingereza.

Bonyeza  picha ifuatayo kutembelea blogu ya Miss Jestina

Stay tuned

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube