Ili uielewe vema makala hii ni vema ufanye kulinganisha kinachojiri Tanzania muda huu baada ya kutangazwa kuingia kwa Coronavirus na kinachojiri katika nchi jirani ambazo pia zimekumbwa na janga hilo la kimataifa.
Tuanze na Kenya. Mara baada ya kuthibitika kuwa taifa hilo lina mgonjwa mmoja aliyeambukizwa maradhi hayo, Rais Uhuru Kenyatta aliongea na Wakenya ambapo pamoja na mambo mengine aliwahakikishia kuwa serikali yake ipo nao bega kwa bega katika kipindi hiki kigumu.
ADDRESS TO THE NATION BY H.E. UHURU KENYATTA, C.G.H, PRESIDENT OF THE REPUBLIC OF KENYA AND COMMANDER-IN-CHIEF OF THE DEFENCE FORCES ON COVID-19, COMMONLY KNOWN AS CORONAVIRUS AT HARAMBEE HOUSE, NAIROBI ON 15TH MARCH 2020https://t.co/8xPwW7ZG49 pic.twitter.com/uC7nqhpgG3— State House Kenya (@StateHouseKenya) March 15, 2020
Twende Afrika Kusini. Mara baada ya kufahamika kuwa nchi hiyo imekumbwa na Coronavirus, Rais Cecil Ramaphosa aliwapatia Waafrika Kusini taarifa hiyo huku akitanabaisha kuwa hakuna sababu yakuona aibu wala kuficha taarifa hiyo kwa sababu ugonjwa huo umezikumba nchi nyingine pia.
President Cyril Ramaphosa outlines the Government plan to address the Coronavirus outbreak, #CoronaVirusSA https://t.co/JwqpsVaSeU— South African Government (@GovernmentZA) March 15, 2020
Kwa majirani zetu wa Rwanda, Rais Paul Kagame alikwenda hatua kadhaa mbele kwa kujipanga vilivyo dhidi ya Coronavirus kabla haijaingia nchini humu ambapo licha ya kuweka sehemu za kuosha mikono katika maeneo mbalimbali,
HE President Paul Kagame means business with the fight against coronavirus. He's moving at the speed of lightning. He has installed modern hand sanitizers on the streets of Kigali within 10 hours. They are also working on ensuring drones spray designated places. pic.twitter.com/v70jNgE4jI— J'rome (@Japex_hq) March 18, 2020
Rais Kagame alimtimua Waziri wake wa Elimu kwa kutoa taarifa za uongo kuhusu vifaa kwa ajili ya Coronavirus.
Rwanda President, Paul Kagame sacks Health Minister Over Mishandling Coronavirus Testing Kitshttps://t.co/Ae6pc0RJMU— corporateedgemag (@corporateedgem1) February 19, 2020
Na baada ya nchi hiyo kukumbwa na janga hilo, Rais huyo aliongea na Wanyarwanda na kuwataka wachukue hatua za tahadhari badala ya kuwa na hofu tu.
Rwanda confirms first coronavirus case; President Kagame cautions against panic - https://t.co/ggAJWBj6WG pic.twitter.com/HhZsyMte7Z— Adom (@Adomonline) March 15, 2020
Na kwa majirani zetu wa DRC, Rais Felix Tshisekedi alihutubia taifa na kueleza mikakati mbalimbali ya serikaliyake katika kupambana na janga hilo la Coronavirus.
#DRC President Tshisekedi took measures Wednesday for curbing the spread of #coronavirus —including barring entry to passenger planes from countries hit by the virus; shuttering schools & churches; banning funeral rites & gatherings of more than 20 people.https://t.co/Mvc8CGVFVi pic.twitter.com/SwkHoqyzwH— alexengwete (@alexengwete) March 18, 2020
Nchini Ethiopia, Waziri Mkuu Ahmed Abiy amekwenda mbali zaidi ya kuwajali Waethiopia wenzie na amefanikiwa kupata sapoti ya mmoja wa matajiri wakubwa duniani Jack Ma, kutoa sapoti kwa mataifa mengine ya Afrika kupambana na janga la Coronavirus.
PM Abiy Ahmed announced on a tweet that he had secured support from Jack Ma to fight the spread of Coronavirus in #Africa. The PMO also announces today that primary and secondary schools, sporting activities and large gatherings will be suspended for the next two weeks. #Ethiopia pic.twitter.com/mlBLN4G2as— AllureEthiopia (@AllureEthiopia) March 16, 2020
Na huko Uganda, licha ya nchi hiyo kutokuwa na maambukizi yoyote ya Coronavirus, Rais Yoweri Museveni amehutubia taifa na kutangaza hatua kadhaaza kujikinga dhidi ya janga hilo
Ugandan President Yoweri Museveni has ordered the closure of all schools and public gatherings for a period of one month amid Coronavirus spread. #africanews #ugandanews #coronavirus https://t.co/xUH4bcf2uA— African Stand (@africanstand) March 19, 2020
Sasa turudi Tanzania kwetu. Mara ya mwisho kwa Rais Magufuli kusikika na kuonekana hadharani ni majuzi ambapo sio tu alidai kuwa Coronavirus haijaingia nchini Tanzania (japo masaa machache baadaye Waziri wake, Ummy Mwalimu alitangaza kuwa in fact tayari Tanzania ina mgonjwa mmoja mwenye maradhi hayo) bali pia hakutangaza hatua zozote za msingi kukabiliana na ujio wa janga hilo. Na kama mzaha vile, alikiri kuwa alikosea kusababisha mkusanyiko wa watu kusikiliza hotuba yake.
Big liar! pic.twitter.com/K8oXIyixUY— Evarist Chahali (@Chahali) March 16, 2020
Lakini siku hiyohiyo, Msemaji Mkuu wa Serikali, Dkt Abbasi aliongea upuuzi mkubwa dhidi ya Watanzania walioonyesha hofu kuhusu janga la Coronavirus.
VIDEO: “Ukiona Mtu kachukuliwa na Ambulance Airport sio kwamba ana corona, hatupimi corona Airport bali ni kupima joto kwanza, juzi ilitokea Kilimanjaro Mtu joto lilizidi Watu mitandaoni Watu corona corona” -Msemaji Mkuu wa Serikali Dkt. Hassan Abbasi https://t.co/nOCECMicRd pic.twitter.com/onRuoA4UoU— millardayo (@millardayo) March 16, 2020
Masaa machache baadaye, Waziri wa Afya Ummy Mwalimu akatangaza kuwa Tanzania ina mgonjwa mmoja wa Coronavirus.
Waziri wa Afya Ummy Mwalimu amesema Tanzania imethibitisha mgonjwa wa kwanza wa Coronavirus akiwa ni Mtanzania aliewasili toka nchi Ubelgiji.Amesema mgonjwa anaendelea vizuri na matibabu na kwamba Serikali inashirikiana na wadau kudhibiti kusambaa zaidi. #PlusXtraUpdates pic.twitter.com/pDl6q8FMIS— Classic FM Radio (@classicfm255) March 16, 2020
Na Waziri Ummy amegeuka simulizi baadaya kupatikana video hii ambapo anatanabaisha kuwa Tanzania haiwezi kukabiliana na Coronavirus.
Yu wapi @MagufuliJP when you need him most? pic.twitter.com/Qg8v4chg54— Evarist Chahali (@Chahali) March 17, 2020
Tangu tutangaziwe uwepo wa ugonjwa huo hatujamsikia tena Magufuli. Sijui amejificha wapi. Na kama ilivyozoeleka katika nyakati za majanga, "ghafla" Waziri Mkuu Kassim Majaliwa "amekuwa Waziri Mkuu tena"
Ghafla Majaliwa "amekuwa Waziri Mkuu tena" kama inavyotokea kila wakati Tanzania ikikumbwa na majanga. @MagufuliJP ni hodari wa maneno tu, lakini nyakati za majaribu anakuwa mdogo kama piritoni. Ndo maana nikatoa wito huu kwa @zittokabwe @SeifSharifHamad na @freemanmbowetz— Evarist Chahali (@Chahali) March 18, 2020
ambapo ndio amekuwa "sauti ya serikali" kuhusu hatua mbalimbali dhidi ya janga hilo, ikiwa ni pamoja na hatua ya kufunga shule za awali, msingi na sekondari na vyuo.
Lakini uzeofu unaonyesha kuwa kila inapotokea Tanzania kukumbwa na janga fulani, Magufuli hukwepa dhamana aliyonayo kama "comforter-in-chief," yaani "mfariji mkuu wa taifa." Uthibiisho kuhusu hilo upo kwenye matukio mengi lakini pengine tukio lililoacha kumbukumbu ya muda mrefu kwa Watanzania ni dharau alizowafanyia wahanga wa tetemeko la ardhi huko Kanda ya Ziwa.
Licha ya yeye kuwa mzaliwa wa eneo hilo, alikaa muda mrefu bila kwenda kuwapa pole wahanga wa tetemeko hilo, na alipokwenda "akawasemea ovyo."
Huu si wakati wa kulaumiana lakini pia huu si wakati wa kuzembea. Ni kwa minajili hiyo nimekuwa nikitoa wito kwa viongozi wakuu wa Upinzani, Mheshimiwa Zitto Kabwe, Mheshimiwa Freeman Mbowe na Mheshimiwa Maalim Seif kutoa ninachokiita "uongozi mbadala wakati huu ambapo Tanzania inakabiliwa na janga kubwa la Coronavirus.
Dears @zittokabwe @SeifSharifHamad na @freemanmbowetz uongozi mbadala unahitajika katika kipindi hiki kigumu kwa taifa letu. I know ni ngumu kwa sababu @MagufuliJP ametumia miaka mitano kujenga chuki lakini utumishi wenu kwa Watanzania dhidi ya #coronavirus hauhitaji ridhaa yake— Evarist Chahali (@Chahali) March 18, 2020
Na endapo Magufuli hatobadilika, kwa maana ya "kuendelea kujificha," basi Watanzania watakuwa na kila sababu ya kutomhitaji tena kwenye uchaguzi mkuu ujao hapo Oktoba mwaka huu
#Coronavirus in #Tanzania: Where is @MagufuliJP? pic.twitter.com/BzkY8yhCH1— Evarist Chahali (@Chahali) March 18, 2020
Nimalizie makala hii kwa kukumbushia umuhimu wa kuchukua hatua binafsi dhidi ya maambukizi ya ugonjwa huu hatari wa Coronavirus. Nimekutengenezea video hii fupi
Mungu atulinde sote. Amen.