Showing posts with label TANZANIA DAIMA. Show all posts
Showing posts with label TANZANIA DAIMA. Show all posts

19 Nov 2011


Kupitiwa, Uzembe au Ufisadi wa Kitaaluma (ya uandishi wa habari)?Leo ni Jumamosi ya tarehe 19 Novemba 2011 lakini tovuti ya Tanzania Daima ina habari za Jumatatu ya tarehe 11 April 2011,zaidi ya miezi saba iliyopita.Hii ni aibu kubwa kwa gazeti ambalo limejipatia umaarufu kwa kukemea ubabaishaji,uzembe na ufisadi...

HOVYOO!!!

2 Apr 2011


Baadhi ya magazeti ya Tanzania yanaelekea kutothamini kabisa uwepo wake mtandaoni.Hivi inaingia akilini kweli kwa msomaji kutembelea tovuti ya gazeti na kukutana na "habari mpya" za Februari 3,2011?Hiyo ndio hali niliyokutana nayo kwenye tovuti ya gazeti la Tanzania Daima.

Awali,gazeti hili lilikuwa makini sana katika kuweka habari mpya kwenye tovuti yake lakini sijui "kirusi" gani kimewakumba.Tovuti yao imeendelea kuwakaribisha wasomaji na ujumbe kuwa ipo "off-line kwa matengenezo".Matengenezo gani hayo ya zaidi ya mwezi mzima?

Tatizo la msingi kwa magazeti yetu mengi ni dhana potofu kuwa toleo la mtandaoni ni kama fadhila kwa wasomaji.Pengine dhana hiyo inajengwa na ukweli kwamba matoleo ya mtandaoni husomwa bure,na hivyo kuwafanya wahusika kujiona kama "wanafanya kazi ya Kanisa" (yaani isiyo na ujira).

Sasa,kama wanataka habari zao zisomwe mtandaoni kwa malipo wanaweza kuanzisha huduma ya kulipia (paywall).Lakini kama wameamua kwa hiari yao kuanzisha tovuti na kuweka habari zisomwe bure basi wanapaswa kuwajibika kwa kutuwekea habari mpya kama inavyostahili.

29 Jan 2011


Katika siku za hivi karibuni,gazeti la Tanzania Daima limeonekana kama linafanya juhudi za wazi kuiweka profile ya Edward Lowassa machoni na masikioni mwa wasomaji wa gazeti hilo.

Ukidhani observation hii ni ya majungu,basi nakushauri uanze na habari zilizo kwenye toleo la kesho Jumapili (mbalo tayari lipo mtandaoni katika tovuti ya gazeti hilo) kisha fanya assessment yako Jumapili ijayo,na nyingineyo.

Je hizi ni sehemu ya kampeni za kumrithi Kikwete 2015?

Nimechokoza tu udadisi,hitimisho nakuachia wewe msomaji

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.