27 May 2012

Naomba kuwaletea toleo la tatu la mfululizo wa Makala za Sauti.Kamanilivyobainisha katika matoleo mawili yaliyopita,hadi sasa bado nipo katika hatua ya majaribio.Ninafanya kila linalowezekana kupata vitendea kazi bora kabisa(ikiwa ni pamoja na softwares mwafaka) ili kukupatia wewe msikilizaji ubora unaostahili.

Katika toleo hili ninazungumzia Vurugu zinazoendelea huko Visiwani Zanzibar na sualazimala Muungano kwa ujumla.Kwa hakika,kiwango cha ubora wa makala hiyo bado sio cha kuridhisha,na pia sijapata kujiamini vya kutosha katika uwasilishaji wa mada husika (kwa mfano kutumia muda kidogo kuamua nitumie neno gani) lakini huu ni mwanzo,na ninadhamiria kwa zaidi ya asilimia 100 kuwa muda si mrefu nitawaletea kitu bora kabisa na mnachostahili kwa dhati.

Labda la mwisho ni kwamba ninafanya kila linalowezekana ili toleo zima la makala husika liwe kwa lugha ya taifa,yaani Kiswahili.Hiyo ni moja ya sababu ya wakati flani kuwa ninahangaika nitumie nheno gani mwafaka la kiswahili.Si kwamba nimesahau lugha yangu ila moja ya madhara ya kuwa huko nje kwa muda mrefu ni hilo.

Karibuni sana,na msisite kunitumia maoni (chagua player yoyote kati ya hizi mbili hapa chini)
 


2 comments:

  1. Hongera kaka, Kazi nzuri, nimeipenda hii sana!!!Kia la kheri.

    ReplyDelete
  2. Fadhil@granite city02/06/2012, 14:02

    Safi sana kaka, mbona kimya mkuu. Good idea, hii unasikiliza huku ukiendelea na shughuli nyingine

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.