.@ccm_tanzania leo inatimiza miaka 46 tangu izaliwe 05.02.1977 kufuatia muungano wa chama cha TANU na Afro Shirazi Party (ASP). pic.twitter.com/RmwalyILV1
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) February 5, 2023
Wakati @ccm_tanzania inazaliwa, Tanzania ilikuwa nchi yenye itikadi ya kitaifa, iliyoitwa Ujamaa na Kujitegemea. pic.twitter.com/aFBwHSILiZ
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) February 5, 2023
Licha ya mafanikio hayo ya "Mimi ni Mtanzania kwanza kisha kabila baadaye", umoja na mshikamano wa Watanzania pia umefanikiwa kuzifanya imani tatu kuu nchini humo - Ukristo, Uislamu na "Dini za Asili za Kiafrika" (African Traditional Religions - ATR) zisiwe juu ya Utanzania pic.twitter.com/P096sXLRX2
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) February 5, 2023
Kwa bahati mbaya - au pengine makusudi - itikadi ya Ujamaa na Kujitegemea ilitegemea sana uwepo wa Baba wa Taifa, Mwalimu Julius Kambarage Nyerere. Na alipong'atuka mwaka 1985, itikadi hiyo ilianza kumomonyoka pic.twitter.com/opriOClcwE
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) February 5, 2023
Unfortunately, tangu wakati huo, @ccm_tanzania imeendelea "kuimba" kuwa "Tanzania ni nchi ya kijamaa" lakini matendo hayaendani na maneno. Kimsingi, kumekuwa na "kuelea kama puto kiitikadi" - kwenye Ujamaa hatupo, na ubepari wetu ni ufisadi zaidi kuliko capitalism as such pic.twitter.com/L1ZZzwTlxv
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) February 5, 2023
Anguko la Ujamaa lilipelekea pia ombwe kijamii na kiutamaduni, ambapo kama ilivyo sasa, kuna sintofahamu kati ya "twende na wakati" (utandawazi) au tujikite kwenye mila na desturi zetu pic.twitter.com/eae8Gxk1pZ
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) February 5, 2023
Kwa bahati mbaya, au pengine makusudi, sio tu kwamba umasikini unachangiwa na rushwa na ufisadi bali pia @ccm_tanzania haijafanya jitihada za kutosha kupambana na tatizo hilo. Kauli za chama hicho zimejikita zaidi kwenye mafanikio yake badala ya changamoto zilizopo pic.twitter.com/PxNx6Ty60a
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) February 5, 2023
Nimalizie uzi huu kwa wimbo huu wa Marquis Du Zaire kusherehekea kuzaliwa kwa @ccm_tanzania. Hepi besdei CCM ☺️ pic.twitter.com/2iTiEku1bK
— 𝐉𝐚𝐬𝐮𝐬𝐢 (@Chahali) February 5, 2023
0 comments:
Post a Comment