1 May 2011


Wanasema "kisasi ni sawa na chakula ambacho ladha yake inaongezeka kinapokuwa kimepoa".Maana ya msemo huo ni kwamba kisasi kinamuumiza zaidi mkosaji pale mkosewa anapomvutia muda mkosaji hadi anasahau kuwa alishawahi kumkosea mtu,kisha mkosewa analipiza kisasi.Inakuwa kama kuchonokoa kidonda kilichokwishapona.

Lakini inaelekea Rais Barack Obama hakutaka kusubiri hadi Donald Trump asahau kuwa alikuwa kinara wa fitna kwamba Obama si raia wa Marekani.Na jana alipata fursa mwanana ya "kumfanyizia" tajiri huyo wa uwekezaji kwenye majengo.

Katika hafla ya kila mwaka ya Waandishi wa Habari wanaoripoti habari kutoka Ikulu ya Marekani ambapo mgeni rasmi huwa Rais,Obama alimrushia Trump vijembe vikali lakini katika hali ya utani,kama ilivyo desturi ya halfa hiyo.

Hikuwa siku nzuri kwa Trump aliyehudhuria hafla hiyo kwa mwaliko wa gazeti la Wahington Post.Alipowasili tu alikumbana na sauti za kuzomewa.Lakini alikuwa Obama aliyemnyong'onyeza tajiri huyo kwa vijembe vikali vya utani wenye ukweli.

Obama alimkebehi Trump kwa kijembe kwamba ana furaha suala la wanaodadisi uraia wake sasa limekwisha kwahiyo Trump atapata wasaa wa kuchunguza kama kweli wataalamu wa anga walifika kweli mwezini,na iwapo Tupac na Biggie (Notorious B.I.G) kweli waliuawa.

Lakini kimbembe kwa tajiri huyo hakikuishia kwa vijembe vya Obama pekee kwani mchekeshaji maarufu Seth Meyer hakubaki nyuma katika "kummaliza" Trump.Alimgalagaza kwa kutanabaisha kuwa "Donald Trump amekuwa akieleza kuwa atagombea urais kwa tiketi ya chama cha Republican,jambo ambalo ni la kushangaza...nilidhani jambo pekee analoweza kugombea ni kuwa kituko".

Kadhalika,Obama aliwatania pia baadhi ya wagombea urais watarajiwa wa Republicans kwa kusema tetesi zinaonyesha kuwa Michelle Buchmann,mwanamama kipenzi cha wahafidhana wa Tea Party Movement,alizaliwa Canada na sio Marekani (na kumkumbusha kuwa majungu huwa yanaanza kihivyo).Pia alimtania mgombea mwingine mtarajiwa Tim Pawlenty kwa kudai amesikia kwamba jina kamili la mwanasiasa huyo ni Tim HOSNI Pawlenty (akimaanisha pengine ana asili ya Misri kwa akina HOSNI Mubarak).

Sio siri.Kwa mara ya kwanza kabisa nilimwonea huruma Trump alipokuwa akipigwa vijembe na Obama na Meyer huku ukumbi ukilipuka kwa mayowe.Lakini ndio hivyo,mkuki mtamu kwa nguruwe lakini kwa binadamu mchungu.

Angalia clip ifuatayo kisha jiburudishe kwa video za Tupac na Biggie (kwa vile walitajwa katika hafla hiyo)




1 comment:

  1. Kweli Obama aliniua mbavu hapa...ukimya ulizidi Trump akajiona he has won...people were just watching him and ridiculing him....where are his supporters now?..it doesnt make sense...from all the presidents who've been in offfice,Obama is the first one to be called out to show out his Birth certificate...by who?...a media mogul who runs beauty pageants and thinks he's got influence coz he can say 'ur fired' on TV.u dont come at a president like that...he should have known...now he is the laughing stock of the country

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.