8 Oct 2008


Inapotokea pundits wa Fox News,Mort Condracke,Bill Kristal,Nina Easton na Fred Barnes, wanakubaliana kitu kimoja "kummaliza" John McCain basi hapo huhitaji kwenda mbali kuhitimisha kwamba mgombea huyo kachemsha.And that's exactly what happened mara baada ya mdahalo kati ya Obama na McCain ambao ulichukua format ya town hall meeting.Kadhalika,mtizamo wa undecided voters kwa mujibu wa Frank Luntz ni kwamba Obama ameshinda tena mdahalo huo ambao ni wa pili kati ya midahalo mitatu iliyokubaliwa na wagombea hao.

Kwa mujibu wa wachambuzi wa uchaguzi huo,McCain alihitaji a kcock-out punch,yaani ilikuwa ni lazima afanye vizuri katika mdahalo huo ili kujiweka vizuri katika jitihada zake za kushinda uchaguzi hapo Novemba 4.Kura nyingi za maoni zinaonyesha mgombea huyo wa Republican akiwa nyuma ya Obama,na ilitarajiwa kwamba kufanya kwake vizuri katika mdahalo huo kungemsaidia kupunguza gap hiyo.Kilichokuwa kinawapa matumaini wafuasi wa McCain ni uzoefu wake katika town hall meetings.Hata hivyo,uzoefu huo unaonekana kutomsaidia mgombea huyo,na pengine fursa yake pekee ni aidha kitoke kitu kisichotarajiwa (hata kama hakihusiani na uchaguzi huo) ambacho kitabadili kabisa landscape ya uchaguzi huo au afanye vizuri kupita kiasi katika mdahalo wa mwisho (na wakati huohuo Obama afanye vibaya).

Moja ya kauli ambazo zinaweza kumgharimu McCain ni ile ya kumuita Obama "that one",na kinyume na mdahalo uliopita ambapo wagombea hao walishikana mikono kabla na baada,safari hii hilo halikutokea baada ya shughuli hiyo pevu ambapo McCain alikuwa wa kwanza kuondoka kitini (pengine kukwepa handshake na Obama).

Kwa uchambuzi na habari zaidi bofya HAPA na HAPA na HAPA

0 comments:

Post a Comment

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.