Showing posts with label DAVID CAMERON. Show all posts
Showing posts with label DAVID CAMERON. Show all posts

18 May 2010Watawala wetu waache magari yao ya kifahari wachekwe?Nchi tajiri lakini viongozi wanaishi kawaida,lakini sie masikini na ombaomba wa kutembeza bakuli viongozi wetu wanaishi kifahari kama wafanyabiashara matajiri.

14 May 2010

Labda na watawala wetu watakuwa na la kujifunza.

Habari kamili bonyeza HAPA.

Kuna wakati najiuliza kwanini sie masikini wa kutupwa ni hodari sana kwenye matumizi ya ovyo ovyo.Moja ya kumbukumbu za serikali ya awamu ya nne ilikuwa kuongeza mishahara ya wabunge licha ya hali yetu mbovu kabisa ya uchumi.Sambamba na hilo ni utitiri wa magari ya kifahari ambayo kimsingi si miongoni mwa vipaumbele kwa taifa masikini kama letu.

Wakati sie tunaendeleza matumizi ya kutapanya huku tukitembeza bakuli kwa wafadhili,serikali mpya ya hapa Uingereza chini ya David Cameron imetangaza kuwa mishahara ya mawaziri itapunguzwa kwa asilimia 5 na hakutakuwa na nyongeza katika mishahara hiyo (pay freeze) kwa miaka mitano.Mshahara wa sasa wa Waziri Mkuu Cameron utakuwa pungufu ukilinganisha na mishahara wanayolipwa meya wa manispaa mbalimbali 61 (kila manispaa hapa inajipangia kiwango cha mishahara ya viongozi wao kulingana na uwezo wa manispaa husika.Kukupa picha nzuri,alichofanya Cameron ni kama JK angeamua alipwe mshahara pungufu kulinganisha na meya wa manispaa ya Temeke au Kinondoni...ah,naota tu.Afanye hivyo achekwe!!!?)Yah,unaweza kusema hizi ni mbwembwe tu za serikali mpya,au manjonjo tu,lakini ukweli ni kwamba serikali makini ni ile inayoonyesha kwa vitendo kuwa inatambua hali inayolikabili taifa.Cameron ameingia madarakani wakati Uingereza ikiwa kwenye msukosuko wa uchumi,na moja ya vipaumbele vya serikali yake ni kurekebisha uchumi mapema iwezekanavyo.

Kwa mujibu wa gazeti la The Sun la hapa,mshahara wa Waziri Mkuu Cameron umepunguzwa kwa pauni 7,500 na kubaki pauni 142,500.Mishahara ya Naibu Waziri Mkuu Nick Clegg na mawaziri wengine waandamizi itakatwa pauni 7,082 na kubaki pauni 134,565 huku mawaziri wa kawaida wakikatwa pauni 5,197 na kubaki pauni 98,740.Mishahara ya mawaziri 'wadogo' itakatwa pauni 4,707 na kubaki 89,435.Hatua hiyo ya kukata mishahara kwa asilimia 5 itaokoa pauni milioni 3.

Wakati hayo yanatokea,gazeti la Mwananchi lina habari kuwa nchi wahisani wanaochangia bajeti ya serikali yetu wameamua kuunguza mchango wao kwenye bajeti ya serikali kwa mwaka 2010/2011 kwa sababu mbalimbali, ikiwamo ni pamoja na kasi ndogo ya serikali katika kutekeleza mageuzi kwenye sekta za umma.

Taarifa ya wahisani hao iliyotolewa jijini Dar es Salaam juzi, inaeleza kuwa mwaka huo wa fedha, watatoa dola za Marekani 534 milioni sawa na Sh721bilioni, ambazo ni pungufu kwa Dola za Marekani 220 milioni sawa na Sh297 bilioni walizotoa mwaka 2009/2010.

Wahisani wa bajeti ya serikali ni Benki ya Maendeleo Afrika (ADB), Canada, Denmark, Jumuiya ya Ulaya (EU), Finland, Ujerumani, Ireland, Japan, Uholanzi, Norway, Sweden, Uswisi, Uingereza na Benki ya Dunia (WB) mwaka jana walichangia Sh1.9 trilioni katika bajeti ya serikali kupitia miradi ya maendeleo na mifuko ya kisekta.

Taarifa hiyo ilitaja maeneo ambayo serikali ilishindwa kufikia malengo kuwa ni mabadiliko ya haraka katika menejimenti ya sekta ya fedha za umma, mategemeo ya kuboreka kwa hali ya mazingira ya uwekezaji na uboreshaji wa huduma kwa kutoka sekta za umma.

Hii ni mara ya nne kwa wahisani hao kuiwekea ngumu serikali katika kuchangia bajeti yake kila inapofikia mwisho wa mwaka, kwa kushindwa kutekeleza mambo wanayofikiria wao kuwa ni muhimu zaidi katika maendeleo ya nchi.

Mwaka juzi wahisani hao waligoma kutoa fedha baada ya serikali kusuasua kuchukua hatua dhidi ya watuhumiwa wa ufisadi wakiwemo wa fedha za EPA mpaka zilipofunguliwa kesi kadhaa ambazo mpaka sasa zinanguruma mahakamani.

Tatizo la viongozi wetu sie ni porojo nyingi na ulaghai mwingi wa kisiasa.Majukwaani wanahubiri kama watu wenye uchungu kweli na nchi yetu,lakini matendo yao tofauti kama kiza na mwanga.Tunapenda kuishi kifahari wakati uwezo wetu ni duni kabisa.Yani kuna wakati naangalia msafara wa Waziri Mkuu hapa,kisha nikikumbuka misafara ya viongozi wetu wakuu nabaki na maswali mengi kuliko majibu.Hebu angalia video hii hapo chini inayoonyesha msafara wa Gordon Brown siku alipokwenda makazi ya Malkia Elizabeth (Buckingham Palace) kuwasilisha ombi lake la kujiuzulu.

13 May 2010

Ndoa ya Mkeka.Haya ni mambo ya pwani zaidi kuliko 'bara'.Kule kwetu Ifakara hakuna vitu kama hivyo,lakini maeneo kama Tanga,Dar,Bagamoyo,nk ndoa za mkeka 'zinakula sahani moja' kwa umaarufu kama ndoa 'za kawaida'.Actually,ilikuwa almanusra 'nipigwe ndoa ya mkeka' wakati nilipoishi Tanga kwa takriban miaka 15 ilopita.Unajua tena mambo ya ujana...ukiyaangalia wakati huu wa utu uzima inabaki kichekesho.Anyway,kwa kifupi ndoa ya mkeka ni mithili ya fumanizi kati ya wanaovunja amri ya sita pasipo minajili ya kuwa wanandoa,na 'katika kuwapa one-stop fundisho na ufumbuzi' wanafungishwa ndoa ya chap-chap.It's like "si mnapenda kuvunja amri ya sita kisirisiri?Okay,sasa tunawahalalishia mtende manyotenda for the rest of your lives"...lol!Tatizo ni kwamba ni nadra kwa ndoa za mkeka kudumu kwa vile huwa ni'za kulazimisha'.Yani hazina tofauti na stori kama binti 'anayejiachia' na kupata ujauzito ili aolewe na mpenziwe.It rarely works!


Well,makala hii inazungumzia 'ndoa ya mkeka ya kisiasa' kati ya chama cha wahafidhina (Conservatives) na kile cha Waliberali (Liberal Democrats) ambao kwa pamoja wameunda serikali ya mseto hapa Uingereza. 

Uamuzi wa kiongozi wa Conservatives kuunda serikali ya mseto na Liberal Democrats umepokelewa kwa hisia tofauti huku watu wengi wakitabiri kuwa mseto huo hauna maisha marefu.Kikubwa kinachopelekea utabiri huo ni itikadi za vyama husika sambamba na tofauti zao katika sera zao.Japo tumeambiwa kuwa moja ya sababu zilizopelekea kufanikiwa kwa mseto huo ni kwa kila chama "kukubali matokeo" kwa aidha kuelegeza au kuachana kabisa na baadhi ya misimamo yao,hiyo haimaanishi kuwa misimamo hiyo imepotea 'vichwani' mwa wafuasi wa vyama hivyo.

Wakati wahafidhina wanafahamika kwa mrengo wao wa kulia na kati-kulia (right wing or centre-right politics) waliberali ni maarufu zaidi kwa mrengo wa kushoto na kidogo kati-kushoto (left wing or centre-left politics).Pengine hili sio rahisi sana kueleweka kama tukichukulia siasa zetu huko nyumbani kama mfano,kwani nadhani tunaweza kukubaliana kwamba nafasi ya mrengo katika siasa zetu huko Afrika ni ndogo sana.Yayumkinika kabisa kusema kuwa fedha za kukiwezesha chama au mgombea kununua kura ni muhimu zaidi kwenye siasa zetu kuliko mrengo wa chama au mgombea husika.Na hili ni tatizo kwa vile chama (au mgombea) kisicho na mrengo (au msimamo) ni sawa na bendera inayoweza kuelekea upande wowote ule kulingana na mvumo wa upepo.

Wenye hofu kuhusu 'ndoa ya mkeka' kati ya wahafidhina na waliberali wana sababu za msingi kwa vile mseto kati ya siasa za mrengo wa kulia na zile za mrengo wa kushoto hauko mbali sana na jitihada za kuchanganya maji na mafuta.Wakati chama cha Conservatives kinafahamika zaidi kwa siasa zake za kuwakumbatia matajiri huku zikiwakalia kooni 'walalahoi' kwa kudi kubwa (tayari kuna taarifa za 'kiama' cha kodi) waliberali wanafahamika zaidi kwa siasa za kuwa karibu na jamii huku vitu kama haki za binadamu,uvumulivu na ushirikiano vikiwa na umuhimu mkubwa.

Wakati Liberal Democrats walikuwa na sera ya msamaha (amnesty) kwa wahamiaji 'haramu' (illegal immigrants) huku wakisisitiza kuwa hatua kali dhidi ya wahamiaji hao si ufumbuzi kwa vile 'zinazidi kuwaficha msituni',chama cha Conservative kiliweka bayana msimamo wake wa kupunguza idadi ya wahamiaji kwa kuweka ukomo (cap) katika idadi ya wanaoingia/kuhamia Uingereza,sambamba na sheria kali za uhamiaji.Na katika hatua inayoweza kuwagharimu Liberal Democrats,chama hicho kimekubali kuachana na sera yake ya msamaha kwa 'wahamiaji haramu' na badala yake kimeafiki hatua ya Conservatives kuweka ukomo kwenye idadi ya wahamiaji wanaoingia nchini hapa.

Kuna tofauti ya kimtizamo kuhusu umoja na ushirikiano wa Ulaya.Wahafidhina wanasifika kwa upinzani wao dhidi ya suala hilo huku waliberali wakipendelea kuona ushirikiano huo ukisambaa zaidi ikiwa ni pamoja na wazo la Uingereza kutumia sarafu ya Euro badala ya Pound Sterling.Katika kufanikisha 'ndoa' yao,Liberal Democrats wamekubali kusitisha mipango yao kuhusu kukuza ushiriakiano wa Ulaya,jambo linaloweza kuwaudhi waumini wa siasa za chama hicho.

Lakini tayari kuna dalili za mpasuko kwenye 'ndoa hiyo ya mkeka' baada ya taarifa kwenye baadhi ya magazeti ya hapa kwamba 'Waziri' mpya wa fedha ((Kansela) George Osborne (wa Conservatives) amepinga vikali wazo kwamba 'Waziri' wa biashara (Business Secretary) Vince Cable (wa chama cha Liberal Democrats) ndiye atakayekuwa na dhamana ya kufanya mabadiiko kwenye mfumo wa mabenki (kwa minajili ya kudhibiti na kuzuwia uwezekano wa mtikisiko wa kifedha/kiuchumi kutokana na 'uzembe' wa mabenki katika utekelezaji wa sheria za fedha).Badala yake,hazina chini ya Osborne ndio itakayoshikilia dhamana ya utekelezaji wa sera ya mabenki na sekta ya fedha kwa ujumla.


Taarifa zaidi zinaeleza kuwa kuna hofu kuwa chama cha Liberal Democrats kitakimbiwa na idadi kubwa tu ya wafuasi wake kufuatia uamuzi wake wa kushirikiana na Conservatives.Hali hiyo sio tofauti sana kwa upande wa wahafidhina kwani kuna idadi kubwa tu miongoni mwao wanaoona 'ndoa hiyo ya mkeka' kuwa jambo lisilofaa.Pengine tatizo kubwa kwa vyama vyote viwili ni wale walio 'mwisho wa upande' wa mrengo wa vyama hivyo,yaani wenye mrengo wa kulia kabisa kwa upande wa Conservatives na wa mrengo wa kushoto kabisa kwa upande wa waliberali.Hawa ni watu wanaoongozwa na imani na itikadi,na haiwaingii akilini kuona mambo hayo ya msingi yakiwekwa rehani kwa minajili tu ya kuunda serikali.

Lakini kuna wanaoona kuwa 'ndoa hii ya mkeka' kati ya David Cameron na Nick Clegg inaweza kudumu kwa vile kimsingi viongozi hao wawili wana mambo kadhaa yanayoshabihiana.Wote walisoma shule 'za bei mbaya',wanatoka familia zenye uwezo mkubwa kifedha na,kimsingi, wanaishi katika tabaka tawala.Kwa minajili hii,baadhi ya wachambuzi wanatabiri kuwa mfanano wa haiba za Cameron na Clegg,na sio tofauti katika itikadi zao,utafanikisha kudumu kwa serikali hiyo ya 'ajabu' kati chama chenye siasa za mrengo wa kulia (conservatives) na kile cha mrengo wa kushoto (Liberal Democrats).

Pamoja na yote hayo,siasa ni mchezo usiotabirika.Siku chache zilizopita ingekuwa jambo lisilofikirika kwa wahafidhana na waliberali kushirikiana katika uongozi wa serikali,lakini leo hii 'habari ndio hiyo'.Basi kwa minajili hiyohiyo,haitokuwa ajabu kwa 'ndoa hii ya mkeka' kudumu muda mrefu kuliko inavyotarajiwa.

Muda utatanabaisha (time will tell).

11 May 2010
Gordon Brown has just announced on live tv that he is stepping down as the Prime Minister.It's now clear that the next PM shall be David Cameron.

3 Dec 2008


According to tomorrow's New Statesman, Barack Obama was unimpressed by his encounter with David Cameron earlier this year and commented: "What a lightweight!"

According to James Macintyre's report, Cameron's attempt to stress his pro-American and Eurosceptic credentials did not meet with Obama's approval. According to Macintyre's diplomatic sources, the Democratic candidate was "distinctly unimpressed" and labelled Cameron a lightweight.

Macintyre notes that 48 hours earlier Obama had delivered a speech in Berlin stressing "the importance of Europe's role in our security and our future".

Following the meeting with Cameron, Obama apparently asked officials for more information on Tory Euroscepticism. Macintyre also speculates that Cameron's support for the Iraq war – which Obama opposed – did not help the relationship either.

The report is sure to dismay Cameron and damage his attempts to portray himself as a world-class statesman – not to mention relations between Obama's incoming administration and a possible future Tory government.

When Cameron met the then-presidential candidate in July, the two held an hour of discussions, and Obama also met shadow cabinet members William Hague and George Osborne.

Photographs showed the pair looking relaxed and comfortable with each other, and Cameron gave Obama gifts including a box of CDs by some of the Conservative leader's favourite British musicians, among them the Smiths, Radiohead, Gorillaz and Lily Allen, and a copy of Hague's recent biography of the anti-slavery campaigner, William Wilberforce.

A senior Labour source told the Statesman: "Obama will want to work with a united Europe, not the 27 divided nations envisaged by a David Cameron, William Hague and [the Eurosceptic backbencher] Bill Cash vision of Europe. Tory isolationism is the last thing Obama's new foreign policy team will want from London."

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.