31 Jan 2012


Rais Jakaya Kikwete amekiri kuwepo kwa mkanganyiko uliojitokeza kufuatia kauli ya Waziri Mkuu Mizengo Pinda kuwa Rais ameridhiria nyongeza ya posho za Wabunge.Rais alisema hayo katika majadiliano kati yangu na yeye kupitia mtandao wa Twitter kama inavyoonyesha picha hapa juu na hapa chini


Awali,Rais Kikwete alifafanua kuwa ni kweli alitoa maelekezo kuhusu suala la posho hizo lakini maelekezo hayo hayakuwa kuridhia jambo hilo.Kadhalika,Rais alibainisha kwamba alikubali haja ya kuangalia upya posho za wabunge na aliwataka wabunge kutumia hekima na busara katika kutafakari.Vilevile aliwataka wabunge kutumia Kikao cha Februari cha Bunge kulizungumzia upya suala hili,na kusistiza ni muhimu.Picha ifuatayo inaonyesha maelezo hayo ya Rais Kikwete kwenye mtandao wa Twitter.


Jana,gazeti la Mwananchi lilikuwa na habari iliyobeba kichwa 'JK ABARIKI POSHO MPYA ZA WABUNGE' ambapo pamoja na mambo mengine habari hiyo ilieleza kuwa Waziri Mkuu Pinda amesema kuwa tayari Rais Kikwete amesaini kuridhia ongezeko la posho za vikao (sitting alllowances) kwa wabunge kutoka shilingi 70,000 hadi shilingi 200,000 kwa siku.Picha ifuatayo inaonyesha sehemu ya habari hiyo:


Hata hivyo,mapema leo Kurugenzi ya Mawasiliano ya Ikulu ilitoa taarifa ya maandishi kukanusha habari hizo, kama inavyosomeka hapa chini

Taarifa Ya Ikulu

Blogu hii inaendelea kufatilia kwa karibu kuhusu suala hilo.

JK abariki posho mpya za wabunge 
Monday, 30 January 2012 20:54
Rais Jakaya Mrisho Kikwete
KILA MMOJA KULIPWA 330,000 KWA SIKU, ZITTO, MAKAMBA, KIGWANGALA WASULUBISHWA KWA KUZIPINGA
Waandishi Wetu, Dodoma  
WAZIRI Mkuu, Mizengo Pinda amesema tayari Rais Jakaya Kikwete amesaini kuidhinisha ongezeko la posho za vikao (sitting allowance) kwa wabunge kutoka Sh70,000 hadi Sh200,000 kwa siku.  Kupitishwa kwa posho hizo ambazo ziliandikwa kwa mara ya kwanza na gazeti hili, kunafanya sasa mbunge kupokea Sh330,000 kwa siku; Sh200,000 zikiwa ni posho ya kikao, Sh80,000 posho ya kujikimu na Sh50,000 nauli.  

Taarifa za uhakika kutoka ndani ya kikao cha utanguzi cha wabunge jana, zilidai kuwa baada ya Pinda kutoa taarifa hiyo, wabunge walishangilia huku Mbunge wa Kigoma Kaskazini (Chadema), Zitto Kabwe, akisimama na kudai kuwa taarifa alizonazo ni kwamba Rais Kikwete alikuwa hajasaini kuidhinisha posho hizo.  

Hatua hiyo ilisababisha Mbunge wa Kondoa Kaskazini, Juma Nkamia (CCM), kusimama na kuhoji iwapo Zitto ni miongoni mwa wasemaji wa Rais kabla ya Pinda kusimama na kuthibitisha kusainiwa kwa posho hizo akisema siyo ajabu kwani hata watumishi wa Serikali wanalipwa kati ya Sh150,000 na Sh200,000.  Hata hivyo, Zitto alitetea msimamo wake kwamba alitarajia baada ya kusainiwa kwa posho hizo na Rais, angepewa masharti mapya ya kazi za ubunge.  

Katika kikao hicho baadhi ya wabunge wanadaiwa kuwashambulia Zitto, Mbunge wa Bumbuli (CCM), January Makamba na Mbunge wa Nzega (CCM), Dk Khamis Kigwangwala kwamba wamekuwa mstari wa mbele kupinga posho hizo hadharani.  Spika wa Bunge, Anne Makinda ambaye anadaiwa kwamba aliungana na Pinda kuthibitisha kwamba Rais Kikwete ameidhinisha posho hizo mpya, pia aliwashambulia wabunge wanaozipinga akisema kwamba wanafuta umaarufu wa kisiasa.

“Wanachotafuta ni umaarufu wa kisiasa tu, mimi ninavyojua umaarufu wa kisiasa unakuja kwa kufanya kazi za kibunge za wananchi lakini siyo kupinga posho,” chanzo chetu cha habari kilimnukuu Makinda.

Mbunge wa Gando (CUF), Khalifa Suleiman Khalifa anadaiwa kwamba alitumia mafumbo  kuwashambulia wabunge hao ambao wamejitokeza kupinga nyongeza hiyo ya posho.  Kauli hiyo inadaiwa kuungwa mkono na Mbunge wa Sikonge (CCM), Said Nkumba ambaye alidai kuwa hawezi kumsemea Zitto kwa sababu ni kawaida yake kupinga, lakini akaelekeza shutuma zake kwa Makamba kwamba ameanza kupinga baada ya kugharamiwa na CCM. “Januari anapinga posho hizo kutokana na CCM kumpa gari, nyumba na analipwa na chama,” kilisema chanzo chetu kikimkariri Nkumba.

 Pia, Mbunge wa Kilindi, Beatrice Shelukindo (CCM), anadaiwa kumshambulia Zitto kuwa lazima apinge posho hizo kwa sababu, anapewa fedha na wafadhili kutoka nchi za nje.  “Shelukindo anasema amefanya ziara nje na kuhakikisha kuna wahisani wanamfadhili Zitto kwa hiyo ana haki ya kupinga posho hizo,” chanzo chetu hicho kilimkariri Shelukindo.
 
Hata hivyo, inadaiwa kuwa baada ya mashambulizi hayo, Dk Kigwangwala alisimama kutetea msimamo wake kwamba ongezeko hilo halina ‘mashiko’ na haliwezi kuelezwa mbele ya umma likaeleweka, lakini alizomewa na wabunge wengi huku wakimtaka kukaa chini.  

Hatua hiyo ilisababisha Zitto kusimama na kueleza kuwa tatizo la wabunge kwamba wana fikra finyu, kauli ambayo alitakiwa na wenzake kuwaomba radhi kuwa amewatukana.  “Zitto ametumia Kiingereza kuwa tatizo la wabunge ‘we think small’,  Shelukindo na (John) Komba wakaja juu wakitaka kuwaomba radhi kwa kuwatukana,” chanzo chetu kilieleza.  Zitto anadaiwa kusema wabunge walitakiwa kujenga hoja ya kuongeza fedha za mafuta ya gari wanayolipwa hivi sasa Sh2.5 milioni kwa mwezi, kutokana na kupanda kwa nishati hiyo, lakini siyo posho.  

Mbunge wa Ubungo (Chadema), John Mnyika alinukuliwa akisema matatizo ya posho yamefikia hapo baada ya kuonekana ni ya watu binafsi siyo mfumo hivyo, wanaopinga wanaonekana kama wanatafuta umaarufu na wana vipato vya fedha, akaitaka kamati ya uongozi ijadili na kupata mwafaka badala ya wajumbe kutofautiana mbele ya umma.  Wabunge wengine wanaodaiwa kutetea posho hizo ni Mbunge wa Rombo (Chadema), Joseph Selasini na Jenister Mhagama (Peramiho CCM).

 Msimamo wa January
Alipoulizwa kuhusu suala hilo, Makamba alijibu: “Si sahihi kwangu kutoa taarifa za kikao cha ndani. Lakini msimamo wangu kwenye suala hilo unajulikana na haujabadilika.  Msimamo wa CCM ulishawekwa wazi na sote tunaujua. Nitalizungumzia suala hili kwa kirefu katika siku zijazo.”

Kuhusu taarifa kwamba anagharamiwa na CCM, alisema hawezi kuzungumzia suala hilo na badala yake kutaka kiulizwe chama hicho.

Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye alipoulizwa kuhusu taratibu za kuwagharamia viongozi wa chama chake ambao ni wabunge alisema: “Mbunge au kiongozi yeyote wa chama mwenye nafasi nyingine anagharamiwa na chama pale anapokwenda kufanya shughuli za chama tu na si vinginevyo.”

“Kwa hiyo kama ni mbunge suala la mafuta, dereva, mahali pa kulala na mahitaji mengine anagharamiwa na taasisi anayoifanyia kazi na siyo chama.”

“Kwa mfano, mimi kwenye sekretarieti hata posho za vikao huwa sichukui, nadhani na mwenzangu January naye sidhani kama huwa anachukua posho, kwa sababu tukifanya hivyo ni kama tunakiumiza chama, huo ndiyo msimamo wetu na uko wazi wala siyo kificho.”

Kwa upande wake, Zitto alisema jana kwamba hakuwa katika nafasi ya kuzungumzia suala hilo na badala yake kuahidi kwamba atalizungumza leo atakapokutana na waandishi wa habari.

Wabunge walia njaa
Taarifa kutoka ndani ya kikao hicho zilisema wabunge hao walilalamikia kucheleweshwa kulipwa posho zao za wiki mbili walizokaa Dar es Salaam wakati wa vikao vya kamati.

Walidai hivi sasa wanaishi kwa shida huku wakihoji sababu za kucheleweshewa.

Imeelezwa kwamba Spika Makinda alidai kuwa fedha hizo zipo na kwamba  kilichochelewesha ni uhakiki wa wabunge waliohudhuria vikao.

Makinda alisema baadhi ya wabunge wamekuwa wakilipwa posho za vikao bila kuhudhuria, hatua ambayo imesababisha Mkaguzi na Mdhibiti Mkuu wa Serikali (CAG), kuhoji maswali mengi.

CHANZO: Mwananchi

Blandina Nyoni

Lucy Nkya

Default Kituko Wizara ya Afya, Blandina Nyoni haivi na Lucy Nkya. Hawasalimiani hata wakikutana kwenye kordo

Ndugu zangu hii taarifa nimeipata kutoka kwa wandani wangu aliopo pale Wizara ya Afya. Kwamba Katibu Mkuu wa Wizara Bi Brandina Nyoni haivi na Naibu Waziri wake, Bi Lucy Nkya. Na inadaiwa kuwa hata wakikutana kwenye kordo huwa hawasalimiani. Kinachowazungumzisha ni Madokezo tu. 


Taarifa inasema kwamba ugomvi wao ulitokana na kitendo cha Katibu Mkuu kutaka kumlazimishia kumpa Dereva (Elias Mkumbo) ambae ni Informer wake. Mama Nkya alipotonywa na watumishi wa pale akamkataa huyo Dereva na ali command alitewe dereva aliyekuwa nae kutoka Wizara aliyokuwepo kabla kama sivyo abadilishiwe. Tangu wakati huo Wakuu hawa wa Wizara wamesusiana (Kama wanavyosema watu wa Pwani). 


Blandina Nyoni amekumbwa na matukio mengi ya kususiana na Wakubwa wenzako toka alipokuwa Katibu Mkuu Wizara ya Maliasili na Utalii ambapo alikuwa haivi na hasalimiani na Waziri wake Bi Shamsi Mwangunga. Alipohamishiwa Afya mwishoni mwa 2008 pia akagombana na Naibu Waziri wa wakati huo Bi Aisha Kigoda na hadi anaondoka Wizarani hapo bado walikuwa hawaivi. Sijui huyu Mama ni Mtu gani? Maana hata watumishi wake kuazia alipokuwa Hazina, Maliasili na Sasa Afya wamekuwa wamkimkataa kutokana na Uongozi wake Mbovu wa kutojali maslahi halali ya watumishi wake mfano malipo ya likizo, uhamisho, extra duty allowances, etc!
CHANZO: Jamii Forums 


Kwa hisani ya  King Kinya na Global Publishers

29 Jan 2012

Hello to everyone, first and foremost thank you to the blogging community for supporting my family though the past couple of years. 
Growing Up African Season II is coming up bigger & better than ever before. As you know sponsorship takes a while so we are working through it. 

Sema Ukweri is a New Blog created by myself Johnson Lujwangana. It's presents my LIFE and my viewpoint living in both Tanzania & America.
The Blog will take you from a street corner in the Bronx to a busy restaurant in Sinza. From a party in las Vegas to a mellow dinner at Sea Cliff. 
Depending on my location and it changes everyday, you'll always get to read a mind scratching article. 
Is Man City the best team? Is college even worth it anymore? Who's the sexiest celeb in Bongo? What's the best trends in the industry?
What hairstyles workout for men? When should a man think about proposing? Is it okay to have a child out of wedlock? Am I my father's MIRROR! 

The BLOG is different and presents a real perceptive on today's issues. We all have issues, so I hope by being truthful it can help some of my readers in theirs.
CLICK ON the LINK BELOW, you thank me for it. 


PS: I decided to spell Ukweri instead of UKWELI just out of respect. 


Problem Solving Flowchart
CHADEMA ndio wamesababisha mgomo wa madaktari

Wanabidii
TAARIFA za kiintelijensia zimebaini kuwa CHADEMA ndio wamesababisha mgomo wa madaktari, mgomo ambao umeendelea kwa siku kadhaa sasa na umehatarisha maisha ya wagonjwa wengi na umesababisha hata madaktari kuvuana uanachama kwenye chama chao cha madaktari.

CHADEMA ndio hao hao wamekuwa wanaratibu migomo mingi kwenye vyuo vikuu, ndio haohao wameratibu mgomo wa madereva wa malori kule Mbeya lakini pia ni CHADEMA walio hakikisha Naibu Waziri wa Afya anagoma kwenda kuonana na madaktari pale kwenye ule ukumbi walioandaa wao maana protokali na
usalama wake ulikuwa hatarini.

Hawa CHADEMA hawafai, maana wanataka nchi isitawalike, Wanafanya haya wakijua kuwa Rais Kikwete yuko kwenye mkutano wa uchumi duniani na kule anakutana na kuongea ikiwa ni pamoja na kupiga picha na Bill Gates na matajiri wengine wa dunia ili watusaidie kujikwamua kutoka kwenye mkwamo wa njaa na uchumi mbovu.

CHADEMA ndio hawa hawa wamesababisha sasa hivi shilingi yetu imeshuka thamani maana muda mwingi wanautumia kuwasumbua watu waliokuwa wanajua matumizi ya shilingi na sasa wamekasirika na matokeo yake shilingi imeshuka thamani.

CHADEMA ni watu wabaya sana, maana baada ya mgomo huu wa madaktari wataandaa mgomo mwingine waliouahirisha na walimu mwaka jana, wanachowaza CHADEMA ni migomo tu ili serikali idorore na nchi isitawalike, CHADEMA ni chama cha fujo na maandamano.

Chama hicho kimewezesha mgomo mpaka ndani ya Chama cha Mapinduzi (CCM) na kusababisha wale makada wenye magamba kugoma kuvua magamba yao! Hiki chama ni kibaya sana kinawanyima usingizi viongozi na makada wa chama cha magamba.

Watanzania mtambue kuwa CHADEMA ni chama kibaya sana maana ndicho kimesababisha minong’ono, eti Dk. Harrison Mwakyembe amewekewa SUMU! Nani amuue kiongozi huyo?

Mwakyembe hana tatizo kubwa anaugua tu mafua na hata ripoti yake ni CHADEMA hao hao ndio wameizua, maana wanajua kuwa ikiwekwa hadharani italeta tena mambo yake yenye harufu ya ki - Richmond.

CHADEMA ni watu wabaya sana, maana wamesababisha maisha magumu kwa kila Mtanzania, tofauti na ahadi za CCM kutaka kuwapa maisha bora kila Mtanzania, chama hicho kimesababisha mpaka umeme unatolewa kwa mgawo na unakatika katika mara kwa mara.

Tusiwaamini watu hawa, maana wanataka kuiondoa serikali iliyoko madarakani kwa maandamano kwa madai kuwa imeshindwa kuboresha huduma za msingi kwa Watanzania.

Nadhani sasa ni wakati muafaka kwa CHADEMA kimsababishe Rais Jakaya Kikwete agome kuingia IKULU, ili nchi iingie kwenye uchaguzi kabla ya mwaka 2015, kwakuwa huko kote kutakuwa mbali sana.

Hii ni siri yako! Hata yale mafuriko yaliyotokea jijini Dar es Salaam na kusababisha ndugu zetu kuhamia kwenye majumba ya nguvu kule Mabwepande, ni jamaa hawahawa wakiongozwa na makamanda wao. Hawa jamaa ni nuksi!


CHANZO: Tanzania Daima



Although this guy claims "I know anytime you sing for god [sic] it doesn't matter how you sound..." this kind of singing could very well annoy God


28 Jan 2012



Kwa niaba ya wasomaji wa blogu hii naomba kukutakia heri kwa siku yako ya kuzaliwa.Ni matumaini yangu kuwa utaendelea kuwa accessible na kudumisha dhana ya uongozi ni pamoja na kuwa karibu na wananchi.Ninatumaini pia kuwa tutaendeleza mijadala mbalimbali kwenye 'kijiwe chetu' cha Twitter.

Enjoy your big day!


Rais Barack Obama akiwa na wageni wake,Rais Mstaafu George H.W. Bush  na mwanae Gavana wa zamani wa Florida  Jeb Bush,walipomtembelea Ikulu ya Marekani Ijumaa iliyopita

CHANZO (na kwa habari kamili): Politico

Jasusi ChatBot

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.