27 Jul 2014

Pengine umeamua kufuta SMS baada ya kuona SMS Inbox yako inajaa au pengine umefuta SMS kwa bahati mbaya. Katika mazingira ya kawaida, ukisahfuta SMS ndio 'imetoka hiyo.' Lakini kimsingi waweza kuzirejesha kwenye inbox japo kitu cha muhimu kabisa na muda. Uwezekano wa SMS ulizozifuta kurejea inbox kunategemea sana uharaka: kadri unavopokea SMS mpya au updates za apps zako ndivyo fursa ya kuzirejesha inavyozidi kuwa ndogo.

Kuna nyenzo kadhaa za PC au Mac za kuweza kukuongoza katika zoezi la kurejesha SMS zako kwenye simu yako.Nyingi ya nyenzo hizo ni za bure, na hata zinazohitaji malipo,zinakupa fursa ya majaribio kabla ya kununua (free trial). Aina gani ya nyenzo uitumie,yategemea mapendezeo yako,lakini zote zafanya kazi moja ku-scan memory ya simu yako,kutambua na kuokoa SMS zilizofutwa. Zitakuongoza katika hatua nne muhimu za zoezi hili: kuunganisha, ku-scan, ku-review na kuziokoa (recover).

Baadhi ya zana za PC au Mac zinazoweza kukusaidia ni pamoja na Coolmuster Android SMS+Contacts Recovery, Wondershare Dr Fone for Android (hii inahitaji simu yako iwe rooted) na Android Data Recovery

Hatua zifuatazo zinaweza kuwa tofauti kutegemea na zana ya PC/Mac utakayoamua kutumia hapa imetumika Wondershare Dr Fone kwa minajili ya maelezo kwa picha).

1. Download moja ya nyenzo nilizotaja hapo juu kwenye PC/Mac yako,kisha iwashe (launch)
2. Unganisha simu yako na PC/Mac kwa kutumia waya wa USB

drfone android sc01
3. Wezesha 'USB Debugging' katika simu yako kwa kwenda kwenye 'Developer Options' katika 'Setting.' Vinginevyo, waweza kwenda kwenye 'About Phone' kisha 'Build Number,' piga eneo hilo na kidole chako mfululizo (tap repeatedly) na hatimaye utapelekwa kwenye 'Developer Options.' Kutoka hapo,nenda kwenye 'USB Debugging' (au Android Debugging kutegemea aina ya simu yako) kisha tiki kiboksi husika.
drfone android sc02
4. Fuata maelekezo kama yanavyoonyeshwa katika zana unayotumia kwenye PC/Mac yako
drfone android sc05
5. Ukishamaliza, sasa utaweza kuona data zilizopo kwenye memory ya simu yako, na SMS ulizofuta kwa bahati mbaya au makusudi-kutegemea kama hakuna SMS mpya au updates za apps,maana kitu chochote kipya kwenye memory kitaondoa uwezekano wa kuokoa SMS ulizofuta.
drfone android sc09

6. Tafuta folder ya SMS,chagua SMS unayotaka/unazotaka kuzirejesha inbox,na aidha tumia option ya 'Recover' kwenye PC/Mac yako au 'save' kwenye kompyuta yako.

Natumaini makala hii itakuwa na msaada na manufaa kwako. Usikose kufuatilia makali nyinginezo za teknolojia katika blogu hii.Bonyeza TEKNOLOJIA hapo juu na utapelekwa moja kwa moja katika makala hizo.1 comment:

  1. mimi napata shida moja aisee ina scan zile za inbox tu ila sms ninayoitaka haipatikan hata kwa program zote zinaleta zile za zaman ambazo sina haja nazo sana

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube