5 Mar 2009

SAKATA la ununuzi wa mitambo ya ufuaji umeme wa dharura ya kampuni ya Dowans Tanzania Limited, jana lilimgusa spika wa bunge la Jamhuri ya Muungano, Samuel Sitta na kuamua kutoa tamko kali la kuitahadharisha serikali dhidi ya azma yake ya kutaka kuinunua mitambo hiyo yenye utata.

Spika Sitta pia ameonya kuwa mkasa wa kampuni tata ya Richmond Development (RDC) LLC uliotikisa kiasi cha kusababisha Edward Lowassa awajibike kwa kujizulu wadhifa wake wa waziri mkuu, lisifufuliwe upya kwa kutumia Dowans, ambayo ilirithishwa mkataba wa miaka miwili wa kufua umeme wa dharura.


Richmond ilishinda zabuni ya kufua umeme wa dharura kwa njia iliyojaa utata kabla ya matatizo ya usajili wake kuzua maswali mengi na kusababisha Dowans warithishwe mkataba huo mwaka 2006.

Katika mkutano wake na waandishi wa habari, Sitta alieleza nafasi ya Bunge katika kuisimamia na kuishauri serikali katika utekelezaji wa majukumu yake, huku akitaka ushauri wa Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini wa kuizuia serikali isinunue mitambo hiyo uheshimiwe.

Sitta pia alisema Kamati ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma haikustahili kufuatwa katika kutaka ushauri kuhusu suala hilo kwa kuwa suala hilo lipo kwenye Kamati ya Nishati na Madini na kwamba kama kuna sababu mbadala, wasi ililazimika kuliwasilisha upya kwa kamati hiyo.

"Naitahadharisha serikali juu ya athari zinazoweza kujitokeza iwapo itaamua kuendelea na mchakato wa ununuzi wa mitambo ya Dowans kwa kupuuza ushauri uliotolewa na Kamati ya Nishati na Madini," alisema Spika Sitta.

Alisema: "Isisahaulike kwamba Dowans ni kampuni iliyopatikana kwa kurithishwa mradi na kampuni ya Richmond katika mazingira yenye utata ambao hadi leo ni kitendawili."

Spika Sitta alifafanua kuwa uhalali wa utaratibu wa Richmond kumkabidhi mradi Dowans ulitiliwa mashaka na kamati teule ya Bunge, na kuongeza kuwa Dowans na Richmond ni kama kitu kimoja.

"Dowans na Richmond ni mtu na binamu yake na si vigumu kukubali kuwa bado wao ni wabia hadi sasa: Pamoja na yote mkasa wa Richmond haufai kufufuliwaaa upya kupitia Dowans," alisisitiza Sitta.

Aliongeza kuwa kama kweli Tanesco na serikali inazo Dola 69 milioni za Kimarekani (sawa na Sh90 bilioni za Kitanzania) ambazo ni bei ya mtambo wa Dowans, ingezitumia fedha hizo kama sehemu ya malipo ya kununua mitambo mipya. Alisema Tanesco ingetafuta ushauri kutoka Mamlaka ya Ununuzi Serikalini (PPRA) ili taratibu za dharula zitumike kununua mitambo mipya kukabiliana na "dharula inayotabiriwa".

Sitta alihoji mantiki itakayotumiwa na Tanesco kutaka kununua mitambo ambayo inamilikiwa na kampuni ambayo imeishtaki kwenye Baraza la Usuluhishi ambalo makao yake makuu yako Paris, Ufaransa.

"Gharama za mitambo na gharama za kuikodi haviwezi kuepukwa kuwa ni sehemu ya shauri lililo Paris," anasema Sitta. "NI kwa mantiki ipi kesi baina yao iendelee na hapo hapo mdaiwa (Tanesco) anunue mitambo kutoka kwa mdai (Dowans.

"Tanzania ilikuwa ikilipa Dowans shilingi za Kitanzania milioni 152 kwa siku (Dola 120,000) sawa na Dola 42 milioni kwa mwaka).

"Pamoja na yote, mkasa wa Richmond haufai kufufuliwa upya kupitia Dowans. Tanesco/serikali waelekeze nguvu zao katika njia mbadala za kulipatia taifa umeme wa dharura, badala ya njia hii ya Dowans iliyojaa utata."

Kuhusu mvutano kati ya Kamati ya Kudumu ya Hesabu za Mashirika ya Umma na ile ya Nishati na Madini, Spika Sitta amsema si sahihi kwa kamati yoyote ya Bunge isiyo ya sekta husika, kutoa maoni yake hadharani na kuishawishi jamii kwamba Bunge lina ushauri unaopingana kuhusu suala husika.

"Si sahihi kwa Kamati yoyote ya Bunge isiyo ya sekta kutoa maoni yake hadharani na kujenga taswira kwa umma kwamba, Bunge lina ushauri unaokinzana kuhusu suala lililo mbele yake. Kamati nyingine, haina budi kupitisha ushauri na maoni yake kwenye kamati ya kisekta," alisema Sitta.

Zitto Kabwe, ambaye ni mwenyekiti wa Kamati ya Hesabu za Mashirika ya Umma, alikaririwa na vyombo vya habari akieleza msimamo wa kamati yake kuunga mkono Shirika la Umeme (Tanesco), kuinunua mitambo ya Dowans kwa maelezo kuwa hatua itasaidia kulinusuru taifa katika janga kubwa la kukosa umeme na kwamba sheria ya manunuzi si msahafu, hivyo inaweza kubadilishwa.

Lakini Kamati ya Nishati na Madini, ambayo mwenyekiti wake ni William Shelukindo, inapinga hatua hiyo ikieleza kuw ainakiuka Sheria ya Manunuzi ya Umma, inayokataza serikali kununua vitu ambavyo tayari vimetumika.

Alisema ushauri kwa serikali kuhusu Tanesco kununua au kutonunua mitambo ya Dowans ulikwishatolewa kwa Wizara ya Nishati na Madini na Kamati ya Bunge ya Nishati na Madini Desemba 14 mwaka uliopita.

"Huo ndiyo ushauri rasmi na sahihi wa Bunge ninaoutambua. Kwa msingi huo hoja ya kuzikutanisha Kamati hizi mbili (ya Nishati na Madini na ya Hesabu za Mashirika ya Umma) ili kurejea uamuzi au maoni yaliyokwishatolewa na Kamati inayohusika, haina msingi," alisema Sitta.

Alisema mkondo rasmi wa ushauri kwa serikali uliokusudiwa kwenye Ibara ya 63 (2) ya katiba ikisomwa na pamoja na kanuni za Bunge za mwaka 2007 ni kupiti Bunge zima au kamati zake za kisekta kila kamati na sekta yake.

Wakati Spika Sitta akibainisha msimamo wake na wa Bunge, mwenyekiti wa CUF, Prof. Ibrahim Lipumba ameunga mkono ununuzi wa mitambo hiyo huku akisema kauli ya Rais Jakaya Kikwete aliyoitoa jana inaweza kukwamisha mchakato wa ununuzi wa mitambo hiyo.

Lipumba alisema katika mfumo wa utawala bora wakati kamati za bunge zinazohusika na mambo hayo na bodi za mashirika zipo, rais hapaswi kujiingiza mapema katika mijadala.

“Katika mfumo wa utawala bora ambao una kamati za bunge zinazohusika na sekta ya umeme na manunuzi, kwa rais kujiingiza kunaweza kuwa ni kikwazo cha mchakato mzima wa ununuzi wa mitambo,” alisema Profesa Lipumba.

Alifafanua kuwa, sheria ya manunuzi ya Serikali ina upungufu kwa kuwa inalazimisha ununuzi wa mitambo mipya, jambo ambalo haliwezekani kwa nchi zinazoendelea kama Tanzania.

“Ununuzi wa mitambo ya kibiashara katika sekta ya biashara huwezi kulazimisha ununuzi wa mitambo mipya hususan katika nchi zinazoendelea kama ya kwetu. Jambo la msingi ni kuangalia uwezo wa mitambo katika kufanya kazi na si kwamba ni mipya au mikongwe,” alifafanua Lipumba na kuongeza:

“Sheria yetu ya manunuzi ni nzuri na inafaa sana kwa kununua vitu vya huduma za serikali, kama magari na vifaa vingine.”

Aliitaka Tanesco kuwa wazi kwa kuwa ni wao waliosema mitambo hiyo hawaitaki hivyo kuamuwa kuvunja mkataba na Dowans iweje leo wanageuka na kusema mitambo hiyo ni mizuri na kuitaka serikali iinunuwe.

“Tanesco walituambia kuwa mitambo hiyo hawaitaki na walivunja mkataba na Dowans, sasa inakuaje leo wanageuka na kusema kwamba mitambo hiyo ni mizuri na inunuliwe kwa ajili ya kuzalishia umeme? Tunahitaji uwazi zaidi kutoka Tanesco,” alihoji Profesa Lipumba.

Naye Stephen Menad ambaye ni mshauri wa masuala ya nishati na mazingira, alisema hakuna kitu kipya kwenye mitambo hiyo ya Dowans hivyo isinunuliwe na badala yake itafutwe mipya ili kuondoa mvutano baina ya wananchi na serikali.

Mussa Hassan, mkazi wa jijini Dar es Salaam ambaye ni mfanyabiashara, alisema ni aibu kwa serikali kula matapishi na kwamba viongozi wasisahau yaliyotokea wakati mitambo ya Richmond ilipokuja na mwisho wake kuwaweka pabaya viongozi waliokuwa serikalini.

Anthony Chambi, ambaye ni mfanyabiashara katikati ya jiji la Dar es Salaam, alisema hataki kusikia kuhusu mitambo hiyo kwa kuwa tayari ilishaiabisha serikali. Alisema anasikia kuna kesi Ufaransa kuhusu mitambo hiyo kitu kinachomshangaza kwa nini serikali inataka kununua mitambo ambayo ina kesi.
CHANZO: Mwananchi
BIG UP,MHESHIMIWA SPIKA.
BINAFSI HADI MUDA HUU SIELEWI HAO WANAOTAKA MITAMBO YA DOWANS INUNULIWE WANA AJENDA GANI!NACHANGANYWA ZAIDI NAPOSIKIA WATU KAMA ZITTO KABWA NA PROFESA LIPUMBA NAO WAKIPIGA DEBE MITAMBO YA DOWANS INUNULIWE.HUU NI UNAFIKI WA MCHANA KWEUPE.WHY?BECAUSE KUNUNUA MITAMBO HIYO NI KUHALALALISHA UJAMBAZI WA DOWANS NA KAKA YAKE RICHMOND.HIVI INAINGIA AKILINI KWELI PALE TAPELI ANAPOKUUZIA MALI FEKI KISHA UKAMKALIA KOONI MPAKA AKAKIRI KUWA KWELI ALICHOKUUZIA NI FEKI,HALAFU UKAISHIA KUONGEZA FEDHA KUNUNUA MALI HIYO FEKI!?
I WOULD ONLY SUPPORT MATUMIZI YA MITAMBO YA DOWANS LAITI INGEKUWA IMETAIFISHWA (NA SIJUI KWANINI HADI MUDA HUU HAIJATAIFISHWA...WE MISS YOU BABA WA TAIFA).ETI AKINA KABWE WANASEMA TUWEKE MBELE UTAIFA KWANZA!UTAIFA KWANZA KWA MANUFAA YA AKINA RICHMOND?HAWA WAMEINGIZWA MKENGE NA VITISHO VYA TANESCO KUWA ETI NCHI IKO HATARINI KUINGIA KIZANI!YALEYALE YA RICHMOND!
WIZI MTUPU!

2 comments:

 1. Mambo vipi Mzee,katika matembezi yangu nimetua katika nyumba yoko
  Kazi nzuri sana na nashukuru kwa link yangu kwako, nami nitaweka yako kwangu

  ReplyDelete
 2. KUMEKUWA NA MAMBO MENGI YA KUSIKITISHA YAMEKUWA YAKIFANYWA NA HUYU MTU ANAYEJIITA ZEUTAMU...WE ALL TANZANIA'S LAKINI TUNAFANYIANA MAMBO YASIYOFAA KWA JAMII..WATU WANAFIKIA HATUA MPAKA KUTENGWA KWA KUHOFIWA NI WAATHIRIKA NA KUWA WANANYOOSHEWA VIDOLE MITAANI..NDOA ZA WATU ZIMEVUNJIKA KWA MAMBO YASIYO NA KICHWA WALA MIGUU YOTE HAYO NI KUTOKANA NA MAWAZO YA MTU MMOJA KUTAKA KUFURAHISHA NAFSI YAKE BINAFSI..
  BILA HATA MSHIPA WA AIBU WAZAZI WETU WANAANDIKWA HAPA KWA KASHFA NA MAMBO YASIYO YA KWELI..

  SIKATAI MTU KUWA NA UHURU WA KUFANYA ANACHOKITAKA BUT ALL IN ALL KUNA BOUNDARIES AU MIPAKA KATIKA KILA MAMBO UNAYOYAFANYA..OFCOURSE SIKATAI YA KWAMBA KILA MTU ANA HAKI YA KUFANYA ANACHOKITAKA.
  HUYU BWANA MDOGO NITAPENDA KUMUITA HIVI KUTOKANA NA KUWA NA UPEO MDOGO KATIKA MAMBO ANAYOYAFANYA INGAWA NI MTU MZIMA ANAYESTAHILI KUITWA BABA..
  TO SOME EXTENT HE HAS DONE SO MUCH WORSE THAN BETTER SINCE HE STARTED HIS BLOG UNOFFICIALLY...
  WHAT BOTHERS NI WATU WANAKOSA AMANI KUHOFIA KUPIGWA PICHA AU KUIBIWA PICHA ZAO KWENYE NETWORKS ESP. SPCIAL ONES WHERE MOST PEOPLE MEET SO AS TO EXCHANGE THEIR IDEAS..
  I BELIEVE EVERYONE HAS THE RIGHT TO EXPRESS HIS OR HER FEELINGS...
  ANYWAYS NISIONGEE MENGI
  I WOULD LIKE TO SHARE THE FOLLOWINGS WITH YOU..

  HII NI EMAIL AMBAYO TUMEIPATA ALIKUWA ANAMTUMIA MTU AMBAYE ANATUMIA JINA LA "MARIAM MOHAMED" WHO HAS A FACEBOOK ACCOUNT with detail

  Account Name: Mariam Mohamed
  Hometown: London UK
  Sex: Female
  Email:[email protected],[email protected] m(the same email ipo kwenye website ya utamu)
  If you can read between the lines you will realise thats a fake account
  this was what The named GERALD KIGISI([email protected]) wrote to Mariam
  "
  Mambo bro,
  ebwana nimekua bizi kinoma, ile forum yani bado kidizaini ila naishughulikia.
  sasa tunakukaribisha kwenye zeutamu blog, unakaribishwa kua blog contributor... yani uweze kuweka posts.... Unaruhusiwa kurusha posts zozote ila PLEASE posts ziwe mambo yakibongo bongo tuuu!!! weka unachotaka lakini kuna boundaries... hizo boundaries tutazijua when time comes...

  Namna ya kulogin: www.************/wp-login.php
  username yako ni: zeutamu
  password ni: *******(privacy but when in need email me)
  Please angalia how wordpress works... jaribu kurusha picha moja au mbili kwa kutest. inahitaji kupractise kdogo lakini sio ngumu.
  I MUST REQUEST YOU TO KEEP THIS INFO AS PRIVATE AS POSSIBLE... kikitokea kitu chochote toka kwako ambacho hakiendani na zeutamu practise ntadelete account yako.
  Any questions please contact me and I will help you..."

  so far this nigga GERALD KIGISI who hosts the web www.************
  The Above Resides at the following adress
  www.************ IP address location & more:
  Host of the IP: www.************ [Whois] [Reverse IP]
  Host IP [?]: 174.132.156.66 Copy [Whois] [Reverse IP]
  IP address country: ip address flag United States
  IP address state: Texas
  IP address city: Houston
  IP postcode: 77002
  IP address latitude: 29.7523
  IP address longitude: -95.3670
  ISP of this IP [?]: THEPLANET.COM INTERNET SERVICES
  Organization: THEPLANET.COM INTERNET SERVICES
  Local time in United States: 2009-03-03 07:08

  The Above graduated at a certain community college in United states of america on 1998
  The college details with the students ID number and Registartion No

  Hutchinson Community College
  Admissions: [email protected]
  Business Office: [email protected]
  General Information: (620) 665-3509
  Accounts Payable: (620) 665-3423

  Gerald Kigisi
  Reg No. Hut8266-423IBB
  Course: Comp Sci & Techn..
  Year of graduation Fall 1998

  HE CURRENTLY WORKS AT THIS COMPANY

  Litton Loan, Houston, TX.
  Litton Loan, Houston, TX., And Fidelity National Field Services, Ohio
  Phone: 800-247-9727
  Fax: 000-02365198

  Litton Loan - Houston TX And FNFS-Ohio
  Houston, Texas, 77081
  U.S.A.


  ANYONE WHO CAN I DENTIFY THEM PLEASE CHECK THE PICTURES BELOW...THE ONE IN A PASSPORT SIZE IS SAID TO BE ISSA KUMBENA AND THE ONE that has appeared twice IS SAID TO BE GERALD KIGISI

  SO FAR THIS GUY ANAANZISHA FORUM IN COMING FEW DAYS WHICH WILL ENABLE HIM TO EARN SOME MONEY WITH EVERYONE WHO WILL REGISTER IN HIS FORUM WILL CONTRIBUTE TO HIS PAYPAL ACCOUNT $2 FOR EACH PERSON THAT WILL REGISTER IN HIS FORUM..
  HE HAS NOT YET LAUNCHED IT BUT I HAVE DECIDED TO POST IT TO THE PUBLIC AND LET YOU ALL MY PALS SEE IT AND WE CAN HELP EACH OTHER TO SEIZE THIS SHIT
  the website is
  http://www.************/kijiweni
  TRY TO LOGIN AND SEE HOW THIS GUY IS A FOOL WASTING TIME CREATING SOME GARBAGES..!!
  please let us help each other katika kumu end up this fool..
  I ts not a hard thing but we need cooperation
  WHAT WE ARE DOING NOW

  WE ARE RETREIVING ALL THE EMAILS THAT USED TO SEND PICTURES AND ALL SHIT TO THIS EMAIL
  [email protected]
  [email protected]
  [email protected]

  So far Those who used to send him pictures I feel sorry for them coz we will let the world know them..!!

  Huyu ni Gerald Kigisi

  Huyu ndio Kigisi

  huyu anajiita issa kumbena ila facebook anajulikana kama MAriam Mohamed

  ReplyDelete

Categories

Blog Archive

© Evarist Chahali 2006-2022

Search Engine Optimization SEO

Powered by Blogger.

Podcast

Chaneli Ya YouTube