6 Jan 2008


Nimesoma makala moja ndefu katika toleo la leo la Sunday Times (la hapa Uingereza) kuhusu hali ilivyo kwa majirani zetu wa Kenya.Kwa kweli inatisha na kusikitisha.Mauaji na ubakaji ni miongoni mwa unyama unaozidi kushamiri nchini humo.Lakini inasikitisha zaidi kuona hata watoto wadogo wa miaka 12 wanakumbwa na ukatili huo.

Lakini kilichonikurupusha kuandika makala hii ni habari kwamba vurugu hizo zinahusisha pia makundi mawili hatari:Mungiki (la Wakikuyu) na Taliban (la Waluo).Kwa namna inavyoonekana,makundi haya ni sawa na magenge ya wahalifu ambayo kwao vurugu za aina yoyote ni sawa na msimu wa mavuno.Inaelezwa kwamba Mungiki wamekuwa wakiwatahiri kwa nguvu "mateka" wao wa Kiluo (kwa mila zao,wanaume wa Kiluo huwa hawatahiri) huku Taliban wakijibu mashambulizi kwa kuwafyeka mapanga Wakikuyu.

Inatisha na kusikitisha kusikia kwamba watu kadhaa waliuawa kinyama kwa kuchomwa moto wakiwa ndani ya kanisa walilojihifadhi.Kwa nchi ambayo asilimia kubwa ya wakazi wake ni Wakristo,hiyo ni ishara kwamba chuki kati ya makundi yanayopingana zimevuka nguvu za mshikamano wa jamii kama dini na utaifa,na inaelekea kinachoangaliwa sasa ni ukabila tu.

Haihitaji ujuzi wowote wa mambo ya uchaguzi kubaini kwamba Kibaki amejirejesha kwa nguvu madarakani.Hivi anajisikiaje wakati yeye yupo Ikulu,mamia ya Wakenya wenzake,ikiwa ni pamoja na Wakikuyu wenzie,wanapoteza maisha yao kila siku huku wengine wanaishi kwa hofu na mashaka ya kuuawa,kubakwa,kutahiriwa kwa nguvu na udhalilishaji mwingine usiopaswa kufanyika katika jamii yoyote ile iliyostaarabika.Damu inayomwagika kila kukicha (sambamba na mateso yanayowakuta wananchi wasio na hatia) iko mikononi mwa Kibaki.

1 comment:

  1. Awari ya yote napenda kuchukua nafasi hii kukupongeza wewe binafsi kama Chahali kwa hatua nzuri uliyofikia kimasomo.Pili kuipongeza blog hii ambayo wewe binafsi unajalibu kutoa mawazo yako binafsi katika nyanja za siasa. Mimi kama mwana Kilombero mwezako niliyopo hapo Urusi mara kwa mara hupenda kutembelea katika blog hii, ingwa mimi siko kwenye fani ya mambo ya siasa lakini huwa napenda kufaham mambo yanayo zunguka jamii katika nyanja tofauti ikiwemo siasa.Katika blog hii huwa nasoma chambuzi zako nyingi ikiwa ni pamoja na habari za OBAMA na uchaguzi wa majirani zetu wa kenya.Kwa leo ningependa kuchangia kuhusu uchaguzi wa majirani zetu wa kenya, ni kweli kabisa kwamba wakenya wengi wamepoteza maisha katika vurugu zilizodumu takribani wiki moja na nusu hivi, na sababu kubwa ni kutokukubariana na matekeo ya uchaguzi hususa wa kiti cha Uraisi katika pande mbili zinazo pingana. Na tukumbuke kwamba Walao na Wakikuyu ni makabila makubwa yanayopingana nchini kenya, pamoja na hayo yote makabira hayo huwa hayaonyeshi upendo miongoni mwao, tofauti na Tanzania ambakowatu wa makabira tofauti hujichanganya katika shughuri mbalimbali za kijamii,Kisiasa,Utamaduni na michezo na hata kiuchum,kwa hiyo mauwaji hayo ni chuki zilizomo katika makabira hayo na uchaguzi huo umetumika kama kigezo tu cha kutimiza matakwa hayo.Na mimi siko mbali na wewe katika kurani mauwaji hayo.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.