Showing posts with label HAPPY BIRTHDAY GREETINGS. Show all posts
Showing posts with label HAPPY BIRTHDAY GREETINGS. Show all posts

13 Aug 2016

14026664_162506520845816_426045486_n
Leo ni siku ya kuzaliwa ya mwana-hiphop mahiri na lejendari nchini Tanzania, Fareed Kubanda a.k.a Fid-Q. Na katika kuadhmisha birthday yake, msanii huyu ambaye sio tu amedumu "kwenye fani" kitambo bali pia ni miongoni mwa waasisi wa Swahili Hip-Hop.

 Kwangu, Fid-Q sio tu ni msanii maarufu kabisa huko nyumbani Tanzania na katika Swahii hip-hop duniani, bali ni mmoja wa watu ambao wamkuwa wakinipatia sapoti kubwa katika kazi zangu za uandishi wa vitabu. Na ndio maana kwa kutambua mchango wake huo, alikuwa mtu wa kwanza kupata nakala dhahiri ya kitabu changu kuhusu taaluma ya uafisa usalama wa taifa (ushushushu) kama inavyoonyesha pichani chini.

 Jana niliuliza huko kwenye mtandao wa kijamii wa Twitter kuhusu wimbo gani wa Fid-Q unawavutia zaidi mashabiki wake. 



Jibu jepesi lilikuwa "kila wimbo wake unavutia." Nimesikiliza hii track mpya ya 'SUMU.' Imesheheni kauli nyingi za busara. Nitamwomba Fid-Q anitumie mashairi ya wimbo hu ili kuwaletea ninyi wasomaji uchambuzi zaidi ya wimbo huo. Lakini hata bila uchambuzi, kwa kuusikia tu, utaafikiana nami kuwa umeshehenu busara tele.

 Na hiki ndio kinachomfanya Fareed aendelee kuwa mmoja wa wasanii wachache na adimu kabisa Tanzania sio tu kuwa waasisi wa fani bali pia wasiochuja: kuwa na nyimbo zenye ujumbe usiochuja. Kama ingekuwa ni muziki wa bendi basi tungelinganisha na timeless tunes za kina Mbaraka Mwinshehe, Marijan Rajabu, Bitchuka, Shaban Dede, nk ambao tungo zao zilituvutia tangu tukiwa utotoni (kwa tulozaliwa enzi hizo) na ni tamu hadi leo. Na utamu so wa ladha tu bali pia relevance ya ujumbe uliomo. 

 Basi nisiandike 'gazeti,' bali nimtakie Fareed heri ya siku yake ya kuzaliwa, na kumtakia kila la heri na fanaka maishani, na kumshukuru kwa sapoti yake kwa kazi zangu, na kumpongeza kwa kutupatia 'SUMU.' Isikilize hapa chini

7 Jun 2016

Heri ya siku yako ya kuzaliwa, dear Sintah. Mwenyezi Mungu akujaalie kila la heri na baraka katika maisha yako. Asante sana kwa kuwa ndugu mwema. Siku zote umekuwa kama ndugu uliyezaliwa tumbo moja nami. Siku yako ya kuzaliwa imeangukia wakati mwafaka, mwanzo wa Mwezi Mtukufu wa Ramadhan, na kwahiyo naomba pia kukutakia Ramadhan Kareem.

9 Dec 2015

Siku ya leo ninaadhimisha birthday tatu kwa mfululizo, mbili zangu binafsi na moja pamoja na Watanzania wenzangu. Wakati Tanzania inatimiza miaka 54 tangu ipate uhuru, nami ninatimiza miaka kadhaa tangu nizaliwe, nikiwa mtoto wa tano wa familia ya watoto wanane ya marehemu baba yangu mpendwa Philemon Chahali na marehemu mama yangu mpendwa Adelina Mapango.

Lakini leo pia ni siku ambayo kampuni yangu ya huduma za ushauri wa kitaalamu (consulting services) inazaliwa rasmi, Kampuni hii ni matokeo ya uamuzi wangu wa kutafsiri ujuzi na uzoefu wangu wa muda mrefu katika maeneo kadhaa na kuufanya kuwa kazi rasmi. 

Jina la kampuni, yaani AdelPhil, ni kumbukumbu ya marehemu mama ADELina na marehemu baba PHILemon,. Imesajiliwa hapa Uingereza lakini itatoa huduma za kimataifa katika maeneo ya Intelijensia na Usalama, mikakati ya siasa (political strategies), na masoko kupitia mitandao ya kijamii (social media marketing). Lengo hasa la kampuni hii ni kuliunganisha eneo la Maziwa Makuu (Great Lakes region) yaani Tanzania, Kenya, Uganda, Burundi, Zaire na Jamhuri ya KidemOkrasia ya Watu wa Kongo (DRC) na dunia kwa ujumla. Awali, msisitizo utakuwa kati ya Tanzania na Uingereza. 

Pamoja na sababu nyingine, kuanzishwa kwa kampuni hii ni katika kuunga mkono jitihada za serikali ya Awamu ya Tano chini ya uongozi uliotukuka wa Rais Dkt John Magufuli, ambaye tangu aingie madarakani amekuwa akifanya jitihada kubwa kuipeleka Tanzania yetu mahali inapostahili. AdelPhil itawasaidia Watanzania - kwa maana ya taasisi za umma na binafsi na watu binafsi - kulifikia soko la huduma na bidhaa hapa Uingereza (kwa kuanzia) na wakati huohuo kuwezesha wateja wa hapa Uingereza kulifikia soko la hudma na bidhaa nchini Tanzania. Baadaye wigo utatanuliwa ili kufikisha huduma hizo kwa nchi zote za Maziwa Makubwa na dunia kwa ujumla (hususan Ulaya Magharibi).

Basi nitumie fursa hii kumshukuru Mungu kwa kunijaalia mwaka mwingine. Japo mwaka huu ninaomaliza ulikuwa mgumu kwangu kutokana na kumpoteza baba yangu mpendwa, Marehemu Philemon Chahali, miaka 7 baada ya kumpoteza mama yangu mpendwa, Marehemu Adelina Mapngo, na sasa kubaki yatima.

Hata hivyo, japo nusu ya pili ya mwaka huu ilianza kwa kifo cha baba, hatimaye nilipata nguvu na kushiriki kikamilifu katika kampeni za uchaguzi mkuu huko nyumbani ambapo hatimaye Rais Dkt Magufuli aliibuka mshindi. Ushiriki huo umechangia sana wazo la kuanzishwa kwa kampuni ya AdelPhil baada ya kupata ushauri kutoka kwa watu kadhaa.

Uchungu mkubwa katika siku hii ni kutokana na ukweli kwamba kila mwaka, siku yangu ya kuzaliwa iliambatana na Marehemu baba kuniimbia happy birthday, kwa simu niwapo mbali na nyumbani, lakini hii ni birthday ya kwanza ambapo nitakosa upendo huo mkubwa wa baba kwa mwanae. Lakini yote ni mipango ya Mungu, na ninaamini wazazi wangu wapendwa huko walipo wanapata faraja kuona mtoto wao naanzisha kampuni ambayo nime-dedicate jina lake kwao.

Kwa Watanzania wenzangu, wito wangu mkubwa kwenu ni kuendelea kuunga mkono jithada za Rais Dkt Magufuli kwa sababu tuna malima mrefu wa kupanda na anahitaji kila aina ya ushirikiano wetu. Mie ndo mchango wangu wa kwanza ni huo wa AdelPhil Consultancy, kampuni ambayo japo inafanya biashara lakini pia ni ya kuwatumikia Watanzania wenzangu na nchi yetu kwa ujumla. Katika siku zijazo nitaelezea kwa undani ni jinsi gani waweza kunufaika na huduma za kampuni hii.

Nimalizie kwa kusema HAPPY BIRTHDAY TANZANIA, HAPPY BIRTHDAY ME, na HAPPY BIRTHDAY ADELPHIL CONSULTANCY

9 Dec 2014

Wakati Tanzania Bara inatimiza miaka 53 ya uhuru, leo pia ni siku yangu ya kuzaliwa. Naitakia nchi yangu kila la heri na fanaka, na Mweneyzi Mungu aiongoze nchi yetu kwenye njia njema, sambamba na kuiepusha na mabalaa. Kwa mujibu wa mambo yalivyo huko nyumbani, hali si ya kuridhisha sana. Basi ni muhimu tuitumie siku hii muhimu kuiombea nchi yetu kwa kila jema.

Kwangu, siku hii ya kuzaliwa ni fursa nyingine ya kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia kuongeza mwaka mwingine katika maisha yangu. Nawashukuru sana wazazi wangu Baba Mzee Philemon Chahali na mama yangu mpendwa, marehemu Adelina Mapango (we all miss you so much mom). Pia nawashukuru wanafamilia wenzangu, ndugu, jamaa na marafiki kwa mema yote waliyonifanyia. Natumaini mtaendeleo kuwa nami siku zote za uhai wangu.

Nwashukuru nanyi wasomaji wa blogu hii, marafiki zangu wapendwa ambao nawafahamu kwa kuangalia idadi ya wanaotembelea blogu hii. Japo pengine wengi wenu hatufahamiani personally, lakini mnapochukua muda wetu muhimu kunitembelea hapa, kuvumilia makelele yangu na 'upuuzi' wmingine ninaoandika, ni faraja kubwa mno kwangu. Nawashukuru kwa kuwa sehemu ya familia yangu kiuandishi.

Nimalizie kwa kumwomba Mwenyezi Mungu azidi kunijalia afya njema, maisha marefu, afya njema kwangu, familia, yangu, ndugu, jamaa na marafiki, na niwe na mafanikio katika kila jambo. Amen

9 Dec 2013

Happy birthday Tanzania
Happy birthday ME
#tweetgram #instamood #tagstagram #instadaily #instagramhub #statigram #igdaily #ignation

Ninapenda kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijali mwaka mwingine katika uhai wangu. Tarehe kama ya leo, miaka kadhaa iliyopita, familia ya Mzee Philemon Chahali na mkewe marehemu mama Adelina Mapango (Mungu ailaze roho yake mahali mema peponi) ilipata mtoto wa tano, wa kiume, na kumpa jina la Jamhuri kwani alizaliwa siku ya Uhuru na Jamhuri. Baadaye mtoto huyo alibatizwa na kupewa jina la Mtakatifu Evarist. 

Mwaka uliopita ulikuwa na majaribu kadhaa, kubwa zaidi ni tukio ambalo kamwe sintolisahau maishani mwangu, tarehe 2 ya mwezi Februari mwaka huu ambapo vyombo vya usalama hapa Uingereza vilinifahamisha kuwa kulikuwa na tishio la kuaminika (credible threat) dhidi ya maisha yangu. Wakati hadi leo sifahamu kwa undani kuhusu waliohusika na mkakati huo wa kidhalimu, wala kufahamu wanausalama wa hapa walifanikiwaje kujua kuhusu mpango huo, habari isiyopendeza ni ukweli kuwa hadi leo bado naishi kwa tahadhari. Wanausalama wa hapa wamekuwa wakini-update mara kwa mara, lakini wanasisitiza kuwa kwa vile hawajapata taarifa yoyote kuwa tishio hilo dhidi ya uhai wangu limekwisha, sina budi kuendelea kuzingatia ushauri wao kuhusu hatua za tahadhari kwa usalama wangu. Kwa hakika ni jambo gumu na la kuogofya lakini kwa sasa imekuwa ni sehemu ya maisha yangu ya kila siku. Hata hivyo, kwa ulinzi wa Mungu na jitihada zangu mwenyewe, ninatumaini kuwa nitaendelea kubaki salama.

Kwa bahati nzuri (au mbaya?) siku yangu ya kuzaliwa inagongana na siku ya kuzaliwa kwa Tanganyika (Tanzania Bara). Nasema kwa bahati nzuri kwa vile inapendeza kushea birthday na nchi yangu. Hata hivyo, kwa bahati mbaya (makusudi?) mwenendo wa birthday buddy wangu Tanzania Bara si wa kuridhisha hata kidogo. Kwa upande mmoja taifa letu linabakwa na mafisadi huku umasikini ukizidi kukua. Kwa hakika ni  vigumu kubashiri hatma ya taifa letu angalau miaka 10 ijayo.

Hata hivyo, kwa vile leo ni sikukuu yetu ya kuzaliwa, basi sina budi kuitakia Tanzania Bara heri na baraka ya kuzaliwa na kujitakia happy birthday mie mwenyewe pia. Ndio maana kichwa cha habari kinasema HAPPY BIRTHDAY TANZANIA BARA, HAPPY BIRTHDAY ME!

12 Aug 2013






3 Jan 2013



Moja ya malengo ya blogu hii kwa mwaka huu ni kusherehesha kazi,matukio na mambo mbalimbali yanayowahusu mabloga wenzangu.

Kwa kuanzia basi, ninapenda kumtakia heri ya siku ya kuzaliwa bloga mwenzetu,Mtanzania anayeishi huko Scandinavia, NAXYLADY ambaye ni mmiliki wa blogu ya AFRICA4LIFE

Ninakutakia siku njema ya kuzaliwa pamoja na kila la heri katika maisha yako.

Enjoy your big day

9 Dec 2012

Nilizaliwa tarehe kama ya leo, miaka makumi kadhaa yaliyopita. Siku yangu ya kuzaliwa 'inagongana' na siku ya kuzaliwa kwa taifa letu la Tanzania (au Tanganyika?) tulipopata uhuru tarehe 9 Disemba mwaka 1961.

Tofauti na wengineo ambao haudhimisha siku za kuzaliwa kwa pati, mie hutilia mkazo zaidi katika sala (kumshukuru Mungu kwa kunijalia miaka yote hiyo,na kumwomba anibariki nipate miaka zaidi) na kufanya tafakuri ya wapi nimetoka,nilipo na ninakoelekea.

Kwa 'somo' wangu Tanzania, yeye birthday yake ni tofauti kabisa na yangu japo tuna-share tarehe moja (ila miaka tofauti). Mwenzangu huadhimishiwa siku yake kwa gwaride na hotuba mbalimbali.Lakini pia kwa vile birthday ya Tanzania inamgusa kila Mtanzania, sikuhii inakuwa na umuhimu wa kipekee kufanya tathmini ya taifa limetoka wapi, lipo wapi na linaelekea  wapi.

Kwabahati mbaya (au pengine kwa makusudi ya wenzetu wachache) kila inapojiri birthday ya Tanzania tunajikuta na maswali mengi zaidi kuliko majibu.Wengi wanajiuliza kwanini tuendelee kuwa masikini wa kutupa ilhali tuna kila aina ya utajiri.Kwamtizamo wangu, wa kulaumiwa zaidi si viongozi tuliowapa dhamana ya kutuongoza bali 'uzembe' wetu wakuchagua viongozi pasi kuzingatia kama wataweza kututumikia kwa dhati na uadilifu.

Enewei, hii sio siku ya kuandika makala ndefu. Namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia kumaliza na kuanza mwaka mwingine huku nikitarajia baraka zaidi kutoka Kwake. Nwashukuru pia wazazi wangu, Baba  Mzee Philemon Chahali na marehemu mama Adelina Mapango kwa kunizaa. Pasi mapenzi ya Mungu na wazazi wangu hao leo nisingekuwepo kuadhimisha siku hii ya kuzaliwa.Nawashukuru piawanafamilia wenzangu,ndugu,jamaa na marafiki kwa kuniwezesha kufika hapa nikiwa hai.

Nawashukuru pia ninyi mnaotembelea blogu hii kwani mmekuwa sehemu ya familia yangu ya kijamii tangu mwaka 2006. Baadhi yenu tunafahamiana,baadhi yenu hatufahamiani lakini kwa umoja wenu mmenifanya kuwa mwenzenu na kupita eneo hilimara kwa mara.

Shukrani pia kwa watu mbalimbali niliofahamiana nao aidha kupitia uandihi wa makala au kwa kukutana kwenye mitandao ya kijamii, hususan Twitter na Facebook.

ASANTENI SANA NA MUNGU AWABARIKI 

13 Mar 2012

Your dad would have  probably sang the following song for you.Now you can sing it for kijana wetu.As Big Will raps,I think sometime you wonder what our dogo will turn out to be when he grows up.."a general,a doctor,or may be an MC (like you his dad)..."

And we all gave some hard time to our moms.It's time to appreciate how they raised us and all the pain we gave them

And these are my special messages for your special day.First,we all have dreams...

And we all know we can be what we gonna be if we work hard at it...

And you know what,the stuff we frequently talk on Twitter makes us like the street radio for unsung heroes..WE DO FOR THE PEOPLE

And although it's hard knock life out there

But hey,it's you big day...we the last ones left...and life should go on

Any birthday is party

And in the evening...enjoy your big day as if it's FIESTA

8 Mar 2012




I didn't forget about your birthday; I just wanted to help prolong the celebration.

I didn't really forget your special day, I just figured you deserved more than one.

Even though this message comes to you a little late, the wish it brings for happiness is good on any day date.

Happy belated birthday.





21 Feb 2012


It's your birthday and I can't be there
But I'll send you a special birthday wish and a little prayer
Have a happy birthday
I hope that all of your birthday wishes come true
May you have a great time today and find happiness in everything you do.






28 Jan 2012



Kwa niaba ya wasomaji wa blogu hii naomba kukutakia heri kwa siku yako ya kuzaliwa.Ni matumaini yangu kuwa utaendelea kuwa accessible na kudumisha dhana ya uongozi ni pamoja na kuwa karibu na wananchi.Ninatumaini pia kuwa tutaendeleza mijadala mbalimbali kwenye 'kijiwe chetu' cha Twitter.

Enjoy your big day!

15 Dec 2011

9 Dec 2011



LEO NI SIKU MUHIMU KWANGU KWANI NINATIMIZA MIAKA KADHAA TANGU NIZALIWE.LAKINI SIKU HII NI MUHIMU PIA KWA TANGANYIKA KWANI NAYO INATIMIZA MIAKA 50 TANGU IZALIWE.


NAMSHUKURU MUNGU KWA MEMA YOTE ALIYONIJALIA,ANAYONIJALIA NA NINAYOAMINI ATAZIDI KUNIJALIA.NAWASHUKURU PIA WAZAZI WANGU-BABA MZEE PHILEMON CHAHALI NA MAREHEMU MAMA ADELINA MAPANGO KWA KUNILETA DUNIANI.LICHA YA KUNIZAA,MALEZI BORA NA MWONGOZO WALIONIPATIA TANGU NIZALIWE UMESAIDIA SANA KUNIFIKISHA HAPA NILIPO LEO.

NAWASHURU PIA NDUGU,JAMAA NA MARAFIKI KWA SAPOTI NA SALAMU ZA HERI KWA SIKU HII MUHIMU.SHUKRANI ZA PEKEE KWA MTU MAALUM ALIYENIPIGIA SIMU LEO SAA 6 KAMILI USIKU (KWA SAA ZA TANZANIA) KUNIPA SALAMU ZA BIRTHDAY.MUDA HUO,MIAKA KADHAA ILIYOPITA NDIO MUDA MAMA ALIKUWA ANAJIFUNGUA MIE (NILIZALIWA SAA 6 USIKU),NA KWA KUKUMBUKA KUNIPIGIA SIMU MUDA HUO KUNIPA HEPI BESDEI NI KAMA UMEMWAKILISHA MAMA AMBAYE KIMWILI HATUPO NAYE JAPO KIROHO YUPO NASI.

NIMALIZIE KWA KUSEMA 
HAPPY BIRTHDAY ME...
HAPPY BIRTHDAY TANGANYIKA




30 Oct 2011




BLOGU HII INAPENDA KUTOA SALAMU ZA HERI YA SIKU YA KUZALIWA KWA JARIDA MWANANA LA RAIA MWEMA AMBALO LILIZALIWA SIKU KAMA YA LEO MIAKA MINNE ILIYOPITA.

BINAFSI,JARIDA HILI NI KAMA SEHEMU YA MAISHA YANGU.TANGU WAHUSIKA WANIPATIE NAFASI YA KUANDIKA KATIKA JARIDA HILO KWWENYE SAFU YA TAIA MWEMA UGHAIBUNI NIMEKUWA NIKISHIRIKIANA NAO HATA NJE YA FANI YA UANDISHI.NILIPOUGULIWA NA MAREHEMU MAMA MWAKA 2008 NA HATIMAYE ALIPOFARIKI,WAHUSIKA WA JARIDA HILI WALIKUWA NAMI BEGA KWA BEGA.

NAKUMBUKA VIZURI SIKU NILIPOZURU OFISI ZAO KWA MARA YA KWANZA NA JINSI NILIVYOPOKELEWA KANA KWAMBA SOTE TULIKUWA TUKITANA HAPO OFINI KILA SIKU YA WIKI.

LAKINI KUBWA ZAIDI NI MCHANGO WA JARIDA HILI KWA JAMII.LICHA YA HABARI ZAKE MAKINI JARIDA LA RAIA MWEMA LIMEJIJENGEA SIFA KUBWA KWA KUWA NA MAKALA ZINAZOANDIKWA KWA UMAKINI WA HALI YA JUU NA LIMEFANIKIWA KWA ASILIMIA 100 KUTOELEMEA UPANDE WOWOTE ZAIDI YA KUSEMA UKWELI NA KUWA SAUTI YA WASIO NA SAUTI.

NAJISIKIA FAHARI KUBWA KUWA MIONGONI MWA WANA-TIMU WA JARADA HILI,NA NI FURAHA KUBWA KUONA RAIA MWEMA LIKITIMIZA MIAKA MINNE HUKO LIKIZIDI KUPAA KWA KUAMINIKA KATIKA JAMII NA KUENDELEA KUUTUMIKIA UMMA KWA UADILIFU.

KWA MARA NYINGINE TENA,NA KWA NIABA YA WASOMAJI WA BLOGU HII,NAOMBA KUSEMA TENA HAPPY BIRTHDAY RAIA MWEMA

29 Jul 2011


Kuna watu wana umuhimu wa kipekee kwa blogu hii na maudhui yake kiasi kwamba kuwatakia heri ya siku ya kuzaliwa kwenye Facebook wall yao pekee ni sawa na utovu wa nidhamu.Didi Vava,Mtanzania mwenzetu mwenye makazi yake huko Marekani,ni mdau mkubwa wa blogu hii,na ni miongoni mwa Watanzania wanaoguswa sana na jinsi nchi yetu inavyotafunwa na mafisadi wakisaidiwa na kiza cha mgao wa umeme.

Basi Mdau Didi, mimi binafsi na wasomaji wote wa blogu hii tunakutakia kila la heri kwa siku hii na katika maisha yako kwa ujumla.

24 Jun 2011

Kijana,heri kwa siku yako ya kuzaliwa.Nakutakia kila la heri katika maisha yako na usisahau kumtanguliza Mungu katika kila ufanyalo.Salamu kwa Mzee Kispuni (kushoto pichani chini) na dadangu Mama K.

20 Jun 2011

 
 
 
 

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.