24 Mar 2009


NAKUOMBA SOMA HABARI MBILI ZIFUATAZO KISHA TUJADILI DHANA YA KULAZIMISHA UWAJIBIKAJI.KWA KIFUPI,KATIKA HABARI YA KWANZA,PAMOJA NA MAMBO MENGINE,DR SLAA ANAONYESHA KUWA CHADEMA INA USHAHIDI WA KUTOSHA KUIHUSISHA CCM NA WIZI WA EPA.KATIKA HABARI YA PILI,MWANASHERIA TINDU LISSU ANAMTAKA MKUU WA MKOA WA SINGIDA,MHESHIMIWA KONE,AOMBE RADHI HADHARANI KUTOKANA NA MADAI KUWA ALIWATUKANA HADHARANI BAADHI YA WANANCHI ANAOWAONGOZA.MJADALA UTAKAOFUATA BAADA YA HABARI HIZO UNAANGALIA MANTIKI YA DR SLAA NA CHADEMA KUENDELEA KUTUELEZA KWAMBA WANA USHAHIDI WA KUTOSHA UNAOIHUSISHA CCM NA UFISADI WA EPA,LAKINI KIONGOZI HUYO NA CHAMA CHAKE WAMEKUWA KANA KWAMBA WANATINGISHA KIBERITI VILE...KWA MAANA KWAMBA KAMA USHAHIDI UPO,KWANINI WASIFUNGUE KESI MAHAKAMANI KWA NIABA YA WANANCHI BADALA YA KUENDELEA KUDAI USHAHIDI TUNAO,USHAHIDI UPO...IRONICALLY,TINDU LISSU,MWANASHERIA ANAYEWATETEA BAADHI YA WAKAZI WA SINGIDA DHIDI YA MH. KONE,SIO TU NI MWANASHERIA WA CHADEMA BALI PIA NI MIONGONI MWA VIONGOZI WAANDAMIZI WA CHAMA HICHO.

ANYWAY,HEBU SOMA KWANZA HABARI HUSIKA

Chama tawala chaambiwa kuacha kutisha wananchi kuhusu ufisadi

Na Mussa Juma, Same.

KATIBU mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemtaka katibu mwenezi wa CCM, John Chiligati, kuacha vitisho dhidi ya upinzani, akisema kuwa wataendelea kufichua ufisadi uliotanda kwenye chama hicho tawala.

Chiligati alivionya vyama vya upinzani kuwa visitumie ufisadi kama ngazi ya kujipatia umaarufu, huku akionya kuwa kuendelea kuishutumu CCM kunaweza kuhatarisha amani kwa sababu kama watu milioni nne watachukia (akimaanisha wana-CCM), hakutakuwa na amani.

Lakini Dk Slaa, mmoja wa wabunge ambao wamesimama imara katika kufichua na kupiga vita ufisadi, alisema hakuna ubishi kuwa CCM imeingia madarakani kwa kuchotewa fedha kutoka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) na kama kinapinga, basi kiende mahakamani. Kauli hiyo ilitolewa jana na Dk Slaa wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Hedaru na Makayanya wilayani Same na baadaye kukutana na waandishi wa habari.

Dk Slaa alisema Chadema ina ushahidi wa maandishi jinsi CCM ilivyokuwa inachotewa fedha za EPA kupitia kampuni ya Kagoda, hivyo kama inaona inapakwa matope, inaweza kwenda mahakamani kulalamika na sio kutoa vitisho kupitia vyombo vya habari.

“Tunamshangaa sana Chiligati na tunamuomba aache vitisho. Tunao ushahidi hadi muhtasari wa kikao kilichoongozwa na rais mstaafu kikielezea jinsi walivyokuwa wanajichotea fedha za EPA na pia ujumbe mfupi kutoka kwa katibu mkuu wa CCM kwenda Benki Kuu kuomba fedha hizo. Sasa wanaposema hawahusiki na EPA tunawashangaa,” alisema Dk Slaa.

CHANZO: Mwananchi
HABARI YA PILI :


RC atakiwa kuwaomba radhi wananchi

na Deogratius Temba

MKUU wa Mkoa wa Singida, Vincent Parseko Kone, ametakiwa kuitisha mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kisasida, Wilaya ya Singida na kuomba radhi kwa wanachi na mwenyekiti wa kijiji hicho, kwa kuwatukana hadharani na kuwalipa fidia ya sh milioni moja.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa kijiji hicho, Ramadhani Mwankumbi, kutoa taarifa kuwa anakusudia kumfikisha mkuu huyo wa mkoa mahakamani kutokana na kumtukana hadharani wakati akiwa katika mkutano wa hadhara kijijini hapo.

Kwa mujibu wa barua aliyoandikiwa jana, Mkuu wa mkoa huyo, kutoka kwa Kampuni ya uwakili ya M/S TUNDU A.M. LISSU Advocates, yenye kumbukumbu namba TAML/SDG/RSM/KSSD/09/01, na kusaniwa na wakili wa kujitegemea Tindu Lissu, ilieleza Februari 24, mwaka huu, mkuu huyo wa mkoa alienda katika kijiji hicho na kutumia cheo chake kwa lengo alilodai kuwa ni kukagua mradi wa kilimo cha umwagiliaji. Badala ya kutembelea mradi huo, kama alivyodai, aliomba kumwona Mwenyekiti wa Kijiji Mwankumbi, na kuanza kumfokea mbele ya wanakijiji wenzake, viongozi wa mkoa na wananchi wengine wengi kwa madai kuwa ameshirikiana na mtu mwingine aitwaye, Josephat Isango, kumchafulia jina lake.

“Mteja wetu alipoomba nafasi ya kujieleza juu ya tuhuma ulizokuwa unamrushia ulikataa na badala yake ulianza kumtukana matusi mazito, baada ya kumtukana ukaondoka na kurudi Singida,” ilieleza sehemu ya barua hiyo. Pia barua hiyo ilieleza kisheria maneno hayo, ambayo yalitolewa na mkuu huyo wa mkoa ni kosa na ni kashfa dhidi ya mteja wao, na yamemdhalilisha, kumnyanyasa, kumvunjia heshima aliyokuwa nayo mbele ya wanakijiji waliomchagua na kumpa dhamana.

“Maagizo kutoka kwa mteja wetu ni kukutaka wewe Parseko Kone, utembelee tena Kijiji cha Kisasida na kuitisha mkutano wa hadhara wa wanakijiji wote na uwaombe radhi hadharani kwa maneno ambayo sisi tutakuelekeza.

“Aidha, tunakuagiza ufanye ziara ya mkutano huo wa kuomba radhi ndani ya siku 14, kutokea leo (jana), pia mteja wetu anadai umlipe sh milioni moja kama gharama za ufuatiliaji kwetu,” ilieleza barua hiyo.

Lissu, alidai kuwa mkuu huyo wa mkoa, endapo atashindwa kufanya hivyo, au kupuuza kutekeleza matakwa yao watamfungulia kesi ya madai katika mahakama watakayoichagua wao. Aliongeza pia kama Kone atashindwa kutekeleza madai yao, hawatasita kumdai fidia zaidi ya fedha na nafuu nyinginezo za kisheria dhidi yao.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Kone alizungumza na Tanzania Daima, alikanusha tuhuma hizo zinazomkabili na kudai kuwa alikwenda katika kijiji hicho kukagua mradi wa umwagiliaji na hakumtukana kiongozi yeyote.

MLOLONGO WA KULALAMIKA,KUTOA VITISHO AU HATA KULIA HAUWEZI KUKOMESHA UFISADI AU KUWAKUMBUSHA WAJIBU BAADHI YA VIONGOZI WANAOJIONA MIUNGU WATU.DR SLAA NA CHADEMA WAMEKUWA WAKITUAMINISHA KWAMBA CCM INAHUSIKA MOJA KWA MOJA KATIKA KUFANIKISHA UJAMBAZI WA EPA.JAPO NAFAHAMU KUWA HUKUMU YA UMMA INA MADHARA ZAIDI YA HUKUMU YA MAHAKAMA ZA KISHERIA,SOTE TUNAJUA NAMNA HUKUMU YA UMMA INAVYOWEZA KUPINDISHWA NA ZAWADI ZA KHANGA,FLANI,KILO YA SUKARI,NK KAMA VIVUTIO WAKATI WA UCHAGUZI.

NGOJA NIFAFANUE KAMA HUJANIELEWA VIZURI.YAYUMKINIKA KUAMINI KUWA CHADEMA INAPOITUHUMU CCM KWENYE MIKUTANO YA HADHARA KWAMBA CHAMA HICHO TAWALA KINA MAHUSIANO NA UFISADI/MAFISADI INATARAJIWA KUWA WANANCHI WATATOA HUKUMU DHIDI YA CCM (HUKUMU YA UMMA) WAKATI WA UCHAGUZI.HILO LINAWEZEKANA KATIKA MFUMO HURU WA DEMOKRASIA,NA MIFANO HAI NI NAMNA HUKUMU YA UMMA ILIVYOFANYA KAZI KATIKA CHAGUZI HUKO HISPANIA MWAKA 2004 NA MAREKANI MWAKA JANA.KATIKA CHAGUZI ZINAZOFANYIKA KATIKA MAZINGIRA YA DEMOKRASIA HURU,HASIRA ZA WAPIGA KURA (AU KURIDHISHWA KWAO) NI MIONGONI MWA MAMBO MUHIMU KATIKA KU-DETERMINE MATOKEO YA UCHAUZI HUSIKA.

SASA SOTE TUNAJUA MAZINGIRA YA CHAGUZI NYINGI ZA "DUNIA YA TATU".KANUNI ISIYO RASMI KUHUSU CHAGUZI ZETU INADAI KWAMBA CHAMA TAWALA HAKIWEZI KUSHINDWA UCHAGUZI.KIKISHINDWA BASI AIDHA KILIZEMBEA KUTUMIA MBINU ZAKE ZA AWALI ZA KUBAKI MADARAKANI AU KILIPIGIWA KURA ZA CHUKI NA WAFUASI WAKE AU KULITOKEA MPASUKO NDANI YA CHAMA TAWALA AMBAO ULIZAA MAKUNDI MAWILI YENYE TAKRIBAN NGUVU SAWA,KILA MOJA LIKIFAHAMU MBINU SAFI NA CHFU ZA KUSHINDA CHAGUZI,NK.WAPO WANAOAMINI KUWA HATA KANU YA MOI HAKIKUSHINDWA UCHAGUZI WA 2002 KWA VILE WAPIGA KURA WALIKUWA WAMEICHOKA (WHICH WAS TRUE i.e. kweli walikuwa wameichoka) BALI NI UTEUZI MBOVU WA MGOMBEA UHURU KENYATA.

VINGI VYA VYAMA TAWALA KATIKA NCHI ZA TATU HUSHIKILIA DOLA KWA MAANA HALISI YA KUSHIKILIA,YAANI WANAITUMIA IPASAVYO KUHAKIKISHA UTAWALA UNAENDELEA MILELE.HAKUNA DHAMBI KWA CHAMA KUWA MADARAKANI MUDA MREFU AS LONG AS KINAWAHUDUMIA WANANCHI IPASAVYO.KWA BAHATI MBAYA,U-KING'ANG'ANIZI WA BAADHI YA VYAMA TAWALA KATIKA NCHI ZA DUNIA YA TATU HAUTOKANI NA MAPENZI YAO KWA NCHI AU WANANCHI BALI HOFU YA KUADHIBIWA KWA MADHAMBI YALIYOWAFANYWA WAKATI VYAMA HIVYO VIKIWA MADARAKANI.KADRI MADHAMBI YANAVYOZIDI KUONGEZEKA NDIVYO KADRI VYAMA HIVYO VINAVYOZIDIWA NA HOFU YA NINI KITATOKEA PINDI VIKITOLEWA MADARAKANI,NA MATOKEO YAKE NI KUTUMIA KILA NJIA KUHAKIKISHA VINATAWALA MILELE.NA KWA VINASHIKILIA DOLA,HILO LINAKUWA SIO JAMBO GUMU.

KWAHIYO,KAMA DR SLAA,CHADEMA NA WENGINEO WANADHANI KELELE KUWA CCM INAHUSIKA KATIKA WIZI WA EPA ZITAFANIKISHA KUPATIKANA KWA HUKUMU YA UMMA KATIKA UCHAGUZI WA 2010 AU BAADAYE,THEY REALLY NEED TO THINK AGAIN.KUFANYA HIVYO NI SAWA NA KUTARAJI KUWA HUYO RC ANAYETUHUMIWA KUWATUKANA WANANCHI ANGEAMUA YEYE MWENYEWE KWA HIARI YAKE KUOMBA RADHI BADALA YA KULAZIMISHWA KUFANYA HIVYO (KAMA ANAVYOTAKIWA NA WAKILI LISSU).NAMNA PEKEE YA CHADEMA,ET AL WANAWEZA KUFANIKIWA KATIKA TUHUMA ZAO DHIDI YA CCM NI KWENDA MAHAKAMANI WAKIWA NA USHAHIDI WANAODAI KUWA NAO.

KUITAKA CCM IENDE MAHAKAMANI (INAPOTUHUMIWA KUWA NA UHUSIANO NA MAFISADI) NI SAWA NA KUMTAKA MTU UNAYEMTUHUMU KUTEMBEA NA MKEO/MUMEO (KUTEGEMEA JINSI YAKO MSOMAJI) AENDE POLISI/MAHAKAMANI.....KWA KIFUPI,ATAENDELEA KUKUIBIA NA HATOTIA MGUU POLISI/MAHAKAMANI.COMMON SENSE INATUELEZA KUWA MWENYE TUHUMA NDIO ANAYEPASWA KUWA NA UHARAKA WA KUZIDHIBITISHA AU KUWA NA DHAMIRA YA KUZITOKOMEZA KABISA.MTUHUMIWA ANAWEZA KUWA NA UHARAKA HUO IWAPO ANAONA ZINAMCHAFULIA JINA.LAKINI WHAT IF TUHUMA DHIDI YA MTUHUMIWA NI ZA KWELI?BADO TUTATEGEMEA MTUHUMIWA AJIEPELEKE KWENYE HUKUMU YAKE?

NAHISI CHADEMA WANACHELEA KWENDA MAHAKAMANI SIO KWA VILE WANAHOFIA KUTOPATA HAKI BALI WANAZITUMIA TUHUMA HIZO KUWA MTAJI WA KISIASA.NA-HYPOTHESIZE KUWA CHAMA HICHO KITAZITUMIA TUHUMA HIZO KWENYE KAMPENI ZAKE ZA UCHAGUZI MKUU WA 2010 KIKIAMINI KUWA ZITAKISAIDIA KUPATA USHINDI KWA HUKUMU YA UMMA DHIDI YA CCM.JAPO LOLOTE LINAWEZEKANA KATIKA SIASA,NA MBINU HIYO YA CHADEMA INAWEZA KUFANIKIWA,WAZOEFU WA SIASA WANAWEZA KUAFIKIANA NAMI KWENYE HYPOTHESIS YANGU YA PILI KUWA MKAKATI HUO HAUTOFANIKIWA.KINACHONIPELEKA KUAMINI HIVYO NI UZOEFU KUHUSU NAMNA CCM INAVYOELEWA UDHAIFU WA MPIGA KURA WA KITANZANIA,FAIDA ZA KILOJISTIKI ZINAZOELEMEA UPANDE WA CHAMA TAWALA,MILKI NA SAPOTI YA DOLA BILA KUSAHAU "MBINU CHAFU."

UCHAGUZI MKUU WA 2010 UNAWEZA KABISA KUPITA NA CCM KUIBUKA KIDEDEA HUKU CHADEMA IKIWA "IMEDODEWA" NA USHAHIDI WAKE DHIDI YA CCM.HILO SIO BAO LA KISIGINO BALI NI MITHILI YA KIBAKA KUKUPORA KISHA ANAKUPIGIA KELELE KUWA WEWE NDIO MWIZI....(AND WE ALL VERY WELL KNOW MOB JUSTICE HUKO NYUMBANI ZILIVYO...WATU WAKISKIA UKELELE WA MWIZI,MWIZI HAWAULIZI ILIKUWAJE.NI KIPIGO TU....PASIPO KUJUA KUWA WANAYEMPIGA NDIO ALOPORWA NA KIBAKA).

2 comments:

  1. Kaka Evarist nimepita kuja kukutembelea na kusema asante kwa kunitembelea kibarazani kwangu. Kazi nzuri kaka.

    ReplyDelete
  2. Jana nimejaribu sana kupost maoni hapa ikashindikana. Hapa najaribu kuona inakuwaje.

    ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube