Showing posts with label FACEBOOK. Show all posts
Showing posts with label FACEBOOK. Show all posts

30 May 2016

Mitandao ya jamii imeturahisishia maisha kwa kiasi kikubwa. Sasa tunaishi katika dunia kama kijiji ambapo tukio likotokea sehemu moja ya dunia linafahamika sehemu nyingine muda huohuo bila kutegemea radio, runinga au gazeti pekee. Kadhalika, mitandao ya kijamii imetuwezesha kufahamiana na watu wengi popote walipo duniani bila kukutana ana kwa ana.

Pamoja na mazuri mengi ya mitandao ya kijamii, kuna upande wa pili usiopendeza kuhusu mitandao hiyo ya kijamii. Licha ya kutupatia fursa ya kufahamiana na watu mbalimbali muhimu, mitandao hiyo pia imetoa fursa kwa watu waovu wanaoitumia kwa minajili ya kufanya maovu yao.

Katika makala hii ninaongelea kuhusu tishio kubwa na lililotapakaa kwenye mtandao wa kijamii wa Facebook, ambapo watu waovu huweka hufungua akaunti feki na kuweka profile feki zinazoambatana na picha za warembo wa kuvutia. Watu hawa wanaweza kuwa aidha wanawake au wanaume lakini hiyo haijalishi kwa sababu lengo lao sio zuri.

Wanachofanya ni rahisi. Wanafungua akaunti feki kwa maana ya jina na taarifa husika, kisha wanaweka picha kadhaa za msichana mrembo. Picha zinazotumika zaidi ni za warembo wa Afrika Kusini. Kama wengi wetu tunavyofahamu, mabinti wengi wa nchi za Kusini mwa Afrika wamejaliwa shepu zenye mvuto. Kwahiyo, tapeli husika anaweka picha kama tano hivi kwa kuanzia, nyingi au zote zikiwa katika pozi za kuvutia kama sio kutamanisha.

Baada ya hapo wanaanza kuomba urafiki (friend requests) kwa kasi ya kimbunga. Kwa makadirio ya chini, mara baada ya kukamilisha profiles zao feki, matapeli hao hutuma friend requests kati ya 100 hadi 300 kwa mkupuo.

Jinsi ya kuwatambua sio ngumu sana. Cha muhimu nikuzingatia kanuni muhimu ya matumizi ya mtandao (Internet) yaani "ukiona ni kizuri kupita maelezo, basi kitlie shaka," wanasema "if it is too good to be true, them may be it is not true." Kanuni hiyo pia ina umuhimu mkubwa katika matumizi ya barua-pepe. Ukipata email kutoka kwa mtu usiyemjua anayedai ana mamilioni ya dola na anataka kuweka kwenye akaunti yako, huyo ni tapeli tu. Hakuna mtu mwenye akili timamu, hata awe tajiri kiasi gani, ambaye yupo tayari kumpatia mtu japo dola 10 tu (achilia mbali hayo mamilioni) mtu asiyemjua.

Kwahiyo, ukipata friend request kutoka kwa binti mrembo kupindukia ilhali hamjuani, basi washa king'ora cha tahadhari. Kitu cha kwanza kabisa ni kuangalia profile husika. Angalia mtu huyo amejiunga lini na Facebook. Pili angalia idadi ya marafiki wapya. Ukikutana na profile inasema "X amekuwa friends na Y na watu 100 au zaidi (kwa mkupuo)" basi uwezekano mkubwa ni kwamba huyo ni tapeli 'anakulia taimingi..'

Kingine ni kuangalia aina ya marafiki zake, Mara nyingi matapeli wa aina hiyo hujifanya wa jinsia ya kike lakini friends wao wengi kabisa kama sio wote ni wanaume. Sio dhambi wala kosa la jinai kwa mwanamke kuwa na marafiki wengi wa kiume kuliko wa kike lakini 'unapaswa kuchezwa na machale.'

Lakini ili kupata uthibitisho zaidi, unaweza ku-save moja ya picha za mtu huyo kwenye computer yako kisha nenda kwenye ukurasa wa kutafuta utambulisho wa picha kwenye Google. 

Ngoja nikuelekeze jinis ya kutumia tovuti hiyo inayoitwa Google Image.

1. Kwanza, ni rahisi zaidi kuitumia Google Image kutafuta utambulisho wa picha kwenye computer kuliko kwenye simu au tablet. Kwahiyo maelezo ninayotoa hapa ni ya kutumia Google Image kwa computer na sio simu au tablet. Andika anwani hii https://images.google.com 


2. Ukishaingia hapo, bonyeza hapo kwenye alama ya kamera kwa ajili ya ku-search kama ilivyo pichani



3. Ukishabonyeza hapo, bonyeza palipoandikwa 'upload an image' kama inavyoonekana pichani,



4. Kisha bonyeza palipoandikwa 'choose file.'



5. Baada ya kubonyeza hapo, nenda sehemu uliyo-save ile picha unayohisi ni feki.



6. Upload picha hiyo



7. Angalia matokeo 

Njia hiyo hapo juu ni muhimu sana sio kwa ajili ya kuangalia kama picha ni feki kwenye Facebook tu bali kwa kuhakiki picha mbalimbali unazokutana nazo mtandaoni.

Hata hivyo, wakati mwingine matokeo ya Google Images search yanaweza yasikupe jibu unalotarajia. Ushauri wangu ni kuzingatia tahadhari nilizotoa awali. Na kumbuka, "if it is too good to be true, may it is not true."

Waweza ku-accept friend request na kusubiri kama huyo 'binti' ataanzisha maongezi nawe. Mara nyingi, akianzisha maongezi, anaweza kukuomba namba ya simu au ya  Whatsapp. Ukimwomba yake atakwambia simu imeharibika aua imeibiwa. Sasa katika mazingira ya kawaida tu, waweza kushawishika kusema "basi nitakununulia simu mpya" au "nitakutumia simu mpya." Hapo utakuwa umeshajigeuza ATM.

Hata hivyo, haina maana kuwa kila binti mrembo atakaye-request friendship kwenye Facebook ni tapeli. Na sio kila friend atakayekuomba msaada kwa Facebook ni tapeli. Kuna watu wanaomba misaada ya dhati. Cha muhimu ni "kuwa na machale."

Ni muhimu kutambua kuwa ushauri niliotoa hapo juu haumaaniishi kwamba 'matapeli wa Facebook' ni mabinti au wanawake pekee. Tunaishi zama za ajabu kabisa ambapo kuna ' vijana wengi tu wa kiume au wanaume wazima wanaowinda akinadada au kinamama wa kuwalea au kuwatapeli.' Kwahiyo ushauri huo ni kwa jinsia zote. 

Kwa akinadada au kinamama , ukikutana na 'handsome boy' mwenye dalili kama hizo hapo juu, basi ni muhimu kuskilizia 'machale' yako. Ndio kuna akina Brad Pitt kibao ambao bado wapo single na wanatafuta marafiki wa kike au wenza, lakini wengine ni matapeli tu.

Endelea kutembelea blogu hii kwa makala mbalimbali kama hii na nyinginezo. Na ususahau ku-share na mwenzio kwa sababu SHARING IS CARING.

19 May 2016


Kuna msemo wa Kiingereza unaoweza kutafsiriwa hivi, "thamani ya fedha ni matumizi." Pesa isiyoweza kutumika haina thamani, inabaki kuwa karatasi tu lenye picha ya kiongozi au alama fulani. Vivyo hivyo, thamani ya elimu/uelewa ni katika kushirikisha watu wengine. Ukiwa na elimu ya kutosha au uelewa mkubwa lakini ikabaki kichwani mwako tu bila kutumiaka basi haina umuhimu. Ni katika mantiki hiyo, sie wengine tumekuwa waumini wakubwa wa filosofia isiyo rasmi ya 'Sharing Is Caring' ambayo mara nyingi huandikwa #SharingIsCaring.

Leo ningependa ku-shea nawe msomaji mbinu muhimu ya ku-post kitu mtandaoni ili kioneknaje au kusomwa na watu wengi. Yaani hapa nazungumzia kuhusu ku-update status yako Facebook iwe ya maneno au picha, au ku-tweet huko Twitter, au ku-post picha yako hujo Instagram.

Tuanze na Facebook. Muda mwafaka wa ku-update status yako ili iweze kusomwa na watu wengi zaidi ni kati ya saa 3 asubuhi hadi saa 1 usiku, lakini muda bora kabisa ni saa 7 mchana hadi saa 9 alasiri.  

Kwa upande wa Twitter, muda mwafaka wa ku-tweet kitu kinachoweza kusomwa na watu wengi zaidi ni saa 6 mchana na kati ya saa 11 jioni na saa 12 jioni.

Kwa Instagram, muda mwafaka ni alfajiri, kwa maana watu wakiamka na kuingia kwenye app hiyo wakutane na picha yako.Lakini mtandao huu ni kimeo na jipu kwa Tanzania. Kwahiyo hata kuelezea kanuni zake ni sawa na kupoteza muda. Mtandao huu umetawaliwa na vitu vichafu na visivyopendeza. Binafsi japo bado ni memba huko lakini siutumii kwa sababu umesheheni kila aina ya maovu.

Maelezo hayo juu ni maalum kwa watu wenye ratiba zao nyingine lakini wanapenda kuwasiliana na jamii kwa kutumia mitandao ya kijamii. Maelezo hayo hayana maana kwa wenzetu ambao wapo mtandaoni kutwa kucha. Yes, kuna wenzetu wapo mtandaoni muda wote.

Kadhalika, maelekezo hayo ni ELEKEZI tu, kwa maana kwamba sio lazima usubiri muda huo mwafaka ndio uposti kitu chako. Muda huo elekezi ni mwafaka kwa minajili ya kuwafikia watu wengi zaidi.

Pichani chini ni infograph kuhusu nilichoeleza hapo juu



Endelea kutembelea blogu hii kwa mada mbalimbali za teknolojia, sambamba na makala zangu za kila wiki katika jarida la Raia Mwema, mada mbalimbali za intelijensia, burudani na michezo, maisha, na kadhalika. Karibuni sana

18 May 2016



Tukubaliane kwamba japo wengi wetu twapenda kutumia mtandao, hususan kutembelea mitandao ya kijamii kama vile Faceboo, Twitter, Instagram, nk bado kuna uelewa mdogo wa mbinu mbalimbali ambazo laiti zikutumika zaweza kuleta ufanisi zaidi katika matumizi ya mtandao au mitandao hiyo ya kijamii.

Siku za nyuma nilikuwa nikiandika makala mbalimbali kuhusu teknolojia lakini kutingwa na majukumu kumesababisha ni we mzembe kidogo. Samahani kwa hile, maana linaathiri ile spirit ya 'Sharing Is Caring.' 

Anyway, long story short, leo nina darasa fupi la jinsi ya kuangalia watu waliotembelea ukurasa (profile) wako wa Facebook. Ni suala la hatua kwa hatua, na nina hakika ukifuata kwa makini utaweza kuona nani ametembelea profile yako. Labda sio muhimu, lakini, hey, kuna watu  wangependa kufahamu vitu kama hivyo.

Samahani, nimejaribu kutafsiri hatua hizo pichani kwa Kiswahili nimechemsha. Natumaini kimnombo kilichotumika sio kigumu, lakini ikitokea mtu hajaelewa vema basi nishtue nitajitahidi kutoa ufafanuzi kwa Kiswahili.


Endelea kutembelea blogu hii kwa mbinu zaidi za mtandaoni pamoja na habari za teknolojia na habari nyinginezo.

Karibuni sana

30 Jul 2011


Mitandao ya jamii ya Facebook na Twitter imetengeneza kizazi kinachoendekeza umimi kupita kiasi kiasi kwamba watu hawajali masuala mengine huku wakiwa na tamaa kama watoto wadogo kuona watu wanasema mazuri kuhusu wao,picha zao,wanayoandika kwenye mitandao hiyo,nk.

Kuendelea kuwepo kwenye mitandao hiyo kwa muda mrefu kunamwacha mtumiaji akiwa na mgogoro wa kujitambua (identity crisis),tamaa ya kutambulika katika namna ileile mtoto mdogo anamwambia mzazi wake, "Mama,nimefanya hivi."

Baroness Greenfield,profesa wa taaluma ya madawa (pharmacology) katika Chuo Kikuu cha Oxford,anaamini kuwa kukua kwa urafiki wa mtandaoni-sambamba na matumizi makubwa ya michezo ya kompyuta-vinaweza kupelekea kuuchanganya ubongo.

Hii inaweza kusababisha upungufu kwenye kukazani mambo ya muhimu,hitaji la kutamani kusifiwa na uwezo mdogo wa mawasiliano yasiyohitaji kutumia maneno (non-verbal communication) kwa mfano kumwangalia mtu usoni wakati wa maongezi.

Zaidi ya watu milini 750 duniani wanatumia mtandao wa Facebook kuonyeshana picha na video na mara kwa mara hubandika maelezo kuhusu mienendo na mawazo yao.

Mamilioni pia wamejiunga na mtandao wa Twitter ambao huwawezesha watumiaji kusambaza ujumbe mfupi na picha kuhusu wao wenyewe.

Baroness Greenfield,mkurugenzi wa zamani wa taasisi ya utafiti ya Royal Institution alisema, "kinachonipa wasiwasi ni ile hali ambapo unaweza kutarajia mtu atawaza au kusema nini ambayo ni hali ya kawaida huko Twitter."

"Kwanini mtu ahitaji kujua umekula nini wakati wa kifungua kinywa?Inanikumbusha jinsi mtoto mdogo anavyosema, 'mama angalia ninachofanya' "

"Ni kama mgogoro wa kujitambua.Kimsingi,hali hii inaufunga ubongo kwenye kuhusisha wakati/muda"

Mwanataaluma huyo alidai kuwa baadhi ya watumiaji wa Facebook wanajisikia wanapaswa kuwa "watu maarufu wadogo wadogo" (mini celebrities) ambao wanaangaliwa na kunyenyekewa na watu wengine kila siku.

"Wanafanya vitu vinavyoendana na Facebook kwani njia pekee wanayoweza kutumia kujitambulisha kwa umma ni kwa kuwafahamisha watu wengine kuhusu kinachoendelea kwenye maisha yao."

"Ni kana kwamba watu wanaishi katika dunia isiyo halisi bali dunia ambayo kinachomata ni nini watu wanafikiria kuhusu wewe au kama wanaweza kubonyeza kwenye picha au ulichoandika," alisema Profesa huyo.

"Fikiria kuhusu madhara kwa jamii ikiwa watu wanajali zaidi kuhusu nini watu wengine wanafikiria kuhusu wao kuliko nini wanachofokiria kuhusu wao wenyewe."

Mawazo ya mwanazuoni huyo yaliungwa mkono na Sue Palmer,mtaalam wa fasihi andishi na mtunzi wa vitabu,ambaye alisema kuwa wasichana hususan wanaamini wao ni bidhaa ambayo lazima iuzwe kwenye Facebook.

Alisema: 'Watu walizowea kuwa na picha ya kuchora (zinazowaonyesha wao) lakini sasa tunaweza kujichora wenyewe mtandaoni.Ni kama kuwa mshiriki kwenye shoo yako mwenyewe ya TV ambayo umeiunda na kuiweka hadharani kwa dunia kuiona.'

CHANZO: Habari hii imetafsiriwa kutoka gazeti la Daily Mail


28 Jun 2011

Pichani ni jengo la "Tanesco ya Senegal",Senelec,lililoshambuliwa na waandamanaji wenye hasira kuhusu kukatika umeme mara kwa mara jijini Dakar.Akina sie tunashambulia kwa matusi,lawama,na manung'uniko huko Twitter na Facebook!!!

Sio siri kwamba upole wa Watanzania ni miongoni mwa sababu kuu za mabaya mengi yanayotokea huko nyumbani.Na kama kuna suala linalosikitisha kuhusu mwamko wa Watanzania kudai haki zao ni tatizo la mgao wa umeme sambamba na ubabaishaji wa hali ya juu wa serikali na Tanesco katika kushughulikia tatizo hilo.

Sasa hivi,mitandao ya jamii ya Twitter na Facebook imetawaliwa na malalamiko ya Watanzania wengi kuhusu mgao.Wengine wanaishiwa na uvumilivu na kuishia kuitukana Tanesco,kana kwamba matusi hayo yatarejesha umeme.Wengine wamekuwa wakipeana taarifa kuhusu maeneo ambayo "Tanesco wameshachukua umeme wao".Kwa kifupi,kinachosikika zaidi ni manung'uniko,lawama,vilio na hata matusi.Cha kusikitisha ni kwamba hakuna dalili yoyote kutafsiri malalamiko hayo into vitendo.

Sio kama nawasimanga ndugu zangu.I really feel you lakini ukweli mchungu ni kwamba kelele zenu haziwezi kumaliza tatizo hilo.Kinachohitajika ni kudai haki kwa nguvu.By "nguvu" simaanishi vurugu bali kuchukua hatua za makusudi kuhakikisha serikali na Tanesco wanawajibika.Mgao utaendelea milele iwapo Watanzania wataishia kulalamika tu.Hakuna miujiza katika kuleta mabadiliko.Either watu wajitoe muhanga kudai haki yao kama walipakodi au waendelee kuteswa na mgao.

Bahati nzuri,wenzetu nchini Senegal wanatuonyesha namna gani matatizo yanayoathiri nchi yanavyoshughulikiwa na umma.Nisieleze kwa maneno yangu bali naomba usome habari ifuatayo:

Associated Press

DAKAR,Senegal: Maelfu ya waandamanaji wameingia mitaani katika mji mkuu wa Senegal kupinga kukatika umeme mara kwa mara.Maandamano hayo ni tukio la tatu la vurugu nchini humo ndani ya wiki.

Wananchi wenye hasira walivamia ofisi za shirika la umeme la Senelec,jijini Dakar baada ya maandamano ya kupinga kukatika kwa umeme kwa muda mrefu.

Watu kadhaa walishambulia majengo ya serikali hapo jana.Wanadaia kuwa baadhi ya maeneo yamekuwa yakikosa umeme kwa masaa 24 au zaidi.

Kama ilivyo kawaida kwa vyombo vya dola barani Afrika,askari wa kikosi cha kutuliza ghasia walipambana na waandamanaji kwa kutumia maji na mabomu ya machozi.Msemaji wa polisi hakuweza kuthibitisha idadi ya waliojeruhiwa katika ghasia hizo.

Alhamisi iliyopita,vurugu kubwa ziliibuka kupinga mpango wa mabadiliko ya katiba ya nchi hiyo

Uchaguzi ni wenu Watanzania wenzangu.Mwendelee kulalama huku Serikali na Tanesco wakiendelea kuwasanifu (mgao wa umeme hauwagusi kwa vile aidha wana jenereta zinazojazwa mafuta na hela yako mlipakodi au maeneo wanayoishi hayakatwi umeme kutokana na unyeti wake) AU muige mfano wa wenzetu wa Senegal.Hakuna njia ya mkato katika kutatua matatizo sugu yanayosababishwa na watendaji wasiotimiza wajibu wao.It's now or never!

13 Sept 2010

Je wajua kuwa licha ya mgombea wa CCM Jakaya Kikwete kukacha mdahalo na wagombea wa vyama vingine anapatikana kirahisi mtandaoni ambapo "anauza" sera zake na "mafanikio" yake?Kama ulikuwa hufahamu basi nenda Twitter kisha tafuta @Kikwete2010 au nenda Facebook kisha tafuta Jakaya Kikwete.

I know siasa za chama kimoja zimeacha kasumba ya kufurahia kugusana mabega na watawala.No wonder kuna wenzetu muda huu wanakenua meno yote thelathini na kitu kwa vile wamepokea ujumbe kama huu "Kikwete2010 is following you..." au "Salma Kikwete is Following you..." 

Si ajabu kuna wenzetu wamefotokopi meseji za aina hiyo wakiamini kuwa Kikwete na mkewe Salma wanawajali saaaana hadi wameamua kuwa-follow up huko Twitter au kuungana nao hapo Facebook.KALAGABAHO!Kwanini hujiulizi WHY NOW?Kikwete na mkewe walikuwa Ikulu tangu Desemba 2005 na HAWAKUKUTAFUTA.Hushangai kwanini leo wanataka urafiki nawe?Well,sio kosa kuwa rafiki na rais au mkewe lakini urafiki huu hauna tofauti na ule wa mtenda tendo la ndoa na kondomu.Zana hiyo (kondom) huwa na umuhimu wa kipekee (kwa wale wanaojali) kabla na wakati wa tendo la ndoa,lakini pindi shughuli ikimalizika kondom huwa ni uchafu usiovumilika.ANGALIA,usijetumika kama kondomu: Kikwete akuone muhimu sasa kwa vile anahitaji kura lakini akakusahau (kama alivyokusahau 2005-till now) baada ya kurejea Ikulu.

Badala ya ku-retweet kila anachoandika,tumia haki yako kama Mtanzania kuhoji masuala mbalimbali yanayolikabili taifa.Twende mbali zaidi ya kupongeza na kuona sifa "kugusana mabega" na watawala.Sio kosa kushabikia lakini ushabiki wenye maana ni ule unaombatana na matumizi sahihi ya akili.

Now you-in case you didn't.Muulize Kikwete,je ile kauli aliyotoa mwaka 2006 kuwa anawafahamu wala rushwa kwa majina ila anawapa muda wa kujirekebisha imefikia wapi?Je wameshajirekebisha?Je anaweza kututajia majina ya waliojirekebisha na waliogoma kufuata ombi hilo la kichovu?

Muulize pia kwamba kabla ya sakata la Richmond aliahidi kuwa tatizo la umeme lingebaki kuwa historia.A few months later,matapeli wa Richmond wakaingia kwenye picha.Today,tatizo la umeme ni as sugu as ufisadi.Mkalie kooni na kumhoji,kama huko nyuma alitoa ahadi ya kutupatia ufumbuzi wa umeme na hakutimiza,kwanini tumwamini sasa?

Muulizie pia kama bado anaamini kuwa mimba za wanafunzi wa kike zinasababishwa na kimbelembele chao.Yah,muulize swali hilo kwa vile hadi sasa bado hajakanusha au kuwaomba msamaha Watanzania kwa kauli hiyo ya kizembe.

Usikose kumuuliza pia kama hadi sasa hajui sababu zinazoifanya Tanzania kuwa masikini maana alinukuliwa akijiuliza swali hilo.Nenda mbali kidogo na kumhoji kama alikuwa hajua kwanini Tanzania ni masikini sasa anafanya nini hapo Ikulu?

Sasa hivi amenzisha hash tag #Mafanikio huko Twitter.Hapo utapata nafasi nzuri ya kujionea waziwazi namna Awamu ya Nne ya Kikwete ilivyoshindwa kuikomboa Tanzania kutoka kwenye umasikini licha ya raslimali lukuki tulizonazo.Hapo Kikwete na wapambe wake wanataja mapato yaliyotokana na utalii na madini.Mkalie kooni na kumhoji kama mapato ndio hayo,kwanini sie bado masikini?Fedha hizo zimeenda wapi kama sio kwenye akaunti za mafisadi?Na kwenye utalii muulize pia kuhusu meno ya tembo yaliyokamatwa huko Hong Kong yakitokea Tanzania.

Kumbuka,usikubali kutumika kwa maslahi ya mtu mwingine.Kumhoji mwanasiasa anayeomba kukuongoza ni haki yako.Usiichezee.Badala ya kujipendekeza kwa RT (Retweets za Kikwete2010) tumia fursa hiyo kumuuliza maswali ya msingi yanayohitaji majibu ya haraka.

PAMOJA TUNAWEZA

19 May 2009


Israel's internal intelligence service urged the public today to exercise caution when using Facebook, saying Arabs are trying to recruit spies on the popular social networking site.

The Shin Bet security agency warned Israelis against answering unsolicited messages or sharing telephone numbers and other sensitive information over the Internet. It said there have been numerous incidents recently in which violent groups tried to recruit Israelis through Facebook and other networking sites...continue

29 Sept 2008

Shirika la Ujasusi la Uingereza (MI6) limeanza kutumia mtandao wa Facebook katika harakati zake za kusaka majasusi watarajiwa.Mpango huo wa mashushushu hao umeanza takriban wiki mbili zilizopita na unalenga kupata waajiriwa wapya kutoka katika kaliba mbalimbali za jamii.
Source: The Guardian


Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.