9 Dec 2011LEO NI SIKU MUHIMU KWANGU KWANI NINATIMIZA MIAKA KADHAA TANGU NIZALIWE.LAKINI SIKU HII NI MUHIMU PIA KWA TANGANYIKA KWANI NAYO INATIMIZA MIAKA 50 TANGU IZALIWE.


NAMSHUKURU MUNGU KWA MEMA YOTE ALIYONIJALIA,ANAYONIJALIA NA NINAYOAMINI ATAZIDI KUNIJALIA.NAWASHUKURU PIA WAZAZI WANGU-BABA MZEE PHILEMON CHAHALI NA MAREHEMU MAMA ADELINA MAPANGO KWA KUNILETA DUNIANI.LICHA YA KUNIZAA,MALEZI BORA NA MWONGOZO WALIONIPATIA TANGU NIZALIWE UMESAIDIA SANA KUNIFIKISHA HAPA NILIPO LEO.

NAWASHURU PIA NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI KWA SAPOTI NA SALAMU ZA HERI KWA SIKU HII MUHIMU.SHUKRANI ZA PEKEE KWA MTU MAALUM ALIYENIPIGIA SIMU LEO SAA 6 KAMILI USIKU (KWA SAA ZA TANZANIA) KUNIPA SALAMU ZA BIRTHDAY.MUDA HUO,MIAKA KADHAA ILIYOPITA NDIO MUDA MAMA ALIKUWA ANAJIFUNGUA MIE (NILIZALIWA SAA 6 USIKU),NA KWA KUKUMBUKA KUNIPIGIA SIMU MUDA HUO KUNIPA HEPI BESDEI NI KAMA UMEMWAKILISHA MAMA AMBAYE KIMWILI HATUPO NAYE JAPO KIROHO YUPO NASI.

NIMALIZIE KWA KUSEMA 
HAPPY BIRTHDAY ME...
HAPPY BIRTHDAY TANGANYIKA
2 comments:

  1. Hongera kaka Evert kwa kutimiza miaka kadhaa na hongera Tanganyika kwa kutimiza miaka 50.

    ReplyDelete
  2. HAPPY BIRTHDAY TO YOU TWO!

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.