Showing posts with label SLAA. Show all posts
Showing posts with label SLAA. Show all posts

24 Mar 2009


NAKUOMBA SOMA HABARI MBILI ZIFUATAZO KISHA TUJADILI DHANA YA KULAZIMISHA UWAJIBIKAJI.KWA KIFUPI,KATIKA HABARI YA KWANZA,PAMOJA NA MAMBO MENGINE,DR SLAA ANAONYESHA KUWA CHADEMA INA USHAHIDI WA KUTOSHA KUIHUSISHA CCM NA WIZI WA EPA.KATIKA HABARI YA PILI,MWANASHERIA TINDU LISSU ANAMTAKA MKUU WA MKOA WA SINGIDA,MHESHIMIWA KONE,AOMBE RADHI HADHARANI KUTOKANA NA MADAI KUWA ALIWATUKANA HADHARANI BAADHI YA WANANCHI ANAOWAONGOZA.MJADALA UTAKAOFUATA BAADA YA HABARI HIZO UNAANGALIA MANTIKI YA DR SLAA NA CHADEMA KUENDELEA KUTUELEZA KWAMBA WANA USHAHIDI WA KUTOSHA UNAOIHUSISHA CCM NA UFISADI WA EPA,LAKINI KIONGOZI HUYO NA CHAMA CHAKE WAMEKUWA KANA KWAMBA WANATINGISHA KIBERITI VILE...KWA MAANA KWAMBA KAMA USHAHIDI UPO,KWANINI WASIFUNGUE KESI MAHAKAMANI KWA NIABA YA WANANCHI BADALA YA KUENDELEA KUDAI USHAHIDI TUNAO,USHAHIDI UPO...IRONICALLY,TINDU LISSU,MWANASHERIA ANAYEWATETEA BAADHI YA WAKAZI WA SINGIDA DHIDI YA MH. KONE,SIO TU NI MWANASHERIA WA CHADEMA BALI PIA NI MIONGONI MWA VIONGOZI WAANDAMIZI WA CHAMA HICHO.

ANYWAY,HEBU SOMA KWANZA HABARI HUSIKA

Chama tawala chaambiwa kuacha kutisha wananchi kuhusu ufisadi

Na Mussa Juma, Same.

KATIBU mkuu wa Chadema, Dk Willibrod Slaa amemtaka katibu mwenezi wa CCM, John Chiligati, kuacha vitisho dhidi ya upinzani, akisema kuwa wataendelea kufichua ufisadi uliotanda kwenye chama hicho tawala.

Chiligati alivionya vyama vya upinzani kuwa visitumie ufisadi kama ngazi ya kujipatia umaarufu, huku akionya kuwa kuendelea kuishutumu CCM kunaweza kuhatarisha amani kwa sababu kama watu milioni nne watachukia (akimaanisha wana-CCM), hakutakuwa na amani.

Lakini Dk Slaa, mmoja wa wabunge ambao wamesimama imara katika kufichua na kupiga vita ufisadi, alisema hakuna ubishi kuwa CCM imeingia madarakani kwa kuchotewa fedha kutoka Akaunti ya Malipo ya Madeni ya Nje (EPA) na kama kinapinga, basi kiende mahakamani. Kauli hiyo ilitolewa jana na Dk Slaa wakati akihutubia mkutano wa hadhara katika kata ya Hedaru na Makayanya wilayani Same na baadaye kukutana na waandishi wa habari.

Dk Slaa alisema Chadema ina ushahidi wa maandishi jinsi CCM ilivyokuwa inachotewa fedha za EPA kupitia kampuni ya Kagoda, hivyo kama inaona inapakwa matope, inaweza kwenda mahakamani kulalamika na sio kutoa vitisho kupitia vyombo vya habari.

“Tunamshangaa sana Chiligati na tunamuomba aache vitisho. Tunao ushahidi hadi muhtasari wa kikao kilichoongozwa na rais mstaafu kikielezea jinsi walivyokuwa wanajichotea fedha za EPA na pia ujumbe mfupi kutoka kwa katibu mkuu wa CCM kwenda Benki Kuu kuomba fedha hizo. Sasa wanaposema hawahusiki na EPA tunawashangaa,” alisema Dk Slaa.

CHANZO: Mwananchi
HABARI YA PILI :


RC atakiwa kuwaomba radhi wananchi

na Deogratius Temba

MKUU wa Mkoa wa Singida, Vincent Parseko Kone, ametakiwa kuitisha mkutano wa hadhara katika Kijiji cha Kisasida, Wilaya ya Singida na kuomba radhi kwa wanachi na mwenyekiti wa kijiji hicho, kwa kuwatukana hadharani na kuwalipa fidia ya sh milioni moja.

Kauli hiyo imekuja siku chache baada ya Mwenyekiti wa kijiji hicho, Ramadhani Mwankumbi, kutoa taarifa kuwa anakusudia kumfikisha mkuu huyo wa mkoa mahakamani kutokana na kumtukana hadharani wakati akiwa katika mkutano wa hadhara kijijini hapo.

Kwa mujibu wa barua aliyoandikiwa jana, Mkuu wa mkoa huyo, kutoka kwa Kampuni ya uwakili ya M/S TUNDU A.M. LISSU Advocates, yenye kumbukumbu namba TAML/SDG/RSM/KSSD/09/01, na kusaniwa na wakili wa kujitegemea Tindu Lissu, ilieleza Februari 24, mwaka huu, mkuu huyo wa mkoa alienda katika kijiji hicho na kutumia cheo chake kwa lengo alilodai kuwa ni kukagua mradi wa kilimo cha umwagiliaji. Badala ya kutembelea mradi huo, kama alivyodai, aliomba kumwona Mwenyekiti wa Kijiji Mwankumbi, na kuanza kumfokea mbele ya wanakijiji wenzake, viongozi wa mkoa na wananchi wengine wengi kwa madai kuwa ameshirikiana na mtu mwingine aitwaye, Josephat Isango, kumchafulia jina lake.

“Mteja wetu alipoomba nafasi ya kujieleza juu ya tuhuma ulizokuwa unamrushia ulikataa na badala yake ulianza kumtukana matusi mazito, baada ya kumtukana ukaondoka na kurudi Singida,” ilieleza sehemu ya barua hiyo. Pia barua hiyo ilieleza kisheria maneno hayo, ambayo yalitolewa na mkuu huyo wa mkoa ni kosa na ni kashfa dhidi ya mteja wao, na yamemdhalilisha, kumnyanyasa, kumvunjia heshima aliyokuwa nayo mbele ya wanakijiji waliomchagua na kumpa dhamana.

“Maagizo kutoka kwa mteja wetu ni kukutaka wewe Parseko Kone, utembelee tena Kijiji cha Kisasida na kuitisha mkutano wa hadhara wa wanakijiji wote na uwaombe radhi hadharani kwa maneno ambayo sisi tutakuelekeza.

“Aidha, tunakuagiza ufanye ziara ya mkutano huo wa kuomba radhi ndani ya siku 14, kutokea leo (jana), pia mteja wetu anadai umlipe sh milioni moja kama gharama za ufuatiliaji kwetu,” ilieleza barua hiyo.

Lissu, alidai kuwa mkuu huyo wa mkoa, endapo atashindwa kufanya hivyo, au kupuuza kutekeleza matakwa yao watamfungulia kesi ya madai katika mahakama watakayoichagua wao. Aliongeza pia kama Kone atashindwa kutekeleza madai yao, hawatasita kumdai fidia zaidi ya fedha na nafuu nyinginezo za kisheria dhidi yao.

Mwishoni mwa wiki iliyopita Kone alizungumza na Tanzania Daima, alikanusha tuhuma hizo zinazomkabili na kudai kuwa alikwenda katika kijiji hicho kukagua mradi wa umwagiliaji na hakumtukana kiongozi yeyote.

MLOLONGO WA KULALAMIKA,KUTOA VITISHO AU HATA KULIA HAUWEZI KUKOMESHA UFISADI AU KUWAKUMBUSHA WAJIBU BAADHI YA VIONGOZI WANAOJIONA MIUNGU WATU.DR SLAA NA CHADEMA WAMEKUWA WAKITUAMINISHA KWAMBA CCM INAHUSIKA MOJA KWA MOJA KATIKA KUFANIKISHA UJAMBAZI WA EPA.JAPO NAFAHAMU KUWA HUKUMU YA UMMA INA MADHARA ZAIDI YA HUKUMU YA MAHAKAMA ZA KISHERIA,SOTE TUNAJUA NAMNA HUKUMU YA UMMA INAVYOWEZA KUPINDISHWA NA ZAWADI ZA KHANGA,FLANI,KILO YA SUKARI,NK KAMA VIVUTIO WAKATI WA UCHAGUZI.

NGOJA NIFAFANUE KAMA HUJANIELEWA VIZURI.YAYUMKINIKA KUAMINI KUWA CHADEMA INAPOITUHUMU CCM KWENYE MIKUTANO YA HADHARA KWAMBA CHAMA HICHO TAWALA KINA MAHUSIANO NA UFISADI/MAFISADI INATARAJIWA KUWA WANANCHI WATATOA HUKUMU DHIDI YA CCM (HUKUMU YA UMMA) WAKATI WA UCHAGUZI.HILO LINAWEZEKANA KATIKA MFUMO HURU WA DEMOKRASIA,NA MIFANO HAI NI NAMNA HUKUMU YA UMMA ILIVYOFANYA KAZI KATIKA CHAGUZI HUKO HISPANIA MWAKA 2004 NA MAREKANI MWAKA JANA.KATIKA CHAGUZI ZINAZOFANYIKA KATIKA MAZINGIRA YA DEMOKRASIA HURU,HASIRA ZA WAPIGA KURA (AU KURIDHISHWA KWAO) NI MIONGONI MWA MAMBO MUHIMU KATIKA KU-DETERMINE MATOKEO YA UCHAUZI HUSIKA.

SASA SOTE TUNAJUA MAZINGIRA YA CHAGUZI NYINGI ZA "DUNIA YA TATU".KANUNI ISIYO RASMI KUHUSU CHAGUZI ZETU INADAI KWAMBA CHAMA TAWALA HAKIWEZI KUSHINDWA UCHAGUZI.KIKISHINDWA BASI AIDHA KILIZEMBEA KUTUMIA MBINU ZAKE ZA AWALI ZA KUBAKI MADARAKANI AU KILIPIGIWA KURA ZA CHUKI NA WAFUASI WAKE AU KULITOKEA MPASUKO NDANI YA CHAMA TAWALA AMBAO ULIZAA MAKUNDI MAWILI YENYE TAKRIBAN NGUVU SAWA,KILA MOJA LIKIFAHAMU MBINU SAFI NA CHFU ZA KUSHINDA CHAGUZI,NK.WAPO WANAOAMINI KUWA HATA KANU YA MOI HAKIKUSHINDWA UCHAGUZI WA 2002 KWA VILE WAPIGA KURA WALIKUWA WAMEICHOKA (WHICH WAS TRUE i.e. kweli walikuwa wameichoka) BALI NI UTEUZI MBOVU WA MGOMBEA UHURU KENYATA.

VINGI VYA VYAMA TAWALA KATIKA NCHI ZA TATU HUSHIKILIA DOLA KWA MAANA HALISI YA KUSHIKILIA,YAANI WANAITUMIA IPASAVYO KUHAKIKISHA UTAWALA UNAENDELEA MILELE.HAKUNA DHAMBI KWA CHAMA KUWA MADARAKANI MUDA MREFU AS LONG AS KINAWAHUDUMIA WANANCHI IPASAVYO.KWA BAHATI MBAYA,U-KING'ANG'ANIZI WA BAADHI YA VYAMA TAWALA KATIKA NCHI ZA DUNIA YA TATU HAUTOKANI NA MAPENZI YAO KWA NCHI AU WANANCHI BALI HOFU YA KUADHIBIWA KWA MADHAMBI YALIYOWAFANYWA WAKATI VYAMA HIVYO VIKIWA MADARAKANI.KADRI MADHAMBI YANAVYOZIDI KUONGEZEKA NDIVYO KADRI VYAMA HIVYO VINAVYOZIDIWA NA HOFU YA NINI KITATOKEA PINDI VIKITOLEWA MADARAKANI,NA MATOKEO YAKE NI KUTUMIA KILA NJIA KUHAKIKISHA VINATAWALA MILELE.NA KWA VINASHIKILIA DOLA,HILO LINAKUWA SIO JAMBO GUMU.

KWAHIYO,KAMA DR SLAA,CHADEMA NA WENGINEO WANADHANI KELELE KUWA CCM INAHUSIKA KATIKA WIZI WA EPA ZITAFANIKISHA KUPATIKANA KWA HUKUMU YA UMMA KATIKA UCHAGUZI WA 2010 AU BAADAYE,THEY REALLY NEED TO THINK AGAIN.KUFANYA HIVYO NI SAWA NA KUTARAJI KUWA HUYO RC ANAYETUHUMIWA KUWATUKANA WANANCHI ANGEAMUA YEYE MWENYEWE KWA HIARI YAKE KUOMBA RADHI BADALA YA KULAZIMISHWA KUFANYA HIVYO (KAMA ANAVYOTAKIWA NA WAKILI LISSU).NAMNA PEKEE YA CHADEMA,ET AL WANAWEZA KUFANIKIWA KATIKA TUHUMA ZAO DHIDI YA CCM NI KWENDA MAHAKAMANI WAKIWA NA USHAHIDI WANAODAI KUWA NAO.

KUITAKA CCM IENDE MAHAKAMANI (INAPOTUHUMIWA KUWA NA UHUSIANO NA MAFISADI) NI SAWA NA KUMTAKA MTU UNAYEMTUHUMU KUTEMBEA NA MKEO/MUMEO (KUTEGEMEA JINSI YAKO MSOMAJI) AENDE POLISI/MAHAKAMANI.....KWA KIFUPI,ATAENDELEA KUKUIBIA NA HATOTIA MGUU POLISI/MAHAKAMANI.COMMON SENSE INATUELEZA KUWA MWENYE TUHUMA NDIO ANAYEPASWA KUWA NA UHARAKA WA KUZIDHIBITISHA AU KUWA NA DHAMIRA YA KUZITOKOMEZA KABISA.MTUHUMIWA ANAWEZA KUWA NA UHARAKA HUO IWAPO ANAONA ZINAMCHAFULIA JINA.LAKINI WHAT IF TUHUMA DHIDI YA MTUHUMIWA NI ZA KWELI?BADO TUTATEGEMEA MTUHUMIWA AJIEPELEKE KWENYE HUKUMU YAKE?

NAHISI CHADEMA WANACHELEA KWENDA MAHAKAMANI SIO KWA VILE WANAHOFIA KUTOPATA HAKI BALI WANAZITUMIA TUHUMA HIZO KUWA MTAJI WA KISIASA.NA-HYPOTHESIZE KUWA CHAMA HICHO KITAZITUMIA TUHUMA HIZO KWENYE KAMPENI ZAKE ZA UCHAGUZI MKUU WA 2010 KIKIAMINI KUWA ZITAKISAIDIA KUPATA USHINDI KWA HUKUMU YA UMMA DHIDI YA CCM.JAPO LOLOTE LINAWEZEKANA KATIKA SIASA,NA MBINU HIYO YA CHADEMA INAWEZA KUFANIKIWA,WAZOEFU WA SIASA WANAWEZA KUAFIKIANA NAMI KWENYE HYPOTHESIS YANGU YA PILI KUWA MKAKATI HUO HAUTOFANIKIWA.KINACHONIPELEKA KUAMINI HIVYO NI UZOEFU KUHUSU NAMNA CCM INAVYOELEWA UDHAIFU WA MPIGA KURA WA KITANZANIA,FAIDA ZA KILOJISTIKI ZINAZOELEMEA UPANDE WA CHAMA TAWALA,MILKI NA SAPOTI YA DOLA BILA KUSAHAU "MBINU CHAFU."

UCHAGUZI MKUU WA 2010 UNAWEZA KABISA KUPITA NA CCM KUIBUKA KIDEDEA HUKU CHADEMA IKIWA "IMEDODEWA" NA USHAHIDI WAKE DHIDI YA CCM.HILO SIO BAO LA KISIGINO BALI NI MITHILI YA KIBAKA KUKUPORA KISHA ANAKUPIGIA KELELE KUWA WEWE NDIO MWIZI....(AND WE ALL VERY WELL KNOW MOB JUSTICE HUKO NYUMBANI ZILIVYO...WATU WAKISKIA UKELELE WA MWIZI,MWIZI HAWAULIZI ILIKUWAJE.NI KIPIGO TU....PASIPO KUJUA KUWA WANAYEMPIGA NDIO ALOPORWA NA KIBAKA).

15 Sept 2008

Some political analysts argue that ruling parties in Africa never lose elections,and if they do,which is rarely,it is likely not because they failed to deliver to the people who put the parties in power but rather either due to their internal conflicts or laxity.One could easily blame majority of opposition parties in Africa for their failures in organizing themselves in quest to remove ruling parties from power.But the fact is,in most African countries,the idea of an opposition party coming into power spells inexplicable uncertainty to the rulers,largely due to their "sins" during their terms of leadership.

In Tanzania,opposition parties have consistently cried foul during elections accusing the ruling party,CCM,of sabotaging them by either inciting conflicts in the parties or "bribing" their leaders to defect.CCM has also been accused of reluctance to reform the electoral system,which the opposition parties,see as unfair and biased.

I strongly believe that our nation's interest should come first,mainly because political parties may come and go but the nation should always remain intact,peacefully and flourishing.Had every Tanzanian looked beyond partisan politics,it is fair to conclude that those who criticize the ruling party for its perceived failure to deals with mafisadi (economic saboteurs),for instance,would not be considered as giving ammunitions to opposition parties but instead they would be given enormous support.

A while ago,I came across this story which in my view would stir trouble in Tanzania's opposition politics.
Mtikila atamka mazito kifo cha Wangwe

Na Waandishi Wetu 

WAKATI mazingira ya kifo cha aliyekuwa Mbunge wa Tarime marehemu Chacha Wangwe yakiendelea kuwa tete, Mwenyekiti wa Democratic Party (DP) Mchungaji Christopher Mtikila, ameibuka na kile alichodai, taarifa za mpango kamili hadi mauaji ya mwanasiasa huyo. 

Akizungumza na waandishi wa habari Dar es Salaam jana, Mchungaji Mtikila alidai mipango ya kumuua marehemu Wangwe ilianza kusukwa mkoani Dodoma na baadaye vikao vya kukamilisha mkakati huo, vilifanyika jijini Dar es Salaam wilayani Kinondoni. 

Aliongeza kuwa wahusika baada ya kukamilisha mpango huo na jinsi utakavyotekelezwa, walikwenda nchini Kenya kukodi watu wawili ambao alidai walilipwa sh. milioni 120 kama ujira wa 'kazi' hiyo. 

Mchungaji Mtikila alidai kuwa wauaji hao, ndio walioshirikiana na Bw.Deus Mallya ambaye anadaiwa wakati huo alikuwa amejenga uhusiano mzuri na marehemu Wangwe. 

Alidai siku ya tukio, marehemu Wangwe hakutaka kusafiri lakini alishinikizwa zaidi ya mara tatu na Bw. Mallya ambaye hadi sasa anashitakiwa kwa kosa la kusababisha ajali na kuendesha gari bila leseni.

"Baada ya kushinikizwa sana, marehemu Wangwe alikubali kuanza safari ambapo Bw. Mallya aliwasiliana na washirika wake ambao muda huo walikuwa eneo la tukio wakiwasubiri," alidai Mchungaji Mtikila na kuongeza kuwa; 

"Wakati huo ilikuwa bado mapema hivyo walimshauri apoteze muda japo wa nusu saa, ndipo alipozusha hitilafu ndani ya gari na kurudi gereji na baada ya muda huo kupita ndipo walianza safari kuelekea jijini Dar es Salaam." 

Huku akidai kuwa ana ushahidi wa tukio hilo na yupo tayari kutoa ushirikiano kwa Rais Jakaya Kikwete, Mchungaji Mtikila alizidi kueleza kuwa Bw. Mallya aliendelea kuwasiliana na washirika wake hadi walipofika eneo Pandambili, wilayani Kongwa na kusimamisha gari. 

"Baada ya kusimamisha gari, washirika wa Mallya walipanda na kumpulizia dawa ya usingizi usoni mara nne na hapo hapo alipoteza fahamu," alieleza Mchungaji Mtikila na kuongeza kuwa baada ya hapo ndipo alipigwa kwa kitu cha ncha kali kisogoni. 

"Kwa kuwa Mungu alimpenda sana hakukata roho, aliendelea kuhema ndipo alipopigwa na nyundo na kummalizia kabisa," alidai. Aliongeza kuwa baada ya kutimiza hilo waliweka jiwe kwenye kiongeza mwendo gari likaondoka kwa kasi na lilipindua ili kuonesha kuwa marehemu alikufa kwa ajali lakini muda huo Mallya alikuwa hayuko kwenye gari," 

Alidai kuwa kabla ya kupindua gari hilo, walimfunga marehemu mkanda na kumwibia sh. milioni tisa alizokuwa nazo pamoja na kompyuta yake ndogo 'Lap top' ambayo ilikuwa na nyaraka zake za siri. 

Alidai kuwa baada ya kufanikisha mauaji hayo, Bw. Mallya alitoa 'line' yake ya simu ambayo alikuwa akiitumia kuwasiliana na washirika wake na kuitupa. Alidai kuwa hadi anakamatwa simu yake haikuwa na 'line' yoyote. 

Kwa mujibu wa Mchungaji Mtikila mauaji hayo yalifanyika kati ya 1.30 hadi saa 2.00 usiku, muda mfupi baada ya kumaliza kuwasiliana na familia yake saa 1.27. 

Huku akijata majina ya watu wanaodaiwa kuhusika kwenye mpango huo, alieleza kuwa kipindi cha mchakato wa mpango wa kumuua, Bw. Wangwe, walikuwa wakisafiri kwenda nchini Kenya kusuka mpango huo. 

Mchungaji Mtikila alielekeza lawama zake kwa askari wote waliohusika na uchunguzi wa mauaji hayo kwa akidai kuwa hawakusema ukweli hivyo nao wanastahili kuunganishwa kwenye kesi hiyo. 

Kutokana na mazingira ya kifo cha marehemu Wangwe kugubikwa na maswali mengi, Mchungaji Mtikila amemuomba Rais Kikwete kuunda tume ya kuchunguza mazingira ya kifo chake kama alivyofanya kwa wafanyabiashara wa madini wa Mahenge, Morogoro ambao wanadaiwa kuuawa na Polisi. 

Alidai kwa wadhifa aliokuwa nao marehemu Wangwe katika jamii akiwa Mbunge wa Tarime, Rais ana nafasi ya kuunda tume. "Naupongeza uamuzi wake wa kuunda tume ya kuchunguza vifo vya wafanyabiashara lakini na kwa hili aunde tume na mimi nitakuwa tayari kutoa ushirikiano,"alisisitiza. 

Aliongeza kuwa kama Rais hatafanya hivyo, yeye ataleta wataalam wake kutoka nje kufanya uchunguzi kwani ameishafanya mazungumzo na ubalozi wa nchi moja ambao hakuutaja. 

Mchungaji Mtikila alidai kuwa atakwenda jimboni Tarime wakati huu wa kampeni ili kuwaeleza wananchi ukweli kuhusu kifo cha marehemu Wangwe. Alisema amesimamisha mgombea kupitia chama chake, Bw. Benson Makanya, ili apate jukwaa la kueleza ukweli kuhusiana na kifo hicho. 

Marehemu Wangwe alikufa kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Pandambili mkoani Dodoma Julai 28 mwaka huu lakini tangu kifo chake, yameibuka maswali mengi huku baadhi ya watu wakidai kuwa aliuawa. 

Hata hivyo uchunguzi uliofanywa na madaktari wawili kwa nyakati tofauti ulionesha kuwa hakupigwa risasi bali kifo chake kilisababishwa na ajali ya gari.

According to one local paper,the suspects are Freeman Mbowe,Dr Wilbroad Slaa and Tindu Lissu.This is how I look at the picture:If the accused trio decide to ignore Mtikila,it goes without saying that the public would buy the story,and it could bring their political careers to an abrupt end.Going to the court might be the only option left on their table,but Mtikila has a long history of winning charges brought against him in various courts.It should be all smiles in the ruling party's quarters as a Swahili saying goes "adui yako mwombee mabaya" (wish evil things to your enemy)

6 Feb 2008

Makala yangu ndani ya toleo la wiki hii la gazeti la Raia Mwema iliandaliwa kabla ya "kimuhemuhe" kilichoanza leo huko Bungeni.Kwa kifupi,makala hiyo inaelezea namna siasa inavyoboa (au ni wanasiasa ndio wanaoboa?) na kutoa mfano wa namna baadhi ya wahafidhina katika chama cha Republicans "wanavyotiana vidole kwenye macho" kufuatia mwenendo mzuri wa harakati za Seneta John McCain kuingia White House kwa tiketi ya chama hicho.

Pia makala hiyo inagusia vimbwanga vya siasa za huko nyumbani kwa kuonyesha mshangao wa namna Spika Samuel Sitta "alivyoruka kimanga" kwamba aliwahi kuweka vikwazo dhidi ya harakati za Dr Slaa kufichua ufisadi wa BoT.Pia makala inazungumzia "utoto" wa CCM (licha ya kuwa majuzi ilitimiza miaka 31) pale inapodai kuwa yenyewe ndiyo iliyoibua hoja ya ufisadi.Hivi Chama hicho kimeishiwa busara namna hiyo hadi kusahau kwamba sababu ya mawaziri wake kuzomewa mikoani ilikuwa ni reactions za wananchi dhidi ya jitihada za vigogo hao kuua hoja za wapinzani kuhusu ufisadi!!!?
Lakini kali zaidi ni pale Spika wa Bunge alipotoa maelekezo kwa Naibu wake kwamba "asikurupuke" kuendesha mijadala ya Richmond na BoT/EPA hadi yeye (Spika) ataporejea kutoka ziarani Marekani.Angalau sasa tunaelewa kwanini Spika alitaka kutumia mbinu za kupoteza muda katika mjadala wa Richmond,kwani RIPOTI YA KAMATI TEULE YA BUNGE KUHUSU MKATABA KATI YA SERIKALI NA KAMPUNI HIYO (BONYEZA HAPA KUISOMA)imemu-implicate Spika kwa namna flani (kwa vile Kituo cha Uwekezaji-IPC-kikiwa chini ya uongozi wa Sitta,kiliiruhusu Richmond iwekeze pasipo kuchunguza uwezo halisi au uwepo wa kampuni hiyo).

Pamoja na makala nyingine zilizokwenda shule ndani ya gazeti hilo,bingirika na makala yangu hiyo kwa KUBONYEZA HAPA.


20 Jan 2008

Makala hii ilitoka kwenye gazeti la Mtanzania siku ya Alhamisi 17Jan 2008.

Hatimaye ugavana wa Dkt Daudi Ballali katika Benki Kuu ya Tanzania umetenguliwa.Sijui kama utenguzi huo ni sawa na tunachosoma,kuona na kusikia kwenye vyombo mbalimbali vya habari kwamba Balali amefukuzwa kazi.Pengine la muhimu kwa sasa ni kwamba mtu huyo ametolewa katika wadhifa huo japo la muhimu zaidi ni kuweka rekodi vizuri kwa minajili ya kuondoa utata uliojitokeza hasa katika neno “KUTENGUA”.

Kuna wanaosema kwamba Ballali ametolewa kafara hasa kwa kuzingatia ukweli kwamba sio rahisi wizi mkubwa namna hiyo uwe umefanywa na mtu mmoja tu.Ni vigumu pia kuamini kwamba uamuzi wa gavana huyo wa zamani kuyazawadia makampuni yaliyotajwa kwenye ufujaji wa fedha hizo ulifanywa na mtu mmoja pekee (Balalli).

Sakata hili lilisabaisha,linasababisha na litaendela kusababisha maswali mengi zaidi kuliko majibu.Sijui kuna wazalendo wangapi hapo Benki Kuu, lakini nashawishika kuhoji uzalendo wao kwani japo si kila mtumishi angeweza kufahamu alichokuwa akifanya Balali na washirika wake,ni dhahiri wapo waliokuwa katika nafasi ya kutoa taarifa kwa vyombo husika lakini wakaamua kukaa kimya.

Nadhani kuna waliojua kinachoendela lakini wakaa kimya kwa vile nao walikuwa washiriki katika ufisadi huo.Hawa hawana cha kujitetea kwani hawana tofauti na Balalli na wanachostahili ni adhabu tu.Kikwazo kikubwa kinachojitokeza katika uwezekano wa kuwaadhibu waungwana hawa ni ukweli kuwa baadhi yao wamepewa nafasi ya kujichunguza wenyewe (kwa vile bado wako madarakani) na sote tunaelewa kwamba hawawezi kujihukumu.Sanasana wataishia kuharibu ushahidi muhimu katika uchunguzi mzima wa ufisadi huo.

Kundi la pili ni wale waliokuwa wakifahamu kinachoendelea lakini hawakuchukua hatua kwa sababu mbalimbali ikiwa ni pamoja na kauli za utetezi zilizokuwa zikitolewa na watu mbalimbali pindi tuhuma za ufisadi huo zilipoanza kuibuka.Tunakumbuka kwamba kuna wakati huko bungeni lilitolewa tishio la kumfikisha Dr Slaa mbele ya vyombo vya sheria akituhumiwa kwamba ameghushi nyaraka zinazohusiana na sakata hilo.Yayumkinika kusema kwamba kauli kama hizo zinaweza kuwa ziliwakwaza baadhi ya watumishi wa Benki Kuu (waliokuwa na ufahamu wa ufisadi huo) kuripoti kuhusu uhuni uliokuwa ukiendelea hapo.
Imeripotiwa pia kwamba moja ya makampuni ya ukaguzi wa mahesabu ya benki hiyo iliripoti kuhusu kasoro zilizokuwepo lakini ikaishia kuona mkataba wake na benki hiyo ukisitishwa.Ni rahisi kukubaliana na “busara” hii kwamba kama kampuni iliyolipwa kuchunguza mahesabu imepuuzwa je “nani atanisikiliza mie niliyeajiriwa kufanya majukumu mengine katika Benki Kuu”.

Miongoni mwa madhara ya kulea ubadhirifu ni kujengeka kwa imani (miongoni mwa wasiojihusisha na ubadhirifu huo) kwamba ubadhirifu sio dhambi kwani ingekuwa haukubaliki basi wahusika wasingeendelea nao pasipo kuchukuliwa hatua.Yeyote aliyehusika na skandali hiyo lakini bado yuko madarakani ni sawa na kansa ambayo isipodhibitiwa inasambaa katika mwili mzima.Ni kama katika familia yenye watoto kadhaa na baadhi yao wanajihusisha na tabia zisizofaa.Ni dhahiri wale wanaoepuka tabia hizo (ilhali wenzao wanaendelea nazo) wanaweza kushawishika kuiga tabia hizo hususan kama wanaona wenzao wananufaika kwa namna flani.

Nakumbuka hivi karibuni,mkongwe wa siasa Mzee Kingunge Ngombale Mwiru alinukuliwa na gazeti moja akieleza masikitiko yake kuhusu namna uzalendo unavyopungua miongoni mwa Watanzania.Ni kweli uzalendo umepungua sana na tusipokuwa makini utapotea kabisa lakini kuwa na wasiwasi au kulalamika pekee hakuwezi kusaidia kurekebisha mambo.Ni dhahiri kwamba moja ya mambo yanayochangia kupungua uzalendo ni pamoja na ufisadi kama huo uliofanyika hapo Benki Kuu.

Hivi mtu atakuwaje mzalendo iwapo wakati yeye anahangaika kutafuta fedha za kumwezesha kupata angalau mlo mmoja wa siku kuna wajanja wanatumbukiziwa mamilioni ya shilingi kwenye makampuni yao pasipo kuvuja tone moja la jasho.Kibaya zaidi na pengine katika kuwaringia walipa kodi wanaoibiwa,mafisadi hawaogopi kuonyesha namna wizi wao “unavyolipa” kwa kuporomosha mahekalu ya gharama kubwa,magari ya thamani ya kutisha na vimbwanga vingine chungu mbovu.Ni kama mtu anakupora mke halafu kesho yake unamwona anatamba nae mtaani.Hii inaongeza chuki na hasira kwa aliyeibiwa.

Kila zinapojitokeza tuhuma za ufisadi huwa nashindwa kujizuia kuhoji uwezo wa TAKUKURU katika jukumu lake la kuzuia na kupambana na rushwa.Taasisi hii imekuwepo kwa muda mrefu sasa lakini bado ni legelege licha ya jitihada kadhaa zilizokwishafanywa iwe na ufanisi zaidi.Naafikiana na baadhi ya hoja kwamba matendo mengi ya ulaji fedha za umma hayafanyiki hadharani,hivyo kusababisha ugumu katika kuyabaini.Hata hivyo,katika sakata hili la ufisadi hapo BoT,tetesi zilikuwepo mtaani na magazetini kwa muda mrefu.Kama ilivyozeleka,kauli za TAKUKURU zilikuwa “taarifa hizo tunazo na tunazifanyia uchunguzi”.Ikumbukwe kwamba katika mazingira ambayo matatizo yanazaliana kila kukicha,kuchelewa kutatua tatizo moja ni sawa na kutengeneza mlima wa matatizo hayo ambapo mwisho wake itakuwa ni suala lisilowezekana kabisa kuyaondoa.

Pengine umefika wakati mwafaka kwa wawakilishi wetu huko bungeni kuhoji uhalali wa kuendelea kuwa na taasisi hiyo ya kuzuia na kupambana na rushwa.Kanuni ya haki katika sheria inatamka waziwazi kwamba haki sio tu itendeke bali pia ionekane imetendeka.Tunaweza kuitumia kanuni hiyo kwa TAKUKURU pia kwamba mapambano dhidi ya rushwa yasiishie tu kuwa ya dhamira bali yaonekane hadharani kuwa yapo na yana ufanisi unaotarajiwa.

Naweza kuonekana mtu wa ajabu iwapo nitashauri kuvunjwa kwa TAKUKURU lakini nina hoja ya msingi napofikiri hivyo.Mamilioni ya fedha yanayoelekezwa kwa taasisi hiyo kupambana na rushwa hayajasaidia lolote katika kupunguza tatizo hilo.Mabadiliko mbalimbali ya kisheria yaliyolenga kuipa meno taasisi hiyo nayo yameshindwa kuifanya iwajibike ipasavyo.Binafsi sioni cha ziada kinachoweza kubadili ulegelege wa taasisi hiyo zaidi ya kuivunjilia mbali na kasha majukumu yake kuhamishiwa kwenye taasisi nyingine kama vile kitengo cha upelelezi katika jeshi la polisi (CID).

Kwa kuzingatia rekodi ya TAKUKURU katika uendeshaji wa kesi inazopeleka mahakamani,sintoshangaa iwapo wanaotajwa kwenye sakata hilo wataishia kuibuka washindi kwenye kesi hizo.Tumeshuhudia namna taasisi hiyo ilivyokuwa “ikipelekeshwa” kwenye kesi dhidi ya Balozi wa zamani wa Tanzania nchini Italia.Kama kesi ya mtu mmoja imekuwa ngoma nzito namna hiyo,tutarajie nini kwenye lundo la kesi linalowahusu watu wenye uwezo mkubwa wa kifedha?

Wengi wanatafsiri vurugu zinazoendelea nchini Kenya kuwa ni matokeo ya ukabila.Lakini baadhi ya wachambuzi wa uchumi wananyumbulisha kwamba vurugu hizo ni sehemu tu ya mapambano ya kiuchumi kati ya wenye nacho na wasio nacho.Migongano ya kidini au kikabila hujichomoza zaidi kwenye jamii isiyo na uwiano wa kimapato kwani mara nyingi washiriki kwenye vurugu hizo huamini kwamba pindi zikifanikiwa zitarekebisha maisha yao ya kila siku.Tuna kila sababu ya kuzuia nchi yetu inayosifika kwa amani na utulivu isiingie kwenye machafuko yanayoweza kusababishwa na wengi wanaoona wachache wakinufaika kwa “ulafi wa kula keki ya taifa” huku wao (wengi hao) wakiendelea kutaabika.Kinachowezekana leo kisingoje kesho.

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.