Showing posts with label Makala za Sauti. Show all posts
Showing posts with label Makala za Sauti. Show all posts

24 Jul 2016


Jana Julai 23, 2016 Rais Dokta John Magufuli alichaguliwa kwa asilimia 100 kuwa Mwenyekiti mpya wa Taifa wa chama tawala CCM, na mtangulizi wake, Rais Mstaafu, Jakaya Kikwete, kung'atuka rasmi. Ufuatao ni uchambuzi wa kina kuhusu mabadiliko hayo ya uongozi wa juu kabisa wa chama hicho kikongwe, hasa fursa na changamoto kwa Mwenyekiti mpya Magufuli. Karibuni
Check this out on Chirbit

15 Jul 2016


Uchambuzi wangu wa kiintelijesnia kuhusu shambulio la kigaidi lililotokea jana usiku katika jiji la Nice, nchini Ufaransa ambapo hadi sasa watu 84 wameuawa na wengine zaidi ya 100 kujeruhiwa baada ya gaidi mmoja kuliingiza lori kwenye kundi la watu waliokuwa wakisherehekea siku ya kitaifa nchini humo. Bonyeza hapo chini kusikiliza uchambuzi huo

Check this out on Chirbit

10 Jul 2016


Check this out on Chirbit

30 Jun 2016


Check this out on Chirbit

4 Aug 2012

6 Jun 2012


Katika Toleo hili la Nne la MAKALA ZA SAUTI ninazungumzia Umoja wetu kama Msingi wa Amani linganifu (relative) tuliyonayo huko nyumbani.Kilichonihamasiaha kuzungumzia hilo ni maadhimisho ya miaka 60 ya utawala wa Malkia Elizabeti wa Pili na jinsi unavyowaunganisha Waingereza.Pia nimegusia lugha yetu ya Taifa Kiswahili na tishio linaloikabili licha ya kuwa moja ya mambo muhimu yanayotuunganisha Watanzania. Basi nisikumalizie uhondo,niskize hapa chini...na karibu sana kunitumia maoni.

27 May 2012

Naomba kuwaletea toleo la tatu la mfululizo wa Makala za Sauti.Kamanilivyobainisha katika matoleo mawili yaliyopita,hadi sasa bado nipo katika hatua ya majaribio.Ninafanya kila linalowezekana kupata vitendea kazi bora kabisa(ikiwa ni pamoja na softwares mwafaka) ili kukupatia wewe msikilizaji ubora unaostahili.

Katika toleo hili ninazungumzia Vurugu zinazoendelea huko Visiwani Zanzibar na sualazimala Muungano kwa ujumla.Kwa hakika,kiwango cha ubora wa makala hiyo bado sio cha kuridhisha,na pia sijapata kujiamini vya kutosha katika uwasilishaji wa mada husika (kwa mfano kutumia muda kidogo kuamua nitumie neno gani) lakini huu ni mwanzo,na ninadhamiria kwa zaidi ya asilimia 100 kuwa muda si mrefu nitawaletea kitu bora kabisa na mnachostahili kwa dhati.

Labda la mwisho ni kwamba ninafanya kila linalowezekana ili toleo zima la makala husika liwe kwa lugha ya taifa,yaani Kiswahili.Hiyo ni moja ya sababu ya wakati flani kuwa ninahangaika nitumie nheno gani mwafaka la kiswahili.Si kwamba nimesahau lugha yangu ila moja ya madhara ya kuwa huko nje kwa muda mrefu ni hilo.

Karibuni sana,na msisite kunitumia maoni (chagua player yoyote kati ya hizi mbili hapa chini)
 


22 May 2012

Kwanza ninawashukuru wote walionipatia mchango wao wa mawazo kuhusu idea hii ya Makala za Sauti.Ninasema ASANTENI SANA.Pili,wengi wa mlionitumia maoni yenu mmezungumzia uhafifu wa sauti.Nimelifanyia kazi hilo na ndio iliyopelekea kutengeneza makal nyingine leo ili kupata mawazo kama kiwango na ubora wa sauti vinaridhisha.

Kwahiyo,makala ya leo imelenga zaidi kutoa shukrani kwa mapokezi niliyopewa kuhusiana na makala za sauti,na kidogo nimejaribu kuongelea jinsi kila mmoja wetu anavyoweza ku-play role yake katika kuifanya Tanzania yetu kuwa bora zaidi.

Basi naomba nikuache unisikilize hapa chini

Ninafanya majaribio ya kuwaletea makala zilizorekodiwa (za sauti) ambapo kama ilivyo hapa bloguni na katika makala zangu gazetini,nitakuwa nikijadili masuala mbalimbali.Ninaanza na sekta ya huduma ambapo mlengwa mkuu ni TANESCO.Nakuomba sana msomaji na msikilizaji unipatie mawazo na ushauri kuhusu wazo hili (hata kuniambia kuwa ni wazo baya ni ushauri pia).

Toleo la kwanza (nataraji kufanya audio hizi angalau mara moja kwa wiki) ni hili hapa Natambua kuwa kiwango cha audio sio cha hali ya juu lakini toleo hili la kwanza ni la majaribio,na iwapo wasomaji mtaafiki wazo hili basi nitajitahidi kupata nyenzo bora ya kurekodia ujumbe husika.

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.