19 May 2016


Kuna msemo wa Kiingereza unaoweza kutafsiriwa hivi, "thamani ya fedha ni matumizi." Pesa isiyoweza kutumika haina thamani, inabaki kuwa karatasi tu lenye picha ya kiongozi au alama fulani. Vivyo hivyo, thamani ya elimu/uelewa ni katika kushirikisha watu wengine. Ukiwa na elimu ya kutosha au uelewa mkubwa lakini ikabaki kichwani mwako tu bila kutumiaka basi haina umuhimu. Ni katika mantiki hiyo, sie wengine tumekuwa waumini wakubwa wa filosofia isiyo rasmi ya 'Sharing Is Caring' ambayo mara nyingi huandikwa #SharingIsCaring.

Leo ningependa ku-shea nawe msomaji mbinu muhimu ya ku-post kitu mtandaoni ili kioneknaje au kusomwa na watu wengi. Yaani hapa nazungumzia kuhusu ku-update status yako Facebook iwe ya maneno au picha, au ku-tweet huko Twitter, au ku-post picha yako hujo Instagram.

Tuanze na Facebook. Muda mwafaka wa ku-update status yako ili iweze kusomwa na watu wengi zaidi ni kati ya saa 3 asubuhi hadi saa 1 usiku, lakini muda bora kabisa ni saa 7 mchana hadi saa 9 alasiri.  

Kwa upande wa Twitter, muda mwafaka wa ku-tweet kitu kinachoweza kusomwa na watu wengi zaidi ni saa 6 mchana na kati ya saa 11 jioni na saa 12 jioni.

Kwa Instagram, muda mwafaka ni alfajiri, kwa maana watu wakiamka na kuingia kwenye app hiyo wakutane na picha yako.Lakini mtandao huu ni kimeo na jipu kwa Tanzania. Kwahiyo hata kuelezea kanuni zake ni sawa na kupoteza muda. Mtandao huu umetawaliwa na vitu vichafu na visivyopendeza. Binafsi japo bado ni memba huko lakini siutumii kwa sababu umesheheni kila aina ya maovu.

Maelezo hayo juu ni maalum kwa watu wenye ratiba zao nyingine lakini wanapenda kuwasiliana na jamii kwa kutumia mitandao ya kijamii. Maelezo hayo hayana maana kwa wenzetu ambao wapo mtandaoni kutwa kucha. Yes, kuna wenzetu wapo mtandaoni muda wote.

Kadhalika, maelekezo hayo ni ELEKEZI tu, kwa maana kwamba sio lazima usubiri muda huo mwafaka ndio uposti kitu chako. Muda huo elekezi ni mwafaka kwa minajili ya kuwafikia watu wengi zaidi.

Pichani chini ni infograph kuhusu nilichoeleza hapo juuEndelea kutembelea blogu hii kwa mada mbalimbali za teknolojia, sambamba na makala zangu za kila wiki katika jarida la Raia Mwema, mada mbalimbali za intelijensia, burudani na michezo, maisha, na kadhalika. Karibuni sana

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube