6 Oct 2014








Maswali ya msingi: Katika michoro tunaona jina la Shumake Rails, lakini taarifa pia zasema kampuni husika ni m/s shumoja. Je mwekezaji ni Shumake Rails (soma HAPA) au m/s shumoja/ shimoja (soma HAPA)? Kwa hakika haiwezekani tuwe tunazungumzia kampuni mbili tofauti au kampuni moja yenye majina mawili.

Tukiangalia hiyo michoro twaweza kujiuliza, huyo mwekezaji alikuja lini Tanzania kabla ya kuiandaa na kuiwasilisha siku ya kuwekeana mkataba? Je mpango huu ulikuwepo kitambo lakini sasa ndio twafahamishwa? Taratibu za zabuni zilikuwaje? 

Na pengine picha hii ya mwezi Septemba mwaka jana kati ya Waziri Mwakyembe na 'mwekezaji' wakati waziri alipozuru nchini Marekani yaweza kutoa 'clues' flani


Hapa chini ni uchunguzi nilioufanya kuhusu tovuti ya shumoja.com. Kama unavyoona, tovuti haina anwani ya ofisi za kampuni hiyo wala namba za simu. 


Na kingine cha kukanganya zaidi ni ukweli kwamba licha ya tovuti hiyo kutokuwa na taarifa zozote za kuonyesha uzoefu wa mradi kama huo tunaoambiwa utawekezwa huko nyumbani, jina hapa ni SHUMOJA RAILS ilhali katika picha za hapo juu tunaona michoro ikiwa na jina la SHUMAKE RAILS

Lakini licha ya tovuti hiyo kutokuwa na habari za kutosha kuhusu kampuni hiyo, picha zifuatazo zaonyesha bayana kuwa ilisajili hivi majuzi tu, yaani mwezi uliopita. Hivi yawezekana kwa kampuni 'kubwa' ya uwekezaji kutokuwa na tovuti muda wote huo, na ghalfa kutengeneza tovuti mpya isiyo na maelezo ya kutosha takriba mwezi mmoja tu kabla ya kutangazwa kuwa itawekeza kwenye mradi wa treni za kisasa huko Dar?

 











1 comment:

  1. Bongo kila kitu deal.. Inawezekana kabisa anayesukuma iende haraka kashafanya yake kama lile deal la rich-monduli

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.