29 Jan 2011


Katika siku za hivi karibuni,gazeti la Tanzania Daima limeonekana kama linafanya juhudi za wazi kuiweka profile ya Edward Lowassa machoni na masikioni mwa wasomaji wa gazeti hilo.

Ukidhani observation hii ni ya majungu,basi nakushauri uanze na habari zilizo kwenye toleo la kesho Jumapili (mbalo tayari lipo mtandaoni katika tovuti ya gazeti hilo) kisha fanya assessment yako Jumapili ijayo,na nyingineyo.

Je hizi ni sehemu ya kampeni za kumrithi Kikwete 2015?

Nimechokoza tu udadisi,hitimisho nakuachia wewe msomaji

2 comments:

  1. Kama yakifanyika mashindano ya unafiki Tanzania nadhani washindi wanaweza kuwa watu wanne. Wa kwanza atakuwa Edward Lowassa, wa pili atakuwa Jakaya Kikwete. Wa tatu watakuwa waandishi wa habari na wa mwisho Wadanganyika au Bongolalalanders.
    Haya mauza uza yanayoendelea yanaweza kukupa picha kamili. Sitaki nimalize utamu.
    Nimalize kwa kukushauri kijana Chahali. Wenzako wanapokutembelea nao watembelee. Quo vadis? Kwa lugha rahisi, twaenda wapi?

    ReplyDelete
  2. Mkuu Mhango,asante kwa maoni.Ukweli ni kwamba natembelea kiwanja chako kila napoingia Google Reader.Kumbuka nilishatamka hadharani kuwa u-miongoni mwa sababu zinazonifanya niendelee kublogu.Nakiri uzembe wangu katika kuacha comments lakini katika maandishi yaliyojitosheleza kama yako,nadhani sio mie pekee ninayechelea kuharibu ladha ya ulichotuandalia bali tunaishia kuafikiana nawe akilini na rohoni.Otherwise,tupo pamoja mkuu.Tunaunganishwa na imani na dhamira zetu katika hatakati tunazofanya.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.